Pengo amtolea uvivu Kikwete

Pengo amtolea uvivu Kikwete

Nakubaliana na Mhashamu Pengo, JK anatakiwa ataje majina na kuwafikisha mahakamani wahusika wote wa madawa ya kulevya. haitakuwa haki kwa wananchi kama kuna watu wanashtakiwa na kufungwa kwa biashara hii haramu halafu kuna wengine wanaogopwa. Pengo kaweka wazi yeyote anayehusika akamatwe bila kujali kazi na dini yake.

Raisi anaonyesha udhaifu wa kulinda katiba kwa kuonyesha kuna baadhi ya watu au taasisi ziko juu ya sheria, hilo sote tunalikataa. Mhasamu kaweka wazi kuwa utawala ni pamoja na kutoa maamuzi na kuachia vyombo husika vifanye kazi yake. Kutuhumu kanisa ni kosa. mbona kanisa linaonyesha ushirikiano mzuri na serikali? kanisa katoliki limekuwa mstari wa mbele kulinda sheria za Mungu, Kanisa na nchi pale zinapofiunjwa bila kujali muumini ni nani, awe padri, sister, au wakawaida.

JK analeta usanii hata kwenye maswala ya imani za watu. Anaonyesha asivyoweza kuelewa kuwa imani sio mtu ila ni taasisi na maisha muhimu ya mwananchi na uhai wa serikali. Imefika wakati wa kuwa na Raisi atakaye weza kulinda sheria na kanuni za nchi bila kulalalmika na kuonyesha uhasama na kikundi kimojawapo cha nchi kwa kutumia udini, ukabila, ukanda au rangi ya wananchi wake.
 
Nchi ilikuwa pepo wakati wa Mkapa ndio maana hatukuwahi kumsikia pengo wala mwanya, ila kwa sasa imekuwa jehanam baada ya Kikwete, shame on wanafiki woote wanaotumia visingizio vya dini na matatizo ya wananchi kueneza chuki zao. Pengo hovyooo kabisa.
watu kama hawa ni kuwapuuza tu..! wandugu mnaweza mkashinda hapa kujaribu kuwaelewesha lakini haitasaidia kitu! kuna mdau huko nyuma kasema ..hawa jamaa wameshashindikana ..tuombe Mungu labda vijazi vyao vijavyo vitapata elimu ya kutosha! I wish yule jamaa niliyemuona kwenye mdahalo wa katiba mpya ...Bashiru Ally......angewasaidia hawa wazee wa madrassa!! wamekosa elimu tu ndiyo maana JK anawatumia vizuri!
 
angewasaidia hawa wazee wa madrassa!! wamekosa elimu tu ndiyo maana JK anawatumia vizuri!

Mimi nadhani hii strategy haiwezi kuwasaidia sana, mnaweza tu kuweka hoja zenu mezani bila kukashifu dini za wengine, mngekuwa mnajifunza haijawasaidia sana na tunapoelekea ndio itakuwa kizuizi kikubwa sana kwenu.
 
Sipo huko ulitaka jina limetajwa, hayo mengine ni frustration zenu tu, poleni kwa kushindwa uchaguzi.

RAIA wanne wa kigeni, Dennis Okechukwu na Paul Obi wote wa Nigeria, Stani Hycenth wa Afrika Kusini na Shoaib Muhammad Ayaz kutoka Pakistan wakitoka kusomewa mashitaka ya kula njama na kuingiza nchini dawa za kulevya aina ya heroin zenye thamani ya sh. bilioni 2.8, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dar es Salaam...ndo mana nimekwambia hamna akili.
 
Hivi ingekuwaje kama rais angekuwa mkristo halafu akaongelee msikitini kwamba kuna viongozi wa dini wanauza madawa ya kulevya?

Kwani ukristo ni DINI? Je unaweza kunipa ushahidi kuthibitisha kama ni Dini?
 
Huyu ni mchungaji wa kanisa, na hili unaliongelea vipi.

Please come up with a convincing evidence to justify what JK said. Huwezi kuwatuhumu viongozi wa dini na hiyo kashfa ukiwa ndani ya kanisa la katoliki then unataja jina la tapeli from nigeria. Kamanda mwenyewe anayeshughulikia madawa ya kulevya ana kashfa ya kumbambikizia mtoto wa mengi madawa. Leo atamshawishi nani kama anachokisema ni kweli. Niambie huyo ni mchugaji wa kanisa gani, kanisa lake liko wapi na linaitwaje
 
Kwani ukristo ni DINI? Je unaweza kunipa ushahidi kuthibitisha kama ni Dini?

I dont have too. Koz u and me are living in a different world and you will neva understand me. Mtafute Suleman Rushd atakusaidia kukuambia dini ni ipi. But the only thing I can tell you is that. U will neva conquer this country or this world!!!
 
Jamani mbona haya hayasaidii kutuondelea umaskini wetu? Ukristo uwe ni dini au sio dini bado haisaidii chochote kwa maendeleo ya nchi na wellbeing ya watu wetu, na ukiluiza hivyo mwingine nae atakuja na hoja kuwa je Uislamu ni dini? hii mijadala ya ya kugusa dini za watu ni ya kijinga na alieianzisha nae ni hivyo hivyo, maana huwezi kwenda nyumbani kwa mtu ukifika umtusi kisha umwambie nahisi tu kuwa ni mwanao na wala sio wewe....
Kwani ukristo ni DINI? Je unaweza kunipa ushahidi kuthibitisha kama ni Dini?
 
<font color="#a52a2a"><b>Wewe kweli ni mchicha mwiba , uliisha ona wapi wahalifu wanatajwa ? mbona hamsemi wahalifu wengine watajwe isipokuwa hawa wa madawa ya kulevya ? waache washughulikiwe kimya kimya. Na nimjuavyo Pengo lazima kuna watu wake wameshikwa pabaya, huyu mzee huwa sio msafi</b></font>
<br />
<br />
kama sio msafi ndio tunataka kikwete aseme pengo siyo msafi sasa au anamuogopa?
 
Huyu ni mchungaji wa kanisa, na hili unaliongelea vipi.
<br />
<br />
humu kuna watu wa ajabu sana na akili zao zimeshabinafsishwa kitambo tu. Hv kuna haja gan ya kumtukana mtu kumsema cjui yuko hv, yan wewe ndo unaonekana taahira cz unaongea upupu tu badala ya kumpinga mtu kwa hoja.
 
Hapo amenenoa lakini, kikwete ni sikio la kufa.
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Pengo: Viongozi wamekiuka misingi ya Uhuru [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"]Send to a friend[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Saturday, 13 August 2011 20:48[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]0diggsdigg

11pengo2.jpg
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo

Fredy Azzah na Ibrahim Yamola
ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesema Watanzania wanasherehekea miaka 50 ya uhuru huku kukiwa na makundi ya viongozi na vigogo nchini wanaojineemesha kupitia migongo ya wananchi bila kujali wanawasaliti, wanawaongezea umaskini na kuwaua.
Kardinali Pendo alilaani akisema: “hayo yamekuwa yakitendeka kinyume na misingi iliyoainishwa na waasisi wa taifa wakati wakidai uhuru kutoka kwa wakoloni ambapo walitamani kujenga Tanzania yenye utukufu.
Kardnali Pengo alisema hayo jijini Dar es Salaam jana, alipokuwa akiongoza ibada ya maadhimisho ya miaka 50 ya Tanzania, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Kristu Mfalme Parokia ya Tabata.
“Waasisi wetu walipokuwa wanapigania uhuru wa taifa hili, lengo na maono yao yalikuwa kutengeneza taifa lenye utukufu, lenye kutawala mataifa mengine …,” alisema Kardinali Pengo na kuongeza:
“Katika miaka 50 tunayoikamilisha, kumekuwa na mafanikio na changamoto nyingi tu, inabidi tujipange ili watakao kuja kuadhimisha miaka 100, au hata miaka 25 ijayo wasije wakasema afadhali wakati wa mkoloni.”
Katika ibada hiyo ambayo pia ilitumika kuliombea taifa, Pengo alisema wakati wa kupigania uhuru lengo ilikuwa ni kulifanya sehemu salama na bora ya kuishi watu wake.
Kardnali Pengo alitahadharisha akisema: “Lakini sasa Taifa lina makundi ya watu wasaliti, wenye ubinafsi na ambao wako tayari kujitafutia utukufu hata ikibidi kuwakandamiza na kuwaua wenzao”.
Kwa sababu hiyo akawataka Watanzania kutafakari katika kipindi hiki cha kuadhimisha miaka 50 ya uhuru, wajiulize wamekuwa wakijitafutia utukufu binafsi au ule ulioasisiwa na taifa wa wananchi wote kufaidi matunda yake.
Kwamba, tumepata utukufu wa aina gani?” Alisema Kardinali Pengo na kuonya; "Baadhi ya watu wanapata utukufu bila hata kujali kama watu wengine wanakufa, jambo ambalo ni hatari kwa taifa."
Kardinali Pengo aliwaonya waliopewa dhamana ya uongozi na kutumia nafasi hiyo kujitajirisha, kuwa ni usaliti kwa Taifa na Watanzania kwa ujumla.

Tuhuma za dawa za kulevya
Katika hatua nyingine, Kadinali Pengo, alilaumu mtindo wa viongozi wa Serikali na dola kutotaja hadharani majina ya watu wanaowatuhumu kuhusika na biashara ya dawa za kulevya huku wakiendelea kulalamika kuwa wapo na wamewakamata.
Alisema hali hiyo haionyeshi nia yao ya dhati katika kupambana na biashara hiyo haramu.
Akikumbushia kauli aliyoitoa Rais Jakaya Kikwete wakati wa Sikukuu ya kumwekwa wakfu na kumsimika Mhashamu Askofu John Ndimbo kuwa Askofu wa Jimbo la Mbinga kuwa baadhi ya viongozi wa dini huuza dawa za kulevya, alisema alitakiwa kuwataja.
Kardinali Pengo alisema kitendo cha Rais Kikwete pamoja na baadhi ya viongozi waliojitokeza kuzungumzia suala hilo huku wakisema hawawezi kuwataja kwa majina, huo ni usaliti mkubwa kwa taifa.
“Haiwezekani mtu mkubwa tu, wala siyo mdogo kuja katika eneo la Kanisa la Katoliki, kukiwa kumejaa Maaskofu kutoka karibu nchi nzima, unasema maneno haya halafu unasema, siyo nyie ni viongozi wa makanisa madogomadogo," alilalamika Kardinali Pengo.
Aliongeza kwamba: "Kama ndivyo hivyo kwa nini sasa uje kuyasema maneno hayo katika eneo la Kanisa Katoliki."
Akasisitiza: "Mapadri, watawa; naomba tujiangalie kama sisi tunaguswa na hii kauli, kama haitugusi tumshukuru Mungu, lakini ni vyema hawa watu wakatajwa. Hata kama ni mimi njoo uniambie, ukisema hunitaji kwa sababu ni kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam, huo ni usaliti mkubwa kwa taifa.”
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge, William Lukuvi, aliwahi kuliambia Bunge hivi karibuni kuwa Serikali ina safari ndefu katika kufanikisha mkakati wa kukomesha biashara hiyo haramu.
Alisema Serikali inaamini kuwa vita ya kuwakamata wanaojihusisha na dawa za kulevya ni ngumu lakini akasisitiza kuwa anaamini mwishowe watashinda uhalifu huo.
Lukuvi alisema mbali na kuwataja hadharani baadhi ya viongozi wa dini, imebainika kuwa wana mtandao mkubwa.
“Hapa sio kuwataja tu maana kama ni kuwataja tayari Serikali ilikwisha wataja na watu wanajua kuwa kiongozi wao ni yule Askofu wa Nigeria, lakini hapa suala ni namna ya kupambana na kuwajua wengine,’’ alisema Lukuvi.
Hata hivyo, mara baada ya Rais Kikwete kutoa kauli hiyo, Jumuia ya Kikristo Tanzania (CCT), ilikuja juu na kumpa saa 48 za kuwataja hadharani viongozi wa madhehebu ya dini wanaohusika na biashara hiyo haramu.
"Rais ataje majina ni kina nani wanahusika na ndani ya saa 48 awe ameyataja la sivyo itakuwa ni aibu zaidi kwake na Serikali," alisema Makamu Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dk Valentino Mokiwa.
Rais Kikwete alijibu wito huo kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu kwamba, viongozi wa dini siyo malaika kwa hivyo wasijivune kuwa hakuna miongoni mwao ambao ni wahalifu.

Source: Gazeti la Mwananchi

My take:
Kweli Pengp amesummarise vizuri behaviour za Kikwete kuwa ni msaliti maana kuna matukio mengi yametokea na hajatoa kauli wala kuchukua hatua zozote sasa kama huu si usaliti kwa wananchi ni nini?

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
humu kuna watu wa ajabu sana na akili zao zimeshabinafsishwa kitambo tu. Hv kuna haja gan ya kumtukana mtu kumsema cjui yuko hv, yan wewe ndo unaonekana taahira cz unaongea upupu tu badala ya kumpinga mtu kwa hoja.


Maoni yako
 
Wana JF wenzangu, leo napenda kuwatahadharisha rasmi kuwa, kuna uwezekano watu wenye hekima na busara wakachoka ama kupatwa na maumivu ya kichwa kwa sababu jukumu la kujibishana na watu ambao wapo hapa sio kwa nia ya kujifunza ama kuelewa kitu bali kutetea mfumo wao. Hapo tulipofikia ni mahali ambapo nafasi ya kutumia hekima kufanya mijadala imefikia mwisho. Kama ilivyo kwenye siasa za sasa hakuna cha hekima ama hoja zenye mashiko zinazoendelea zaidi ya ujanja na ghiliba. Tizameni kwenye Bunge letu, angalieni kwenye CC na NEC, wala msiache kuangalia kwenye vyuo vikuu vyetu nk Hekima inazidi kuachwa na ama inapungua kadiri muda unavyo zidi kusonga.

Jambo la pili ni kuwa: Kuna uwezekano wa 100% kuwa kuna majini (mapepo) yanayotumia avatar za wafu (fuatilieni) kupotosha mada za kizalendo ili kuondoa uwezekano wa kufikia hitimisho lenye tija kwa jamii yetu. Lakini pia, kuna watu ambao si wao wanaoongea, bali ni majini yaliyomo ndani yao. Sasa hivi mawakala wa shetani (majini au mapepo) ni wengi mno katika Jamii Forum na Tanzania kupita wakati mwingine wowote. Mikakati iliyopo ni kuharibu kabisa mtandao wa haki katika nchi na kusimika mtandao wao na kuimarisha maslahi ya kifisadi zaidi ili kuiteka nchi yetu.

Wale mnaojitahidi kujibishana nao, very soon mtachoka na mtanyamaza, kwa sababu ya uchovu, maumivu ya kichwa na kukata tamaa. Hamtaweza kudumu kutumia ubongo wenu kutengeneza majibu yenye hoja zenye nguvu ya hoja na falsafa ya kutetea haki na ukweli siku zote. Huo ndio ukweli wa hali halisi hapa JF na TZ yetu. Poleni sana ... Lakini kwa wale wenye pumzi nyingi nawatia shime waendelee, kwa sababu wanafanya kazi njema na yenye baraka za Mungu Mkuu na Baba wa mbinguni.
 
Jamani mbona haya hayasaidii kutuondelea umaskini wetu? Ukristo uwe ni dini au sio dini bado haisaidii chochote kwa maendeleo ya nchi na wellbeing ya watu wetu, na ukiluiza hivyo mwingine nae atakuja na hoja kuwa je Uislamu ni dini? hii mijadala ya ya kugusa dini za watu ni ya kijinga na alieianzisha nae ni hivyo hivyo, maana huwezi kwenda nyumbani kwa mtu ukifika umtusi kisha umwambie nahisi tu kuwa ni mwanao na wala sio wewe....

Nafikiri ukichukulia Kauli ya Rais wenu Kikwete ni kuwatuhumu kuwa viongozi wa Dini ......

Sasa ili mtu alalame ni lazima a fall kwenye category ya DINI. Kwani ukisoma kwenye Quran 3:103-104 zimesema wazi kuwa Uislam ni DINI. sasa nauliza upande wa pili je kuna andiko lolote ndani ya Bible linalonena wazi wazi kuwa Ukristo ni DINI.

Na Uyahudi ni dini soma
[SUP]Matendo 2:9-10.[/SUP][SUP][/SUP]
[SUP]9[/SUP]Hapa kuna Waparthi, Wamedi, Waelami, wakazi wa Mesopotamia, Yudea Kapadokia, Ponto na Asia, [SUP]10[/SUP]Frigia, Pom filia, Misri na pande za Libya karibu na Kirene; na wageni kutoka Rumi, Wayahudi na watu walioingia dini ya Kiyahudi

Suala langu je Ukristo ni Dini. naomba andiko kuthibitisha hilo .
Ili sasa tujue malalamiko ya Pengo
 
Back
Top Bottom