Peter Lijualikali aweka wazi uozo ndani ya CHADEMA

Peter Lijualikali aweka wazi uozo ndani ya CHADEMA

Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mkoani Morogoro kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mheshimiwa Peter Lijuakali ameweka bayana mambo mbalimbali yaliyojicha katika chama juu ya matumizi mbalimbali ya Chama ikiwemo fedha zinazopatikana na kuingia katika Chama kile, Mheshimiwa Peter Lijuakali ameenda mbali zaidi na kueleza kwamba...
Kwa vile ameamua kusema ukweli, hivyo vielelezo siyo sehemu ya ukweli? Si avitoe tu?
 
CAG hajafanya Forensic Accounting kwa kiswahili Ukaguzi Maalum bali alifanya Normal Auditing kuangalia by sampling sasa kwa kuwa kuna wabunge wamelalamika kuna wizi ndiyo hapo TAKUKURU au Polisi wanaingia kufanya Forensic Investigation wakiona inafaa basi wanaweza kumwomba CAG kufanya Forensic Accounting ama la.
Nilikua nataman uingie kingi na umeingia, ishu iko hivi CAG alikagua ruzuku na sio michango ya wabunge, ki-sheria Ile ni kesi ya madai na sio jinai, kwa sababu mbowe anashutumiwa kula michango na sio ruzuku, haina tofauti na mtu aliyekula michango ya harusi.

Cha ajabu Takukuru wanaendaje kukagua michango ya wabunge ambao waliitoa kw ridhaa yao, kunawalakini
 
Nilikua nataman uingie kingi na umeingia, ishu iko hivi CAG alikagua ruzuku na sio michango ya wabunge, ki-sheria Ile ni kesi ya madai na sio jinai, kwa sababu mbowe anashutumiwa kula michango na sio ruzuku, haina tofauti na mtu aliyekula michango ya harusi.

Cha ajabu Takukuru wanaendaje kukagua michango ya wabunge ambao waliitoa kw ridhaa yao, kunawalakini
Labda hujamsikikiza Mh. Lijuakali ametoa siri nyingi sana ikiwemo kukwepa kodi wakati wa kununua gari la chama ambapo kuna mbunge mmoja alitumia tax exemption yake kununua hilo gari then akawapa Chadema hiyo ni jinai tena ni predicate offence ya Money Laundering kama hujui tulia wanaojua wachambue mambo!
 
Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mkoani Morogoro kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mheshimiwa Peter Lijuakali ameweka bayana mambo mbalimbali yaliyojicha katika chama juu ya matumizi mbalimbali ya Chama ikiwemo fedha zinazopatikana na kuingia katika Chama kile, Mheshimiwa Peter Lijuakali ameenda mbali zaidi na kueleza kwamba :-

"Wengine wanasema mbona CAG (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali) hajaona ubadhirifu wa CHADEMA, niwaambie tu kwamba, CAG haingii kwenye vikao vya chama (CHADEMA) na wala hajui tuliambiwa nini,” Peter Lijualikali, Mbunge wa Kilombero.
"CAG anachoangalia ni kile kilichomo kwenye makaratasi, na sisi tunazungumza tulichokubaliana kwenye vikao, kama CAG anakuaga anauliza, hakuja kwenye vikao vya wabunge wakati mwenyekiti anatujaza"

“Halafu watu wengi hawajui. Hivi ni wana CHADEMA wangapi wanajua akaunti mama zote za chama kuwa 'mwamba' ndiyo anayetia saini ikiwemo akaunti ya fedha za ruzuku,”

“Mwamba ni mwenyekiti wa chama na ni mtia saini, na ndiye anayeteua Katibu Mkuu ambaye naye ni mtia saini katika akaunti, halafu mwamba kwa kukaa na katibu mkuu ndiyo wanashauriana kuteua Mkurugenzi wa Fedha ambaye pia ni mtia saini, hesabu za kazi hizi"
“Hakuna waziri ambaye ni mtia saini wa akaunti za wizara, hakuna hata akaunti moja ambayo Rais Dk. John Magufuli na hata marais waliopita wanatia saini. Lakini huku kwetu huku mwamba ndiyo mtia saini na ndio maana watu wanasema ni Saccos"

"Sehemu zote zinazopigwa hela jamaa ndio anasaini na wenzake halafu mzigo unatoka, kwa hiyo sisi, yaani mimi Lijualikali ambaye nilikuwa jela ninachangia hela kwenye chama, nilifungwa jela miezi sita na nimekaa ndani miezi mitatu, kila mwezi nilikuwa nachangia"

Mbunge wa jimbo la Kilombero mkoani Morogoro, Mhe. Peter Lijualikali amesema kwamba, watu wa karibu wa Mwenyekiti wa CHADEMA akiwawemo Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mheshimiwa Peter Msigwa (CHADEMA) na timu yake hawakuwahi kutoa hata Sh 100 hadi leo, na kama wanabisha yuko tayari kumuomba Spika atoe vielelezo kama ataona inafaa.
Mh Lijuakali akijiunga na kikundi cha kusaidia atakuja hapa kusema alilazimishwa kutoa michango yako wakati ni katiba aliyoridhia ndiyo inaelekeza kutoa michango.

Haya akajilimie miwa ndio kama hatachangia chama cha wakulima wa miwa ili awe mwanachama
 
Kwa upuuzi huu ccm itatawala milele.

chama kimeanza kuaminika wanaleta ujinga et unagoma kwenda bungeni kuogopa corona halafu baada siku 14 unarudi mule mule,,pumbavuuu nishahama bora nikae bila chama

Umeelewa uzi?
 
Chadema kwisha Habari yake

Tunasubiri October tuwafutilie mbali
Kwa hiyo ikiisha wewe utapata faida gani? Au hujui kuwa Zanzibar ipo CCM peke yake)hakuna upinzani,je matatizo ya Wazanzibar yameisha! Je Zanzibar imebadilika na kuwa ulaya?kaa kimya, Subili mama aje akupe ugali.
 
Mh Lijuakali akijiunga na kikundi cha kusaidia atakuja hapa kusema alilazimishwa kutoa michango yako wakati ni katiba aliyoridhia ndiyo inaelekeza kutoa michango.

Haya akajilimie miwa ndio kama hatachangia chama cha wakulima wa miwa ili awe mwanachama
Ndo hapo michango ulirudhia kuchanga leo unakuja kulalamika,
 
Labda hujamsikikiza Mh. Lijuakali ametoa siri nyingi sana ikiwemo kukwepa kodi wakati wa kununua gari la chama ambapo kuna mbunge mmoja alitumia tax exemption yake kununua hilo gari then akawapa Chadema hiyo ni jinai tena ni predicate offence ya Money Laundering kama hujui tulia wanaojua wachambue mambo!
Sheria ya kodi Ina loop-hole nyingi ndo mchezo wanaofanya wafanyabiashara dunia nzima, ni ngumu sana kumtia hatiani mtu aliyetumia loop-hole kwenye sheria za Kodi kukwepa Kodi.

CAG aliwakagua anaangalia risiti zote na chadema wakajibu quarrels zote za CAG ndo maana wanapewa hati safi

Kuna mwaka Amazon alilipa zero tax watu waliishia kumlalamikia bezos, lakin wanalindwa kumtia hatiani sababu alicheza na loop-hole zilizopo kwenye sheria ya kodi ya marekani. Kwa mtu mwenye utimamu wa akili hawez msupport lijualikali anaongea international pumba point, unless awe mshabiki wa ccm
 
Kwa lipi? Chadema iingekwisha Zitto alipotolewa, Chadema kingekwisha Dr Slaa alipotoka. Hizi tuhuma za hawa jamaa mbona ni za siku nyingi sana. Cdm is here to stay.!
Eti CDM isife baada ya kutoka Dr. Slaa leo ife kwa upuuzi wa huyu Lijualikali anayejulikana Ifakara tu.
 
Waliohama CDM october ikifika ndio watajua walikuwa hawajui...
 
Mwamba anapiga mihamara
Misukule inatetea hata kibwetele wakati anawapanga kuna watu kama lijua lijali walishtuka mbaka leo bado wako hai
hawa Misukule wakija kugundua ukweli watakufa na presha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haaaaaaaaaaaa .Bwana mdogo Lijua Likali umeteleza . Huwezi kuaminika tena una maanisha hata ukiwa waziri siku moja utatoa siri za Baraza la mawaziri. pole sanaaaa ndo umekwisha hivyo
 
Wanasiasa bhana. So wakati yupo kule alikuwa anaunga mkono bila kutwambia. Now katoka, ndio anaweka vitu hadharani.

Tutajuaje kama ni kweli anayoyasema, kwambia sio fitina na uzandiki kwavile hayupo nao tena?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Hana kifua cha kiume Kama za mwita, utadhani mwanamke aliyeaacha haya ilitakiwa aseme kabla ajafukuzwa ndio angeeleweka.
 
Back
Top Bottom