Picha: Itatuchukua miaka 500 kumuonyesha rais dole!

Picha: Itatuchukua miaka 500 kumuonyesha rais dole!

Kila nchi na utaratibu wake... Tanzania unaruhusiwa kumkosoa Rais lakini siyo kumtusi
Hakuna kitu kma icho. Magufuli si wa kukosolewa. Yeye hata ukimyoshea tu kidole kosa. Sasa ukimpga dole itakuaje?
 
4028.jpg

Mwendesha baiskeli anae share barabara na msafara wa Rais Donald Trump huko Sterling, Virginia, akimuingiza Rais "dole."

Wanasema Rais wa USA ndio mtu mwenye nguvu kupita wote duniani, lakini nguvu zake za kibabe mwisho wake Chumbe kwa kwenda mbele, hazingii ndani ya nchi, juu ya raia. Kumpinga Rais kwa namna yeyote ile "ruksa"!

Kwa hapa Afrika huyo mama angekamatwa angemeza hiyo baiskeli. Iliwahi kutokea South Afrika mwaka 2010, ma bodyguard wa Jacob Zuma waliruka kwenye magari wakambeba raia Chamani Maxwell aliyemuingiza Rais Zuma dole, wakaondoka nae.

Source:

Na wewe itakuchukuwa miaka mingapi kumuonyesha Babako mzazi dole?
 
Kila nchi na utaratibu wake... Tanzania unaruhusiwa kumkosoa Rais lakini siyo kumtusi
Kwa sasa hata kumkosoa unaweza shtakiwa.
Kama huamini itisha mkutano na waandishi halaf sema "Mwaka 2015 bei ya sukari haikuwa 5000/- ilikuwa 1500/-,au sema barabara ya Bagamoyo ilijengwa chini ya kiwango ndio maana kwa sasa inevimbavimba"
 
Hilo jambo halihusiani na ukomavu wa demokrasia bali ni upotofu mkubwa wa maadili.......ni vitu ambavyo si vyema kuigwa kwenye jamii zetu za kiafrika ambapo walau tuna chembe za maadili........

Kuna aina nyingi za ku onyesha kutokubaliana na mtu lakini si kwa kumtusi....kwani nje ya tofauti zenu za kisiasa huyo mtu ana ana familia inayomtazama kama kioo.....
Mkuu wewe upo hapa tz??
Kuna MTU alihoji PhD ya mkulu akapotea mpaka Leo,kuna mtu anashutumiwa kununua madiwami kwa rushwa kapandishwa cheo na kuwa RC, kuna MTU anaapa viapo vya kisheria kwa jina la MTU mwingine lakin mpaka Leo ni Mkuu wa mkoa,hana vyeti na wengine wamefukuzwa.

Utalisikia lipumbufu limoja linaharisha hapa eti sisi tunautamaduni wetu na hatupaswi kuiga mambo yao hayana maadili!!!? Tuchukue mambo mazuri tu kutoka kwao.... Haya sasa , mbona hampendi watu kuhoji? Mbona mnakumbatia rushwa?? Mbona kunawatu wapo juu ya sheria??
Mbona hakuna demokrasia, ushindi kwenu hata kama watu hawawapendi Lubuva anawabeba!!!! Mambo gani mazuri kwenu mnayoona yanafaa kuigwa huko kwa nchi za wenzetuu??

Pumbafu zenu kabisaaaa
 
Wenzio haya mambo hata kwenye familia zao yapo .....sasa na wewe anza kumuingizia dole babako aliekuzaa hapo kwenu uje na ushahidi hapa alafu ndo tujadili hoja yako.
shubaaaamit
Na wenzetu kwenye familia zao baba anadanganya tu familia?Maana huku tunajua sukari haikuwa 5000/- ila tuliambiwa na tukapiga [emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Kwanza huku kwetu inawezekana vipi uwe hapo barabarani wakati mheshimiwa anapita??

Hata USA haiwezekani pia, hiyo ni show, kama wanafunga Air space wkt mwingine mji mzima kabla hata Raisi wa USA hajafika ije kuwa uendeshe baiskeli njia yake?
 
Kwa sasa hata kumkosoa unaweza shtakiwa.
Kama huamini itisha mkutano na waandishi halaf sema "Mwaka 2015 bei ya sukari haikuwa 5000/- ilikuwa 1500/-,au sema barabara ya Bagamoyo ilijengwa chini ya kiwango ndio maana kwa sasa inevimbavimba"
Mbona hayo wamesema sana tu wanainchi kuhusu bei ya sukari kuwa mwaka 2015 haikuwa 5000
 
Yule mama nesi wa Mbeya baada ya kutimuliwa kazi nini kuliendelea aloh!
 
Nje ya kamera hilo jambo hata kwenye jamii za Wamarekani halikubaliki na unaweza ukachukuliwa hatua za kisheria...........au kama ni kwenye maeneo yenye vurugu kama Detroit au Michigan inaweza kupelekea kupoteza uhai........

Ni mambo yanayorushwa kwenye mitandaoni au media ili kupromote jambo fulani..........

Wamarekani wenyewe ni maadui wa demokrasia ingawa wanajitanabaisha ulimwenguni kuwa na wakomavu wa demokrasia.......

Jiulize wako wapi wale wana vugu vugu waliokuwa wakichochea kujitenga kwa jimbo la California.....!!?

Lakini wao wapo mstari wa mbele kupigania kujitenga jimbo la Tibet na Taiwan huko Uchina........huku wakiwasihi watu wa Catalunya wasijitenge na Uhispania......

Waafrika wengi hawawaelewi Wazungu, uko sawa kabisa huwo ni usanii tu, kwanza Raisi wa USA huwa wanafunga hata air space akipita!
 
Ni ujinga kuamini kila anachokifanya mzungu tunapaswa kukiiga licha ya ukweli wameendelea kuliko sisi.

Uruhusiwe kumnyooshea rais madole then upate faida gani baada ya kumnyooshea ni ujinga usiopaswa kushangiliwa na kuigwa eti kisa tu umefanywa na mzungu.
Na rais anapata faida gani kukuita wewe KILAZA au MPUMBAVU?
 
Mbona hayo wamesema sana tu wanainchi kuhusu bei ya sukari kuwa mwaka 2015 haikuwa 5000
Wamesema wapi?Tangu rais aseme hayo ni mwananchi gani alojitokeza mbele ya kamera kupinga hiyo KAULI
 
Dah.... Kumuingiza dole mwanaume wa kiafrika ni tusi lisilovumilika....Angekuwa rais wa kiafrika angeshuka mwenyewe amshughulikie..[emoji13] [emoji87] [emoji41]
 
Na rais anapata faida gani kukuita wewe KILAZA au MPUMBAVU?
Swala hilo ni nje ya maada inayojadiliwa.Maada inahusu raia kumtukana rais na mtoa uzi anatamani ingetokea Tanzania.

Hata hivyo kosa moja siyo sababu ya kuidhinisha kosa la pili.Rais akitukana raia ni kosa na inabidi ajirekebishe ila hiyo sio sababu ya kusema na raia amtukane rais kisa rais alifanya hivyo.

Kwa anaeshadadia rais atukanwe kisa yeye rais alitukana mimi namuona mjinga tu.
 
Hilo jambo halihusiani na ukomavu wa demokrasia bali ni upotofu mkubwa wa maadili.......ni vitu ambavyo si vyema kuigwa kwenye jamii zetu za kiafrika ambapo walau tuna chembe za maadili........

Kuna aina nyingi za ku onyesha kutokubaliana na mtu lakini si kwa kumtusi....kwani nje ya tofauti zenu za kisiasa huyo mtu ana ana familia inayomtazama kama kioo.....
kula like mkuu umeongea kama GT.
 
Mtz/Mwafrika bwana!!!! kwa hiyo unaamini kila kinachofanywa na mzungu ni sahihi!!!

vipi mleta maada wewe hapo nyumbani kwako itachukua miaka mingapi kuja kumuingizia dole mzazi wako?

ngoja nimalizie hii mihogo nitarudi!!!
 
Swala hilo ni nje ya maada inayojadiliwa.Maada inahusu raia kumtukana rais na mtoa uzi anatamani ingetokea Tanzania.

Hata hivyo kosa moja siyo sababu ya kuidhinisha kosa la pili.Rais akitukana raia ni kosa na inabidi ajirekebishe ila hiyo sio sababu ya kusema na raia amtukane rais kisa rais alifanya hivyo.

Kwa anaeshadadia rais atukanwe kisa yeye rais alitukana mimi namuona mjinga tu.
Yaani huyo mwanamke kuonesha Dole ka kati "tusi" na raia kuitwa wapumbavu "tusi" unatenganishaje?
Wote wametukana sasa kwanini wasijadiliwe kwa pamoja?
 
Back
Top Bottom