Pengo: Nchi imeoza!

Pengo haitaji kitabu cha kiarabu ili kukemea uovu. Yeye kama mtanzania ana kila sababu ya kukemea ufisadi wa serikali ya Kikwete na mpango wa kutaka kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kiislam

Leta hicho cha kwake na unioneshe wapi kimemuamrisha kukemea ufisadi?

Kama anafanya mambo kutokana na fikra zake na sio muongozo wa Mungu kwa nini atumie kivuli cha dini?
 
Pengo haitaji kitabu cha kiarabu ili kukemea uovu. Yeye kama mtanzania ana kila sababu ya kukemea ufisadi wa serikali ya Kikwete na mpango wa kutaka kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kiislam

Leta hicho cha kwake na unioneshe wapi kimemuamrisha kukemea ufisadi?

Kama anafanya mambo kutokana na fikra zake na sio muongozo wa Mungu kwa nini atumie kivuli cha dini?

Sasa kama amezungumza kama Mtanzania kwa nini ullitwa waraka wa katoliki-why tie it to dini kama sio kutaka kutuletea vurugu?
 

Kama ukatoliki unaongozwa na Biblia tupatie aya za Biblia zenye kuunga mkono hoja yako.

Kama wanaweza kujisemea lolote hata kama hakuna backing ya wanachosema ndani ya Biblia hapo kuna tofauti gani kati ya ukatoliki na chama cha siasa ama cha mpira wa miguu?

Waislamu wameamrishwa waziwazi ndani ya kitabu chao kwamba wasidhulumu wala wasidhulumiwe kwa hiyo wameamrishwa kukemea dhuluma katika jamii na kutofanya hivyo ni dhambi kubwa.
 
Alichosema kinaeleweka na sikukihoji.
Nimehoji uhalali wa yeye kusema aliyoyasema.
Amri ipi ndani ya kitabu chake inachompa yeye uhalali wa kukemea maovu?
Kama una ushihidi bring it on badala ya kulaumu al arabiya.
Hakuna dini hata moja hapa duniani inayobariki uovu. Na hakuna kitabu chochote cha dini kinachoruhusu watu kutenda uovu. Usilete quotation za bible out of context. Jaribu kutumia logic na sio kutoa hoja za kutoka pale kwenye midahalo ya kiislamu pale mwembechai.
 

Kama kweli unasema hayo kutokana na utafiti makini naomba unipe aya za Biblia zinazowaamrisha waumini wakemee maovu.

Unless you are telling me that mafundisho ya Kikristo hutungwa kutokana na human logic.

Nipe quotation za Bible zinazomwamuru anayeamini Biblia akemee maovu.
 
Kwa sababu hizo mahakama zingine sio za kutoka uarabuni ili kueneza dini hapo Tanzania. Hiyo ndiyo tofauti kubwa hapo juu.

Hizo mahakama zingine zilitoka wapi? Sumbawanga? au hujui historia ya mahakama?

Uelewe hata hilo neno Mahakama na Sheria, yote hayo ni ya Kiarabu na si ya kibantu wala Kiyuropa.
 
Hapana Omari,

wakatoliki walipomsifia Kikwete kuwa kachaguliwa na mungu, hakuna aliyesema kuwa wanachanganya dini na siasa. Leo wanapinga ufisadi na swala la mahakama ya kadhi ndio kila mtu macho yanamtoka.

Kwani unyemkubalia jambo moja ni lazima ukubaliane naye kwa kila jambo.

Leo ukiunga mkono hoja yangu kwani ni lazima na kesho nikija na hoja mpya uiunge mkono?
 

Hayo yote ingekuwa JMK kuwafunguwa vinywa na macho msingeyaona wala msingeyasikia, tafuta mwanzo wa yote uliyoyataja hapo juu, yalianzia wapi?
 

Upewe quotation za Bible ukiwa kama nani? Huko madrasa uliyosomea kiarabu hakuna biblia za kiarabu?
 

Kama umekuwa tied na katoliki au pentekoste wewe una tatizo na hilo? Au mpaka kingekuwa tied na Afghanistan today ndipo ungeelewa vizuri!
 
Hayo yote ingekuwa JMK kuwafunguwa vinywa na macho msingeyaona wala msingeyasikia, tafuta mwanzo wa yote uliyoyataja hapo juu, yalianzia wapi?

JMK kamfungua kinywa nani? bonge la fisadi anaona aibu kuwa yametoka na sasa hata anatumia dk kibao kuelezea swala la richmond ambalo kahusika kwa kila kurasa ya mkataba wake.

Na bado una guts za kuelezea usafi wa Kikwete na Mwinyi? Au kwa vile wote wanafuata dini ya waarabu?
 
Nafikiri watu wanamatatizo ya kiakili!! sasa Mwadhama Kardinali Pengo akisema nchi imeoza kuna uongo hapo au ni ukweli??? kama kateuliwa na Roma au na Ikulu ya Tz au kachaguliwa vyovyote vile utakavyowaza hapa hoja iliyombele yetu in moja tu, je kazusha uongo au kasema ukweli! I think this is common sense dictation hutakiwi kuwa msomi hata darasa la saba kujua kuwa Tz ufisadi unatupeleka kubaya na watu wengi msichoona ni hiki,viongozi wa kidini au watanzania wenye upeo na upendo na nchi yetu wasipokemea sasa hivi nchi itakwenda pabaya zaidi ebu fikiria wewe utakubali kufa njaa wakati ukijua akina RA na EL na genge lao wamekwiba maela mingi namna hile? maana hapa kuna matabaka yanataka kujengwa kwamba watu waibe na kuifanya Tz na watu wake si tu maskini bali ni wajinga pia!! sasa kundi la watu wenye njaa likaamka itakuwa shughuli, hapa si udini wala siasa ni moral obligation ya kila mtazania kumwimiza mwenzie tusiibiwe tena kiasi kile sasa Mwadhama akikemea hilo shida iko wapi huyu anatakiwa atiwe moyo na kuwa applauded!! siyo this rubbish!! watu wengine mnakuja nayo ati katoka Vatican , lakini haya angesema G,Brown au Obama ambao si watz ungekuwa kimya it is absurd!! be objective na maudhui na siyo kujadili pesonality kwa kutaka kupotosha ukweli wa hoja !! Aksante Mwadhama Kardinali Pengo endelea kukumea ouvu na uozo wa nchi!! Mungu akupe nguvu ujasili na hekima zaidi, MUngu Ibariki Tanzania
 

Logically uko right lakini factuall totally wrong! Kumbuka kwamba waislamu mmedai kwamba mahakama za kadhi ni sehemu ya ibada wakati mahakama za biashara na nyinginezo sio sehemu za ibada! Itakuwaje basi serikali isiyo na dini iendeshe ibada ya dini moja? Kumbuka Ibara ya 19(2) ya Katiba inakataza serikali kujihusisha na uendeshaji na utangazaji wa dini!
 
Samahani sana kwa kuleta habari za uongo, OIC si kama ulivyofafanua wewe, sijui umeitowa wapi hiyo?

OIC ni Organization of Islamic Conference na si kama utakavyo wewe. Tafadhali usibabaishe watu, ukiandika uwe na uhakika na unachokiandika.

Unajua maana ya neno Islamic? Pia umesoma OIC Charter ambayo inasema kwamba moja ya malengo yake ni kueneza Islamic Culture and Civilization na kulinda Islamic symbols na pia kumaintain Islamic Character of Palestine + Jerusalem ambao waislamu mnauita Al Quds? Sasa nchi isiyo ya Kiislamu inakuwaje inalinda na kuendeleza mambo ya waislamu? Tunadanganywa eti tutapewa unafuu wa misaada, kama hawataki kutupatia hizo ambazo Waziri Membe aliziita fedha za shetani waache tu, kwani hiyo misaada ya nchi mbalimbali imetusaidia nini?
 

Unaweza ukawa Profesa lakini mawazo yako yakawa questioned. Asiyeweza kusahihishwa ni Mungu pekee! Lipumba alikuwa anabeza kauli za wana-CCM kwamba Chama chao kimefanikiwa kuifanya nchi kuwa na amani! Response yake ni kwamba watz "kwa asili ni watu wa amani." Huyu JK naye ameuchuna, style ya mbuni kuficha kichwa mchangani amejisahau, mechukuliwa na upepo wa "watz kwa asili ni watu wa amani" na kufikiri mambo yataliset menyewe!
 
Mwandishi wa hiyo makala yupo biased, wewe Zawadi Ngoda unataka kutimiza malengo yako ambayo huenda ni ya kidini au yanasukumwa na chuki za kidini.

Kwa baadhi wameenda mbali zaidi na kuona kuwa, waraka huo si tu unailenga CCM, bali ni Rais Kikwete na washabiki wake serikalini kwa kuonekana kutolisikiliza kanisa katoliki kama ilivyokuwepo kwa akina Nyerere na Mkapa.

Kikwete hajasikiliza nini toka katoliki? Je, Mkapa na Nyerere ndo walikuwa wanasikiliza katoliki? Mwinyi je? au kwasababu ni muislam kama Kikwete?


you are damn wrong! Katoliki walikuwa na nguvu au ushawishi gani ambao hawana sasa? Kikwete kataka lini kutenganisha dini na Serikali? au kwa kutaka kuingiza mahakama ya kadhi kwenye katiba? Ukitaka kujua ukweli, kipindi hiki cha Kikwete ndo kime-attempt kuingiza dini kwenye Serikali kuliko wakati mwingine wowote.

Unasema juu ya mataifa ya magharibi kuingiza dini kwenye siasa, kwanini usisema mataifa ya uarabuni yanayoongozwa kwa kitabu cha dini kama katiba? kuna mataifa yanayoingiza dini kwenye Serikali kama waarabu? Ukiondoa Ujerumani mataifa mengine ya magharibi yametenga dini na Serikali.


Hii nayo ni kuweka ice sugar kwenye keki yako unayoipika sasa. Kama unataka kujenga hoja substantiate, pole sana.


ok, ungeandika aya hii tu, ungeeleweka, kwani hiki ndo kiini cha hoja yako.


So, Kikwete kapanga watu wake hadi vigangoni (lowest level)! Naa hao watu wote wanatakiwa kuondolewa! kanisa limeweka mpango wa muda mrefu kufagia Kikwete? lol jamaa kama ni kumtishia nyau Rais unajitahidi. Hivi hao watu wa Kikwete hakuna wakatoliki! kama wapo maanayake wanaweka mpango wa kujiondoa wenyewe? not logical at all.


so far unamwongelea Pengo siyo kanisa katoliki? au? ok, Unamaanisha wafuasi wa Kikwete walitumwa wakaupinge waraka lakini on the way wengine wakasaliti na kuunga mkono! Unamaanisha bunge letu limetawaliwa na udini? tena kwa kumuunga mkono Pengo for what?

We jamaa acha viwaraka vyako visivyoeleweka hivi. Unachofanya ni kutaka kutenganisha Watanzania badala ya kuwaunganisha. Kibaya zaidi wahariri tulionao wanaweza kuichapa hii gazetini kama ilivyo ukiwapelekea.

Ninakushauri uachane na chuki za kidini.
 
Msukumo mkubwa nyuma ya waraka wa kanisa ni UFISADI. Hali iliyopo Tanzania ya kuiba na kupoteza mali za Taifa ndiyo sababu kubwa ya kanisa kutoa waraka huo.

Kanisa halijatoa waraka kwa sababu ya OIC na mahakama ya kadhi, issue ya OIC na mahakama ya kadhi ni ya muda mrefu sana.

Kingunge ni moja kati ya watu wanaoimaliza Tanzania (FISADIS) anajua wazi kwamba waraka huo una lengo la kuwamaliza mafisadi na kuwafumbua macho wanyonge, kwa mantiki hiyo alikurupuka na kujibu waraka huo.

Matatizo yetu ni ufisadi na wala si udini. Tusipokuwa makini hawa mafisadi watatumia pesa zao kubadilisha mtazamo huu na kuufanya uonekane kwamba tatizo letu ni udini na wala si ufisadi. Na hicho ndicho kingunge anachotaka kukifanya.

Ili kumaliza tatizo la ufisadi katika Tanzania ni lazima tupate viongozi waadilifu, wenye mapenzi ya dhati ya nchi yetu, na ambao watachaguliwa kwa haki wala si kwa rushwa (Sokoine type).

Option ya pili ni kufanya mapinduzi na kuwakamata viongozi wote waliotuibia na kuwapiga risasi hadharani ili iwe fundisho kwa viongozi wajao. Hili litawapa viongozi woga wa kuiba, hivyo mali za Taifa zitapona.(China style).

Serikali ya Jakaya kupambana na ufisadi ni kichekesho kwani haiwezekani mwizi kujipeleka kituo cha polisi. 99.9% ya viongozi ndani ya serikali ya Jakaya ni wezi wa kupindukia, sasa nani atamkamata nani?. Hata wakikamatana na kupelekana mahakami unakuwa ni mchezo wa kuigiza, ambao unatuingizia gharama na kutupotezea muda kama "kesi" zao zilizo mahakamani kwa kipindi hiki.
 
Kuanza kuwasema waislamu na wakristo, au kwa ufupi kuwachonganisha wasilamu na wakristo ni dangerous and cheap politics. Ni kulifumbia macho tatizo na kuelekeza ufuatiliaji kwingine ili kupoteza lengo. Tunajua TATIZO tulilonalo ni kuwa nchi yetu inabadilika, CCM imetekwa na serikali imetekwa na nchi imetekwa. Wahalifu wanapeta na wananufaika na nchi na kulindwa. Wasio wahalifu wanateseka na kuhangaika na wengine wako magerezani(si kila mfungwa alikuwa mhalifu, si kila aliyeuraiani ni raia mwema).

Ni lazima tutambue kuwa kuna udhaifu mkubwa sana kwenye serikali yetu ya sasa. Ninaposema hivi sina maana ya individuals Kikwete, Pinda au Kingunge (Mwislamu, mkristo na mpagani), ni serikali yote na ikiwa ni viongozi na dini zao. Toka ngazi ya taifa, mkoa, wilaya hadi mashinani. Viongozi wote wakristo, waislamu na wapagani walioko ndani ya serikali ya sasa wako kwenye kapu moja. Wameshindwa kuonesha leadership, accountability na vision.

Tatizo tunaona kuwa nchi imekamatwa na mafisadi, mpaka rais wetu amesema ni wajanja na hawakamitiki. (sijui kama ni kweli au vipi). Tumeipa serikali madaraka lakini inayatumia kwa manufaa ya wachahce na sio ya manufaa yetu. Wale wanaotaka kutusaidia sasa ndio wameanza kuonekana maadui.

Issue inabadilishwa kuwa dini, wakati tatizo ni ufisadi what a cheap trick! Kingunge anajulikana wazi kuwa amebadilika, si kingunge tena aliyekuwa anasimamia haki, anayepinga rushwa, anayekemea viongozi wabovu anayesimamia maslahi ya Chama. Yeye ni mlinzi wa ufisadi an mafisadi, pure and simple. Hana hoja nyingine, sasa hivi hawezi kuleta hoja ya ukoministi kwa kuwa umepitwa na wakati, kwa hiyo hoja pekee aliyonayo sasa ni kuwatetea mafisadi.

CCM ya sasa sio chama cha mapinduzi tena, kilichokuwa cha wakulima na wafanyakazi, kilichokuwa kinatetea maslahi ya watanzania na kuwaendeleza.

Angalia maisha ya mkulima wa Tanzania, au mfanyakazi wa Tanzania jaribu kuwangalia kama kweli CCM inareflect chama inayosema kinawawakilisha. Jibu ni hapana.

Issue sio mahakama ya kadhi, sio OIC, sio Pengo na mufti. Issue Tanzania ni ufisadi na kupotea kwa ile CCMambayo tulikuwa tunaiita nambari one. Mambo yakjo tofauti kabisa.
 


Solomon waste no time na huyu Darisalama . Yeye michango yake yote anasukumwam na nguvu ama hisia za Uislam na upwani hakuna zaidi .So okoa muda wako .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…