Peter Noni na Rostam - The EPA Connection

sio kwamba tumeanza kuchanganya mambo? sitaki kuamini kwamba haya ni mapambano ya kikabila. nadhani tuchimbe kwa undani na kurejea historia ya matabaka na historia ya uchumi wa nchi yetukwani kwa kuanza kusema kwamba kuna usukuma na uchaga tunarahisisha mno mambo.
 
Then mkuu hii ni vita ya kikabila kati ya wasukuma na wachaga!?

Inawezekana maana wengi waliopo mahakamani ni kina Kweka, Komu, Mramba, Mgonja nk

MKUU Limbani, thats a myopic observation, sasa hivi mahakamani vilevile yupo Chenge!
 
sio kwamba tumeanza kuchanganya mambo? sitaki kuamini kwamba haya ni mapambano ya kikabila. nadhani tuchimbe kwa undani na kurejea historia ya matabaka na historia ya uchumi wa nchi yetukwani kwa kuanza kusema kwamba kuna usukuma na uchaga tunarahisisha mno mambo.

Mkuu uko sawa kabisa, na hilo tumesha litwanga na ant- venom,

Ni sumu tu ilikuwa imeandaliwa makusudi isambazwe kwa ajili ya kututoa kwenye hoja ya msingi ya kuyakaba makoromeo ya mafisadi.

Waliamini itafanikiwa kama vile walivo ieneza 2005! wasijue watanzania wa leo sio wale wa 2005!

Mkuu inkosi, karibu sana kwenye uwanja wa mapambano, hakuna kulala hadi mafisadi warudishe kilicho chetu.
 
kwa bahati mbaya nilikuwepo pale white house wakati mambo ya ccm kupitishana kugombea kula nchi yetu. Lakini pia bahati mbaya nyingine nilikuwepo pale chimwaga wakati wajumbe wa ccm wanatuchagulia balaa awe rais wa nchi yetu.

Amini usiamini mambo ya ukabila yalipandikizwa na wanamtandao kwa kutumia propaganda kwenye vyombo vya habari ili wawashinde dk.(wa kweli) salim ahmed salim, sumaye na mwandosya.

Watu wa kanda ya ziwa waliambiwa watu wa kanda ya nyanda za juu kusini na kusini wameunda kitu kinaitwa "mtwara corrido' wanataka kuiteka nchi!

Watu wa kusini na ruvuma,iringa na rukwa waliambiwa kuwa wanyakyusa wanamtaka mwandosya ili nchi iendeshwe kikabila. Kanda ya kaskazini wakaambiwa ni heri kikwete kuliko sumaye kwani kikwete ni mtu anayejali sana maslahi ya wamasai chalinze.

Zanzibari wakaambiwa salim ni mpinzani wa mapinduzi ya zanzibar! Kikwete akapita katikakati kama mtakatifu. Hakuna ukabila ila watu wa mtandao ndiyo mpaka leo wanataka kupandikiza hofu ya udini na ukabila!

dhambi ya ubaguzi, ukisha ipanda ni kama mchawi, ukila nyama ya watu utaendelea kula nyama za watu-jk nyerere.
Dhambi ya maelezo hapo juu inaitafuna nchi
 
Hii thread kuna mtu au watu wanaiyumbisha maksudi kuzungumzia dini mara ccm na kanda! Hamna lolote, stick to hoja my people..sijaona katika maswali ya mwanakijiji akiongelea udini wala kanda....BOT ni Bank Binafsi ya watu wachache huo ndo ukweli wenyewe sisi tuendelee kuomba mikopo CRDB,NMB, Barclays nakadhalika na tukidefault tunachukuliwa mali zetu....ukitataka kumjua Noni fuatilia nani amekaa kwenye boards zilizo set CIS and EPA. How did BOT end up with such economically unsound schemes??
 
CCM kama chama wamevuta hela BOT for so long that it became the norm. Kwanza zilikuwa ni mikopo ya siri ambayo ilitakiwa kurudi through biashara mbalimbali za CCM kwa makubaliano maalum. CCM baada ya kushindwa biashara zao mbalimbali ikaona bora kuhusisha wafanyabiasha wakubwa tanzania mainly wa kiasia na weusi wachache, wajanja wakala na kujifanya kudelay payments knowing serikali haiwezi kujifuatilia yenyewe through kick backs. Ndo maana tumefika hapa tulipo leo ni kwasababu no one had the balls to say, Hizi hela zinahitajika na jamii na kwamba zinaaffect kikuzo cha uchumi wa nchi, kwasababu kila mtu alikuwa analinda maslahi yake na maslahi ya chama. Ntaendelea na msemo wangu HATUNA SERIKALI, MICHEZO HII YA KUVUTA BOT IMEANZA WAKATI WA MWALIMU KWA NIA NJEMA NA KUGEUKA GRANT SYSTEM YA WAJANJA.
 
Peter Noni na Rostam ni wabia wa biashara (Vodacom). Peter Noni ni shahidi wa serikali katika kesi za EPA zinazoendelea. Alikuwa ni bosi wa kina Imani Mwakosya, Esther Komu na Bosco Kimola. Katika ushahidi wake mwanzoni mwa mwaka huu aliiambia mahakama kuwa malipo ya EPA yalifanyika kwa idhini na ujuzi wa moja kwa moja wa Gav. Ballali. Alishuhudia mwenyewe kuwa taarifa zilitoka kwa Gavana kuja kwake, na baadaye kwenda kwa kina Imani.

Niliandika kwenye kijarida cha Cheche wakati nazungumzia mafisadi (mwishoni mwa mwaka jana) kuwa Peter anatakiwa kuwa miongoni mwa watuhumiwa wa wizi huu lakini nilielewa kwanini asingeweza kusimamishwa kizimbani - kwa sababu ni mtu mmoja ambaye anajua connection ya Rostam.

Mfanyakazi wa BOT ambaye ana uwezo na fedha ya kuanzisha kampuni ya Planetel (ningependa kweli kujua kampuni hii ilianzishwa lini na wana hisa wake!) na kuwa na hisa kubwa tu kule Vodacom ambazo walikuwa waziuze (sijui kama tayari wameziuza) kwa kampuni ya Mirambo inayomilikiwa na Rostam!

Mpango huo ulifanikiwa kwa ushirikiano mkubwa na usaidizi wa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu Bw. Andrew Chenge.

Well.. je waridi likiwa na rangi nyingine laweza kuwa si waridi?

Mzee Mwanakijiji. Sasa una over-reach. Hivi Noni kuwa mbia na Rostam huko Vodacom basi kumewafanya washiriki katika EPA?

Huyu Rostam ambae unadai kuwa alikuwa ana hisa pamoja na Noni kwenye Vodacom, sasa unadai kuwa alitaka kujiuzia mwenyewe kwenye kampuni ambayo anamiliki? Na huko nyuma mmetuambia kuwa hawezi kuajiri watu 6000 kwa vile hamiliki kampuni!

Zaidi ya yote, tangu lini kuuza na kununua hisa imekuwa ufisadi? Si ndiyo maana tuna stock exchanges?

Chenge kama waziri wa miundombinu ata-facilitate vipi uuzaji wa shares katika private company? Labda utuambie TTCL lakini si Vodacom.

Amandla......
 
Mzee Mwanakijiji. Sasa una over-reach. Hivi Noni kuwa mbia na Rostam huko Vodacom basi kumewafanya washiriki katika EPA?

Huyu Rostam ambae unadai kuwa alikuwa ana hisa pamoja na Noni kwenye Vodacom, sasa unadai kuwa alitaka kujiuzia mwenyewe kwenye kampuni ambayo anamiliki? Na huko nyuma mmetuambia kuwa hawezi kuajiri watu 6000 kwa vile hamiliki kampuni!

Zaidi ya yote, tangu lini kuuza na kununua hisa imekuwa ufisadi? Si ndiyo maana tuna stock exchanges?

Chenge kama waziri wa miundombinu ata-facilitate vipi uuzaji wa shares katika private company? Labda utuambie TTCL lakini si Vodacom.

Amandla......

Mkuu nakushauri u google tcra and chenge together... its in the open that he was supporting the change of the law ili mirambo iuze shares zao kwa foreigners. Ndo ujiulize mpaka waziri wa miundombinu anasema haya bila kuwaza implication zake on a wider scale??

ThisDay
 
Mkuu nakushauri u google tcra and chenge together... its in the open that he was supporting the change of the law ili mirambo iuze shares zao kwa foreigners. Ndo ujiulize mpaka waziri wa miundombinu anasema haya bila kuwaza implication zake on a wider scale??

ThisDay

Bado unanichanganya. Foreigners hapa ni nani na Mirambo ni nani? Itakuwaje sheria inayoruhusu Mirambo kuuza share zake kwa foreigners imwezeshe Rostam na Noni kuuza share zao kwa Mirambo?

Amandla........
 
Bado unanichanganya. Foreigners hapa ni nani na Mirambo ni nani? Itakuwaje sheria inayoruhusu Mirambo kuuza share zake kwa foreigners imwezeshe Rostam na Noni kuuza share zao kwa Mirambo?

Amandla........
"The former Attorney General and infrastructure development minister made no secret of his strong support for plans by the shareholders to sell their stake to foreign investors.

Official government records show Chenge advised the Ministry of Communications, Science and Technology, that there was no ’ongoing obligation’ for Vodacom to retain its partial local ownership.

He backed the arguments put forward by the local shareholders suggesting that their minority stake was just a requirement for licensing purposes.

Chenge argued forcefully in favour of the local shareholders that it was supposedly well within their rights to sell their stake in Vodacom to foreign investors, even though the existing regulations clearly state that all telecoms companies in the country shall have at least 35 per cent local ownership".

Mkuu nani kasema rostam kauza shares zake Vodacom? He simply moved them from Caspian to a holding group (Mirambo) thats all...hamna mauzo.
 
VODACOM SHARES ROW:AG issues legal opinion




THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

ATTORNEY General Johnson Mwanyika has advised the Ministry of Communications, Science and Technology to propose relevant amendments to legislation governing the country’s telecommunications sector in the wake of the row over the intended sale of a 35 per cent stake held by local shareholders in Vodacom Tanzania Limited to foreign investors.

Mwanyika avoided taking sides in the tug-of-war between Vodacom’s local shareholder, Mirambo Limited, and the Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), and instead suggested that amendments should be made to relevant legislation to resolve the matter.

In a letter addressed to TCRA in May this year, the AG advised the Ministry of Communications, Science and Technology currently headed by Dr Shukuru Kawambwa to initiate a process of amending the existing legislation and regulations.

’’Regarding the question of Vodacom (T) Ltd shareholder, Mirambo Ltd, wanting to use its shares as collateral for a loan from a foreign bank on condition that the shares can be sold to any non-Tanzanian should the company default on the loan, we wouldn’t want to issue an opinion because we are not the appropriate decision-makers on this matter,’’ said Mwanyika in his letter to TCRA, which was also copied to the Ministry of Communications, Science and Technology.

The AG supports the assertion by Vodacom’s local shareholders that both the Tanzania Communications Act of 1993 and the Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) Act of 2003, which govern the licensing of telecoms firms and most regulatory matters, are silent on the ’ongoing obligation’ for Vodacom to retain 35 per cent local ownership after receiving a licence to operate in the country.

However, Mwanyika, who is the government’s chief legal advisor, was careful not to make any formal opinion either in favour of the sale of the local shares to foreign investors or otherwise.

Well-placed sources say Vodacom’s shareholders are reportedly seeking a loan of more than $20.5m (approx. 27bn/-) from a South African investment bank, using their shares in the mobile phone company as collateral.

According to the shareholders, the foreign bank has set strict conditions that the 35 per cent stake in Vodacom Tanzania should be available for purchase or ownership by a non-Tanzanian entity, before it issues the loan.

The shareholders maintain that the 35 per cent local ownership clause was merely an ’eligibility requirement’ for acquiring a telecoms licence in Tanzania, which does not prohibit them from selling their stake to foreigners after Vodacom was granted a licence to operate in the country.

If the minority shares in Vodacom are indeed sold to a foreign company, the telecoms company would thus become 100 per cent foreign-owned, since 65 per cent of the shares are already owned by Vodacom Group (Pty) Limited of South Africa.

Industry watchers say TCRA is fiercely opposed to the proposed sale of the minority shares in Vodacom to would-be foreign investors because doing so would violate the Communications (Licensing) Regulations of 2005, which clearly state that all telecoms companies in the country shall have at least 35 per cent local ownership.

While Mwanyika was careful to avoid directly taking sides in the matter, ex-cabinet minister Andrew Chenge was all-out in favour of the controversial proposal by Vodacom’s local shareholders.

The former Attorney General and infrastructure development minister made no secret of his strong support for plans by the shareholders to sell their stake to foreign investors.

Official government records show Chenge advised the Ministry of Communications, Science and Technology, that there was no ’ongoing obligation’ for Vodacom to retain its partial local ownership.

He backed the arguments put forward by the local shareholders suggesting that their minority stake was just a requirement for licensing purposes.

Chenge argued forcefully in favour of the local shareholders that it was supposedly well within their rights to sell their stake in Vodacom to foreign investors, even though the existing regulations clearly state that all telecoms companies in the country shall have at least 35 per cent local ownership.

Before Mirambo Ltd, a locally-registered company, bought the minority stake in Vodacom, local shareholders of the company were listed as Caspian Construction Limited (19 per cent) and Planetel Communications Limited (16 per cent).

Vodacom (Tanzania) Ltd, the largest mobile phone operator in the country with more than 5 million subscribers, was licensed in the year 2000.

Imetoka hapa:ThisDay

Mbona mnachanganya mambo? Kutokana na taarifa mnayo quote, Caspian Construction Limited ambayo inajulikana kuwa ni ya wakina Rostam walikuwa na asilimia 19 za share za Vodacom na Planetel ambayo kutokana na maelezo ya Mzee mwanakijiji ni ya Noni, ilikuwa na asilimia 16, jumla kwa pamoja walikuwa na asilimia 35. Inavyoelekea ( ingawa si wazi) Planetel na Caspian waliuza share zao kwa Mirambo ( ambayo inadaiwa tena kuwa ni ya Rostam). Inavyoelekea tena ni kuwa Mirambo ilikuwa ikitafuta mkopo kutoka nje za nchi na walitaka kutumia share zao kama collateral kwa mkopo huo na si kuwauzia hao wageni. Share hizo zingeuzwa kama wange default kwenye mkopo huo. Sasa kuna ufisadi gani kwa mfanyabiashara kuomba kibali cha kuweka share zake mwenyewe kama collateral? Au tatizo ni kuwa benki yenyewe ni ya kigeni? Katika hii dunia ya kisasa ambapo fedha hazina mipaka lazima suala hili lingejitokeza. Kudai kuwa kujitokeza huko ni alama ya ufisadi ni unfair.

Amandla.........
 
Sasa jamani mwenzenu Ra alibanwa na CC ajisafishe au awajibike ndio maana akayasema aliyoyasema. Kwa hilo la kumtoa nyoka pangoni Mengi anstahili pongezi. Inafaa vifisadi vyote vimuige Mengi kwa angalau kulipa kidogo ndipo upate uhalali wa kusema. Alicvhofanya Mengi ni kuanzisha utaratibu wa Truth and Reconciliation ambao Mhe Zitto kabwe aliwahii kuupendekeza.

Hebu tuwaruhusu hawa watu wafanye kama Mengi kwa kulipa japo kidogo na kuja mbele ya Watanzania na kusema tazama angalau nimelipa hizi. Tuwasamehe ili warudishe mitaji waliyoficha nje hapa nyumbani tusonge mbele. La sivyo tutalishwa maneno matupu huku wenyewe wakijichana na mapesa yetu. Hakuna mwenye sheria ya kuwashtaki hawa ni kiini macho tu.
 
Ukifuatilia mada utagundua wengi wansuggest kuwa Vodacom inamilikiwa kwa kiwangi kikubwa na RA, hivyo misaada inayotolewa na Vodacom kwa upande mwingine inatolewa na RA. Then hoja kuwa RA hatoi misaada sio ya kweli. Labda hataki publicity. La msingi hapa ni kumuomba RA chonde chonde watanzania twaafaa!! punguza kasi ya kufisadi kidogo ili umaskini upungue kwa kuwa ukifisadi kweny energy sector ndio ushlifisadi taifa zima. Suala la kuburuzana mahakamani hapa halipo na naomba tulisahau kabisa, kwa kuwa tayari watu wameshaanza kujilinda kimajimbo. Hoja kuwa ni wachagga ndio waka mahakamani bado haijaniingia vizuri. Kwa kuwa wachagga wamekamata posts nyingi sana kutokana na kukua na kupanuka kwa elimu uchagani, hivyo idadi yao ya kufikishwa mahakamani lazima iwe kubwa pia. Mbona wapo akina Farijala hatuwataji. Tukienda huko tutapotea kwa kuwa mbona linasenwa sasa na halikusemwa wakati wanaenjoy matunda ya hizo posts.

Tanzania is breaking up. Truth and Reconciliation Commision is the solution ili tufute ya nyuma tusonge mbele na waliowahi waweze kurejesha mitaji waliyopora. Aliyenacho anacho tu. Ukiendelea kuchonga tutakufa njaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

RA kesha tuzidi katangulia. Lakini Mengi ameonyesha mfano kwa kulipa japo kidogo kabla hajapiga kelele. Ra na wewe basi lipa lipa mwanangu, ili ukaze buti kiaina.
 
Kwa bahati mbaya nilikuwepo pale White House wakati mambo ya CCM kupitishana kugombea kula nchi yetu. lakini pia bahati mbaya nyingine nilikuwepo pale Chimwaga wakati wajumbe wa CCM wanatuchagulia balaa awe Rais wa Nchi yetu.

Amini usiamini mambo ya ukabila yalipandikizwa na wanamtandao kwa kutumia propaganda kwenye vyombo vya habari ili wawashinde Dk.(wa Kweli) Salim Ahmed Salim, Sumaye na Mwandosya.

watu wa kanda ya ziwa waliambiwa watu wa kanda ya Nyanda za juu kusini na kusini wameunda kitu kinaitwa "mtwara Corrido' wanataka kuiteka nchi!

watu wa kusini na Ruvuma,iringa na Rukwa waliambiwa kuwa Wanyakyusa wanamtaka Mwandosya ili nchi iendeshwe kikabila. kanda ya kaskazini wakaambiwa ni heri Kikwete kuliko Sumaye kwani Kikwete ni mtu anayejali sana maslahi ya wamasai chalinze.

Zanzibari wakaambiwa Salim ni mpinzani wa Mapinduzi ya Zanzibar! kikwete akapita katikakati kama mtakatifu. Hakuna ukabila ila watu wa mtandao ndiyo mpaka leo wanataka kupandikiza hofu ya udini na ukabila!

Afazali uwaaambie watu Ukweli, Hawjui Kuwa hizi siasa zipo sana CCM na Tanzania kwa ujumla.Watu wanafikiri kusema ukweli ni dhambi, we need to say these things so that they dont keep us hostage.
 
Afazali uwaaambie watu Ukweli, Hawjui Kuwa hizi siasa zipo sana CCM na Tanzania kwa ujumla.Watu wanafikiri kusema ukweli ni dhambi, we need to say these things so that they dont keep us hostage.

Leo, wote tunajua Madhambi ya wana mtandao hadi kuwaambia watu kwamba Salim ni muhizb sijui?, sasa hayo ya mtandao si ndo unaona yana watafuna na kuwamaliza? lakini siyo kweli kwamba hilo ni swala la taifa zima, hako ni kagenge tu kaliko undwa na mafisadi ambako ndo tunapambana kukaangamiza!

Kwa vile tunajua kanaijua mbinu hii ya kuwagawa watu kwa misingi ya kanda, kabila rangi na imani,ndo maana tunapoona upepo huo unapenyezwa hapa na kwingineko Tz katika vita hii ya ufisadi, lazima tuipinge kwa nguvu zetu zote!

Mkuu, saa hii ni saa mbaya, dakika za majeruhi, hatuhitaji kurudi nyuma na kuruhusu hisia kama hizi za kutugawa, kama kuna wakati inabidi watanzania tushikamane na kupendana ni sasa, Inabidi tuwe kitu kimoja kuhakikisha tunalikomboa taifa letu mikononi mwa mafisadi.

Huyo Fisadi papa Kiongozi, Rostamu Aziz hawezi nunua taifa zima, hako ka kakundi atakako nunua tukiungana kwa nguvu zetu wote tukakapinga kata kwishilia mbali. Kaza buti ndo kwanza kumechangamka!
 
LeoKweli... CCM wenyewe wanasema 'chama kama chama hakikumtuma mtu kufanya ufisadi, ni watu wenyewe'.. Hilo swalii la nguvu za RA ni swali ambalo historia itachukua muda kulijibu.

Ndani yao kwenye CCM kuna watu wenye nguvu zaidi (nguvu ya dola) ambao wanaweza kuamuru mvua ikanyesha ikanyesha! RA ana nguvu kubwa, nguvu yake inatokana na ujuzi siyo fedha (kwani wapo wengi tu wenye fedha). Ni nguvu ya mtumishi anayejua nani kafanya nini... ni nguvu aliyoionesha juzi kwenye taarifa yake na ni nguvu aliyoionesha kwa Mtikila...

Kwenye Mafia hakuna mtu ambaye anaogopwa kama anayejua..... ndiyo maana RA hagusiki.... sikiliza maneno yangu: siku RA atasimama na kusema kuwa anataka kusema ukweli juu ya EPA n.k.. that same day itakuwa ni mwisho wake (literally). Amina Chifupa .... Ana nguvu kuliko malaika wa shetani!


RA hana Nguvu kama wewe mwanakijiji unavyo suggest. Uwezo wa RA unasabishwa na sisi kumpa kichwa. RA Nguvu yake Imeongezeka baada ya Mwanakijiji na wengine hapa kwenye forums kwa makusudi kuikwepa kuiblame CCM kwa EPA, Sijui mwanakijiji, umeahidiwa nini na CCM.
Kama RA ni golikipa wa CCM katika swala la EPA tukisema CCM ni mafisadi kwa nguvu tunaweza kuwaforce kumtoa kafara golikipa wao lakini kwasasa they cant do that because sio tatizo la Kichama na tunalifanya kuwa individual problem
 
mambo yanayomsibu RA vodacom
RA ni shareholder wa vodacom by default , ili vodacom waingie TZ inabidi kampuni iwe local 35% lakini local shareholders hawana hela za kufanya serious investment needed
kwenye expansion or miundo mbinu ya simu.
kwa hiyo vodacom sa ndio wamefanya hiyo investment mnayoiona na kwa ajili RA ni sleeping partner hawezi kupata dividend mpaka wale jamaa watoe loan yao, na karibu kila mwaka wana expand kwa kutumia retained earnings na mkopo
hivi vyote vikija kutolewa vodacom TZ inabakiwa na hela kidogo sana as dividend payment ya kuliva mirambo na vodacom sa

ni kama vile yeye alivyofanya new habari, yeye ndio ametoa hela ya invstment mpya kwa hiyo wakina salva wanakuwa wadogo pamoja na hisa zao
 
Rostam aliandamwa sana alipodai kuwa kampuni zake zimetoa ajiri kwa watu zaidi ya 6,000. Sasa humu tunaambiwa kuwa kampuni yake ya Mirambo ina asilimia 35 za share za Vodacom. Hivi Vodacom imetoa ajira kwa watu wangapi Tanzania? Kuanzia hao wa maofisini kwake, wauza vocha n.k.? Hawajafika 6000? Bado Caspian ambaye yumo sana kwenye migodi! Kwa kutanguliza chuki na munkari kwenye suala hili, hatutafika kokote. Kama kweli mnataka kumuwajibisha Rostam itabidi mtulie na kupanga mikakati iliyo bora kuliko hii iliyojazana humu!

Amandla........
 
icon1.gif
Re: Ripoti ya Richmond Bungeni

Kamati yawahusisha Waziri Mkuu, mawaziri Kashfa ya Richmond
* Richmond ni ujasiri wa kifisadi
* Zabuni ilitolewa kwa shinizo

* Uongozi wa Takukuru kitanzini


Na Waandishi Wetu, Dar na Dodoma


1. KAMATI Teule ya Bunge ya Kuchunguza Mchakato wa Zabuni ya Uzalishaji Umeme wa Dharura imependekeza kuwa viongozi wote waliosimamia na kuhakikisha kuwa Kampuni ya Richmond Development LLC inashinda zabuni hiyo wawajibishwe.


2. Akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo bungeni jana, Mwenyekiti wake, Dk Harrison Mwakyembe, alisema wamebaini na kuridhika ukiukaji mkubwa wa taratibu na sheria za nchi.


3. Dk Mwakyembe alisema, kamati imeona mawasiliano ya karibu kati ya Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Waziri wa Nishati na Madini wa zamani, Dk Ibrahim Msabaha na wa sasa, Nazir Karamag, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Arthur Mwakapungi katika hatua mbalimbali za zabuni hiyo, lakini hawakukiri kutumwa au kuagizwa kubeba kampuni hiyo ya Marekani na kwamba, kwa mfumo wa uongozi na utawala bora wanawajibika wenyewe.


3. Baada ya uchunguzi wake na kubaini mianya inayoashiria rushwa, kamati imependekeza wahusika kuwajibishwa na mamlaka husika, huku Waziri Mkuu akitakiwa kupima uzito wa suala hilo kwa kuamua kuwajibika mwenyewe au bunge kumwajibisha.

4. Lowassa amehusishwa na upendeleo wa kampuni hiyo kutokana na barua yake Juni 21, 2006 akiagiza kuwa Richmond ipewe zabuni hiyo na kwamba.
Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema, Ibara ya 52 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inatamka wazi kuwa Waziri Mkuu ndiye mwenye madaraka ya juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hadi siku wa kazi na shughuli za serikali na ndiye kiongozi wa shughuli za serikali Bungeni.


5. Alisema kamati haikufurahishwa na taarifa zinazomgusa moja kwa moja Lowassa katika kupendelea Kampuni ya Richmond Development na kwamba, kamati imetimiza wajibu wake kwa uwazi na ukweli kama ilivyoagizwa na Bunge. "Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shughuli za serikali na uongozi wa nchi kwa ujumla, ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya Bunge," alisema na kuongeza:


6. Hata hivyo, Dk Mwakyembe alisema, Dk Msabaha akiwa nje ya kiapo alieleza kamati kwamba, yeye ni mbuzi wa kafara kwa sababu biashara hiyo ilikuwa ya Lowassa na mshirika wake, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.


 
Back
Top Bottom