Pengo: Nchi imeoza!

Pengo: Nchi imeoza!

JIBU LANGU: mi naona kuwa unachanganya mambo. Kardinale na maaskofu walibariki waraka wa dini yao na si wa serikali. Naomba hili ulielewe. Waraka ule si wa waislamu wala wapagani. Ni waraka wa wakatoliki, sasa kama wewe si Mkatoliki waraka ule unakuhusuje? Mbona wakatoliki hawaujadili ila watu wasio wakatoliki wanauvalia njuga kama wao?

Na hapo ndio kwenye tatizo. Asasi ama uongozi wa kidini kutoa misimamo, maelekezao ama matamshi yanayohusu SIASA tena uhcaguzi wa viongozi wa kuwawakilisha watanzania wote kwa ujumla wao, wawe waislamu ama wakristo ni kuvunja, kukiuka ama kudharau misingi ya taifa letu na zaidi kuhatarisha mustakabali wa taifa letu haswa katika swala la maelewano, mepenzi na kuaminiana miongoni mwa watanzania....

Ahaaa! UFISADI! Je wewe unapenda Mafisadi? Kama unawapenda basi naona una kila sababu ya kuupinga waraka ule maana umegusa mioyo ya mafisadi zaidi. Kama si fisadi, naomba vilete vipengele vya waraka unavyovipinga ili tuvijadili!

Nakushauri usome hotuba ya Mwalimu Nyerere inayoitwa TUJISAHIHISHE aliyoitoa mwaka 1962 akihutubia bunge la Tanganyika. Hii tabia ya kukimbilia kuwatuhumu watu wanaoipingana ama kutofautiana na mitizamo na hoja zenu kuwa sio wazalendo, wana chuki na dini za wengine ama watu wengine, wajinga, wanafiki, mafisadi ama wanapenda au kutetea ufisadi, ni tabia mufilisi ambayo haisaidi taifa kuondokana na madhila na hatari tunazokumbana nazo. haina tofauti na wale wana CCM wanaofikiri kuwa watu wote wasiokubaliana na utawala wao ni wapinzani, wasio wazalendo, wana choyo, wana uchu wa madaraka, wakorofi n.k

Ni lazima TUJISAHIHISHEili tuweze kuondokana na huo Uozo tunaoushutumu. Ama sivyo tutafanikiwa kuondoa uozo mmoja na kuingiza UVUNDO mwengine.

Ninapinga zaidi mantiki, uhalali na mazingira ya utolewaji wa WARAKA na MUONGOZO zaidi ya yaliyomo ndani yake. Hata kama yaliyomo ndani yake yanaweza kuwa yanahitajika sana lakini kushindwa kuheshimu MISINGI YA UTAIFA WETU na kutambua mazingira ya kisiasa na kijamii tuliyo nayo sasa kunaondoa uhalali wote wa kilichoandikwa ndani ya ILANI cum WARAKA ama MUONGOZO ......

omarilyas
 
Halafu kardinale kama kiongozi yeyote yule wa dini yeyote anaweza kumshauri mheshimiwa Rais. Zaidi ya hayo kardinale ni mtanzania vile vile.

Ushauri wa kiungwana na wenye nia njema ya kujenga kati ya watu wawili wanaoheshimiana na ambao ni viongozi wa kitaifa hautolewi majukwaani na kwa kuanzisha movements....Pia ukumbuke kuwa Waraka haukuwa wazi kwa wote hadi pale waandishi wa habari walipoamua kutumia ujasusi kuupata na kuutoa magazetini. Nalijua hilo kwa undani wake.

Waraka unaipa changamoto ya serikali kupambana na mafisadi. Ila haupingi serikali. Ila kwa bahati mbaya, baadhi ya viongozi wa serikali ni mafisadi. Ndio maana wanasema waraka una malengo ya kisiasa zaidi ya kutoa elimu ya uchaguzi kwa wakatoliki.
Ni kweli Waraka unaipa changamoto serikali lakini pia unahatarisha amani na maelewano kati ya watanzania na hivyo kutishia usalama wa taifa kama ambavyo hao viongozi walio mafisadi wafanyavyo. Naamini kuna njia zingine makini za kutoa changamoto hilo ambalo linahitajika sana lakini sio katika njia za Waraka wala Muongozo..Ama kwa kutimia Makanisa ama Misikiti...

Hakuna elimu ya urai isiyo na malengo ya kisiasa....tuache kudanganyana. Na wala sio dhambi kuwa na malengo ya kisiasa lakini ni muhimu kutekeleza malengo hayo bila ya kuvunja misingi na maadili ya UTAIFA wetu haswa pale inapohusisha suala la tofauti za kiimani ama nyinginezo za kijamii katika taifa ambalo halina asasi imara za kiutawala kama ilivyo hapa kwetu Tanzania.

omarilyas
 
every person has is own perception.Thats is how Kardinali view the all issue.

But mind you its better always to see and focus things in the three dimensions especially those with national interest.and government will not allow anybody who tries to shake national peace and security.
 
Ndugu yangu Omarilyas uliandika: "Na hapo ndio kwenye tatizo. Asasi ama uongozi wa kidini kutoa misimamo, maelekezao ama matamshi yanayohusu SIASA tena uhcaguzi wa viongozi wa kuwawakilisha watanzania wote kwa ujumla wao, wawe waislamu ama wakristo ni kuvunja, kukiuka ama kudharau misingi ya taifa letu na zaidi kuhatarisha mustakabali wa taifa letu haswa katika swala la maelewano, mepenzi na kuaminiana miongoni mwa watanzania...."

Hoja yangu ni:
Mi nadhani bado hujaelewa kuwa waraka wa wakatoliki ni waraka kwa ajili ya wakatoliki kuwaelimisha kulingana na imani yao juu ya jamii yao kimwili, kiroho, kijamii, kisiasa, n.k. Waraka hauna malengo ya kumweka mtu madarakani bali unawakumbusha wakatoliki kuchagua viongozi wenye busara na wasio mafisadi. Maana imani za kikatoliki hazikubali ufisadi. Zinataka kuwaelimisha wananchi. Sasa ni jinsi gani waraka huu unahatarisha usalama wa taifa? Mambo ya wakatoliki ni ya wakatoliki, si ya waislamu, si ya wanasiasa, bali ni ya wakatoliki. Pingeni mpaka mchoke waraka ndo hivyo umeshatoka na wakatoliki tutatekeleza maagizo ya viongozi wetu. Maaskofu msichoke kupinga ufisadi, tunawaunga mkono. Hongereni sana! Tumsaidieni Rais Kikwete kupigana na mafisadi, hawatufai katika Tanzania yetu hii tunayoipenda. Wakatoliki tu Watanzania tunaipenda nchi yetu na hatujavuruga amani na hatuna mpango wa kuvuruga amani. Amina.


Ndugu yang Omarilyas umeandika: Nakushauri usome hotuba ya Mwalimu Nyerere inayoitwa TUJISAHIHISHE aliyoitoa mwaka 1962 akihutubia bunge la Tanganyika. Hii tabia ya kukimbilia kuwatuhumu watu wanaoipingana ama kutofautiana na mitizamo na hoja zenu kuwa sio wazalendo, wana chuki na dini za wengine ama watu wengine, wajinga, wanafiki, mafisadi ama wanapenda au kutetea ufisadi, ni tabia mufilisi ambayo haisaidi taifa kuondokana na madhila na hatari tunazokumbana nazo. haina tofauti na wale wana CCM wanaofikiri kuwa watu wote wasiokubaliana na utawala wao ni wapinzani, wasio wazalendo, wana choyo, wana uchu wa madaraka, wakorofi n.k

Hoja yangu:

Ndio mna chuki binafsi na wakatoliki. Mbona ule wa waislamu hamuupingi! Kulikoni! Kwani waraka wa wakatoliki unahatarisha vipi taifa. Mi sioni hatari yeyote. Waraka haujawataka watu waingie Msituni wala hauchochei uadui baina ya wananchi na dini zao. Unapinga tu matendo ya kifisadi. Naomba tusilete hoja za Baba wa Taifa ambazo ukizisoma haziingiliani kabisa na dialogue hii. Tumwacheni baba wa taifa apumzike mahali pema peponi amina. Kazi aliyoifanya ni kubwa, tumweshimuni na tumtoe katika suala hili maana nadhani si vizuri kumwingiza katika hoja zetu.


Ndugu ya Omarilyas umeandika: Ni lazima TUJISAHIHISHEili tuweze kuondokana na huo Uozo tunaoushutumu. Ama sivyo tutafanikiwa kuondoa uozo mmoja na kuingiza UVUNDO mwengine.

Ninapinga zaidi mantiki, uhalali na mazingira ya utolewaji wa WARAKA na MUONGOZO zaidi ya yaliyomo ndani yake. Hata kama yaliyomo ndani yake yanaweza kuwa yanahitajika sana lakini kushindwa kuheshimu MISINGI YA UTAIFA WETU na kutambua mazingira ya kisiasa na kijamii tuliyo nayo sasa kunaondoa uhalali wote wa kilichoandikwa ndani ya ILANI cum WARAKA ama MUONGOZO ......


Hoja yangu: Ok. wewe pinga tu waraka huu. Waraka ndo hivyo tena umeshatoka. Ni kama unapiga ngumi ukuta, utaishia kujiumiza mwenyewe. Sisi vita yetu ni juu ya mafisadi na si juu ya usalama wa taifa!
 
My friend Nyuki. You wrote: every person has is own perception.Thats is how Kardinali view the all issue.

But mind you its better always to see and focus things in the three dimensions especially those with national interest.and government will not allow anybody who tries to shake national peace and security.


My opinion: I think what you are trying to say is that the circular has shaken national peace and security. Well, that is not the case at all. Those who are of that opinion are trying to dismiss its intended objectives. The circular has issues with corrupt leaders. If we have conmen with their con-plans, where will the nation go? Remember Fisadis are conmen! That is what the circular is trying to say. We don't need con-leaders at all!
 
Waraka wenyewe naona jamaa wameamua kuuficha. Kwa hakika tuna usongo sana na mwongozo huo. Lakini kwa bahati mbaya hakuna hata mmoja aliyeuleta. Tunawaomba maustadhi mliomo humu mtuletee huo mwongozo.

Babuyao!
Nakushukuru kwa kuwakumbusha ni zaidi ya wiki moja sasa niliomba mtu mwenye huo mwongozo wa Shura ya Maimamu KWA WAISLAMU aliokuwa akiuza sHEKHE Issa Ponda lakini mapaka leo sijaupata au ulikuwa wa maruhani! Kama uliuzwa na bei ilikuwa 2000/= walionunua hawawezi kutuwekea hata scanned au Pdf tukausoma badala ya kuanza kuubeza. Bila utafiti hakuna ruksa kusema!

Tangu mwanzo nilikuwa nan hisia isije kuwa jamaa walihitaji tu vijsenti vya kupata futari na nguo za Eid kwa wake zao wakafanya DECI vinginevyo wautoe au umekwenda alijojo!
 
Pingeni mpaka mchoke waraka ndo hivyo umeshatoka na wakatoliki tutatekeleza maagizo ya viongozi wetu.


Ndio mna chuki binafsi na wakatoliki. Mbona ule wa waislamu hamuupingi! Kulikoni! Kwani waraka wa wakatoliki unahatarisha vipi taifa. Mi sioni hatari yeyote. Waraka haujawataka watu waingie Msituni wala hauchochei uadui baina ya wananchi na dini zao. Unapinga tu matendo ya kifisadi.

Ok. wewe pinga tu waraka huu. Waraka ndo hivyo tena umeshatoka. Ni kama unapiga ngumi ukuta, utaishia kujiumiza mwenyewe. Sisi vita yetu ni juu ya mafisadi na si juu ya usalama wa taifa!

Ni wazi umeishiwa na hoja.....ndiyo jamiiforums hii sio unaingia bila ya hodi ukadhani utakaribishwa mpaka chumbani



Naomba tusilete hoja za Baba wa Taifa ambazo ukizisoma haziingiliani kabisa na dialogue hii. Tumwacheni baba wa taifa apumzike mahali pema peponi amina. Kazi aliyoifanya ni kubwa, tumweshimuni na tumtoe katika suala hili maana nadhani si vizuri kumwingiza katika hoja zetu.
Yeyote anayejidai kumheshimu Mwalimu Nyerere na hapohapo kuunga mkono ama kujaribu kujustify ILANI cum WARAKA WA WAKATOLIKI na ama MUONGOZO WA SHURA YA MAIMAMU ni ama hajui ni kwanini tunamuita Baba wa Taifa na au ni mnafiki mkubwa......

Na daima tutamtumia Mwalimu Nyerere kwani ndio msingi pekee wa UTANZANIA ambao hadi sasa tamaa za MAFISADI wa enzi Ruksa, Uwazi na Ukweli, Ati Mpya na hata wale mafisadi mbadala wanaosubiri wakati wao hazijafanikiwa kuubomoa.....

omarilyas
 
kulingana na gazeti la majira la leo askofu wa jimbo kuu katoliki la dar es salaam, muadhama polycarp kardinali pengo ameibuka tena na kutangaza mapambano mapya dhidi ya mafisadi huku akidai nchi imeoza na kamwe kanisa halitakaa kimya na kulea hali hiyo.

  • asema kamwe kanisa halitakubali kunyamaza.
  • asema watapambana na ufisadi hadi mwisho.
  • aapa kupambana na yeyote anayetetea uovu.
  • asema katoliki haliandai mgombea urais mwaka 2010.
  • adai anayeogopa waraka wa kanisa ni fisadi.

muadhama pengo katafute mke kwanza wa kuowa..halafu ndio utaje mafisadi...unafiki tuuu kazi yako....kwa sababu rais kikwete ni muslam sio ? Hebu tutajie ufisadi ulofanywa tangu kikwete aingie madarakani!!!! ... Mtabaki na na richmond ....mbona wewe pengo ulinyamaza pale mkapa alipouza nyumba za serikali kwa bei yakutupa ??? Mawaziri hawana pa kukaa wanakodi mahoteli...mbona hukunyanyua domo lako...nbc iliuza na mkapa..kawa bei ya cheee kabisa...nyumba zote za mjini za national housing nhc..ziliuzwa wakati wa mkapa na mkewe walinunua kibao kuwapa wachaga..mbona ulipiga kimyaaaa......mkapa katoa vitalu vyote vya migodi ya dhahabu kwa wageni...na ati tz ipewe mrahaba wa 4% haaaa weee pengo mbona hukunena ?????mkapa ndie aliebinafsisha bandari na kuleta hawa tiscan ..mbona uliufyataa mkia....ka sababu ni mkatoliki mwenziooooooo..huna hoja...wewe ni mchochezi na mdini ..mbona mkapa aliua pemba kule hata kukemea kuona uchungu raia kuiliwa..lakini ukapongeza umwagaji wa damu...ni wakati huo tulishuhudia vifo vya akina kolimba na mwaikambo...na malima....ni mkapa alonunua radda tena mramba alisema wacha tule majani lakini rada itanunuliwa...na imefahamika wazi kuwa ni bomu ..ni rushwa tupu...nani alinnua ndege ya rais ..ni mkapa...ndege bomu kabisa na sasa inajulikana kama ni rushwa...sasa unaposema hii serikali ya kikwete ni ya mafisadi..kwa ufisadi upi????

Wacha udini na chuki anaposhika madarka ya urais muislam....mulifanya hivi hivi kwa mzee mwinyi...lakini mnatahayari sasa kuona kwamba mzee huyu alikua msafi kuliko nyerere.

Nani karuhusu nchi kuwa na machinga wa kichina??? Ni mkapa.....kwa kupewa uwanja wa mpira.....kikwete ni safi....huwezi kumlinganisha na mkapa....lakini ila yake ni uislam tuu...
 
na epa nayo ilitoka kwa mkapa..lakini kimyaaaakwanini ...why ??? Kwa sababu ni mkatoliki...na pengo huna sifa ya kutaja mafisadi....wewe hujachaguliwa na wakatoliki wa tanzania amekuteua benedict wa roma....unafanya kazi kwa niaba yake...yakiharibika utaenda huko..kama wale maaskofu wa rwanda..walifanikisha mauaji then wakafichwa vatican...
Chuki za kidini hazifa.i katika nchi kama tanzania ...mtu ambaye analeta chuki na kugombanisha kwa nyaraka za uchaguzi hana uwezo wa kufikiri...haoni mbali.....na akili yake ni finyu...hapa watu wanaoana mpaka wa dini tofauti..lakini hawa kina pengo wao wanafanya kazi kwa niaba ya mafia wa italy.vatican...wanadhani wao tu ndio washike nchi hii...hilo haliwezekani....bado kikwete ni msafi katika africa hana mfano wake.....anaaminika.....na serikali yake ni safi..mnaipiga vita za udini basi......
 
Ndugu yangu Omarilyas umeandika: Ni wazi umeishiwa na hoja.....ndiyo jamiiforums hii sio unaingia bila ya hodi ukadhani utakaribishwa mpaka chumbani

Hoja yangu: Sikubali kama nimeishiwa na hoja. Umeshindwa kujibu maswali yangu na unaishia tu kusema sina hoja. Jibu maswali yangu tuendelee na mjadala.

Ndugu yangu Omarilyas umeandika: Yeyote anayejidai kumheshimu Mwalimu Nyerere na hapohapo kuunga mkono ama kujaribu kujustify ILANI cum WARAKA WA WAKATOLIKI na ama MUONGOZO WA SHURA YA MAIMAMU ni ama hajui ni kwanini tunamuita Baba wa Taifa na au ni mnafiki mkubwa......

Na daima tutamtumia Mwalimu Nyerere kwani ndio msingi pekee wa UTANZANIA ambao hadi sasa tamaa za MAFISADI wa enzi Ruksa, Uwazi na Ukweli, Ati Mpya na hata wale mafisadi mbadala wanaosubiri wakati wao hazijafanikiwa kuubomoa.....


Hoja yangu:
Mi nadhani tofauti kati ya mimi na wewe ni ya kiitikadi tu. Kumbe hata wewe unaupinga ufisadi! Hongera! kumbe wote ni askari tunaopiga vita ufisadi. Kwa hilo nakuunga mkono ndugu yangu Omarilyas. Tuendeleze vita dhidi ya ufisadi. Na tuzidi kuujenga utanzania wetu.
 
Ndugu yangu MZINGANYIKA, naona umeshindwa kabisa kujibu swali langu? Nilikuuliza wewe ni muumini wa dini gani? Na kwamba utoe ushaidi kuhusu yale uliyoyasema kuwa kanisa halitakiwi kupinga ufisadi. Umeshindwa kujieleza. !

Jina langu ni mzanganyika, sio mzinganyika ndugu.

Nimeleta makala ya Padri aliyeeleza wazi wazi kwamba mission ya Yesu haikujumuisha worldly affairs. Pia nimesema hakuna maamrisho ndani ya Biblia yanayowaamuru utekelezaji wa any code of conduct katika worldly affairs.

Biblia haina muongozo wa maswala ya kiulimwengu kwa sababu hiyo haikuwa mission ya Jesus. Mission yake ilikuwa in spirituality tu.

Umenielewa ama bado?

Ndio maana nilihoji Pengo anadhibitiwa na nini kwa sababu amezungumza mambo yaliyo nje ya Biblia.

Biblia haizungumzii maswala ya utawala na uongozi.Kama unaona maneno yangu si kweli jaribu kuleta code of leadership in the Bible kama utaiona.

Angezungumza kama Raia ingeeleweka ni raia kazungumza, yeye kazungumza kama kiongozi wa kanisa, sasa iweje kiongozi wa kanisa ahubiri mambo amabayo yako nje na yaliyo ndani ya kitabu chake kitakatifu?

Soma kitabu cha "100 most influencial persons in History' by MIcahel Harte, huyo ni mwandishi, mwanasheria, ni mtafiti na pia ameonesha wazi kwamba mission ya Jesus ilikuwa pure spiritual.

Sielewi kwa nini unapata taabu kuelewa kwamba kila mtu anatakiwa kuwa na scope ya anayoyafanya na kuyasema kutokana na capacity yake.Kwani hutambui kwamba viongozi wa dini wana mipaka?ama unaamini wanaweza kusema lolote kwa kivuli cha dini?

Kesho Shehe wa Kiislamu akianza kuhubiri mambo ambayo hayapo ndani ya Uislamu kwa kivuli cha dini itakuwaje?

Kwa nini dini yangu ikusumbue, wewe angalia hoja zangu and prove me wrong kama unaamini hoja zangu zina makosa ili nami nione wapi hoja yangu ina upungufu.
 
Last edited:
Waraka wenyewe naona jamaa wameamua kuuficha. Kwa hakika tuna usongo sana na mwongozo huo. Lakini kwa bahati mbaya hakuna hata mmoja aliyeuleta. Tunawaomba maustadhi mliomo humu mtuletee huo mwongozo.

Huenda usongo wako ndio umewazuia watu kuuleta -hahaha

It will be interesting kusoma waraka wa Waislamu nao unasema nini
 
Ukitaka ujadili vizuri point zako inabidi kwanza uelewe unachoongea. What is politics in first place? Maana wewe unatenganisha kabisa politics na maisha ya kila siku. Lazima ujue kuwa Siasa ndiyo tunaishi nayo kila siku, na ndiyo ina-shape our lives. Please go back to learn and come to discuss. Pengo, Kikwete, Myself and yourself are ruled by politics and our destiny detrermined by political affiliation a country moulds itself to. Kwa mfano Siasa ya ujamaa ili-affect vipi maisha yetu. Je sasa, maisha yetu yote yako impacted na hisi siasa. Hata dini inashape vile vile kwa sababu wale watu nao wanaomini hizo dini wako shaped na hizi political za uchwara! Wakeup please!!

Sidhani kama umeipata pointi yangu.

Wadau wamehalalisha ya Pengo kwa kusema hata Sitta na Makamba hunukuu vitabu vitakatifu. Hawa wamemfananisha na wanasiasa.

Kwa mtazamo wangu kuhalalisha maneno ya kiongozi wa dini na maneno ya kiongozi wa dini ni kutomtendea haki kiongozi wa dini kwa sababu kiongozi wa dini mawazo yake huongozwa na maneno ya MUngu, mwanasiasa huongozwa na fikra na malengo binafsi na katiba yake.

Ninatambua kwamba we are all affacted by politics, hiyo ni elimu ya darasa la nne.
 
bwana Mzanganyika!! siku moja nilienda Temeke, karibu na Mwembe yanga back in 1999 au mwanzoni mwa 2000, nikakuta sheik mmoja kakaa na kundi kubwa anawaambia kuwa VAT (ni wakati huo VAT ilikuwa introduced in Tz tax system)sasa huyu sheik anasema hii ni hela inapelekwa VATICAN given wakati hule mtawala alikuwa Mkapa (mkatoliki) sababu ya VAT kuwa ina elufi kama za mwanzo wa VATICAN sasa nikawa tempted kuingilia kati na kueleza wale watu nini maana ya VAT, lakini nikaangalia nikaona sintaeleweka at most wataniumiza. Sasa kama wewe uelewa wako ni kama wa yule Sheik unataka tukusaidieje? maana hiyo mistari ya Biblia uliyonukuu na unavyoitumia huna tofauti kabisa na yule Sheik!! kwa msingi huo nakushauri take your time soma Biblia vizuri na unapokwama uliza ile sheria anayozungumzia Paulo ni nini au ilikuwa inalenga nini usidandie mambo usiyoyajua na uka qoute tu!! inawezekana ulishinda madlasa kwa kukariri Koran na ukaisema ilivyo Biblia ni tofauti haiitaji kukariri inahitaji uelewa zaidi tofautisha mambo kaka!! na kwa maana hiyo.Kadinari pengo ana kila mandate ya kukemea ufisadi kutoka katika Biblia .
 
Jina langu ni mzanganyika, sio mzinganyika ndugu.

Nimeleta makala ya Padri aliyeeleza wazi wazi kwamba mission ya Yesu haikujumuisha worldly affairs. Pia nimesema hakuna maamrisho ndani ya Biblia yanayowaamuru utekelezaji wa any code of conduct katika worldly affairs.

Biblia haina muongozo wa maswala ya kiulimwengu kwa sababu hiyo haikuwa mission ya Jesus. Mission yake ilikuwa in spirituality tu.

Umenielewa ama bado?

Ndio maana nilihoji Pengo anadhibitiwa na nini kwa sababu amezungumza mambo yaliyo nje ya Biblia.

Biblia haizungumzii maswala ya utawala na uongozi.Kama unaona maneno yangu si kweli jaribu kuleta code of leadership in the Bible kama utaiona.

Angezungumza kama Raia ingeeleweka ni raia kazungumza, yeye kazungumza kama kiongozi wa kanisa, sasa iweje kiongozi wa kanisa ahubiri mambo amabayo yako nje na yaliyo ndani ya kitabu chake kitakatifu?

Soma kitabu cha "100 most influencial persons in History' by MIcahel Harte, huyo ni mwandishi, mwanasheria, ni mtafiti na pia ameonesha wazi kwamba mission ya Jesus ilikuwa pure spiritual.

Sielewi kwa nini unapata taabu kuelewa kwamba kila mtu anatakiwa kuwa na scope ya anayoyafanya na kuyasema kutokana na capacity yake.Kwani hutambui kwamba viongozi wa dini wana mipaka?ama unaamini wanaweza kusema lolote kwa kivuli cha dini?

Kesho Shehe wa Kiislamu akianza kuhubiri mambo ambayo hayapo ndani ya Uislamu kwa kivuli cha dini itakuwaje?

Kwa nini dini yangu ikusumbue, wewe angalia hoja zangu and prove me wrong kama unaamini hoja zangu zina makosa ili nami nione wapi hoja yangu ina upungufu.


Mzinganyika nakuuliza kidogo.

Juzi JK kaongea pale kwenye vyombo vya umma .Means wana CCM na Vyama vya Upinzani na wasio kuwa na vyama .Wanalipia kodi na aliongelea CCM sana . Je aliongea kama Rais , Raia ama mwenyekiti wenu ?
 
Ndugu yangu Mzanganyika, mimi bado napata ugumu wa kuzielewa hoja zako. Kwa mfano unasema:

"Nimeleta makala ya Padri aliyeeleza wazi wazi kwamba mission ya Yesu haikujumuisha worldly affairs. Pia nimesema hakuna maamrisho ndani ya Biblia yanayowaamuru utekelezaji wa any code of conduct katika worldly affairs. "

Hoja yangu: sasa wewe unataka kusema, kwenye biblia wakristu wanaambiwa wasijihusishe na mambo ya kisiasa hivyo wakubali tu matendo na michezo michafu ya kisiasa. sio hivyo. Nadhani hapo unakosea, hata biblia haiwakatazi wakristu kujihusisha na siasa!. kama umeisoma biblia sema ni sehemu gani inasema hivyo. Kumbuka wakristu ni binadamu vile vile, kupinga ufisadi tutaupinga kwa sababu hauko katika ukatoliki. Ukatoliki haukumbatii ufisadi. Sisi vita yetu ni kwa mafisadi. Sasa kama wewe Mzanganyika uko fisadi, jua kuwa wewe ni mmoja wa maadui zetu. Tutakusakama mpaka uache ufisadi. kama si fisadi, basi safi jiunge nasi kupambana na mafisadi!

"Mzanganyika unasema: Biblia haina muongozo wa maswala ya kiulimwengu kwa sababu hiyo haikuwa mission ya Jesus. Mission yake ilikuwa in spirituality tu.

Umenielewa ama bado?
"

Hoja yangu:

Naomba nikuulize mission ya Yesu ilikuwa ni nini? Kama binadamu, Je roho na mwili si vitu vinavyotegemeana? sasa ukiwa na mwili utahitaji yanayokwendana na mwili kimahitaji na siasa ina athari zake katika hili. Halafu ili binadamu ukamilike unahitaji roho. Umenipata hapo?

Mzanganyika umeandika:
"Ndio maana nilihoji Pengo anadhibitiwa na nini kwa sababu amezungumza mambo yaliyo nje ya Biblia.

Biblia haizungumzii maswala ya utawala na uongozi.Kama unaona maneno yangu si kweli jaribu kuleta code of leadership in the Bible kama utaiona."


Hoja yangu: Siwezi kukupa code za biblia kwa sababu utazitafsiri vibaya na kupotosha umma. Ila tu kwa taarifa yako zipo. Wewe una chuki binafsi na Kardinali Pengo. Ungejua Kardinali wala hana chuki na wewe. Unajiangaisha tu kumchafulia jina. Sisi kama wakatoliki tunamuelewa kiongozi wetu pamoja na viongozi wengine na ana kila support yetu. Hivyo ukae ukijua kuwa huwezi kuwadhibiti maaskofu au mashehe kwa hoja zako. ujue unajisumbua tu! Kama unasema unaweza, jaribu uone, hautafanikiwa! Sasa unataka kudhibiti viongozi wa dini ili iweje? Turudi tena kwenye ukomunisti na udikteta! Hapana Tanzania yetu hatutakubali sera za ukomunisti na udikteta. Mbona Amini alithibiti watu, je aliweza? Si alishindwa. Musolini, je? naye alishindwa. Hitler, je? Hata yeye alishindwa! Nakushuri usome historia ili uelewe kusoma alama za nyakati!

"Mzanganyika umeandika:

Angezungumza kama Raia ingeeleweka ni raia kazungumza, yeye kazungumza kama kiongozi wa kanisa, sasa iweje kiongozi wa kanisa ahubiri mambo amabayo yako nje na yaliyo ndani ya kitabu chake kitakatifu?
"

Hoja yangu:

Kwani kiongozi wa kanisa si raia? Halafu waraka haukuandikwa na Kardinali, umeandikwa na wakatoliki. Tena kwa taarifa yako Pengo anazungumza na waumini wake. Sasa je Pengo hana haki ya kuzungumza na waumini wake? Mashehe je, hawana haki ya kuzungumza na waumini wao? Ni jambo lipi alilohubiri pengo ambalo liko nje ya biblia? Nadhani hapo umeishiwa hoja ndugu yangu Mzanganyika, maana yote yaliyoko kwenye waraka hayaupingi ukristu wala utanzania wa mtu yeyote!

Ndugu mzanganyika umeandika:
"Soma kitabu cha "100 most influencial persons in History' by MIcahel Harte, huyo ni mwandishi, mwanasheria, ni mtafiti na pia ameonesha wazi kwamba mission ya Jesus ilikuwa pure spiritual
."

Hoja yangu: Hata mimi ni msomi na nimeandika vitabu. Hivyo si lazima nikubaliane na huyo mwandishi. Leteni hoja wewe na mwandishi wako ili tuichanganue kiutaalamu, nipo tayari kwa hili. Tafdhari refer to my maelezo kuhusu roho na mwili ili kuelewa suala la spirituality. Asante.

Ndugu Mzanganyika umeandika:
"Sielewi kwa nini unapata taabu kuelewa kwamba kila mtu anatakiwa kuwa na scope ya anayoyafanya na kuyasema kutokana na capacity yake.Kwani hutambui kwamba viongozi wa dini wana mipaka?ama unaamini wanaweza kusema lolote kwa kivuli cha dini?

Kesho Shehe wa Kiislamu akianza kuhubiri mambo ambayo hayapo ndani ya Uislamu kwa kivuli cha dini itakuwaje?

Kwa nini dini yangu ikusumbue, wewe angalia hoja zangu and prove me wrong kama unaamini hoja zangu zina makosa ili nami nione wapi hoja yangu ina upungufu
."

Hoja yangu:

Hivi naomba uniambie mipaka ya kupambana na ufisadi ni ipi? Huwezi kusema lolote katika kivuli cha dini. Mapambano dhidi ya ufisadi si ya kidini tu, ni ya kisiasa, ni ya kijamii na ni ya kisheria vile vile. Hivyo wakatoliki wamefanyia kazi sehemu yao, viongozi wa kisiasa watafanyia kazi sehemu yao na kadhalika. Sasa mbona waraka wa kiislamu umepinga ufisadi na wewe hauulaumu? Mbona unalaumu tu wa wakatoliki?

nasubiri hoja yako mkuu.
 
Last edited:
Sikusema imeandikwa maovu yasikemewe. Nimesema hakuna sehemu inayomuamuru muumini wa Biblia akemee maovu na ndio maana nimesema the one who can prove me wrong alete ushahidi.ia nimesema Paul ameamuru ndani ya Romans kwamba 'hakuna tena sheria ya righteousness'. Biblia pia inasema 'deeds are filthy rags' sasa kama wema na uadilifu ni filthy rags mbele ya Mungu kuna umuhimu na uhalali gani wa kuhubiri uadilifu?

Huwezi kuleta ushahidi wa kisichikuwepo, ushahidi huletwa kwa lililopo sio kwa kisichopo.

Kwenye thread nyingine kuna mchangiaji mwenye signature ya quotation ya Biblia ambaye pia amesema kwamba Yesu hakuhubiri worldly affairs. Anakiri kwamba the scope does not cover hayo ya Pengo na kuna dalili kwamba huyo ni muumini wa kitabu hichohicho.

Sasa wewe prove me wrong kwa kuleta amri ya kukemea maovu na kwamba aliyyoyakemea ni maovu kwa mujibu wa maandishi. Nipe maandishi yanayowapa waumini sifa za uongozi ili tuone kama hizo sifa katoa ndani ya kitabu ama maoni binafsi.

Kama hakuna Biblical writings zinazo support aliyoyasema kuna tofauti gani kati ya maneno yake na maneno ya Mrema, ama Slaa, ama Lowassa, ama Kingunge?

Try to talk sense, please! Hatuwezi kupoteza muda kujadili mawazo ya kitoto kama hayo! The Bible gives the basic message that is translated into responsible action. Mfano, hakuna kwenye Biblia ipalipoandikwa mtu ale mara 3 kwa siku au aende haja kubwa na ndogo; au akiandika atumie computer na akitaka kuwasiliana na mtu wa mbali atumie fax, e-mail, telex au simu, yet vyote hivyo tunavitumia kwa utaratibu mzuri tukijua tumejealiwa na Mungu.

Huwezi kukuta kwenye Biblia imeandikwa kuwa Tanzania itakuwa na Uchaguzi Mkuu 2010. Yet, inapokuja kuwachagua viongozi lazima tuangalie uadilifu na sifa za uongozi kwani vigezo hivyo ndivyo vinavyofamfanya kiongozi amudu kazi yake na aifanye kwa manufaa ya watu waliomchagua.

Uadilifu umefundishwa kwenye Biblia na pia sifa za viongozi zimefundishwa kwa maneno kama. Kuliko mtu mwingine akutafutie, wewe mwenyewe kama una nia ya kuelewa zitafute. Kama nia yako ni kubisha, hapo hakuna sababu ya kuzitafuta kwa vile kubisha siyo lazima uwe unaelewa kitu.

Hata kwenye Qur'an hutakuta imeandikwa Waislamu wachague viongozi wa Bakwata au mskiki ukijengwa upakwe rangi fulani na uandikwe majina au uwekewe vipaza sauti juu na kila asubuhi, mchana au jioni mtu aite waamini wenzake kwa kutumia maneno yanayotumiwa kila siku.

Hayo yote yamefanywa kwa kufuata ujumbe wa jumla ulio kwenye Qur'an unaohusu maisha ya Waislamu kwa ujumla. Hata kwenye Biblia ni hivyo: hutakuta jina Kardinari Pengo au papa. Lakini wote hao uwpo wao umetokana na inspiration wanayoipata kutoka kwenye Biblia. The Bible is there to inspire believers and not as a history book! And when you talk about proof what do you mean? Legal proof, empirical proof, psychological proof, theological proof, historical proof, logical proof or ontological proof?
 
ongera sana nduyu yangu Magobe T. kwa kumwelimisha vizuri ndugu yetu Mzanganyika. Naona sasa ukichukua maelezo yako na yangu atakuwa ameelewa vizuri tu, unless otherwise hataki kuelewa.
 
Yes,lazima aseme nchi imeuzwa na imeoza akikaa kimya nani aongee????????????????
 
Pengo anayo right kuzungumzia suala la ufisadi kama kiongozi wa dini lazima ikumbukwe kwamba issues zote zinazohusu masuala ya morality huwa zinazuungumzwa na viongozi wa dini kwanza duniani kote kabla hata ya wana siasa kuanza kuzizungumzia mfano ni suala la same sex marriages huko US watu walioipinga hiyo hoja wakwanza walikuwa ni viongozi wa dini kwanza,hao ndio wenye power kubwa sana over citizens than even state itself,tieni maanani haya maneno yangu kwanza kabla ya kukurupukia kuanza kumshambulia mzee Pengo ambaye yeye anatimiza wajibu wake kama kiongozi wa madhehebu ya dini fulani yenye wafuasi wengi sana nchini.
Baba Manka
 
Back
Top Bottom