Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,076
- 463,977
- Thread starter
- #281
SEHEMU YA 154
Nikola alipoondoka, naye akarudi uwanjani mpaka tamasha lilipoisha saa sita usiku na kisha kuelekea sehemu ya kuegeshea magari kwa ajili ya kuondoka. Muda wote huo, Buffet hakuwa na furaha, alionekana kuwa na hofu kubwa huku kwa kumwangalia tu ungegundua kwamba kulikuwa na kitu alichokuwa akikijua ambacho kilimsumbua moyoni mwake.
Mara baada ya kusaini vitabu vya mashabiki wake, Tatiana akaingia garini huku akiwa na furaha tele, aliwapungua mikono, vioo vikapandishwa na kuanza kuodoka mahali hapo huku akiwa na msafara wa magari matano.
Moyoni alifarijika mno, hakuamini kama alimaliza vizuri kufanya shoo ile iliyokuwa imehudhuriwa na watu wengi. Msafara wa magari hayo ukaanza safari kuelekea hotelini, kila mmoja alikuwa kimya garini, walipofika kwenye makutano ya
Barabara ya Welsing na Bulsberg, hapohapo ukasikika mlio mmoja mkubwa, gari alilopanda Tatiana ambalo lilikuwa katikati ya magari hayo yaliyosimama kwenye mataa, likaanza kubimbilika, watu walioshuhudia tukio lile, wakashika vichwa vyao, vilio vikasikika, kila mtu akabaki ameduwaa, gari alilokuwa amepanda Tatiana, lilikuwa nyang’anyang’a.
“Tatiana.....” alijikuta akiita Buffet, hapohapo akateremka kutoka garini na kuanza kukimbia kule lilipokuwa gari lile alilokuwa Tatiana.