PhD za heshima: Msimu wa shahada za Ikulu umeanza tena

Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,698
4,693
Kuna wakati tuliambiwa China walimpa u-profesa JK. Hapo ilikuwa ni baada ya kupewa PhD za heshima huku na huko! Sasa tena mambo yameanza!

La kujiuliza eti chuo kikuu cha India kinaona mchango wa Rais wa TZ ni mkubwa kwao kuliko Waziri mkuu wao. Watu fulani wanashangilia, lakini kwa tunaojali nchi, hapo kuna jambo. Ni wepesi wa kuelewa udhaifu wa viongozi wetu.

Si mulionesha njia kwa UD kumpa rais wetu PhD ya heshima? Eti baada ya mwaka mmoja tu Chuo kikongwe cha UD kikaona huyu ni kiboko kwa mchango wa maendeleo. Ila hiyo ilikuwa kabla ya kuuza bandari zetu.

India waliona na waliskia na naamini ubalozi wao ulitoa taarifa hizo kwamba PhD ni dili kwa Ikulu yetu. Sasa PhD zitamiminika sana! Lakini tujiandae kupoteza vingi. NI sawa na biashara ya shanga kwa dhahabu na almasi za shinyanga.
 
Kituo cha Demokrasia Tanzania nacho kingekuwa na utaratibu wa kuwaenzi Wanademokrasia kila mwaka.

Tuzo yao mwaka huu 2023 ingeenda kwa Uongozi wa SAUTI YA WATANZANIA.
 
PHD zinaenda na vilio kwa wavuja jasho. Mkwere alipewa PHD tulikiona cha Moto bagamoyo. Huyu nae mjiandae .
 
ed271473-87d3-4034-ac09-8826b2b4941a.jpg
 
Mtahuzunika saaana mnao muonea gere mama. Pia fahamuni honorary degrees ni heshima ambayo inatolewa kwa vigezo maalum.

Kuna wasomi katika vyuo vikuu watu wanajua na kuthamini uongozi wa mh rais Samia katika:
1. Kuendeleza amani nchini hasa katika kipindi cha mpito baada ya kifo cha hayati Magufuli.
2. Kupunguza heka heka na wapinzani na kuwapa nafasi ya kuendesha shughuli zao.
3.Kuendeleza na kuongeza miradi mikubwa muhimu ya miundo mbinu itakayo panua uchumi wa taifa.
4. Ajira na nyongeza za mishahara.
5. Kupanua uhusiano na nchi nje ili kuvutia uwekezaji.
6. Kuongoza juhudi za kuimarisha na kupanua sekta ya utalii..
7.Kuboresha huduma za kijamii hasa katika elimu na afya, maji na mawasiliano
8. Ni mwanamke wa kwaza kywa rais nchini na amekua mfano wa kuwainua wanawake.

Mama chapa kazi tu usipoteze muda na distractors.
 
Tatizo kwa vile bongo phd imekua vita vya machoz jasho na damu imekua ukiskia mtu kapewa unaona hakustahil.kapataje pataje kirahis hajateseka hata na research hajakaa field. Phd za filosofia za heshima unapewa kwa kutambua mchango wa kitu fulan. Acha makasiriko mzee.
 
Sijui kwanini baada ya utawala wa Kikwete PhD zimekuwa deal kwa MaRaisi wetu.

Dr Jakaya Kikwete
Dr John Magufuli
Dr Samia Suluhu
Dr .............ajaye

Mbona jambo hili la Dokta......halipo Kenya

Rais Mwai Kibaki
Rais Uhuru Kenyata
Rais William Ruto
N.k

Sisi tuna shida mahali 🙌
 
Sijui kwanini baada ya utawala wa Kikwete PhD zimekuwa deal kwa MaRaisi wetu.

Dr Jakaya Kikwete
Dr John Magufuli
Dr Samia Suluhu
Dr .............ajaye

Mbona jambo hili la Dokta......halipo Kenya

Rais Mwai Kibaki
Rais Uhuru Kenyata
Rais William Ruto
N.k

Sisi tuna shida mahali 🙌
Huyu alipata ya halali siyo maigizo, pamoja na kwamba alikuwa ni dikteta lakini kichwani alikuwa ni mzima, wakenya hawaamini katika sifa wanaamini katika vitendo
 
Back
Top Bottom