Gari jipya,,mileage mfukoni,,,,

Gari jipya,,mileage mfukoni,,,,

nzalendo

Platinum Member
Joined
May 26, 2009
Posts
12,889
Reaction score
14,596
Naaam ni alfajiri safari inaanza,,,gari ishakula nundu ina ambaa ambaa mitaa ya ''Port access'',,,,siku hizi mnaita Mandela road...chombo inapita mitaa ya Ubungo inakata kushoto,,,,kipindi hicho hakuna double road kama sasa,,,ofcoz na magari hayakuwa mengi kama hivi leo,,,

Naam chuma inainuka maeneo ya Kibo kuitafuta Kimara ...wakati huo minazi minazi na migomba,,,,,mdogo mdogo huku unakula ''bolingo'' muziki wa kiZaire...enzi hizo Zaire...... siku hizi mnaita Congo.... ilikuwa maarufu sana kwa muziki Afrika na nje ya bara la Afrika,,,nasikia hawa jamaa kilichowaangusha ni kukosa discipline(nidhamu).

Safari inazidi kukolea mizani ni kama hakuna ukilinganisha na sasa hivi,,,,,kama waelekea TANZAM road...kituo MIkumi kupata msosi halafu mitaa ya Ruaha tulikuwa na kasumba ya kupata bafu yaani tunaoga mtoni,,,ilikuwa raha sana,,,,,

Ilula ilikuwa ni sehemu ya kulala....na kwa sisi waonjaji tulikuwa tunakunywa komoni,,,nyakati hizo komoni ilikuwa tamu sana ukinywa unashiba,,,,kama ni msimu wa ulanzi pia twagonga,,,hapo tunapata dili kwamba wakati wa kurudi tutapata mizigo ya kupaleka Dar,,,zingatia nyakati hizo mizigo ilikuwa si taabu,,malori yalikuwa machache sana,,,,

Alfajiri safari inaendelea kuna sehemu inaitwa Tanangozi,,,palikuwa maarufu sana kwa nyama choma au supu kwa asubuhi,,,ninasikitika sana kuna kipindi Tanangozi ilikuwa kama mahame(this is another story).


Ngoma inainuka twapanda Ihemi ,,,,ni kigongo kisicho onekana kwa macho.....mara chap Ifunda hii hapa kama wataka kutoa lock haya...kama wataka kupofoa yote kheri tu.......Mafinga,,,,n.k n.k.

Chap kwa haraka Igurusi kigiza giza twa egesha kupata Ufyetere kidogo,,,kila kichochoro wasikia bolingo,,,,tunapata oda ya kuleta cassetee mpya za bolingo toka Dar...

Asubuhi chuma inainuka Tunduma Nakonde n.k n.k.

Kwa njia ya kati tukisha zunguka Msamvu chuma mdogomdogo yadema....... mawazo yakiwa Chalinze mbuzi,,,baada ya hapo Dodoma Inn

Cheki spring,,,,pakia mizigo ya kutosha vaa nguo za safari,,,,tafuta kampani ya kuongozana,,,,mbele mbele pale baada ya kibao cha PEPSI twaanza piga shimo,,,,

Tafuta miba ning"iniza nyuma piga shimo,,,kituo misigiri,,,,kula ''mtukuru'',,,,asubuhi shuka sekenke,,,mpaka shelui,,,, kula tena ''gongo'' safari yaendelea mpaka Nzega,,,mtafute Said Mgoha ana kila aina ya spana ,,kagua springi safari inaendelea>>>>>>
 
Hapo penye bolingo la zaire ilikua inapigwa BANDEKO YA PAZI ya mtaalam FRANCO RUAMBO RUANZO MAQIAD inaezapigwa mara 100 na watu tusiichoke yan toka changarawe mafinga mpaka igurusi ni hio hio...

hapo igurusi nanunua gongo ya 100(ilikua lita 1) nikikata nusu hapo naanza kuiimba hiyo nyimbo vile najua mimi tena kwa sauti yan "mandeko ya basi yoyo yoooyo,mandeko ya basi sibanzi lizalitee,ona niiinyooo yoyoyo"...
Humo kila mtu atacheka kivyake..
 
Back
Top Bottom