TUJITEGEMEE
Platinum Member
- Nov 6, 2010
- 27,509
- 28,445
......
Jambo jingine nimejiuliza kama washtakiwa huwa wana faragha ama hawana wanapoongea na Mawakili wao wakiwa Kizimbani. Maana kwa namna yoyote hii picha inaonesha kwamba 1. Askari huyo anasikiliza kwa makini sana kinachoongelewa kati ya Lema na wakili wake. Ili iweje?
Lakini pia Lema anaheshimiwa hata na watesi wake. Pamoja na kumsema vibaya na kujaribu kumdhalilisha. 2. Lema analindwa na Askari Magereza mwenye cha Nyota moja. Maana yake hata hao wanaomchukia Lema wanaijua hadhi yake! Lakini siye akina yakhe huwa tukiingizwa Mahabusu ni lazima siku hiyo hiyo tunyolewa nywele. Walisahau kumnyoa nywele Lema ama ni heshima waliyo nayo kwake?
matukio yote mawili siyo mazuri:
1. Umakini wa Askari, inaonyesha Mh. Lema ahamini kama mahabusu, na Askari analazimika kuwa makini zaidi asije 'akamtoroka'. Ndiyo askari anasikiliza kama Mh. Lema anaweza akawa anaagiza kama ya DrugLord wa Mexico (ni samehe kwa mfano huu lengo ni kutaka kuhakikisha mnaelewa ninachokimaanisha), kumtorosha mahabusu. Huwezi kumlaumu askari katika mazingira haya. Kukosa kuaminiwa hasa kwa vyombo vya usalama si jambo zuri wala la kujisifia.
2.Bado hii inampunguzia Mh. Lema sifa muhimu ya kuaminika kama raia mtiisheria bila shuruti. unajua huyo askari nyota kaipataje? Jibu ni baada ya kukidhi vigezo muhimu sana vya kudhibiti mahabusu ama wafungwa. Sasa kama jeshi la Magereza linalazimiaka kutumia rasilimali watu muhimu kabisa walioiva, maana yake kuna shida mahali. Si vyema kujisifia mambo yanayotupunguzia sifa.
NOTE: Wewe Allen Kilewella na Mimi TUJITEGEMEE, maaelezo yetu juu ya hiyo picha hayana mashiko, hivyo hayatakiwi kutiliwa maani. Sababu kati yetu, hakuna anayejua askari yule anawaza nini, wala hatuji Mh. Lema alikuwa anawaza nini, na mkuu wa magereza aliyempanga huyo askari wa nyota alikuwa anawaza nini! Tusitumie maelezo yetu haya ku'justify' jambo lolote. Kikubwa tuombe wahusika wahakikishe haki inatendeka, na Mh. Lema arudishiwe uhuru wake kwa utaratibu sahihi unaojali haki na utu.