PhD ya Dkt. Rais Magufuli iko sahihi, uthibitisho huu hapa

PhD ya Dkt. Rais Magufuli iko sahihi, uthibitisho huu hapa

Wanaotilia mashaka usomi wa JPM hawana hata degree moja, na ndio wengi hapa JF kama, kiongozi wao Mbowe ambaye alifeli UK na kurejea bongo kabaki kubangaiza bangiza tu na mbuzi aliyewauzia Chadema kwenye gunia aka Jambazi Sugu. Wanao bisha waweke shahada zao hapa hadharani ku-prove the point! Hawawezi I can bet you a nickel, watakuja na hadithi ndefu tu , we chubiri uone. Wengi wao wako marekani.
Kuna tetesi kwamba kufuli lugha ya malkia haipandi! Je hizo degree tatu alisoma kwa kiswahili au kisukuma??? Na kama ni english alifauluje???
 
Hujui ni nini unachokizungumzia. Na kama HUJUI usifanye UNAJUA.
Maelezo yako does not hold waters!

KWA UFUPI ni kuwa PhD ya Magufuli ni AUTHENTIC/Ni ya JASHO lake.
Hata kama wakati mwingine TUNAMKOSOA na KUMSIFIA in equal measure kama mimi .

Lakini katika hili la PhD yake Yeye yuko sawa kabisa. HAIHITAJI maelezo finyu!
Katika lugha ya Chato kijijini nasikia wanatumia neno "Getegete"/ meaning Perfect/ KAMILI kabisa.
Phd ya mwendo kasi
 
Upuuzi Wa hali ya Juu ni kujadili PhD ya mtu tena anaekuzidi kila kitu wakati wewe hapo ulipo hata certificate tu huna Huenda humu JF unatumia simu ya Shemeji ako kulog in...
 
Hivi ni nani wa kulaumiwa aliyepewa hiyo phd (MAGU) au udsm waliotoa hiyo phd. Mi nadhani hizo hoja kwamba phd ya mkulu Magu ina walakini (kama kuna ukweli uliothibitishwa) basi waliotoa ndio walaumiwe kwa namna yoyote ile uwezekanayo kwani MAGU hakuwashikia mtutu wa bunduki ili wampatie hiyo phd.
Kwanini ma lecturer wengi wa ud ndio wanaoteuliwa??
 
Kwa sisi tuliopita chuo kikuu ... hawa wazee wa spana kingereza huwa hakipandi sana kama wazee wa ngwini...hilo lipo wazi.....ndio maana somo la ds...walikuwa wanachemka mbaya ....kunyosha sentesi ilikuwa issue mpaka ...wakawekewa utaratibu wao wa kujibu maswali....wao ukinarate points inatosha haina haja ya maelezo mengi
Ivi kufuli ni injinia au mwalimu wa chemistry?? Mbona unatuaibisha wahandisi wewe mtoto??
 
Huyu mzee ndo maana alisema agejua asingegombea urais
 
Bongo kwa elimu ya vyeti hamjambo tuna ma injinia kibao lakini barabara zetu wanajenga wachina.utanielewa baadae
 
Hahaa.Namuonya Kim awe makini asijepelekwa kwa pilato na kuadhibiwa kwa kumkashifu na kumtusi kim sun chato.
 
Jamani nyie mnao hoji phd za watu wekeni kwanza za kwenu tuzione alafu ndo mjadili za wengine... Ndo tutaelewana..
 
Kuna tetesi kwamba kufuli lugha ya malkia haipandi! Je hizo degree tatu alisoma kwa kiswahili au kisukuma??? Na kama ni english alifauluje???
Kwa hiyo unaamini tetesi zaidi? Kwa hiyo na wewe ni katika wale ma - GTs? Weka yako kwanza, wewe ni wa level gani kabla hatujaendelea?
 
Upuuzi Wa hali ya Juu ni kujadili PhD ya mtu tena anaekuzidi kila kitu wakati wewe hapo ulipo hata certificate tu huna Huenda humu JF unatumia simu ya Shemeji ako kulog in...
Aiseee unaawudhi kweli, ngoja waje uone wanavyoporomosha maneno .. ... .. khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Mh. Rais amesoma PhD yake kwa jasho kabisa tena akijitahidi mno. Sasa wale ambao wanaishuku PhD yake ninataka wao watuonyeshe za kwao. Kumbukeni UDSM elimu yake si mchezo na Phd ilikuwa inachukua muda sana tofauti hata na vyuo vya nje ambavyo wengi ndiko walikopatia PhD fake. Acha Rais wetu aendelee kutumbua tu, hata angekuwa na elimu ya lowe Second mimi siangalii bali ninaangalia utendaji wake wa kazi. Kwani PhD itatufikisha wapi kama tutaendelea kulea mafisadi na wezi? Yaani acha abane ili tuwe na adabu na heshima mtaani iendelee.

Yaani Watu kama Wewe ndio wanaofanya Afrika iendelee kua masikini.
 
PhD ya Rais Dkt.Magufuli IKO SAHIHI.

Kuna aina 5 za PhD duniani zote ni za kitaaluma. PhD nayozungumza hapa ni ya ki Falsafa. Zifuatazo ni Sifa ambazo MTU huweza kutunukiwa PH D.

1. PhD ya Darasani: Unasoma degree ya kwanza(Bachelor), baadae unasoma degree ya pili(masters) baadae unasoma degree ya tatu katika mfumo WA utafiti(PhD). Basi unakuwa na sifa ya kuwa Daktari WA falsafa.

2. PhD ya Tukio: umesoma degree ya kwanza na ya pili, lakini ukaja kufanya jambo la kiutafiti bila kujua ambalo likasaidia jamii. Hapa vyuo hutunuku Masters na PhD kwa wakati mmoja au kama una masters unatunukiwa PhD moja kwa moja na chuo kinachoendana na jambo ulilofanya, mfano: kusuluhisha migogoro migumu na ukafanikiwa, kutoa mwongozo kwa jambo Fulani na likafanikiwa, umekuwa MTU mashuhuri kwa mambo ya kujenga jamii na jamii ikafuata na ikafanikiwa, n.k hapa unatunukiwa PhD bila pingamizi. Rejea PhD ya Dkt. Jakaya Kikwete na mgogoro WA Kenya 2007 baada ya kuwaweka sawa Wapinzani na Watawala.

3. PhD ya Utafiti: Umekuwa na degree moja au mbili na umekuwa ukifanya Dissertation mbalimbali ambazo zimekuwa zinasaidia jamii, hapa unatunukiwa PhD kwa kuzingatia juhudi binafsi za kujitolea.

4. PhD ya uandishi WA Vitabu: hapa unaweza usiwe hata na degree yoyote ile ukawa na cheti au diploma au degree(if possible), kutokana na MTU kuandika vitabu Mara kwa Mara vya kusaidia maswala mbalimbali ya kijamii na jamii ikanufaika na hivyo vitabu, basi mhusika kwa kuzingatia umhimu WA jambo hutunukiwa vyote kwa wakati mmoja yaani degree ya kwanza, ya pili na ya tatu PhD.

5. Tuzo ya Heshima: Hapa inategemea umefanya jambo gani katika jamii yako kitaifa au kimataifa ambalo jambo hill limeleta Neema kwa Taifa lako au Kimataifa. Hapa unaweza kutunukiwa tuzo ya Sir au PhD, unamkumbuka Sir George Kahama na tuzo ya mwingereza.

NB: Na sikila MTU hutunukiwa maana inategemeana na jambo lenyewe. Mimi Deogratius Kisandu, na washauri vijana wenzangu kabla huja hoji Elimu ya MTU, cha kwanza jifunze mfumo WA utoaji taaluma na Tuzo Duniani. Ndipo sasa uhoji. Kati ya hizo moja wapo Mheshimiwa wetu yupo.

Hongera Rais Dkt. John Magufuli kwa PhD ya Falsafa. Na kheri ya Mwaka Mpya.

deogratius Nalimi Kisandu
2 January 2017.
Kahama-Tanzania.

Nafikiri tatizo sio kwamba watu hawajui kama kuna PhD za heshima, wala uhalali

Watu wanachohoji ni kama kuna haja Ya Mtu kutunukiwa PhD kwa sababu za hatua za kisiasa au kuleta heshima au kwa kuonyesha Shukrani kwa sababu tu mtu amefanya kazi anayotakiwa kufanya kisheria ila imetokea kaifanya vizuri. Na hii imetokea muda huu ambapo viongozi wengi wanatunukiwa sio Hapa kwetu tu, Lakini kwa hapa kwetu ndio kuna Marais wawili mfululizo.

Sio Hivyo tu, hata Diamond alitaka kupewa PhD pale UDSM sema watu wakaipigia kelele sana.

Kwa nini kelele?....well, Kifupi ni kwamba hata maana Ya PhD ni mtu wa utafiti na ufumbuzi, kwa hiyo kuna haja Ya kuitunza heshima Ya hii hatua Ya PhD. Haina maana PhD Ya heshima sio kitu, ila lazima tukubali kuongeza misingi Ya kuifikia kama ilivyo kwa wanazuoni anaokesha kuisomea.

Ieleweke kwamba, kuna tunzo kama Nobel prize za wanasayansi na wavumbuzi na wana harakati lakini sio kila mwanaharakati wenye kupiga hatua kubwa amepata.

Kwa kufanya hivyo tutafanya hatua hii iwe sio tu na heshima ya kipekee, bali pia inakua ya kihistoria.imagine Rais wetu ndio kwanza ana mwaka kapata PhD..baada ya hapo?

Sasa fikiria kama angepewa kipindi anapoachia ngazi kama Shukrani na heshima kwa mchango wake Kipindi anatawala.nafikiri ingekua poa sana.

Lakini pia, kuna Njia nyingi za kuwatunuku watu wenye harakati...vyuo visikalie PhD tu.


Heri Ya Mwaka Mpya Pia.
 
Mkuu kumbe tunatofautiana uelewa. Publication nlivyokuelewa ni andiko ambalo limebandikwa kwenye journal/ jarida linalokubalika kwa ajili ya matumizi ya uma.

Aiseee!!

Ebu soma maana ya neno publication hapa:

"the act of printing a book, a magazine, etc. and making it available to the public; a book, a magazine, etc. e.g. that has been published"

"[mass noun] The preparation and issuing of a book, journal, or piece of music for public sale: e.g.
‘the publication of her first novel’

"[count noun] A book or journal issued for public sale: e.g. 'scientific publications’

Source: publication - definition of publication in English | Oxford Dictionaries

Halafu rudia tena kusema ulichokisema!! Hata gazeti ni publication. Sema kuna aina tofauti tofauti za publications: scientific publications, academic publications, government publications, popular publications n.k.

Monograph yaweza kuwa hata library halijafika mkuu. Na kama ni hilo unataka nenda UDSm au muombe jpm

Unafahamu kweli hata taratibu za kumaliza PhD? Maana unanishangaza kusema monograph yaweza kuwa hata library halijafika!! Unafahamu kwamba katika ku-submit copies za monograph, copy ya library ni moja ya hizo copies? Yaani kwa Magufuli aliyemaliza PhD yake kitambo hivyo, halafu hadi leo monograph isiwe library?!?

 
Back
Top Bottom