Pete katika ndoa

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,845
207317_10150138608128235_186498368234_6527991_1645896_n.jpg

...hiyo pete uliyoivaa ("ya ndoa") maana yake nini?
:(
 
ina maana kwamba upendo wenu hauna mwisho.Mtapendana Forever and ever, endlessness love na kwamba love lenu halitavunjika.
Lakini cha ajabu watu wana ndoa na bado kucheat kama kawaida, tena mtu anaamua kuvua kabisa hiyo pete, hasa wanaume, ukichunguza asilimia kubwa ya wanaume hawapendi kuvaa pete za ndoa ukilinganisha na wamama. Utamkuta mama kabebesha pete zote engagement na wedding rings.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa wanandoa inamaanisha kuwa ninyi ni wenzi halali kwa kipindi chote mtakapokuwa pamoja. Uhalali huu hutakiwa kwenda sambamba na kiapo cha uaminifu mlichokitoa na kuhakikisha mnakifuata.

Kwa wanajamii- Ina maanisha kuwa fulani (mwenye pete) hayuko available ni mali ya mtu tayari na hivyo vishanshuda na mangurumbene wakae mbali na kifaa hicho.

Kwa siku hizi inamaanisha : Hata mie nshatoa nuksi (kwa wanawake) na wanaume inaonyesha uwezo alionao wa kutunza familia (hata kama hatunzi)
 
...kwa maana hiyo, 'inakuwa rahisi' kujirusha nje ya ndoa iwapo utaivua hiyo pete?
 
Pete ya ndoa ni symbol inayosymbilize muungano wa watu wawili walioamua kuishi kwa kupendana kwa wakati wote wa shida na raha.

NYONGEZA:
Kwa kuongezea tendo la kuvalisha pete ya ndoa, hufanyika kidole cha pili kutoka kidole kidogo cha mkono wa kushoto kwa sababu maalumu ya KIHISTORIA.

Ugiriki ya kale zama za akina SOCRATE, utafiti ulifanyika na kuonekana kuwa kidole hicho kitumike kuvalisha pete hiyo ya ndoa kwani ndicho ambacho kina mshipa wa damu unaoelekea moja kwa moja kwenye moyo.

Hivyo chochote kinachosemwa wakati wa kuvalisha pete hiyo kinakuwa transmitted direct to the heart of mwenza wako.

Hicho ndicho chanzo cha kuvaa pete ya ndoa kidole hicho na si kingine.
 
...kwahiyo mamsap akiiacha pete nyumbani ujue ndoa ipo mashakani?
 
Kwa wanandoa inamaanisha kuwa ninyi ni wenzi halali kwa kipindi chote mtakapokuwa pamoja. Uhalali huu hutakiwa kwenda sambamba na kiapo cha uaminifu mlichokitoa na kuhakikisha mnakifuata.

Kwa wanajamii- Ina maanisha kuwa fulani (mwenye pete) hayuko available ni mali ya mtu tayari na hivyo vishanshuda na mangurumbene wakae mbali na kifaa hicho.

Kwa siku hizi inamaanisha : Hata mie nshatoa nuksi (kwa wanawake) na wanaume inaonyesha uwezo alionao wa kutunza familia (hata kama hatunzi)

Duh!

The world is revolving jamani.

Kwa kweli ukizubaa na huu ulimwengu utajikuta train imekuacha Kigoma!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
ina maana kwamba upendo wenu hauna mwisho.Mtapendana Forever and ever, endlessness love na kwamba love lenu halitavunjika.
Lakini cha ajabu watu wana ndoa na bado kucheat kama kawaida, tena mtu anaamua kuvua kabisa hiyo pete, hasa wanaume, ukichunguza asilimia kubwa ya wanaume hawapendi kuvaa pete za ndoa ukilinganisha na wamama. Utamkuta mama kabebesha pete zote engagement na wedding rings.

Pretty inaonekana yamekuku Dada ,maelezoyako yamekuwa kama ya mtu asifie mvuwa iliyomneshea. Hili la kucheat limekukaa rohoni ,niafadhali unalizungumzia ili uweze ku (get over it )it will take time but you get there. kusaidiana ndio huku .
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
nyemba haivai ndio nini tena jamani ?makubwa haya!!!.
Babylon
Penny kaandika Njemba akimaanisha mwanaume/mume siyo nyemba.. Yaani kama mamsap havai pete ya ndoa ujue na njemba hana na yeye kabisaa.

Mbu!
Swali: Je kwa wasabato imekaaje? Maana katika suala la kufunga ndoa hamna kuvalishana pete kanisani labda baadae kwa wakati wenu mvalishane maana ni kama fasheni. Ina maana usipokuwa na pete wakati umeoa/kuolewa unaonekanaje kwenye jamii?
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Hali inavyokwenda humu ndani ya JFkuna uwezekano wa wanachama wake kuazisha Blind date siku moja kwa kutumia vijineno vya ujanja ujanja
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Nadhani ndoa kati wawili ni maafikiano kati ya watu wawili kuwa
wanapendana,
wataheshimana,
watajitahidi kwa pamoja kuboresha maisha yao na kuwa kila mmoja atakuwa nguzo ya mwenzake.

Hayo mengine kama pete, vizawadi, sherehe kemkem ni hali ya binadamu kupenda kuweka alama yake. kama wanyama wanavyo kojoa kuwaonya wengine.

La muhimu ni kwa binadamu huwa huru kufanya anachotaka, hata ukamvisha pete ya nyota, ikiwa kati yenu hamna hayo manne yaliyoko hapo juu basi ndoa yenu haiendi popote.
 
Babylon
Penny kaandika Njemba akimaanisha mwanaume/mume siyo nyemba.. Yaani kama mamsap havai pete ya ndoa ujue na njemba hana na yeye kabisaa.

Mbu!
Swali: Je kwa wasabato imekaaje? Maana katika suala la kufunga ndoa hamna kuvalishana pete kanisani labda baadae kwa wakati wenu mvalishane maana ni kama fasheni. Ina maana usipokuwa na pete wakati umeoa/kuolewa unaonekanaje kwenye jamii?

...sijui! eti wasabato mnasemaje???
 
Ndo maanake...ukikuta mamsap havai ujue hata njemba haivai.

Some blast from the past! Penny umepotelea wapi? Au na wewe umeunga tela la kuwa na majina kem kem kama ilivyo ada ya wana JF siku hizi?
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Back
Top Bottom