Pesa mkononi mwako kwa njia ya mtandao

Mmakedonia

Member
Sep 1, 2021
21
12
Mfumo ambao dunia imejiwekea wa kumtafsiri mtu na mtu au hata taifa na taifa kupitia vipato vyao (pesa) umekuwa ukiweka maswali mengi sana kichwani kwangu, moja kati ya swali ambalo mpaka leo bado sijapata majibu ni lile lililo kwa watu wengi kwamba "Hela zinatengenezwa wapi? Na ni kozi gani ambayo mtu anasomea ili akatengeneze ela??"

Mtu mmoja pia aliniuliza swali ambalo kiukweli liliniduwaza, kwamba "Ni nani anayetoa ruhusa ya kutoa kopi pesa?

Yaani kama tunalalamika pesa imekua ngumu kwanini serikali isitoe tu kopi ela kadhaa halafu zikaingizwa kwenye mfumo watu wakazipata??" Lakini nimekuja kugundua kuwa ili dunia iendelee na ijengeke mambo hayatakiwi kuwa mepesi kiasi hicho.

Kama pesa zikigawiwa kwa watu, basi pesa itakosa uthamani wake na haitaweza tena kuitwa pesa kwani hakuna mtu atakayeweza kumuamrisha mtu mwingine kupitia pesa.

Sipo apa kwa ajili ya kuelimisha watu namna gani ya kupata pesa bali naomba kufungua PLATFORM hii kwa ajili ya watu kuweza KUPATA PESA ONLINE, najua JF ni forum aambayo ina watu wengi wa aina tofauti tofauti hivyo naomba kufungua uzi huu kwa ajili ya wale wote wenye uelewa wa namna ya kupata pesa online, watufundishe ili na watu wengine tuweze kunufaika🙏🙏

NB: Kwa mtu utakayetaka kujihusisha na biashara yoyote ya online utakayoelezwa na mtu tafadhari kuwa makini kwanza kutafakari ili kuepuka matapeli

Karibuni wote mtujuze kuhusu njia za kupata pesa online.
 
Back
Top Bottom