Peter Msigwa: Biblia na viongozi wa dini wasitumike kupumbaza watu

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,206
103,779

Hakika nimemuelewa sana Peter Msigwa. Kuna viongozi wa dini muda wote ni kusifu tu, hata pale yanapotolea mambo ya hovyo hutawasikia wakikemea. Wale wachache wanapokemea wanaitwa wachochezi na wanaingilia siasa.

Waacha unafiki. Wanapopata fursa ya kukutana na viongozi wasifie na kuonya,huo ndio utumishi wa Mungu wa kweli
 
Tatizo njaa haiangalii mtu. Baadhi ya watumishi wa Mungu wa siku hizi za mwisho nao ni waganga njaa tu.

Wamekosa "credibility" ya kusimama kwenye nafasi zao kukemea na kuonya wanasiasa, wamebaki na unafiki tu.

Ndugu zangu wa upande wa pili nimewasikia chinichini wakisema wanatengwa kwenye teuzi mbalimbali ila sioni wakichukua hatua. Huu nao ni unafiki.
 
Kazi ya kiongozi wa dini Sio kuhubiri dhambi kazi yake Ni kuhubiri neno la Mungu

Msigwa kapotoka

Huwezi simama madhabahuni ukaanza kuhubiri kuwa Leo tutaongelea dhambi ya mchungaji Msigwa kuzaa na yule kimada wake kinondoni Wakati Ni mchungaji.Biblia imeagiza kuhubiri neno la Kristo Sio kuhubiri watu .Ikifika huko yeye mwenyewe Msigwa hatapona watoto wake wa nje ya ndoa wataletwa madhabahuni
 
Tuwaache na vitabu vyao vitukufu
Msigwa anachotaka ni kuwa viongozi wa dini wasimame madhabahuni na kuanza kuhubiri watu mfano unasimama unaanza kuhubiri kuwa Leo tutaongelea Jinsi sugu alivyotelekeza mkewe aliyezaa naye na tukimaliza tutaongelea kwa kirefu mahusiano ya nje ya ndoa Kati ya Joyce Mukya na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe!!!
 
Tanzania saivi ukiniambia nihesabu viongozi wa dini kwangu hawazidi 10. Hapo kuna Bagonza, Sheikh Ponda, Mwamakula, Niwemugizi, Munga na wengine wachache sana!

Wanaobaki hapo sio viongozi wa dini waite wafanyabiashara kupitia dini!!
 
Ni mjinga peke yake ambaye hajui ilo hadi ashikiwe akili na kiongozi wa dini mwenye maslahi binafsi.Nikweli dini zinatumika vibaya na matokea yake dini zimekosa hadhi watu wamebaki kua waumini na wafuasi wa dini kwaajili yakupata huduma ya maziko lakini sio kwa ajili yakusimama katika matendo mema kweli na haki.Ndo maana tunaona kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili uku tukiwa na lundo la nyumba zakuabudia.
 
Sugu unamuonea hajawahi telekeza mke. Faiza sio mwanamke a kusema sugu alimtelekeza,hana heshima,adabu etc alimuaibisha sana sugu na mama yake. Kwa pale sugu hana makosa na bado anamlea mwanae vizuri tu.
Msigwa anachotaka ni kuwa viongozi wa dini wasimame madhabahuni na kuanza kuhubiri watu mfano unasimama unaanza kuhubiri kuwa Leo tutaongelea Jinsi sugu alivyotelekeza mkewe aliyezaa naye na tukimaliza tutaongelea kwa kirefu mahusiano ya nje ya ndoa Kati ya Joyce Mukya na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe!!!
 
Sugu unamuonea hajawahi telekeza mke. Faiza sio mwanamke a kusema sugu alimtelekeza,hana heshima,adabu etc alimuaibisha sana sugu na mama yake. Kwa pale sugu hana makosa na bado anamlea mwanae vizuri tu.
Sugu ndiye alimsababishia kuwa chizi kwa kumfrustrate alipopata ubunge akamuona zilipendwa

Usimlaumu nwanamke mental torture ndio ilimfanya awe vile
 
Kuna saa nilikua namtetea faiza ila baada ya kumfahamu hapana kwa kweli na walikutana wote mapipa sio pipa kwa mfuniko,wasingewezana
Sugu ndiye alimsababishia kuwa chizi kwa kumfrustrate alipopata ubunge akamuona zilipendwa

Usimlaumu nwanamke mental torture ndio ilimfanya awe vile
 
View attachment 1537640

Hakika nimemuelewa sana Peter Msigwa. Kuna viongozi wa dini muda wote ni kusifu tu, hata pale yanapotolea mambo ya hovyo hutawasikia wakikemea. Wale wachache wanapokemea wanaitwa wachochezi na wanaingilia siasa.

Waacha unafiki. Wanapopata fursa ya kukutana na viongozi wasifie na kuonya,huo ndio utumishi wa Mungu wa kweli
Wamejifungia wakifanya mazoezi kwa ajili ya Jumatatu ijayo wakizindua kampeni ya miradi ya CCM.
 
Yaani nyie wa kupinga tuuu ndo wanafiki kabisa! Msigwa kasha changanyikiwa, kwanza Iringa mjini hatumpi kabisa ubunge ! Aliamua kumuachia Kaisari kayakimbia madhabahu, sasa anawashwa washwa nini?
 
Ye aliacha madhabahu akafanya anachokitaka..awaache na wenzie wafanye wanachokitaka..akiona wanapwaya aache siasa apande madhabahuni ahubiri kile anachotaka wachungaji wahubiri sababu bado anayo hiyo fursa..kinyume na hapo ni unafiki tu.
 
Kufanya unachotaka ni pamoja na kusema ukweli na kusimamia haki ya jamii pale unapoona haki haitendeki.ila kwako kama mtu kuwaasa viongozi wa dini wakemee maovu na kuwakumbusha watawala umuhimu wa Haki ni unafiki basi utakua ufikiri sawasawa.
 
Back
Top Bottom