PICHA: Hii gari inapaa acha tu.Wachina hatari

PICHA: Hii gari inapaa acha tu.Wachina hatari

Sitaki kukubali ulichosema nataka kuamini umepita mtaa Fulani ukakuta hicho kigari kimepaki ukashangaa siku nzima huka ukipiga picha zisizo na idadi ukajikuta umechelewa feli hapo mwanza sasa umeamua tu ulale utaondaka kesho

.......
Hiyo ni Mali ya mjerumani
Anazitoaga kama ofa Kwa Wateja wakubwa wanaoweka order za magari
Mfano kampuni ya Volkswagen ,au macerdez Benz

Kwa Wateja wakubwa tu..
 
asee hicho labda kiwe chakuendea kliniki

Sasa huyo mtoto ndo utamuweka kwa wapi hapo na hicho kinabeba mtu mmoja tu? Ukiongeza mtu wa pili lazima mtoe tanki la mafuta kisha mafuta muweke kwenye chupa ya maji kilimanjaro ya lita moja na nusu
 
Aisee hicho kikobe hata ukigongana na vitz au passo tu kinakufinya ndani unafia humohumo
 
zipo gari ambazo zinapaa labda kama hujawahi kuona
Zipae kwani ni ndege??? Apart forom vile vigari za mashindano vinaruka juu kwenye miinuko na kushuka chini sijawahi hizo gari za kupaa. Hebu niambie ndio zipi nitoe ushamba
 
Kidude hicho ukikimbize si unahatarisha maisha yako? Chepesi na itokee unakumbana na magari hata sijui kitabaki nini hapo.
 
Kigari kama hiki unaweza paki ukakuta watu wamekaiba wanakabeba mmoja mbele mwingine nyuma wanakimbia nacho una amani!
 
Haka si ndo hata kukaosha unakatia kwenye beseni la kuoshea vyombo kisha unakikausha la taulo la kuogea, usiku unakiingiza bedrum unakiweka nyuma ya mlango.
hahahahahaha...!!jion yngu itakuwa nzuri,asante sana maana nmecheka mpaka mbavu znauma...
 
Back
Top Bottom