Picha: Itatuchukua miaka 500 kumuonyesha rais dole!

Picha: Itatuchukua miaka 500 kumuonyesha rais dole!

Nijuavyo msafara was rais wa marekani huwa haupishani na kitu
 
Uko sahihi kabisa mkulu, Marekani wana desturi za hovyo nyingi tu. Na hizo wala hazina uhusiano na maendeleo. Ni ujuha wao tu ndo unawafanya wawe hivyo. Mbona Japan ambao wako mbele sana kwenye welfare of the citizens zaidi ya Marekani wana desturi nzuri ajabu?


Amanijua usifikiri kukiwa na maendeleo basi pia nayo maadili yanakuwa juu. wamerakni wamechanganyikiwa maadili yao yako kwa kiwango cha chini sana.
Hicho anachofanya huyo muendesha baiskeli kwa maadili yetu hakikubaliki kabisa. ni utovu wa nidhamu. hata katika ngazi ya familia mtoto akimfanyia yeyote yule achilia baba, lazima apewe nidhamu.https://www.jamiiforums.com/members/amanijua.213446/
Huyu Mama kafukuzwa kazi

Woman fired for making gesture at Trump
 
Hapana, tusiige kila kitu, bali yale mazuri tu, kama hili la kuruhusu kumpinga Rais kwa gesture zinazotumiwa na raia dhidi ya raia wa kawaida wanavyopingana mtaani.

Okay, na wewe jaribu ku deal na hili swali ambalo kati yenu watetezi wa Rais hakuna aliyeweza kunijibu siku ya tatu leo:

Huo utamaduni wetu wa kutotukana unamlinda kila Mtanzania au ni utamaduni kwa mtu mmoja tu, Rais?
Mtetea matusi kwamba ndo democracy huyu Mama kafukuzwa kazi hiyo democracy ipo wapi

Woman fired for making gesture at Trump
 
Ata sisi tunanyoosha mbona tena sisi viwili[emoji111] [emoji111] [emoji111]
 
Nje ya kamera hilo jambo hata kwenye jamii za Wamarekani halikubaliki na unaweza ukachukuliwa hatua za kisheria...........au kama ni kwenye maeneo yenye vurugu kama Detroit au Michigan inaweza kupelekea kupoteza uhai........

Ni mambo yanayorushwa kwenye mitandaoni au media ili kupromote jambo fulani..........

Wamarekani wenyewe ni maadui wa demokrasia ingawa wanajitanabaisha ulimwenguni kuwa na wakomavu wa demokrasia.......

Jiulize wako wapi wale wana vugu vugu waliokuwa wakichochea kujitenga kwa jimbo la California.....!!?

Lakini wao wapo mstari wa mbele kupigania kujitenga jimbo la Tibet na Taiwan huko Uchina........huku wakiwasihi watu wa Catalunya wasijitenge na Uhispania......
Exactly, huyo Mama kafukuzwa kazi sijui hiyo democracy ya matusi wanayoteteaga watu humu ipo wapo

Woman fired for making gesture at Trump
 
4028.jpg


Mwendesha baiskeli anae share barabara na msafara wa Rais Donald Trump huko Sterling, Virginia, Jumamosi October 28, akimuingiza Rais "dole."

Wanasema Rais wa USA ndio mtu mwenye nguvu kupita wote duniani, lakini nguvu zake za kibabe mwisho wake Chumbe kwa kwenda mbele, hazingii ndani ya nchi, juu ya raia. Kumpinga Rais kwa namna yeyote ile "ruksa"!

Kwa hapa Afrika huyo mama angekamatwa angemeza hiyo baiskeli. Iliwahi kutokea South Afrika mwaka 2010, ma bodyguard wa Jacob Zuma waliruka kwenye magari wakambeba raia Chamani Maxwell, wakaondoka nae.

Source:
Huyu Mama kafukuzwa kazi sijui hiyo democracy ya matusi unayotetea ipo wapo

Woman fired for making gesture at Trump
 
Kama alishafariki je?
Haiondoi kuwa alikuwa nyumbu! What matters are the genes which are transmitted to the offspring! Watu wanasahau kuwa maneno hayo ni matusi, hivyo unapoliandika , ukijibiwa usikasirike, tegemea jibu lolote na uwe na ustahimilivu. Kwaheri. we end there!
 
That's another thing.

Kamwe hawafungi barabara eti Rais anapita.

Huku kwetu mtu hata hajaondoka mjini, yuko Ikulu anaoga, ana safari ya Airport, watu wa Chanika, Chang'ombe, Gongo la Mboto, Vingunguti, Buguruni, Temeke Vetenari, mnasubiri mshafungiwa barabara rais anapita.

Barabara ikisafishwa nyeupe na mwendo ule wa misafara ni dakika 15, 20, tu kutoka mjini mpaka Airwing pale. Sasa kwa nini tunazima magari masaa mawili tunasubirishwa Rais anapita? It means wakati mnapoanza kusimamishwa huwa yuko Ikulu anaoga au bado kalala na mkewe! Kwani uongo?

Eti Rais wa Wanyonge. Unajali wanyonge gani we mzee?
We unajuaje kuwa kalala na nkewe? Wewe pia ni mmojawapo wa masikini na wanyonge anaowajali
 
Tuambie pia itakuchukua mudagani kumuonyesha babayako mzazi 'dole'....
Kwamfano akisema nilipomuoa mama yenu sukari ilikuwa sh. 5000 lakini sasa imeshuka hadi 2600 Nitamnyooshea kidole ilikumpinga. Au akisema Sadam ni rais wa Kuweit
 
Haiondoi kuwa alikuwa nyumbu! What matters are the genes which are transmitted to the offspring! Watu wanasahau kuwa maneno hayo ni matusi, hivyo unapoliandika , ukijibiwa usikasirike, tegemea jibu lolote na uwe na ustahimilivu. Kwaheri. we end there!
Hivi neno linakuwa tusi katika mazingira gani. Mbunge mmoja alisema waziri mkuu ni mpumbavu. Wakampeleka mahakani. Mahakama ikasema sio tusi. Rais akiwa jukwaani kuwasubiri madiwani "waliojiuzulu" kisha kutotokea tulimsikia akisema ni wapumbavu kabisa! Pia Rais alisema wale wanafunzi waliofukuzwa Udom walikuwa ni vilaza. Hakupekwa mahakamani. Mtu mmoja baadaye akasema rais ni kilaza namba moja. Akapelekwa mahakani na kuhumiwa kifungo miezi 6 au faini mil 5 Akalipa faini. Pro CCM wanapenda kuwaita wapinzani nyumbu. Hili kwao sio tusi. Lakini kesho mtu akimuita mwanaccm nyumbu ghafla tutaambiwa ni tusi. Mkuki kwa nguruwe
 
Back
Top Bottom