Jela jela tu, mambo ya fitness siri yake au labda kama umemkagua mwili mzima. Tunamkaribisha uraiani.Aiseee yuko fit
Wewe TUJITEGEMEE, usijitoe ufahamu kudai askari kakidhi vigezo, unakumbuka kipindi kile cha ziara ya Rais Obama hapa nchini jinsi askari mmoja wa kwetu alivyotaka kumzuia Mwandishi yule wa kike kwa ukali tena akiwa na kitambulisho shingoni hadi ikabidi askari wa FBI aingilie kati. Maaskari wa kwetu kwa kawaida hawatumii weledi hata kidogo , wao ni misuli zaidi.matukio yote mawili siyo mazuri:
1. Umakini wa Askari, inaonyesha Mh. Lema ahamini kama mahabusu, na Askari analazimika kuwa makini zaidi asije 'akamtoroka'. Ndiyo askari anasikiliza kama Mh. Lema anaweza akawa anaagiza kama ya DrugLord wa Mexico (ni samehe kwa mfano huu lengo ni kutaka kuhakikisha mnaelewa ninachokimaanisha), kumtorosha mahabusu. Huwezi kumlaumu askari katika mazingira haya. Kukosa kuaminiwa hasa kwa vyombo vya usalama si jambo zuri wala la kujisifia.
2.Bado hii inampunguzia Mh. Lema sifa muhimu ya kuaminika kama raia mtiisheria bila shuruti. unajua huyo askari nyota kaipataje? Jibu ni baada ya kukidhi vigezo muhimu sana vya kudhibiti mahabusu ama wafungwa. Sasa kama jeshi la Magereza linalazimiaka kutumia rasilimali watu muhimu kabisa walioiva, maana yake kuna shida mahali. Si vyema kujisifia mambo yanayotupunguzia sifa.
NOTE: Wewe Allen Kilewella na Mimi TUJITEGEMEE, maaelezo yetu juu ya hiyo picha hayana mashiko, hivyo hayatakiwi kutiliwa maani. Sababu kati yetu, hakuna anayejua askari yule anawaza nini, wala hatuji Mh. Lema alikuwa anawaza nini, na mkuu wa magereza aliyempanga huyo askari wa nyota alikuwa anawaza nini! Tusitumie maelezo yetu haya ku'justify' jambo lolote. Kikubwa tuombe wahusika wahakikishe haki inatendeka, na Mh. Lema arudishiwe uhuru wake kwa utaratibu sahihi unaojali haki na utu.
Ni ajabu sana pale watu wanapojifanya kukufagilia na kukupa matumaini bandia huku ukiwa ktk mateso gerezani,acheni kumdanganye mwenzenu eti upo ngangari wakat amesota gerezani na nyie mpo huru uswahilini
Nonsense.sasa kama yuko fit dhamana anataka ya nini?
si aendelee kukaa huko huko tu!
Nani anaondoka wa kwanza kati ya Hakim na mtuhumiwa baada ya Hearing ???Inavyoonekana court session imeisha ndio wakili akaenda pale kuongea nae........hapo lazima askari awe karibu maana hakunasessioon......ulinzi wa askari magereza unachukua nafasi
Asante sana Mkuu kwa kuto-kuulea upuuzi.Nonsense.
Hakimu ndio wa kwanza!!! Mnaachwa hapo polisi na magereza wanawazunguka kwa waliokosa dhamana!! Unaendaga mahakamani kweli au ndio akili za mitandao ubishi bila facts?Nani anaondoka wa kwanza kati ya Hakim na mtuhumiwa baada ya Hearing ???
Mmh maccm bhana,hata Farao aliamrisha mzaliwa wa kwanza kiume wa Waisrael wauwawe lkn na yeye alikufa. Kuuwawa na kupotea kwa viongozi wa upinzani si salama kwenu hata nyie mmeshakufiwa na viongozi wenu pia.Mkuu pamoja na kusema yote hayo lakini bado hakupunguzi adha za Binadamu kuwa Rumande au Gerezani. Nakuhakikishia kuwa Wewe unaweza labda ukawa unamwona Mheshimiwa Lema yupo ngangari ila nikuambie tu kuna uwezekano mkubwa tu moyoni mwake anaumia mno tena kwa mengi ila anajikaza tu kwa nadharia yao ya Ukamanda.
Kama Wewe unaona Mheshimiwa Lema huko alipo sijui rumande au gerezani anapata raha inayompelekea kutokuwa na hofu basi kaombe kubadilishana nae yeye atoke halafu Wewe ukae huko hata kwa siku tatu ( 3 ) kisha uje utupe mrejesho wako humu.
Namkubali sana Mbunge Lema ila akae akijua kuwa Siku zote sikio halizidi Kichwa na kama ile Kauli tunayoambiwa aliongea jana Mbunge mwenzie Kiukamanda Nassari kuwa yoyote anayepinga yanayofanywa na Serikali ya Rais Dkt. Magufuli ni taahira na akapimwe akili ni ya kweli basi Mheshimiwa Mbunge Lema amejitakia mwenyewe na inabidi tu sasa awe mpole.
Awamu hii ya Mr. Sulphuric Acid siyo ya Ki sport sport jamani Wanasiasa wa Upinzani hivyo nendeni nae kwa akili mno na mahesabu makali otherwise you will all be doomed.