''Kuna walioandaa wagombea wao, na taasisi zao ambazo ni taasis za heshima zikagharamia uchapishaji wa majarida, wakaandaa semina, makongamano, na kufanya kampeni kwenye kila ibada. Lakini hawakufanikiwa kupenyeza mtu wao kwenye nafasi walioitaka, sasa hii tunayoishuhudia ni kuchanganyikiwa kwao na ndio maana nilieleza kule Dodoma wakati wa sherehe za kuzaliwa CCM kuwa, kuna baadhi yetu bado wamenuna na matokeo ya uchaguzi. Kwa bahati mbaya hata wakiendelea kununa, rais wa nchi hii ataendelea kuwa yule yule, hakuna mwingine, na shida zao watakuja kuniambia mimi hawana pakwenda.'' Huu ndio ujasiri wake Jakaya Mrisho Kikwete rais wa awamu ya nne, Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.