Hatumchagui mtu kwa dini yake..ukatoliki na serikali wapi na wapi. Makanisa yote na misikiti husajiliwa na wizara tu ambayo ni home affairs. Unadhani ukitaja RC umetaja jambo kuuuubwa?! Ni NGO tu hiyo baba. Na sasa imekuwa civic and profitable organization...inakosa hata hadhi ya Religious NGO. Ombeeni Taifa siyo kulumbana kisiasa. Aliomba audience na Rais aseme linalomkwaza au analotaka kushauri akanyimwa appointment? Anatumia media apate publicity ili iweje?Na kwakuongezea hapo,hayo mamlaka aliyonayo huyo anayemtetea yatakwisha come 2015,Pengo is there to stay as kiongozi wa kanisa mpk pale Mungu atakapochukua maisha yake.By the way,hivi mh Rais alivyokuwa anaongea hivyo,haoni kuwa amewakwaza waumini wa kanisa katoliki including kina Pinda?
Kweli hukubaliki kama jina lako lilivyo..Reject.....Kumbe kweli umeishiwa hoja! Duh!
dawa ya moto ni motowakuu tunaomba sana tupunguze jazba kwani thread hii inaelekea kuongeza hisia za kidini , tunaipenda Tanzania tusingependa hisia hizi ziongezeke sana.
pls wana JF tusiingize udini kama hoja zijengwe kwenye utendaji na si udini wakuu
Kweli hukubaliki kama jina lako lilivyo..Reject
Umenipa hadhi kubwa mno ya usalama. Inshallah mdomo wako uwe wa kheri ili taifa letu liwe salama zaidi nikinyaka ajira hiyo.tena katumwa huyu ni usalama kuendelea kumujibu tunapunguza umaarufu wetu ni bora kumuucha aendeleee kuonesha ujinga wake
tatizo ni rais kuwafaham wahalifu na kukataa kutueleza kwa kututajia majina hao wahalifu.INA MAANA PENGO ALISHAWAHI AU ANAO WATOTO? MWANAMKE MJAMZITO KAMWONA WAPI? SI MUOE JAMANI...YA NINI KUJITESA NA KUCHAFUA MASHUKA USIKU...UNAJUA USIPOLALA NA MWANAMKE MIAKA MINGI UNAATHIRIKA KISAIKOLOJIA? HUYU MZEE AMEATHIRIKS KISAIKOLOJIA NAMSAMEHE BURE
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Pengo: Viongozi wamekiuka misingi ya Uhuru
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"]Send to a friend
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Saturday, 13 August 2011 20:48
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]0diggsdigg
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo![]()
Fredy Azzah na Ibrahim Yamola
ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesema Watanzania wanasherehekea miaka 50 ya uhuru huku kukiwa na makundi ya viongozi na vigogo nchini wanaojineemesha kupitia migongo ya wananchi bila kujali wanawasaliti, wanawaongezea umaskini na kuwaua.
Kardinali Pendo alilaani akisema: hayo yamekuwa yakitendeka kinyume na misingi iliyoainishwa na waasisi wa taifa wakati wakidai uhuru kutoka kwa wakoloni ambapo walitamani kujenga Tanzania yenye utukufu.
Kardnali Pengo alisema hayo jijini Dar es Salaam jana, alipokuwa akiongoza ibada ya maadhimisho ya miaka 50 ya Tanzania, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Kristu Mfalme Parokia ya Tabata.
Waasisi wetu walipokuwa wanapigania uhuru wa taifa hili, lengo na maono yao yalikuwa kutengeneza taifa lenye utukufu, lenye kutawala mataifa mengine , alisema Kardinali Pengo na kuongeza:
Katika miaka 50 tunayoikamilisha, kumekuwa na mafanikio na changamoto nyingi tu, inabidi tujipange ili watakao kuja kuadhimisha miaka 100, au hata miaka 25 ijayo wasije wakasema afadhali wakati wa mkoloni.
Katika ibada hiyo ambayo pia ilitumika kuliombea taifa, Pengo alisema wakati wa kupigania uhuru lengo ilikuwa ni kulifanya sehemu salama na bora ya kuishi watu wake.
Kardnali Pengo alitahadharisha akisema: Lakini sasa Taifa lina makundi ya watu wasaliti, wenye ubinafsi na ambao wako tayari kujitafutia utukufu hata ikibidi kuwakandamiza na kuwaua wenzao.
Kwa sababu hiyo akawataka Watanzania kutafakari katika kipindi hiki cha kuadhimisha miaka 50 ya uhuru, wajiulize wamekuwa wakijitafutia utukufu binafsi au ule ulioasisiwa na taifa wa wananchi wote kufaidi matunda yake.
Kwamba, tumepata utukufu wa aina gani? Alisema Kardinali Pengo na kuonya; "Baadhi ya watu wanapata utukufu bila hata kujali kama watu wengine wanakufa, jambo ambalo ni hatari kwa taifa."
Kardinali Pengo aliwaonya waliopewa dhamana ya uongozi na kutumia nafasi hiyo kujitajirisha, kuwa ni usaliti kwa Taifa na Watanzania kwa ujumla.
Tuhuma za dawa za kulevya
Katika hatua nyingine, Kadinali Pengo, alilaumu mtindo wa viongozi wa Serikali na dola kutotaja hadharani majina ya watu wanaowatuhumu kuhusika na biashara ya dawa za kulevya huku wakiendelea kulalamika kuwa wapo na wamewakamata.
Alisema hali hiyo haionyeshi nia yao ya dhati katika kupambana na biashara hiyo haramu.
Akikumbushia kauli aliyoitoa Rais Jakaya Kikwete wakati wa Sikukuu ya kumwekwa wakfu na kumsimika Mhashamu Askofu John Ndimbo kuwa Askofu wa Jimbo la Mbinga kuwa baadhi ya viongozi wa dini huuza dawa za kulevya, alisema alitakiwa kuwataja.
Kardinali Pengo alisema kitendo cha Rais Kikwete pamoja na baadhi ya viongozi waliojitokeza kuzungumzia suala hilo huku wakisema hawawezi kuwataja kwa majina, huo ni usaliti mkubwa kwa taifa.
Haiwezekani mtu mkubwa tu, wala siyo mdogo kuja katika eneo la Kanisa la Katoliki, kukiwa kumejaa Maaskofu kutoka karibu nchi nzima, unasema maneno haya halafu unasema, siyo nyie ni viongozi wa makanisa madogomadogo," alilalamika Kardinali Pengo.
Aliongeza kwamba: "Kama ndivyo hivyo kwa nini sasa uje kuyasema maneno hayo katika eneo la Kanisa Katoliki."
Akasisitiza: "Mapadri, watawa; naomba tujiangalie kama sisi tunaguswa na hii kauli, kama haitugusi tumshukuru Mungu, lakini ni vyema hawa watu wakatajwa. Hata kama ni mimi njoo uniambie, ukisema hunitaji kwa sababu ni kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam, huo ni usaliti mkubwa kwa taifa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge, William Lukuvi, aliwahi kuliambia Bunge hivi karibuni kuwa Serikali ina safari ndefu katika kufanikisha mkakati wa kukomesha biashara hiyo haramu.
Alisema Serikali inaamini kuwa vita ya kuwakamata wanaojihusisha na dawa za kulevya ni ngumu lakini akasisitiza kuwa anaamini mwishowe watashinda uhalifu huo.
Lukuvi alisema mbali na kuwataja hadharani baadhi ya viongozi wa dini, imebainika kuwa wana mtandao mkubwa.
Hapa sio kuwataja tu maana kama ni kuwataja tayari Serikali ilikwisha wataja na watu wanajua kuwa kiongozi wao ni yule Askofu wa Nigeria, lakini hapa suala ni namna ya kupambana na kuwajua wengine, alisema Lukuvi.
Hata hivyo, mara baada ya Rais Kikwete kutoa kauli hiyo, Jumuia ya Kikristo Tanzania (CCT), ilikuja juu na kumpa saa 48 za kuwataja hadharani viongozi wa madhehebu ya dini wanaohusika na biashara hiyo haramu.
"Rais ataje majina ni kina nani wanahusika na ndani ya saa 48 awe ameyataja la sivyo itakuwa ni aibu zaidi kwake na Serikali," alisema Makamu Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dk Valentino Mokiwa.
Rais Kikwete alijibu wito huo kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu kwamba, viongozi wa dini siyo malaika kwa hivyo wasijivune kuwa hakuna miongoni mwao ambao ni wahalifu.
Source: Gazeti la Mwananchi
My take:
Kweli Pengp amesummarise vizuri behaviour za Kikwete kuwa ni msaliti maana kuna matukio mengi yametokea na hajatoa kauli wala kuchukua hatua zozote sasa kama huu si usaliti kwa wananchi ni nini?
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Ofisi ya RAIS ni kielelezo cha utaifa wa Tanzania. Ni vyema viongozi wa kidini kama Mhashamu Pengo akaiheshimu hii ofisi kwa sababu ni kilelezo cha utaifa wa Tanzania, taifa isiyofungamana na dini yoyote.
Lugha inayotumiwa na viongozi wa kidini wa Tanzania ni lugha kali na ni lugha inayobeza utaifa wetu. Sijawahi kumsikia Baba Mtakatifu akitoa lugha kali dhidi ya kiongozi yoyote duniani kama zinazotolewa na baadhi ya viongozi wetu wa kidini hapa Tanzania.
Hii lugha haikuwepo kabisa wakati wa Urais wa Baba wa Taifa. Endapo viongozi wa kidini hawampendi Jakaya Mrisho Kikwete kama mwananchi angalau tuiheshimu OFISI YA RAIS ambayo ni kielelezo cha utaifa wetu. Ingawa tunawaheshimu sana viongozi wa kidini, tukumbuke kuwa sisi wengine hatujui ni nani kawachagua VIONGOZI WA KIDINI kuongoza taasisi zao na vigezo vilivyotumika kuwachagua.
RAIS wa JAMHURI yetu tulimchagua na tunajua utaratibu uliotumika kumpata RAIS. Tusitumie majukwa ya kidini kubeza UTAIFA wetu. RAIS, BUNGE na MAHAKAMA ni VIELELEZO VYA UTAIFA WETU UNAOTIMIZA MIAKA 50.
Nilishtushwa sana jana Gazeti la TANZANIA DAIMA la tarehe 14 AGOSTI 2011 lilimuita Rais MSALITI. Hii ni lugha iliyojaa hasira dhidi ya Rais kama kielelezo cha utaifa wetu. Huu sio Uhuru wa Habari. Ni UHURU ULIOPINDUKIA MIPAKA. Lugha hii haitumiki hata hizo nchi kama Uingereza ambazo wengi tunadhani kuwa zina UHURU wa HABARI wa KUPINDUKIA. Hata Uingereza machafuko ya Juzi yamefanya waangalie upya UHURU wa HABARI upya na kuangalia mapungufu yanayochochea uvunjifu wa Amani kupitia. Na Maandamano YANAYOPINDUKIA MIPAKA ndio yanafanya watu wengine WAJENGE HOJA za kurudisha nyuma HAKI ZA KUKUTANA na kushirikiana na wengine zilizopatikana kwa taabu tangu mwaka 1992.
Matumizi mabaya ya UHURU hurudisha nyuma mazuri yaliyopatikana.
VIONGOZI WA KIDINI WAKUMBUKE KUWA TANZANIA NI SECULAR STATE NA KWA MATAMHI YAO WATUSAIDIE ILI TUENDELEE KUMHESHIMU RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BILA KUJALI YEYE NI WA DINI YAKE.
tatizo ni rais kuwafaham wahalifu na kukataa kutueleza kwa kututajia majina hao wahalifu.
kwa nini polisi isumbuke kwa kutumia rasilimali nyingi kupambana na madawa ya kulevya wakati mkuu wa nchi anaweza akawaweka ndani hao said maaskofu mara mmoja na kutuokolea taifa?
rais ana mafungamano gani na hao maaskofu mpaka akatae kuwataja?
rais anamwogopa nani?
urais hauna shareholders, yupo huru kimawazo so atusaidie mara mmoja kumaliza tatizo la madawa ya kulevya kama anaipenda tanzania
Nadhani tuna haja ya kupima akili na ubongo wa Pengo, katika watu wanafiki yeye ni 1 . Hili jambo liliisha fafanuliwa na ikulu na Bunge, anachokitaka ni kipi ? . Huwezi kuwataja watu wakati uchunguzi bado unaendelea na wana mtandao mrefu. Hili ni jambo la kushughulikia kimya kimya na kwa vile amelipigia kelele nadhani kuna watu wake wa karibu wamekamatwa pabaya.
hapo blue: Uchunguzi unaendelea kivipi alisema hadharani maaskofu ni wauza misuba?Nadhani tuna haja ya kupima akili na ubongo wa Pengo, katika watu wanafiki yeye ni 1 . Hili jambo liliisha fafanuliwa na ikulu na Bunge, anachokitaka ni kipi ? . Huwezi kuwataja watu wakati uchunguzi bado unaendelea na wana mtandao mrefu. Hili ni jambo la kushughulikia kimya kimya na kwa vile amelipigia kelele nadhani kuna watu wake wa karibu wamekamatwa pabaya.
inawezekana hata pengo akawa mchafu as yeye pia ni binadamu.Wewe kweli ni mchicha mwiba , uliisha ona wapi wahalifu wanatajwa ? mbona hamsemi wahalifu wengine watajwe isipokuwa hawa wa madawa ya kulevya ? waache washughulikiwe kimya kimya. Na nimjuavyo Pengo lazima kuna watu wake wameshikwa pabaya, huyu mzee huwa sio msafi
Wewe kweli ni mchicha mwiba , uliisha ona wapi wahalifu wanatajwa ? mbona hamsemi wahalifu wengine watajwe isipokuwa hawa wa madawa ya kulevya ? waache washughulikiwe kimya kimya. Na nimjuavyo Pengo lazima kuna watu wake wameshikwa pabaya, huyu mzee huwa sio msafi
Ayawasilishe maoni yake ktk lugha za heshima. Unajua tafsiri ya neno msaliti?Nachunga mdomo wangu nisije nikajikuta nimeropoka kama meya Masaburi kwamba wengine wanafikiri kwa makalio badala ya ubongo lakini samahani.
Tunapojadili jambo tunatakiwa to concentrate kwenye topic tunayoongelea. Mwalimu asiyefuata mlolongo wa silabas ya kufundishia wanafunzi anawachanganya na kuvuruga mtiririko wa uelewa wa wanafunzi.
Nikupe pole sana ndugu Son of Africa, maana umechepuka na kuwa nje ya maudhui tunayoongelea hapa, na ukiangalia wengi hawakuelewe kwa vile unaongelea kuvua samaki baharini ya Hindi wakati sisi wenzako tunaongelea uvunaji wa pamba huko kanda ya ziwa.
Kama umepumua yameisha pumzika sasa sisi tulio na machungu ya maisha hatutarudi nyuma hadi tufikie kwenye kuzima kiu ya nja ambayo nawe ni mwadhirika wa kwanza.
Mwadhama Policarp Cardinali Pengo angekuwa na roho kama ya kwako asingethubutu kuhangaikia kutetea wanyonge kwa vile yeye kama Mwadhama hana njaa kama yangu na wewe, hana shida ya usafiri kama wako na mimi, uwezo wa kupata umeme anao, na kama shida inaongezeka anaweza kuondoka kwenda Vatican kwa sababu za kusingizia kikazi kama Kikwete afanyavyo ukitilia maanani kwamba Mwadhama Pengo ni kati ya makardinari wachache walio kwenye halmashauri ya Pontific huko Vatican na wengi wa makadinari hawajabahatika kupata heshima hiyo.
Anachotetea Mwadhama ni uchungu kwa wananchi wa Tanzania kama mtetezi wa Afrika Kusini Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglican Desmon Tutu. Utajiri tunaotafuta duniani hapa ni wa kupita na wangapi wamehangaikia na kuishia kutokamilika na wanakufa wangali wanahangaika kutafuta pesa? Jiwekeeni hazina mbinguni kusikoharibika kitu kwa nondo au kutu.
Asumpta es Maria in celum, laudes angelis, laudantes benedictum Dominum.
be blessed!Huo ni ulofa na hatutegemei nchi iongozwe kiwoga namna hiyo! Sijawahi kuona nchi ya hovyo namna hiyo duniani isipokuwa Tanzania ya awamu ya 4 tu. Lakini haya yana mwisho! Wahalifu wote wanatakiuwa kutajwa jamii iwaelewe ijitenge nao kisha mkondo wa sheria uchukue hatamu. Kinyume cha hayo ni ulofa ni kujenga mazingira ya rushwa na ni kinyume cha kanuni za utawala bora za za openness & Transparency.
KUJUA MHALIFU NA KUKATAA KUMTAJA NI NINI KAMA SIO KUSALITI?Ayawasilishe maoni yake ktk lugha za heshima. Unajua tafsiri ya neno msaliti?