Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,378
- 18,738
Mfanyabiashara, Rostam Azizi kupitia kampuni yake ya Taifa Gas Tanzania Limited, kwa kushirikiana na Amber Energy Investment L.L.C-FZ, wameingia makubaliano ya kununua biashara ya gesi ya kampuni ya Orca Energy Group nchini Tanzania inayomiliki mradi wa Songo Songo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatatu, Aprili 13, 2026, Orca imesaini makubaliano ya mwisho ya ununuzi wa hisa (Share Purchase Agreement) na wanunuzi hao, ambapo itauza hisa zote za kampuni yake tanzu ya PanAfrican Energy Corporation (PAEM), inayomiliki shughuli zake zote za gesi nchini Tanzania.
Chini ya makubaliano hayo, Taifa Gas itanunua asilimia 49 ya hisa za PAEM huku Amber Energy ikichukua asilimia 51, hatua itakayokamilisha uhamisho wa umiliki wa mradi wa gesi wa Songo Songo kwenda kwa wawekezaji hao wapya.
Kulingana na taarifa hiyo Bodi ya Wakurugenzi ya Orca imeeleza uamuzi wa kujiondoa kwenye biashara ya Tanzania umetokana na tathimini ya muda mrefu ya hatari na changamoto zinazokabili shughuli zake nchini.
Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na migogoro inayoendelea, madai mbalimbali, pamoja na kutokuwa na uhakika wa hatima ya kuongeza muda wa leseni ya maendeleo ya Songo Songo na mikataba ya kugawana uzalishaji (PSA).
Soma Pia: Rostam Aziz anunua kampuni ya Nation Media Group ya Kenya
Ndani ya makubalinao
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Orca itauza hisa zake zote za PAEM kwa bei ya mfano ya dola 10 za Marekani, mbali na masharti mengine ya kimkakati na kibiashara yaliyokubaliwa.
Kabla ya kukamilika kwa mauzo hayo, Orca inaweza kulipwa madeni inayodai kutoka kwa kampuni zake tanzu, na pia inaweza kugawa gawio kwa wanahisa wake kulingana na masharti ya kifedha.
Aidha, Orca itapata asilimia 50 ya mapato yoyote ya ziada yatakayopatikana kati ya muda wa kusaini na kukamilika kwa makubaliano hayo.
Baada ya kukamilika kwa mauzo hayo, Orca haitakuwa tena na umiliki wowote katika biashara ya gesi nchini Tanzania, wala haitakuwa na wajibu wowote kuhusiana na matokeo ya baadaye ya leseni ya Songo Songo au migogoro yoyote na Serikali.
Aidha, kukamilika kwa makubaliano hayo kunategemea idhini kutoka kwa Tume ya Ushindani (FCC), Waziri mwenye dhamana nishati, wanahisa wa Orca, pamoja na mamlaka nyingine za udhibiti. Orca imeeleza kuwa itaitisha mkutano maalumu wa wanahisa wake ili kupiga kura kuidhinisha makubaliano hayo.
Mali zinazohusika
Kupitia kampuni yake tanzu ya PanAfrican Energy Tanzania Limited (PAET), Orca ilikuwa inamiliki haki zote za mradi wa gesi wa Songo Songo, ikiwa ni pamoja na mikataba ya uzalishaji, makubaliano ya masoko ya gesi na mali nyingine zinazohusiana na mradi huo.
Hata hivyo, kampuni imeeleza kuwa kwa kuzingatia hali ya mali hizo, thamani yake halisi kwa sasa ni ndogo kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo taarifa zote za kijiolojia zinamilikiwa na Serikali, na mali nyingi za kudumu zitarejea kwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) baada ya leseni kuisha.