BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,377
- 8,120
Kupitia Twitter mwandishi wa habari mkongwe Eric Kabendera amesema ameitwa kuwasilisha vielelezo vyake baada ya kutishiwa na aliyekuwa DPP wa Serikali Dr. Biswalo Mganga
Binafsi nimeombwa kuwasilisha maelezo ya maandishi kwa mamlaka husika kuhusu vitisho alivyovitoa Ndugu Biswalo dhidi yangu mara kwa mara baada kuachiwa huru na nimefanya hivyo.
Si mara ya kwanza zoezi kama hili kufanyika; Rais Mwinyi aliunda tume ya kupitia upya kesi zote ya uhujumu uchumi alizoziendesha Sokoine baada ya kuingia madarakani na kuna watu walirudishiwa mali zao.
Tuhuma dhidi ya Mwendazake kuanzisha na kuendesha genge la kihalifu nje ya mfumo wa serikali na kutoa maelekezo kwa genge hili kuwaua viongozi wa vyama vya upinzani, CCM na viongozi wakuu wastaafu ambao wangekuwa kikwazo kwake kutawala milele zichunguzwe pia.
Kuna mfanyabiashara maarufu alipitia mateso makali kwa kipindi cha miaka minne, ikiwemo kubinywa korodani, akilazimishwa aseme uongo kuwa alitoa dola milioni 100 kwa Rais Kikwete. Mwendazake alitaka kutumia ushahidi huo kumkamata Kikwete. Ni lazima atendewe haki.
Wale mliouza mali zenu kupata pesa za kuhonga kusaidia plea bargain zenu zikubaliwe mjitokeze kutoa ushahidi. Wafanyabiashara mliopelekwa ofisi maarufu ya serikali, mkatishwa kwa mitutu ya bunduki wakati Mwendazake akiangalia kupitia CCTV, mkalazimishwa kutoa pesa mjitokeze.
Pia soma: Erick Kabendera: Mwendazake aliendesha genge la wahuni na alikusudia kumkamata Rais Mstaafu Kikwete