Picha la kutisha: Hiki ni choo cha mtu na kuna wapangaji, Serikali mpo wapi?

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Kuna haja ya mamlaka kuwachukulia hatua wenye nyumba wasiojenga vyoo hebu oneni hiki ni choo cha kushare na wapangaji wapo wa kutosha usiangalie kama una moyo mdogo

Kuna Post nimeiona huko mtandaoni mtu kaenda kupanga chumba Kigogo maeneo ya Mburahati huko alisahau kukagua choo kwasababu aliambiwa chooni kuna mtu anaoga akalipia kuja kuhamia choo chenyewe ndo hiki sasa!!

Nimeamini Tanzania kuna watu wanaishi maisha magumu hiki choo ni hatarishi sana. Hivi mnatoa wapi ujasiri wa kwenda kupanga huko kwenye Slums uswahilini?

Nimewaza nyumba inakuaje na choo kama hiki??Nimeona kinyaa kabisa kuna haja ya serikali au mamlaka husika za mitaa au wahusika wa mazingira na mabibi na mabwana afya na kuja na ukaguzi wa vyoo maana ni hatari sana

Choo chenyewe ndo hiki👇👇

1693839322729.jpg
View attachment 2738902
 
Kuna watu wamekariri kuwa Chooni ni sehemu chafu,

Choo kinatakiwa kiwe kisafi kuliko hata chumbani mwako,

Ukienda sehemu na ukataka kupima ustaarabu/usafi wa wa hiyo sehemu, anza kwa kukagua choo, ukikuta choo ni kisafi basi kila sehemu ya hiyo sehemu itakuwa ni safi.
 
Back
Top Bottom