CHIPESI NAMISUKU
Member
- Oct 7, 2019
- 51
- 157
Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mkoani Morogoro kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mheshimiwa Peter Lijuakali ameweka bayana mambo mbalimbali yaliyojificha katika chama juu ya matumizi mbalimbali ya Chama ikiwemo fedha zinazopatikana na kuingia katika Chama kile, Mheshimiwa Peter Lijuakali ameenda mbali zaidi na kueleza kwamba:-
"Wengine wanasema mbona CAG (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali) hajaona ubadhirifu wa CHADEMA, niwaambie tu kwamba, CAG haingii kwenye vikao vya chama (CHADEMA) na wala hajui tuliambiwa nini,” Peter Lijualikali, Mbunge wa Kilombero.
"CAG anachoangalia ni kile kilichomo kwenye makaratasi, na sisi tunazungumza tulichokubaliana kwenye vikao, kama CAG anakuaga anauliza, hakuja kwenye vikao vya wabunge wakati mwenyekiti anatujaza"
“Halafu watu wengi hawajui. Hivi ni wana CHADEMA wangapi wanajua akaunti mama zote za chama kuwa 'mwamba' ndiyo anayetia saini ikiwemo akaunti ya fedha za ruzuku,”
“Mwamba ni mwenyekiti wa chama na ni mtia saini, na ndiye anayeteua Katibu Mkuu ambaye naye ni mtia saini katika akaunti, halafu mwamba kwa kukaa na katibu mkuu ndiyo wanashauriana kuteua Mkurugenzi wa Fedha ambaye pia ni mtia saini, hesabu za kazi hizi"
“Hakuna waziri ambaye ni mtia saini wa akaunti za wizara, hakuna hata akaunti moja ambayo Rais Dk. John Magufuli na hata marais waliopita wanatia saini. Lakini huku kwetu huku mwamba ndiyo mtia saini na ndio maana watu wanasema ni Saccos"
"Sehemu zote zinazopigwa hela jamaa ndio anasaini na wenzake halafu mzigo unatoka, kwa hiyo sisi, yaani mimi Lijualikali ambaye nilikuwa jela ninachangia hela kwenye chama, nilifungwa jela miezi sita na nimekaa ndani miezi mitatu, kila mwezi nilikuwa nachangia"
Mbunge wa jimbo la Kilombero mkoani Morogoro, Mhe. Peter Lijualikali amesema kwamba, watu wa karibu wa Mwenyekiti wa CHADEMA akiwawemo Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mheshimiwa Peter Msigwa (CHADEMA) na timu yake hawakuwahi kutoa hata Sh 100 hadi leo, na kama wanabisha yuko tayari kumuomba Spika atoe vielelezo kama ataona inafaa.