Personal Plea Kwa Rais Magufuli: Kama ameweza kuwasamehe wabakaji, wauaji, mafisadi, wahujumu, anaweza pia kumsamehe Eric Kabendera, amzike mama yake

Mkuu mayala, wakati unasoma pale udsm sheria kama sikosei na mm nlikuwa undergraduate na ulikaa mabibo hostel block F. Unaijua sheria vizuuriiii. Rais haingilii uhuru wa mahakama kwa kusamehe mtu ambaye bado kesi yake haijamalizika. Huwa anaroa msamaha kwa wafungwa. Acha kibendera apate haki yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla,

Kabendera yu mahabusu. Hivi rais anayo mamlaka ya kusamehe mahabusu?

Kukanganyika huko kunakuja kwa sababu ya kutozingatia sheria wala Katiba. Kukomoana kumetangulizwa mbele mno kuliko haki. Wenye nafasi za kushauri au kuonya nao ndiyo hao wameufyata kwa kulinda matumbo yao.

Magufuli hana cha kufanya na mahabusu.

Kabendera anayo haki ya kuachiwa kwa dhamana kama mtuhumiwa yoyote ambaye atapatikana muda wowote akihitajika. Hili ni kwa watuhumiwa wote wa aina hiyo wala si Kabendera peke yake.

Haka ka mdudu ka kutafutiana sababu za kukomoana kanapaswa kukoma. Hako kakikoma haki ika tamalaki yote yatafuata mkondo wake wala hakutakuwa na rai hizi zisizokuwa za kisheria wala Katiba za rais kuachia mahabusu.

Hivi huyu JPM amekumbuka hata ka token rambirambi kwa kabendera? Je wapambe wake nao je? Au wanaogopa kuhatarisha ulaji wao?
 
Mkuu mayala, wakati unasoma pale udsm sheria kama sikosei na mm nlikuwa undergraduate na ulikaa mabibo hostel block F. Unaijua sheria vizuuriiii. Rais haingilii uhuru wa mahakama kwa kusamehe mtu ambaye bado kesi yake haijamalizika. Huwa anaroa msamaha kwa wafungwa. Acha kibendera apate haki yake

Sent using Jamii Forums mobile app
Nafikiri hawa Ngosha wamevimbiwa na madaraka, eti mwanasheria tena with honors of udsm na unahamasisha rais avunje sheria ya kumuachia mahabusu. Yaani Mayala na jiwe wote lenu linajulikana, ulimchochea Kabebendera kwa vimakala vya uongo baada ya kutumwa na Ngosha mwenzio. Sasa dhambi ya kumsababishia mwenzio mateso na mauaji ya Mama yake inakutafuna. Ni bora ukatubu mbele ya Mungu na si hapa jf

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vitu vyote vilivonyooka duniani huwa havipigiwi kelele...ila ukiona kelele kwenye jambo fulani

Ukiwa na akili timamu unajua kuna shida.

Kuna shida pahala..baadae itajulikana tu.

Uzuri wa mambo haya hayatabiriki.Leo unaweza kufurahia kwa comments nyingi mbaya lakini baada ya 10 yrs..

Unajishangaa mwenyewe na tayari muda umekwisha.

Nimeelewa tu Jinsi Judge Mkuu alivyoongea ...ukiwa mwendawzimu huwezi kuelewa.

Kuna wanaume wengine wanapigania maisha ya wanaume wengine ili leo wapate kuandika nyuma ya Keyboard kwa mapovu na dhihaka.
 
Pasco kosa lake ni lipi? Rudini kwenye makala zake mseme wapi kamchongea Kabendera?

Btw zile makala zilipewa umaarufu hapa Tanzania kupitia uchokonozi wa Pasco na hata "waandishi" wake watakuwa walifurahia ile "airtime" na uchokonozi wa Pasco maana ujumbe wao ulifika kama walivyokusudia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
binadam wanafki sana, mara sheria itumike(mwishowe muulize kifungu gan kimetumika), mara Humanitarian reasons zitumike, huyo mama akiwa anaomba msaada ilihali mnajua mtoto wake yupo matatizon kuna waliojitokeza kumsaidia? Kama hamkujitokeza basi achen kujali wakati ameshaondoka( iwe mnajiita mpo nyuma ya. Kabendera ama against, mmeshindwa kuonyesha kua pamoja nae katika hili basi huo ni unafki): Hizo karma mnazotaja kumtisha nan? Kwamba nyie hamtakufa au!
Binaadamu matatizo kusaidia mgojwa kwa wakati hua taabu saana lakini akifariki ndo utaona misaada mingi na michango..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashindwa kukubaliana na hoja yako iliyojaa ubaguzi kimsingi uko bias.

Jambo la kutafakari kama taifa ni kuhusu dhamana hili ni tatizo kubwa na limekuwa likiwaresa watanzania hata kuliko ukoloni ulivyo tutesa.

Kisheria mtuhumiwa hastahili adhabu mpaka pale kesi yake itakapo thibitishwa mahakamani bila kuacha shaka yoyote.

Mtuhumiwa anazuiliwa mahabusu ili siku ya kesi yake aweze kupatikana ili jambo halieleweki kwa jamii na kwa bahati mbaya limepenya mpaka kwa watu wenye mamlaka!

Kama nia ni kupatikana siku ya kesi yake ili aweze kujibu tuhuma dhidi yake ni kweli hawa wadau washeria wa upande wa mashtaka wanatoa wapi hofu kwamba mtuhumiwa atatoroka?

Hapa migogoro yote inatokana na kutotekeleza matakwa ya katiba kuhusu mtuhumiwa nk.

Viongozi kupenda kuwakomoa kwa kuwaweka watuhumiwa mahabusu na kusema umeona nilivyo na mamlaka? hivyo kutumia mamlaka zao kutoa adhabu huku wakijua au kutokokujua kwamba hayo siyo mamlaka yao.

Sheria inatambua kosa la kumzuia mtu mahabusu kinyume na sheria na kumshtaki mtu bila halali ni kosa tatizo wanasheria wanakaa pembeni na kuacha mambo yaende ndivyo sivyo.

Suluhisho la haya ni kufungua kesi dhidi ya sheria kandamizi,pia kufungua kesi dhidi ya kuwazuia wananchi wakati wanadhamana ya kutosha ya kuwafanya wafike mahakamani watakapo hitajika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla,
Hii kesi inatumiwa kuwashikisha adabu wale wote wanaojiona ni wajuzi au wasomi wa haki na blabla za kimagaribi. Wenye akili watakuwa wanatafakari kwanza consequences za wanayotaka kuandika au kusema, kabla hawajachukua hatua hizo. Watu hujisahaulisha kuwa siku ya siku, msalaba wako ni wako peke yako, wapambe hawatakusaidia kuubeba.
Kabendera, kwa mkono wake mwenyewe, alipanda mbegu pasipo na rutuba ya kutosha. Mavuno yake tunayaona.
 
Pascal Mayalla,
Magu alishatueleza kitambo kuwa inawezekana tuna freedom of speech, but NOT TO THAT EXTENT! Nakama kuna kitu tumejifunza kwa Magu, vitisho vyake huwa sio vya utani, njemba anamaanishaga anachosema. Watanzania tusiwe wagumu wa kuelewa. 5 more years, tukikazana na sala, naimani tutapata raisi kama JK 2025, ili turudi toka kwenye hiki kifungo.
 
Seconded
binadam wanafki sana, mara sheria itumike(mwishowe muulize kifungu gan kimetumika), mara Humanitarian reasons zitumike, huyo mama akiwa anaomba msaada ilihali mnajua mtoto wake yupo matatizon kuna waliojitokeza kumsaidia? Kama hamkujitokeza basi achen kujali wakati ameshaondoka( iwe mnajiita mpo nyuma ya. Kabendera ama against, mmeshindwa kuonyesha kua pamoja nae katika hili basi huo ni unafki): Hizo karma mnazotaja kumtisha nan? Kwamba nyie hamtakufa au!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom