PreGE2025 Peter Madeleka ajiunga na Chama cha ACT Wazalendo

PreGE2025 Peter Madeleka ajiunga na Chama cha ACT Wazalendo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Just because amehama chama haimaanishi urafiki umeisha
Politician or not, madeleka ana every right ya kupambania ndoto yake
Namuonea huruma mtu yeyote mwenye ndoto na ubunge wa CCM

Hivi ni mwanaCCM gani atakubali akose ubunge kisa madeleka ndiye apate

wakati wameshaambiwa wale kwa urefu wa kamba zao

na vitongoji, vijiji, mitaa yote ni ya CCM

Anyways, wacha aendelee kuota mchana, atazinduka akipigwa kitu kizito na maFISIEMU
 
anataka kugombea Tabora mjini...chadema haitshriki, sasa kama ana ndoto za hela nyingi za bure za ubunge lazima ahame. He was in chadema kutafuta fursa na si kupigania haki
Hiki ulichoandika kimetusaidia kuzijuwa rangi halisi za Wanasiasa wengi wa Tanzania.

Peter Serukamba naye anaacha Ukuu wa mkoa anakwenda kugombea ubunge Kigoma na kule atawadanganya anataka kuwatumikia kumbe anataka kutumikia tumbo lake.
 
1. To me hii ndiyo tafsiri sahihi ya madeleka kuhamia ACT.

2. Chadema haitashiriki uchaguzi, na hivyo kuua ndoto ake.

3. Tabora anahisi anaweza kutoboa , aende wapi penye "ka mwanga"....ACT!

4. Unakaa unagonga meza, 200,000 Tsh hela za bwelele/bure zinaingia, why not fight for that position if you see some light ahead

He is right!
 
Hiki ulichoandika kimetusaidia kuzijuwa rangi halisi za Wanasiasa wengi wa Tanzania.

Peter Serukamba naye anaacha Ukuu wa mkoa anakwenda kugombea ubunge Kigoma na kule atawadanganya anataka kuwatumikia kumbe anataka kutumikia tumbo lake.
sure, kule kuna hela za bure, unakaa unagonga meza, 200,000 za kugonga meza zinaingia
 
Alipoanza kutoa maoni tofauti, chadema mitandaoni wakawa wanamtukana matusi ya nguoni. Inasikitisba kuona vijana na mengine mazee kabisa hayajui kujibu hoja, wanatukana
 
Huu ndio muda wa siasa inasemekana Wakili na Polisi mstaafu Peter madeleka amehamia ACT Wazalendo
 
Aiseeee leo ni bandika bandua! Kila sehemu moto! Mzee wa kesi katimkia zake ACT Wazalendo bana, yeye hajataka kwenda kula ubwabwa😂😂

=====

ACT Wazalendo wanafanya mkutano na waandishi wa habari muda huu Makao Makuu ya chama Magomeni, Dar es Salaam Mei 20, 2025


Isihaka Mchinjita - Makamu Mwenyekiti Bara ACT
Mkutano huu umefanyika ukiwa na lengo la kumpokea mwanachama mpya - Peter Madeleka katika chama hicho.


Binadamu angekuwa hana tumbo angekuwa mtu mzuri sana.

Wewe kaa unajidanganya yupo mtu wa kukutetea, kila mtu yulo kwenye shughuli fulani iwe siasa, biashara au taaluma sababu ya pesa.

Hao unaodhani wanakutetea kama wakina Heche wakienda ziara waambie walipiwe hoteli wale bure, walipiwe gest walale bure lakini wasipewe posho hawatakubali kwa sababu mwisho wa ziara wanataka chenji ibaki warudi nayo nyumbani kupelekea watoto. Wakikubali kulipiwa hawatarudi na pesa nyumbani.

Maria Sarungi ansishi Nairobi anafadhili harakati Tanzania unafikiri anafanya bure, kuna wafadhili kishawandikia paper kuomba pesa na kapewa kwa ajili harakati anatumia na zingine anachukua.

Mfano tukio la kuzuiwa Airport kwa wanaharakati wa Kenya Maria atakuwa anefurahi sana maana tayari ni sababu tosha ya kuendelea kuombea pesa kwa wafadhili wao maisha yanaendelea.

Ndio maana kuna watu wanapromote ushoga nchini ila wao hawaukubali kabisa lakini kwa sababu ya pesa,wanapromote ili wapate mkate.
 
Wapiga kura sio.wana twitter X mwambieni. Mzee wa uhujumu uchumi madeleka. Mzee wa kufyatua viza kia kwa watalii
 
Back
Top Bottom