Viongozi wa dini acheni kujidhalilisha

HUSSEN KAMBI

Senior Member
Dec 4, 2023
175
212
Nyinyi ni watumishi wa Mungu kwanini mnajidhalilisha kwa wana siasa, mbona wao viongozi wa kisiasa hawa jidhalilishi kwenu?

Kwanini nimesema mnajidhalilisha, kwa wana siasa, hasa wa chama kinachotawala, mnapo ongea maneno yenye kuwafurahisha.

Hata kama mnaongopa, watawa alika ikulu chakula mtalishwa na bahasha mtapewa, nakuwaambia nyinyi ni watu muhimu sana katika taifa, lakini mnapo amua kusema ukweli mambo yanayo wauma hata kama mtasema kweli, watawaita wachochezi na kesy watawafungulia na jera watawapeleka, na wapo baadhi ya viongozi wa dini.

Baada ya kugundua viongozi wa kisiasa wanataka kusifiwa tu hata kama sifa hizo hawana, na wao wameamua kua machawa kazi yao kila siku kutoa sifa tu kwa kiongozi hata kama sifa hizo hana.

Yaani wameacha kazi yao ya utumishi wa Mungu kuamrisha mema na kukataza mabaya, wao wamekua watu wakusifia tu.

Mbona wao viongozi wa kisiasa hawawa shobokei, pamoja mmekua chawa wao lakini mkiwakera tu wanawaita wachochezi, na kesy wanawafungulia, na jera wanawaeka hawajali kama chawa wao au kunguni wao, acheni kujidhalilisha, kwa wana adamu wenzenu.

Ninyi ni watumishi wa Mungu mtumikieni Mungu kama alivyo wateua, fanyeni kazi yake yakuamrisha mema na kukataza maovu acheni unafiki wenu kama vipi amueni moja,kama mwenzenu gwajima, kaacha kumtumikia Mungu.

Sasa hivi anamtumikia shetani, maana huku alipo sasa hili huonekane bora lazima ujitoe ufahamu yai useme embe na embe useme yai ndio utaonekana unafaa
 
Back
Top Bottom