Personal Plea Kwa Rais Magufuli: Kama ameweza kuwasamehe wabakaji, wauaji, mafisadi, wahujumu, anaweza pia kumsamehe Eric Kabendera, amzike mama yake

Uliandika kujikosha tu lakini nasisitiza lazima ulipe gharama za kumuuza Erick. Juzi uliingia 18 pale Mbeya ila wakakuonea huruma. Ya Time is up for a catch. Pole. Malipo ni hapa hapa duniani.
Mimi najihesabu kama muumini number 1 wa karma humu JF, hivyo kama ni kweli ni mimi ndie niliyemsabishia madhila yale, then for sure, karma yangu ipo and it will act on me!.

Lakini kama mimi sihusiki, you will see me shining and smilling as ever.

Ni kweli juzi kati nilikuwa Mbeya na nyie mashetani mkaniwekea kauzibe nisimfikie, nakuhakikishia kuna siku nitamfikia, your days to keep on doing evil, are numbered, na siku zenu zikifika, baadhi yenu mtafanywa kuni kwa maovu mnaowatenda wana wa Adamu wasio na hatia hapa duniani!.

Nilidhani baada ya lile tukio, you'll have learned your lessons kumbe...
watch me... kuna watu ni watu wadogo sana kama sisimizi tuu, lakini don't play them... kama naniliu, pamoja na ukubwa wote, ulinzi wote na powers zote, na uwezo wote, na watu wote, na mambo yote na bado amenaniliu... utakuwa wewe kinyangarika tuu...?!. Usicheze kabisa na sisimizi wengine!, ni hatari!, sisimizi anaua tembo!, akiingia kwenye ule mkonga, tembo anajibamiza kwenye miti mpaka anakufa!, kisha sisimizi huyoo anatoka zake na kuendelea kujivinjari!.

P
 
Mimi najihesabu kama muumini number 1 wa karma humu JF, hivyo kama ni kweli ni mimi ndie niliyemsabishia madhila yale, then, then for sure, karma yangu ipo and it will act on me!.

Lakini kama mimi sihusiki, you will see me shining and smilling as ever.

Ni kweli juzi kati nilikuwa Mbeya na nyie mashetani mkaniwekea kauzibe nisimfikie, nakuhakikishia nitamfikia na siku zenu zikifika, baadhi yenu mtafanywa kuni kwa maovu mnaowatenda wana wa Adamu wasio na hatia hapa duniani. Nilidhani baada ya lile tukio, you'll have learned your lessons kumbe... watch me... kuna watu ni watu wadogo sana kama sisimizi tuu, lakini don't play them... kama naniliu, pamoja na yote na bado amenaniliu... utakuwa wewe kinyangarika...!. Usicheze kabisa na sisimizi, anaua tembo, akiingia Kwenye ule mkonga, tembo anajibamiza kwenye miti mpaka anakufa!.
P
Hapa umekanyaga moto, next time hutoboi. Utajua hujui.
 
Hapa umekanyaga moto, next time hutoboi. Utajua hujui.
Kwa vile sisi wote hapa ni wasafiri tuu, anayeamua nani atotoboa na nani hatoboi sio wewe, then you just can't say for sure nani atatoboa na nani hatoboi!, kama nyie mashetani mlimiminia zile pyu pyu 36 na bado mtu aka survive what do you expect
?.
P
 
Kwa vile sisi wote hapa ni wasafiri tuu, anayeamua nani atotoboa na nani hatoboi sio wewe, then you just can't say for sure nani atatoboa na nani hatoboi!, kama nyie mashetani mlimiminia zile pyu pyu 36 na bado mtu aka survive what do you expect
?.
P
Nishakuhesabia. Subiri hapo hapo
 
Wanabodi
Tangu kukamatwa kwa Mwandishi wa habari za kiuchunguzi Eric Kabendera, na kukamatwa kule kukahushishwa na makala zake, na kwa vile ni mimi niliyekuwa natafsiri makala za majarida ya nje na kuzileta humu jf, hivyo nikatuhumiwa kuwa ni makala za jf ndio zimemchongea Eric Kabendera kukamatwa, sijawahi kujibu chochote kwasababu Eric Kabendera hajakamatwa kwa ajili ya makala zake au kazi ya kalamu yake , bali ameshitakiwa kwa makosa mengine na sio makosa ya kiuandishi.

Lakini leo baada ya kupokea taarifa hii

Shocked!.
Kama ni kweli Eric Kabendera anashikiliwa kwa sababu ya kalamu yake hivyo hayo mengine yote ni kisingizio tuu, na yeye ndiye alikuwa tegemeo la mama yake na mama yake amefariki baada ya kukosa huduma na usongo wa mawazo wa kukamatwa kwa mwanaye, na hatimaye huyu mama amekufa, then usually karma ya kifo, hulipizwa kwa kifo!. Hivyo karma ya kifo cha huyu mama, isipokuwa reversed, then itakuwa ni janga kubwa au italeta majanga makubwa na haina mfano, na inaweza kula kichwa au vichwa vya wahusika regardless hao wahusika ni kina nani!.

Naandika kwa kutuma ombi kwa rais Magufuli, kama akiingiwa na huruma na kifo cha huyu mama, na kama akiamua kumsamehe Eric Kabendera na kumwachia huru, anaweza ku reverse the impending karma, hii itapunguza tuu makali ya karma ya kifo cha huyu mama, ambaye kabla ya kifo chake, alimlilia Magufuli.


Kilio kama hiki cha huyu mama kumlilia mwanae na kumuombea msamaha, is not a small thing, kama kuna watu wa karibu na JPM wanaojua karma ni nini, wamfikishie kilio hiki, maana if anything happens to huyu mama kutokana na kukamatwa kwa mwanae, the consequences would be bad kwasababu karma haijui nani ni nani, au labda huyu ni rais, when karma hits back, it just hits!.

Kama rais Magufuli ameweza kuwasamehe watu waliokutwa na hatia ya kubaka na kuthibitishwa na mahakama na wakahukumiwa vifungo na akawasamehe, kuna watu waliokutwa na hatia ya kuua, wakathibitishwa na mahakama wakahukumiwa vifungo lakini rais Magufuli akawasamehe, atashindwaje kumsamehe Kabendera?.

Kama rais Magufuli ameweza kuwasamehe watuhumiwa wa ufisadi, uhujumu na utakatishaji fedha, na sasa hivi tunavyo zungumza tuko nao huru huku mitaani, then rais Magufuli, ikimwingia huruma kuhusu Eric Kabendera, Rais Magufuli akiamua, anaweza!.

Mimi na Eric Kabendera
Nimetokea kumfahamu Eric Kabendera miaka mingi nyuma kama mmoja wa waandishi mahiri kabisa kutokea hapa nyumbani Tanzania.

Ili mtu kuwa mwandishi mahiri, sio suala tuu la kujua kusoma na kuandika, bali unahitaji kuwa na brain yenye intelligence fulani ambayo kiukweli hapa Tanzania tuna waandishi wachache wenye intelligence ya kiwango cha Eric Kabendera, na mimi niko very proud kusema kuwa niliingia fani ya uandishi baada ya kupasi vizuri masomo yangu shule ya sekondari ya Tambaza na Ilboru, ndipo nikasomea uandishi wa habari na hata baada ya kuwa mwandishi wa habari bado nilijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kusomea sheria LL.B na kuhitimu with honours, wale wanaijua sheria ya UDSM halafu ukasikia mtu ametoka with honours, mtaelewa, lengo sio kutambia honours ya sheria, bali kuwajulisha kuwa kuna watu tumeamua kuwa waandishi wa habari sio kwasababu ni vilaza bali kwa upenzi wa fani hii, hivyo Eric Kabendera ni miongoni mwa waandishi vichwa vya ukweli.

Kuna siku mimi nilikuwa moderator wa panel ya mjadala kuhusu "freedom of expression in Tanzania ya sasa"


Kuna maneno mazito sana Eric Kabendera aliyaongea kuhusu Freedom of expression,

View attachment 1310614
Kwenye picha hapo, mimi ndio moderator wa huo mjadala wa Kwanza Kulia ni Eric Kabendera.

Tuhuma za Kumchongea Eric Kabendera
Kwanza naomba kukiri kuwa ni kweli mimi ndiye nilikuwa naleta makala za majarida mbalimbali ya nje yanasema nini kuhusu Tanzania humu jf. Wakati naleta makala hizo, kwanza sikuwahi kufahamu waandishi wake, wala hadi sasa ninapoandika hapo sina uhakika waandishi wa makala hizo ni kina nani, hivyo hakuna any direct linkage ya makala zangu na kukamatwa kwa Eric Kabendera, hivyo nawaomba sana wazushaji wa humu msinizushie. Ila kama ni kweli Erick amekamatwa kwa sababu ya kazi ya kalamu yake, na kama mimi nisinge tafsiri kwa Kiswahili, viongozi wetu vilaza wa kizungu wasinge jua, then na mimi I have my karma payback to pay, for my role.

Msamaha kwa Eric Kabendera, ninao muombea hapa, is purely on Humanitarian Grounds and not on criminal liabilities.
Nimejitokeza kumuombea Eric Kabendera asamehewe on Humanitarian grounds kufuatia kilio cha Mama yake kumuombea msamaha mwanae, hadi huyu mama amekufa na kinyongo, hivyo nimeguswa na kuumizwa na kilichomtokea Eric Kabendera kama mwandishi mwenzangu hivyo ombi hili kwa rais Magufuli ni kumsamehe tuu kama alivyo wasamehe hao wengine.

Why Kabendera and What's So Special About Him.
Kama nilivyoeleza hapo juu mimi nimesoma sheria hivyo nafahamu taratibu zote za mashitaka ya kijinai, mamlaka ya rais ni yapi kisheria na mwenye mamlaka ya kufanya kitu ni DPP, lakini maombi haya nayatuma kwa rais Magufuli kwa sababu fulani.
Japo kuna mahabusu wengi na mashitaka mengi ila issue ya Eric Kabendera tangu kukanatwa kwake, taarifa za polisi kujikanganya mara ahojiwe kuhusu uraia na kisha ndipo yakaibuka hayo mashitaka kunaleta mashaka fulani kwa sisi waandishi critical kwa sababu ambazo naomba nisiziseme hapa ila naamini kwa wajuzi wa hizi mambo wanazielewa na wana nielewa.

Hoja za Kisheria za Eric Kabendera Kuruhusiwa Kumzika Mama Yake


Namalizia kwa kusisitiza karma is real na haina mswalie Mtume.
Natoa Pole sana Eric Kabendera
Mungu akufariji na Mungu akupiganie
Na kumuomba rais wetu Magufuli aguswe na madhila anayopitia huyu mwandishi wa habari mwenzetu Eric Kabendera.

Nawatakia Mwaka Mpya Mwema.

Paskali.
Rejea.
Kwa faida kwa wasio nijua, hii sio mara yangu ya kwanza kumuombea msamaha mhalifu au mahamubusu, nimewaombea msamaha wengi kwenye nyuzi hizi
Kifo Cha Kanumba: Ni Uzembe Tuu? Sio Lulu!

Political Capitalization: Kufuatia Kupendwa na Wengi na Kumhurumia, Jee Tumuombee Msamaha wa Rais, ili Aachiwe Huru?.

Hukumu ya Lulu Gerezani Imesaidia Wengi, Imesaidia Mengi!, Babu Seya Nje, TV Hadi Magerezani, Mazuri Mengi Zaidi Yaja!.

Mhe.Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!.

Karma imefanya kazi yake Tena Kwa wakati.

Mungu wa mbinguni ni Fundi haswa, Ibilisi kwisha habari yake.
 
Back
Top Bottom