Kosa ulifanya tokea mara ya kwanza,ukishaoa hupaswi kuanzisha mahusiano ya kudumu mahai popote,kwingine,na haya magonjwa ya sasa hivi!Na je unapokuwa kwako na mkeo usiku unajua yeye anakuwa wapi?Mimi kwa uzoefu wangu wanawake wa aina hiyo huwa ni waongo na kama sikosei umesema ni single mother,kwanini aliyemzalisha hakumuoa?Jiulize sana na iko siko utakuja uona ukweli.Inawezekana ni mzoefu wa kuvunja nyumba za watu,thats why aliyemzalisha pia may be alikuwa mume wa mtu.Nakueleza hivyo kwani hata mimi nilikutana na hali kama hiyo na iliniletea sana shida mke wangu alipojua ila nashukuru mungu nimeweza kuachana naye mwaka sasa na nimejifunza kutokana na hilo,na pia uzinzi si kitu kizuri kabisa wapende wanao na mkeo.