Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,054
- 463,971
- Thread starter
- #301
SEHEMU YA 166
Maisha yao yakafana jijini Munich, msichana Tatiana akasahaulika kichwani mwake, hakuwepo moyoni, aliyekuwa akimfikiria kwa wakati huo alikuwa Nikola tu ambaye alikuwa kwenye mapenzi ya dhati huku wakianza kuweka mikakati ya kuanza kuishi pamoja kama mume na mke, kwa kifupi ni kwamba walitaka kufunga ndoa, mpaka mwezi mmoja unakatika, walikuwa kama pete na kidole.
***** Tatiana alikuwa kwenye hali mbaya, pale kitandani hakupata nafuu hata mara moja, siku zilikatika na bado hali yake ilizidi kuwa mbaya kiasi kwamba madaktari wakaogopa mno kwa kuona muda wowote ule mwanamuziki huyo angeweza kufariki dunia.
Dunia nzima ilikuwa kimya, ilikuwa ikisikilizia kile kilichokuwa kikiendelea kule Ujerumani, wengi walishauri kwamba ingekuwa vizuri kama Tatiana angechukuliwa na kupelekwa katika moja ya hospitali nchini Marekani lakini madaktari hawakutaka kutoa ruhusa hiyo kutokana na hali yake mbaya aliyokuwa nayo.
Siku zikakatika, madaktari wakashangaa, hawakuelewa mpenzi wake na Tatiana alikuwa mahali gani kwani tayari wiki nzima ilikuwa imepita lakini mwanaume huyo hakurudi tena hospitalini. Jambo hilo lilizua maswali mengi yasiyokuwa na majibu.
Taarifa juu ya kutokuwepo kwa Buffet hospitalini zikaanza kutolewa, watu walishangaa, hawakujua alipokuwa mwanaume huyo na sababu gani iliyomfanya kumkimbia msichana huyo mrembo katika kipindi alichokuwa hoi hospitalini.
Watu wakahofia kwamba inawezekana Buffet akawa ametekwa na kuuawa na mwili wake kutupwa sehemu lakini mawazo hayo yakafutika kwani polisi nao walikuwa makini kufuatilia lakini hawakuambulia chochote kile.
“Where is this buddy?” (Mshikaji yupo wapi?) aliuliza jamaa mmoja, alikuwa ameshika Gazeti la New York Times la nchini Marekani, lilitoa taarifa kuhusiana na kutoweka kwa Buffet hospitalini.
“I don’t know, maybe he has been kidnapped,” (Sijui, labwa atakuwa ametekwa)
“Impossible.” (Haiwezekani)
“Why not?” (Kwa nini isiwezekane?)
“I don’t know, but it is impossible,” (Sijui lakini haiwezekani)