Pengine Zitto hana kosa....

Pengine Zitto hana kosa....

nakubaliana nawe kabisa. wanachama wengi wapo katika dilema. mimi nimeandika mawazo haya ikiwa tafakuri ya kutafuta a way out of the dilema. lakini pia naamini njia ambayo ni sahihi ni kutafuta compromise ya hizi kambi mbili. na harakaharaka nadhani compromise inawezekana kabisa kutafuta neutral group ipewe madaraka--tena haraka. Na sijui ni nani atayewezesha hili kutokea. kuleta neutral people kwenye safu ya uongozi itaondoa hisia ya either group kushinda. chadema ni chama kikubwa kuliko kinavyoonekana machoni pa watu. kwa hiyo hapatakuwepo shida kupata neutral group. tatizo nani awezeshe hilo?

Dialema?Labda ninyi 'wasomi'ndio mko njiapanda kwa kuwa kujua kwingi huondoa maarifa.Sisi tunajua,tena kwa uhakika,Zitto tangu ateuliwe tume ya Buzwagi,alinunuliwa na hadi akajengewa shule kwao na barrick gold na akawa mpole bungeni kabisa.Alichobakiza ni kuwa mpinzani wa viongozi wake.Alipoamua wazi wazi kuipigia kampeni nccr ili kafulila ashinde,Laiti ningekuwa na uwezo ningelimfutilia mbali uanachama wake aende huko nccr.Huyu ni nyoka na hatakiwi kuonewa huruma hata kidogo.Kama hahongwi anatoa wapi pesa ya kununua gari la fahari?msitwambie kitu bana huku tunaishi na mamluki wake wengi na wanatamba huwa anawapa pesa za matumizi na wanakiri wanataka nao wawe na madaraka!Hakuna anayewaza kumkomboa mwananchi kutoka kwa wakoloni weusi

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Bado naendelea kuamini kwamba mgongano huu wa kifikra kati ya wanachama wa CHADEMA dhidi ya CHADEMA kutokana na maamuzi ya kamati kuu hauzingatia utulivu wa kifikra katika kuona ukubwa na mantiki iliyopo wakati huu wa kuelekea katika mapambano makali zaidi ya kisiasa.Ni fumbo ambalo si rahisi kutegua ni nini kinaweza kutokea lakini vilevile kuthibitisha kile ambacho kinafikirika kwa manufaa ya upande mmoja dhidi ya mwingine.Kwa mtu ambaye hawezi kujenga nguvu ya kuona kwa kutumia fikra zake kuliko kile ambacho anaweza kukiona kwa macho si rahisi kukubaliana na jambo moja kubwa muhimu kwamba ni mgangano ambao haumdhoofishi Mh.Zitto tu kisiasa bali ni mgongano ambao unatengeneza uwanja mpa wa mapambano dhidi wa wanachama wa CHADEMA kwa CHADEMA.

Binafsi naamini kwamba vita ya kuongea ni mbaya sana kuliko vita ya kusikiliza. Iwapo tutajenga msingi wa kuzungumza kwa maana ya kujibu mapigo CHADEMA kwa CHADEMA kwa kutumia kejeli na dharau ni kuhalalisha kwamba bado hawamini katika nguvu ya ndoto zao kisiasa. Kwa kufanya hivyo angefungua uwanja mpya wa malumbano ambayo hayana tija kwa uhai wa chama. The Dream will remain a Dream kama hakuna michakato ya kufikia ndoto zenyewe. Lazima kuset goals ambazo zitajenga msingi imara wa kubomoa mabomu ya kipopraganda ambayo yanajengwa zidi ya CHADEMA

Lakini kwa upande mwingine CHADEMA kama chama kitapoteza rasilimani muhimu sana ambayo ni muda kujibu mapigo dhidi ya maadui kisiasa japokuwa katika misingi ya kujenga nidamu na uaminifu ndani ya chama kinapaswa kuwa “risk-takers”. Lakini ukiwa na malengo makubwa ni muhimu kupima madhara yanayoweza kujitokeza katika kufikia malengo.

Muhimu ni kujenga utashi wa kifikra na kujenga msingi na mtazamo mpya kuelekea mafanikio makubwa zaidi ya kisiasa.

Mbelwa Germano
Lushoto Constituent
 
Nadhani umetazama kiini cha tatizo ambacho kimekaa kiimani bila kutazama madhara ya maamuzi kwa mustakabali ya chama. Umakini wa kifikra unatokana na jinsi gani unatatua matatizo kinyume chake ni kukurupuka. Yawezekana kabisa ukawa na ushahidi au usiwe na ushahidi wa yote hayo unayosema, jambo unaloshindwa ni kujua madhara ya maamuzi ambayo yanatoa taswira ya mwenendo na mustakabali ya CHADEMA kama chama.

Hapa simtetei Zitto hata chambe bali natumia uwezo wa kifikra kwa kutazama athari za maamuzi kwa ukubwa wake. Ni Watanzania wangapi kwa uelewa wako wanajua kama Zitto alihongwa? Na ni muda gani ambao CHADEMA watatumia kujibu hoja za Wapinzani wa chama iwapo Zitto atamua kujitoa ufahamu?Kumbuka kila sentensi anayongea Zitto wapinzani wa CHADEMA wananote points of weakness na tambua kabisa wananchi wengi bado ni waumini wazuri wa propaganda kuliko facts. Ukichukua maamuzi ya kukurupuka tu madhara yake ni makubwa si kwa Zitto bali kwa chama kwa ujumla.
 
Mawazo yako mazuri lakini kuna kasoro moja tu! CHADEMA SIO TEGEMEO LA WANANCHI. tegemeo la wananchi ni CHAMA TAWALA.
 
Zito angekubali kuitwa john Paulo angekubalika chadema ila na uzuberi wake unatarajia nini? Chadema inamsafisasha aliyekubali kutenda makosa wazi ambaye ni dr. Kitila na kumshambulia anayetuhumiwa. Double standard inayosababisha na nguvu ya kiimani. Ni mtazamo yangu.
udini umekujaa waislam kule mtwara wamejua kuwa CCM ni majambazi wa rasilimali za nchi, miaka kumi umekula umevimbiwa ukiwa chadema ,mpaaka baba yako katakata ndio unatambua kuwa wewe ni mwislamu
 
Nadhani umetazama kiini cha tatizo ambacho kimekaa kiimani bila kutazama madhara ya maamuzi kwa mustakabali ya chama. Umakini wa kifikra unatokana na jinsi gani unatatua matatizo kinyume chake ni kukurupuka. Yawezekana kabisa ukawa na ushahidi au usiwe na ushahidi wa yote hayo unayosema, jambo unaloshindwa ni kujua madhara ya maamuzi ambayo yanatoa taswira ya mwenendo na mustakabali ya CHADEMA kama chama.

Hapa simtetei Zitto hata chambe bali natumia uwezo wa kifikra kwa kutazama athari za maamuzi kwa ukubwa wake. Ni Watanzania wangapi kwa uelewa wako wanajua kama Zitto alihongwa? Na ni muda gani ambao CHADEMA watatumia kujibu hoja za Wapinzani wa chama iwapo Zitto atamua kujitoa ufahamu?Kumbuka kila sentensi anayongea Zitto wapinzani wa CHADEMA wananote points of weakness na tambua kabisa wananchi wengi bado ni waumini wazuri wa propaganda kuliko facts. Ukichukua maamuzi ya kukurupuka tu madhara yake ni makubwa si kwa Zitto bali kwa chama kwa ujumla.

Kama CC itafanya maauzi kwa kangalia watu watasema nini umekosea I thought you were brave enough unatanguliza emotions badala ya reality uiogope kufanya maamuzi kijana
 
Nyerere sio msahafu na ukweli hakuna kinamuangamiza zito zaidi ya dini, kabila lake na kanda atokayo. Yeye mwenyewe kaligusia hilo kuwa kama mtu ananyanyaswa bila makosa ya wazi je wale wanaodhani kuna udini, ukabila au ukanda si watasema au kupata nguvu katika madai yao? Na huo ndio ukweli kwani anachoogopa zito ni kusema wazi jambo hilo.

Alidhani na anaenflea kudhani cdm haitamchukulia hatua kali kwa usaliti wake kwa kuogopa propaganda za kitoto kama hizo za ukabila na udini.mbona hujuma wakati wa uchaguzi hajazikana? Mbona mawasiliano yake na tiss na yale ya email za lukuvi,mwigulu na nchimbi? NA KUHUSU KUMUUNGA MKONO KAFULILA NA KUMHUJUMU MGOMBEA WA CHAMA CHAKE HUKU AKIWA KIONGOZI MKUBWA TENA MWENYE KUTAKA UENYEKITI,hivi ingekuwaje kama mbowe au slaa angemuunga mkono mgombea wa chama kingine na kumtosa yule wa cdm? acheni unafiki zitto hafai kuwa kiongozi wa cdm hata wa kata tu.
 
Nadhani hali inayoendelea ndani ya Cdm itakichangia kuwa imara sana kwani wagombanao ndio wapatanao. Hizi changamoto zitafanya kila upande kufuata maadili ili kuhakikisha kila upande unaridhika na hapo ndio chama kitakuwa imara sana. Minyukano hii kwa kiasi kikubwa imekuzwa na CCM ili kufaidika na madhaifu yanayojitokeza. Ila sasa ni vyema maana kila upande umejua madhaifu yake hivyo kuheshimiana kutakuwepo. Na iwapo Cdm watacheza karata zao vizuri kwa kumaliza mzozo huu na kuwa wamoja basi ujue kwa upande wa CCM mambo yatakuwa mabaya sana, kwanza wananchi wameshajua ni chama gani kinaweza kufanya maamuzi bila kusita, na pili utawafanya ccm nao kuiga maamuzi ya aina hiyo kutokana na uelewa wa wananchi. Na iwapo ccm wataiga maamuzi haya ni lazima kipasuke kwani hawana utamaduni wa maamuzi magumu kwani wameshika dola hivyo wanapoozana kwa kupeana vyeo.
 
Kama CC itafanya maauzi kwa kangalia watu watasema nini umekosea I thought you were brave enough unatanguliza emotions badala ya reality uiogope kufanya maamuzi kijana

Inawezekana umekurupuka kunijibu kwasababu umeshindwa kutambua niliandika maandishi yangu katika muktadha gani. Ili nikusaidie nilikuwa ninamjibu @kibaravumba na unaweza pitia bandiko lake hapo juu. Lakini vilvile unaweza kusoma mabandiko yangu mawili ya awali na kujua nini namaanisha.Nimezungumza wazi kabisa kwamba lazima kukubali kuwa "risk-takers" katika kujenga nidhamu na uaminifu ndani ya chama. Lakini wakati huohuo lazima ujenge internal mechanisms kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza katika kufikia malengo ya jumla ya chama kisiasa. Hii ndivyo brave people wanafanya
 
Nadhani hali inayoendelea ndani ya Cdm itakichangia kuwa imara sana kwani wagombanao ndio wapatanao. Hizi changamoto zitafanya kila upande kufuata maadili ili kuhakikisha kila upande unaridhika na hapo ndio chama kitakuwa imara sana. Minyukano hii kwa kiasi kikubwa imekuzwa na CCM ili kufaidika na madhaifu yanayojitokeza. Ila sasa ni vyema maana kila upande umejua madhaifu yake hivyo kuheshimiana kutakuwepo. Na iwapo Cdm watacheza karata zao vizuri kwa kumaliza mzozo huu na kuwa wamoja basi ujue kwa upande wa CCM mambo yatakuwa mabaya sana, kwanza wananchi wameshajua ni chama gani kinaweza kufanya maamuzi bila kusita, na pili utawafanya ccm nao kuiga maamuzi ya aina hiyo kutokana na uelewa wa wananchi. Na iwapo ccm wataiga maamuzi haya ni lazima kipasuke kwani hawana utamaduni wa maamuzi magumu kwani wameshika dola hivyo wanapoozana kwa kupeana vyeo.

tindo nakuunga mkono kwa bandiko lako hapo juu, minyukano hii ndani ya chama lazima ijengewe mazingira ya maafikiano, minyukano hii haimdhofishi Zitto pekee bali ni minyukano inayoweza kuendelea kwa muda mrefu na kupoteza focus ya chama. Maadui wa chama wako macho kutengeneza mabomu yenye lengo la kufaidika na mnyukano huu.

Itakuwa ni ufinyu wa maono kuendelea kushindana kujibu mapigo kutoka kila upande na kumfaidisha adui wa nje badala ya kumdhoofisha.
 
Tatizo kubwa kwetu ni MAPANDIZIKI. Kwa wenzetu huko Majuu, Usalama wa Taifa na vyombo vya upepelezi, hufanya ulinz wao ili kujua kama mtu anapata fedha zake kihalali au anazitoa sehemu za ajabu ajabu ili kununua Serikali. Kwetu sisi hilo halipo na ndiyo maana unaweza kuona Zitto anaishi Highlife ingawa hapokei Posho.

Ingelikuwa kwa wenzetu, tayari ukweli ungelikuwa umeshajulikana kama kweli alikuwa akilipa watu fedha. Tungelijua anaishi vipi kwa hali hiyo wakati Posho kazigomea. Kwa USA, huko ni Secret Service wangelikuwa wameshamaliza mzizi wa fitina na ikibidi hata CIA au FBI kuingilia kati. Nafikiri hata Waingereza nao wana vyombo kama hivyo vingi tu. Ingelikuwa hivyo, hata wizi wa EPA usingelifanyika na Rostam Azziz asingelikuwa mungu ndani ya CCM kwa miaka ya 2005-2010. Kwetu sisi kulazimisha Demokrasia ya West, bado sana. Labda kwanza tuboreshe vyombo vya Upelelezi.
 
Dialema?Labda ninyi 'wasomi'ndio mko njiapanda kwa kuwa kujua kwingi huondoa maarifa.Sisi tunajua,tena kwa uhakika,Zitto tangu ateuliwe tume ya Buzwagi,alinunuliwa na hadi akajengewa shule kwao na barrick gold na akawa mpole bungeni kabisa.Alichobakiza ni kuwa mpinzani wa viongozi wake.Alipoamua wazi wazi kuipigia kampeni nccr ili kafulila ashinde,Laiti ningekuwa na uwezo ningelimfutilia mbali uanachama wake aende huko nccr.Huyu ni nyoka na hatakiwi kuonewa huruma hata kidogo.Kama hahongwi anatoa wapi pesa ya kununua gari la fahari?msitwambie kitu bana huku tunaishi na mamluki wake wengi na wanatamba huwa anawapa pesa za matumizi na wanakiri wanataka nao wawe na madaraka!Hakuna anayewaza kumkomboa mwananchi kutoka kwa wakoloni weusi

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Kuna kajazba kidogo katika hoja lakini nikiri kwamba umenipa taarifa muhimu ambazo sikuwa nazo. Red inahusika sana hapo. Asante sana Mkuu. Mengi katika haya unayoniambia sikuyajua kabisa kwa kweli. Nikupe shukrani nyingi kwa kunielimisha hapa.
 
Bado naendelea kuamini kwamba mgongano huu wa kifikra kati ya wanachama wa CHADEMA dhidi ya CHADEMA kutokana na maamuzi ya kamati kuu hauzingatia utulivu wa kifikra katika kuona ukubwa na mantiki iliyopo wakati huu wa kuelekea katika mapambano makali zaidi ya kisiasa.Ni fumbo ambalo si rahisi kutegua ni nini kinaweza kutokea lakini vilevile kuthibitisha kile ambacho kinafikirika kwa manufaa ya upande mmoja dhidi ya mwingine.Kwa mtu ambaye hawezi kujenga nguvu ya kuona kwa kutumia fikra zake kuliko kile ambacho anaweza kukiona kwa macho si rahisi kukubaliana na jambo moja kubwa muhimu kwamba ni mgangano ambao haumdhoofishi Mh.Zitto tu kisiasa bali ni mgongano ambao unatengeneza uwanja mpa wa mapambano dhidi wa wanachama wa CHADEMA kwa CHADEMA.

Binafsi naamini kwamba vita ya kuongea ni mbaya sana kuliko vita ya kusikiliza. Iwapo tutajenga msingi wa kuzungumza kwa maana ya kujibu mapigo CHADEMA kwa CHADEMA kwa kutumia kejeli na dharau ni kuhalalisha kwamba bado hawamini katika nguvu ya ndoto zao kisiasa. Kwa kufanya hivyo angefungua uwanja mpya wa malumbano ambayo hayana tija kwa uhai wa chama. The Dream will remain a Dream kama hakuna michakato ya kufikia ndoto zenyewe. Lazima kuset goals ambazo zitajenga msingi imara wa kubomoa mabomu ya kipopraganda ambayo yanajengwa zidi ya CHADEMA

Lakini kwa upande mwingine CHADEMA kama chama kitapoteza rasilimani muhimu sana ambayo ni muda kujibu mapigo dhidi ya maadui kisiasa japokuwa katika misingi ya kujenga nidamu na uaminifu ndani ya chama kinapaswa kuwa “risk-takers”. Lakini ukiwa na malengo makubwa ni muhimu kupima madhara yanayoweza kujitokeza katika kufikia malengo.

Muhimu ni kujenga utashi wa kifikra na kujenga msingi na mtazamo mpya kuelekea mafanikio makubwa zaidi ya kisiasa.

Mbelwa Germano
Lushoto Constituent

Nimependa sana maeneo niliyoweka rangi. Pamoja na ku-beat around the bush kwa kiasi fulani lakini pamejitokeza viashiria vinavoonesha kuwa mimi na wewe tunakubaliana. Blu zinahusika hapo. Asante.
 
Bwana Highlander,pamoja na mawazo yako mazuri ya kuelimisha,naomba nikuulize swali moja:
Wakati Zitto anaenda kujibu tuhuma pale Serena hotel;ukumbi ule ambao angeutumia Zitto kujibu mapigo,uliandaliwa na kupambwa na Stellah Mwampamba na baadhi ya vijana wa ccm;---- uhusiano gani hapo?

mimi sikuhudhuria mkutano huo, ingawa wapashaji habari wangu wamesema fikra za zitto nyingi zilitolewa na kituo FRONT COMPANY cha CCM kinachoitwa CLOUDS FM. Kwa hiyo upo uwezekano mkubwa kwamba unachokiona wewe ni sahihi. Lakini, pamoja na mimi kutokuwa mwanasiasa, bado naona ipo haja ya kuweka muda wa kutosha kumwacha mtu ajinyonge. Unapotoa hotuba zako kwenye kituo cha propaganza za chama ambacho kinajulikana kuwa ni FRONT company ya propaganda za chama fulani, tayari unaji-associate na chama hicho. Kama kweli eneo la Mkutano liliandaliwa na kulindwa na vijana wa chama pinzani, hilo pia ni association ya wazi.

Lakini je, unamfukuza mke kwa mtindo upi kama unajua kuna mtu anasubiri kufaidika na taraka hiyo? Utasema toka sasa hivi? au utamsumbua kisaikolojia kujitia bado mkeo ili tu wakijifungia ndani awe anakosa raha kumfanya akidhani bado unaye?

Kama unachokisema kinaonesha association za wazi-wazi kati cha Zitto na hao ambao ametuhumiwa kwa muda mrefu kuwa na association nao, basi Ningependa niunge mkono fikra za Kamati kuu kuchezea saikolojia ya Zitto na CCM. Basi Kamati Kuu inacheza karata zake vizuri. CCM na Zitto mwenyewe watakuwa hawana akili tosha kujua kwamba kinachotolewa hapo ni kamba ndefu ya kujinyonga nayo Zitto--yaani kama hilo unalolisema na hizo taarifa nimepewa jana na washikazi zangu ni kweli. Kamati Kuu itakuwa imecheza karata zake vizuri to lead the 'w.ho.re' into more vivid exposure!

Yeye atakuwa anadhani kwa kufanya hivyo anawatangazia umma kuwa ana mahali pa kuenda. Ukweli ni kwamba atakuwa amewatangazia watanzania kwamba yote yalikuwa yanasemwa nyuma kuhusu yeye kuwa mamluki yalikuwa kweli.
 
Yaani kamati kuu yote wakiwemo Prof. Baregu, Prof. Safari na Mabere Marando wamefuta mkubo tu na kuburuzwa ili kumuweka Zitto hatiani? Sidhani. Zitto alijua nini kilikuwa kinaendelea na Dr. Mkumbo amejitolea tu kumkingia kifua Zitto. Tusubiri tutasikia mengi kuhuu hili sakata. Zitto ana mazuri yake lakini ana udhaifu wake pia-Haeleweki vizuri kimsimamo.
 
kwa hoja zako ZZK yuko katika umamluki mkubwa, hongera kwa kutufumbua macho zaidi. maana associates wake ndo hao wapinzani wa CDM, anaongea nao nini ndo hizo nyaraka, na anafadhiliwaje ndo hizo romours
 
Yaani kamati kuu yote wakiwemo Prof. Baregu, Prof. Safari na Mabere Marando wamefuta mkubo tu na kuburuzwa ili kumuweka Zitto hatiani? Sidhani. Zitto alijua nini kilikuwa kinaendelea na Dr. Mkumbo amejitolea tu kumkingia kifua Zitto. Tusubiri tutasikia mengi kuhuu hili sakata. Zitto ana mazuri yake lakini ana udhaifu wake pia-Haeleweki vizuri kimsimamo.

naamini hivyo pia. yapo!
 
Zito angekubali kuitwa john Paulo angekubalika chadema ila na uzuberi wake unatarajia nini? Chadema inamsafisasha aliyekubali kutenda makosa wazi ambaye ni dr. Kitila na kumshambulia anayetuhumiwa. Double standard inayosababisha na nguvu ya kiimani. Ni mtazamo yangu.
Aa wapi!!! Hapa hakuna udini wala ndugu yake udini. Mambo yako wazi! Kosa ni undumilakuwili na rushwa!! Pole kwa kununuliwa na Mwigulu!
 
Inawezekana umekurupuka kunijibu kwasababu umeshindwa kutambua niliandika maandishi yangu katika muktadha gani. Ili nikusaidie nilikuwa ninamjibu @kibaravumba na unaweza pitia bandiko lake hapo juu. Lakini vilvile unaweza kusoma mabandiko yangu mawili ya awali na kujua nini namaanisha.Nimezungumza wazi kabisa kwamba lazima kukubali kuwa "risk-takers" katika kujenga nidhamu na uaminifu ndani ya chama. Lakini wakati huohuo lazima ujenge internal mechanisms kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza katika kufikia malengo ya jumla ya chama kisiasa. Hii ndivyo brave people wanafanya

Napishana na wewe kwa sababu wewe unataka kupanua dhana ya kulindana Kwa mfano Zito ni mtu ambaye amekaa kati na kuanzisha mtandao ndani ya chama rejea kesi ya masalia yaani ameedelea kuanzisha chama kingine ndani ya chama mtu kama si wakuogopa na wakuzabwa na kusimashwa hila zke papo
 
Back
Top Bottom