Pete katika ndoa

kamanda, ni taasisi nzima imeporomoka maadili yake bro.

Sidhani kama kuna manusura tena baada ya haya yanayotokea.
Chombo kishakata nanga, kinafuata upepo tu. Liwalo na liwe,
Kwenye nchi za kimagharibi mambo ndio yeshaharibika kabisaa,...afadhalia ya
Africa na barani Asia kidogo (baadhi ya nchi)

we acha tu, i dont know why lakini kuna ka upepo kamepita imefikia kila kitu tunafanya kama fasheni... siku hizi hata kuwa na mpango wa kando ni sunna, inauma sana uchungu lakini kwa wengi tunaoishi Dar tunayaona, sijui mikoani au nje hali ikoje lakini kwa dar ni balaa

Kuna siku (kama alivyotoa mfano chauro) nilikuta dada ana peke kama nusu kilo hivi ya ndoa na nyingine ya engagement... lakini alivyokua amekaa chobingo na jinsi alivyokua amekula chicha na mambo aliyokua anayafanya huwezi kuamini

I think there is a need for a social campaign kuhamasisha jamii kuamka na hali iliyopo..............


Kwenye sector ya Recreation, hospitality and tourism vituko vinavyoonekana
humo unaweza lia machozi. Lakini bila kwenda mbali, na washkaji ambao ni Taxi Drivers
hapo mjini Dar,...aisee story zao kuhusiana na janga hili, ...unaweza angua machozi.
Unaukumbuka ule wimbo ♫ "wote ni abiria wangu ee, mimi ni taxi Driver!" ♫...

nimekumbuka kibwagizo hiko pekee, sikumbuki bendi gani miaka ile ya 80s...
 

Sidhani kama kuna manusura tena baada ya haya yanayotokea.
Chombo kishakata nanga, kinafuata upepo tu. Liwalo na liwe,
Kwenye nchi za kimagharibi mambo ndio yeshaharibika kabisaa,...afadhalia ya
Africa na barani Asia kidogo (baadhi ya nchi)



Kwenye sector ya Recreation, hospitality and tourism vituko vinavyoonekana
humo unaweza lia machozi. Lakini bila kwenda mbali, na washkaji ambao ni Taxi Drivers
hapo mjini Dar,...aisee story zao kuhusiana na janga hili, ...unaweza angua machozi.
Unaukumbuka ule wimbo ♫ "wote ni abiria wangu ee, mimi ni taxi Driver!" ♫..
nimekumbuka kibwagizo hiko pekee, sikumbuki bendi gani miaka ile ya 80s...


Alikua maalim gurumu, maalim kinyasi na sikinde

Ukitaka kufanya research fanya na Taxi drivers (unganisha vibajaji humohumo), madereva wa serikali na mashirika mengine na wafanyakazi wa mahoteli/guest house

Ni balaa
 
Maana yake umeoa/umeolewa. Huna uhuru wa kufanya unachotaka bila kushirikisha upande wa pili.
 
MTM yaani umeiweka sawa kabisa hali halisi, Kamanda hongera sana I dont have anything to add to your posts.
 
with_this_ring2.jpg
...pamoja na tafsiri zote, kuvishwa PETE na umpendae ni the best feeling ever!

Mbu hili ni kweli .........unapoivaa ya yule ambaye unamfeel kiukweli. Sasa najiuliza kama huko mbele ya safari mambo yanageuka yanakuwa mambo......kuna mawili: Unawezajikuta bado unavaa kwa vile tu wewe moyoni mwako bado unampenda, despite of everything! So pete yake ni kama inakufariji
Lakini pia unawezajikuta unashindwa kuendelea kuivaa kwa sababu
1. Moyo umeingia chuki juu yake na hutamani tena kumkubuka (Ishu ni kama mna kikumbushio kama mtoto- hii ni mtihani kidogo na nadhani ni thread inayojitegemea!!
2. Ukaivua kwa kuwa kuivaa kunaikumbushia machungu na wewe bado unampenda na huwezi m'comisha' back.......inakubidi tu uyalazimishe maisha yasonge.
 

...Kiongozi, are you proud to wear your ring?...ni swali la kizushi tu.
Unajiskiaje ukiwa umeivaa...

Unajua kuna hisia fulani hunipata kila nikivaa ring yangu, hebu nisikie na wenzangu mnasemaje.

Duh hapo kwenye Blue hapo.........mbona unatutisha?? Kwa hiyo kama mtu anakuwa na hisia kama zako halafu ukimkuta kavaa pete unamtafsirije??
 
Duh hapo kwenye Blue hapo.........mbona unatutisha?? Kwa hiyo kama mtu anakuwa na hisia kama zako halafu ukimkuta kavaa pete unamtafsirije??

...Lohhh, Mwj1 samahani nimechelewa kukujibu...nilikuwa kibaruani nikichangia pato la taifa.
Well, hisia zangu kwa pete ile niloamua kuivua haikuwa zaidi ya kujifeel betrayed!...

Yaani kila nikiivaa, maneno yananirudia yale ya "...ni ishara ya uaminifu wangu kwako!"...wakati hapakuwa na
uaminifu huo...nikajiamulia hii pete inanizibia mzunguko wa damu tu kidoleni.

Kama wenzangu na mie wameamua kufa na tai shingoni japo pete zinawabana haya...'hiari yashinda utumwa!
 
...hhahha,...Ikunda usishtuke bana, ndio hali ya dunia na mapito yake,
ila hapo kwenye ubuluu, umenichekesha sana...wengi hujifanya wameisahau juu ya dressing table
Halafu upo kazini unashtukia simu/sms ..."umeiachia nini pete nyumbani?"---Problem Solved.

Dawa tosha hiyo saa ingine.

umeonaaaa lol, wakati mwingine kujifanya hamnazo kunasaidia.
 
Ila mabinti wa siku hizi ni balaa. Enzi za ujana wangu sikuwahi kumpa nafasi mtu mwenye pete aniambie kuwa ananipenda. Kwanza nilikuwa nahoji mpaka jamaa anaona amekutana na padri alomfungisha ndoa. I thank God sijawahi tembea na mume wa mtu mpaka naolewa na sijawahi hata kumtamani. Nikiona pete tu hata uwe handsome vipi nilikuwa nakuona kama kaka yangu. Siku hizi wame za watu ni fashion.


hapo nilipopigia mstari kwa maana hiyo sasa ivi unaweza/unatoka na mume wa mtu sababu nifasheni?
 
Back
Top Bottom