Kwanini fikra zetu kuhusu pesa ni hasi?

Kwanini fikra zetu kuhusu pesa ni hasi?

Paul Da Ud

New Member
Joined
Feb 12, 2022
Posts
2
Reaction score
2
1000108564.png


Kama ilivyo picha ya huyo mwanamke hapo juu, ndo zilivyo fikra za watu wengi linapokuja swala zima la kuwa tajiri.

Ukisikia neno tajiri nini kinakuja kichwani kwako haraka?
Kila Muda neno tajiri linapotajwa watu hufikiria kuhusu mtu mwenye mavazi ya kisasa, anaye miliki saa ya milioni kadhaa, anayekaa kwenye apartment flani hivi juu ghorofa, wakati huo Gari la milioni Mia tano limepaki hapo nje. Hizo fikra sio sahihi pekee bali ni hatari kwa maisha. Fikiria mtu anaye Pambana Kila kukicha, Ana amka mapema na anachelewa kulala, yote hayo anafanya kwa sababu ya ndoto ya kununua Gari ya milioni Mia tatu, kulala kwenye hotel yenye hadhi ya nyota tano au hata kutoka kimapenzi na wasanii na watu maarufu. Ndo maana nasema jinsi Jamii inavyofikiri kuhusu pesa ni hatari kwa maisha.

TUNZA PESA, WEKA BAJETI NA ISHI CHINI YA KIPATO.
Hizo kanuni tatu ndio msingi wa Kuwa tajiri, kiufupi kiwango cha mshahara au mapato unayo yapata kina uhusiano mdogo Sana na wewe kuwa tajiri au maskini. Mike Tyson Alikuwa anaingiza hela nyingi Sana kupitia mchezo wa ngumi lakini alikuja kuishia kwenye madeni.

Wengi tumetoka katika Familia ambazo hazikuwa na utaratibu wa bajeti kwenye matumizi. Hata ile ambayo watu wengi huita bajeti sio bajeti, Huwa ni Orodha tu ya Mahitaji ya kwenda kununua ili asisahau vitu vya muhimu. Bajeti inabidi iwe kwenye matumizi yote, sio kupanga bajeti ya chakula tu, kwenye nguo na vitu vingine eti una acha.

Utajiri Unajengwa na muda, kutunza pesa na kuishi chini ya kipato. Tusitake kufuata maisha ya watu tunaofikiri ni matajiri. Mtu kununua Gari la milioni Mia moja haitupi jibu la kwamba Ana milioni Mia au utajiri wa thamani hiyo, Ila Inatupa jibu kwamba huyo mtu alikuwa na milioni Mia hapo mwanzo bila kujali kama sahivi anazo au raa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom