Pengine Zitto hana kosa....

Pengine Zitto hana kosa....

nnyakyala uko juu pia nikuongezee serena hotel garama za pale hotel ya nyota tano katoa nani hv alishindwa kwenda ofis yake kuongea mpaka aende serena hotel?kuna jamaa yangu anafanya kazi serena kaniambia vikao vyA chukuachako mapema hufanyka pale na kabla ya tukio walionekana eakisema wakubwa ngoja tumsafishe dogo kwisha hbr yake mjingasana yule.
 
foolish wewe chamviga.udini udini. so low! pambaf
 
Nilitegemea sana kuwa Zitto Kabwe angekuwa mtu wa kwanza kuwanyoshea kidole wale walioandaa waraka wa siri wa mabadiliko bila kumuhusisha nakumweka kwenye hali tata aliyonayo na chama cha CHADEMA. Nasema hivi kwa misingi ya kile kinachosemwa kuwa - imedaiwa hakuhusika na hakujua lolote kuhusu huo waraka. Kwa mantiki za kikawaida alitakiwa amutuhumu kwa nguvu zote Dr.Kitila na wenzake kwa hilo la uandaaji wa waraka unaomuhusu bila ridhaa yake. Kinachoonekana yeye Zitto anaungana na kundi la Kitila katika kuushutumu uongozi wa chama kwa hatua zilizochukuliwa. Iweje mtu makini ukubaliane kirahisirahisi vile na kundi la watu (hata kama ni rafiki zako) walioandaa waraka unaokutumbukiza kwenye matatizo bila kukupa taarifa kabla? Kuna siri gani hapo?!!!!!!
 
Zzk ni MM sasa connect dots hapo mipango ifanywe bila mkuu kujua itawezekana?Yuda kakamatwa pabaya..
 
Nilitegemea sana kuwa Zitto Kabwe angekuwa mtu wa kwanza kuwanyoshea kidole wale walioandaa waraka wa siri wa mabadiliko bila kumuhusisha nakumweka kwenye hali tata aliyonayo na chama cha CHADEMA. Nasema hivi kwa misingi ya kile kinachosemwa kuwa - imedaiwa hakuhusika na hakujua lolote kuhusu huo waraka. Kwa mantiki za kikawaida alitakiwa amutuhumu kwa nguvu zote Dr.Kitila na wenzake kwa hilo la uandaaji wa waraka unaomuhusu bila ridhaa yake. Kinachoonekana yeye Zitto anaungana na kundi la Kitila katika kuushutumu uongozi wa chama kwa hatua zilizochukuliwa. Iweje mtu makini ukubaliane kirahisirahisi vile na kundi la watu (hata kama ni rafiki zako) walioandaa waraka unaokutumbukiza kwenye matatizo bila kukupa taarifa kabla? Kuna siri gani hapo?!!!!!!

Ndani ya cc Kitila mwenyewe alikiri kufahamu kila kitu na ndiye alimtaja Zitto.
Sasa na wewe unadhani Zitto hakuhusika? Zitto huyo huyo alihusika kwa akina Shonza na Stella Mwampamba katika PM7 ni msaliti mzoefu. Afukuzwe kabisa katika chama!
 
Zito angekubali kuitwa john Paulo angekubalika chadema ila na uzuberi wake unatarajia nini? Chadema inamsafisasha aliyekubali kutenda makosa wazi ambaye ni dr. Kitila na kumshambulia anayetuhumiwa. Double standard inayosababisha na nguvu ya kiimani. Ni mtazamo yangu.
Mtazamo wako ni FINYU sana.Una ELIMU gani ndugu?
 
Nimewiwa kumtetea Zitto Kabwe na Freeman Mbowe na Dk. Wilbrod Slaa. Nina mashaka sana hakuna mwenye makosa, na kwamba tunachokiona kama machafuko katika CHADEMA katika hizi siku mbili tatu unaweza uwe ni mgongano tu wa taaluma mbili ndani ya Chama.

Kama Zitto Kabwe alipata Elimu ya Political Economy pale Chuo Kikuu Mlimani au kwingineko, yeye ni Mwanasiasa wa Kusomea. Sifa za Wanasiasa duniani zinajulikana. Ni watu wa kutafuta sifa, kujikweza na kutaka dunia nzima isikie na kujua kwa uhakika ni kipi hasa walichofanya.

Kwa hiyo Siwezi kushangaa kama nitasikia Zitto Kabwe akijisifia kupandisha bendera ya CHADEMA akiwa na umri wa miaka 16. Huyu ni mwanasiasa wa kusomea, na hapo atakuwa anafanya siasa kadri ya mafunzo yake.

Nasita kumzungumzia sana Dk. Kitila Mkumbo kwa kuwa hakuna ninachokijua zaidi ya kwamba ni Mwalimu wa Chuo Kikuu. Lakini wote tunajua huwezi kumtenga sana mwalimu na siasa kwa kuwa hii ni taaluma inayohusu kujieleza, na mwanasiasa sharti ajue kujieleza. Kwa hiyo naomba nimwite Dk, Kitila Mkumbo kuwa na yeye ni mwanasiasa wa kusomea.

Nitamjadili zaidi Zitto Kabwe hapa kwa sababu mzozo unaoonekana kuwapo katika CHADEMA leo unaonekana kuwahusu zaidi watu wawili hata kama wengine wameingizwa humo: huu mgogoro unamhusu Zitto Kabwe na Freeman Mbowe.

Freeman Mbowe ni Mfanyabiashara kama mimi, japokuwa tunapishana viwango kwa mbali kama ardhi na nyota. Lakini ndege ni ndege tu—awe analala katika banda au kwenye mti; watakuwa na mambo yanafanana.

Sisi wafanyabiashara huwa tahupendi urasimu. We are doers. Kikao cha familia kikishakubaliana kuwa tunataka duka lijengwe hivi mahali, lipakwe rangi hii, tuweke nondo kwenye madirisha. Kitu cha muhimu ambacho huwa kinabakia hapo huwa ni results! Siyo Nani katoa hela, zilitoka saa ngapi, mkono gani ulizishika wakati zinatoka na upuuzi mwingine wa kuchelewesha results.

Nimeamka mapema sana leo kuandika mawazo haya kwa sababu sitaki kuona ugomvi katika CHAMA tegemeo la wananchi baada ya “CHAMA kaka” kuharibiwa. Pengine ni kweli Mbowe kafanya unilateral decisions katika mambo yanahusu fedha. Naamini hilo litakuwa lilifanywa kuharakisha results. Urasimu una desturi ya kuchelewesha sana results. Nionavyo mimi Chama kimefanya mambo mengi sana mazuri na kuna mafanikio makubwa yamefikiwa na yanaonekana hadi hapa tulipo chini ya uongozi wa Mbowe.

Tatizo ni kwamba mambo yanayofanywa na fedha za chama hayajapeleka sifa kwa kila mwanasiasa ambaye angependa fedha za CHAMA zitumike kumpa sifa na yeye pia. Hapa kuna tatizo la sifa!

Naamini Mbowe hajaiba fedha CHADEMA kama kambi ya Zitto inavyotuhumu. Naamini kinachoelezwa kuwa udikteta wa Freeman Mbowe katika CHADEMA ni mgongano wa mitizamo ya utendaji unaojitokeza kutokana na taaluma mbili kugongana. Zitto Kabwe angependa kila kinachotendeka kilete sifa kwake pia. KInachotendeka pale katika chama kinaleta sifa kwa mtu mmoja tu anayeamua kipi kifanyike.

Inawezekana kabisa ni kweli Mbowe anafanya maamuzi ya kiimla. Wafanyabiashara wengi wapo hivyo mara nyingi kwa sababu ya kuwahi kukamilisha lengo. Tupo Goal Oriented. Na ni rahisi sana kuwakwaza watu katika mazingira hayo kutokana na sifa za manunuzi say ya pikipiki zinunuliwe wapi kutokumpatia sifa na Zitto Kabwe. Maswali ambayo napenda kusikia wanaCHADEMA wakiuliza ni haya: Mbowe kaiba Sh. Ngapi? La pili likiwa hili: kwamba ni kitu gani katika manunuzi ya CHAMA kilipangwa kufanywa ili kufaidisha chama hakijafanywa na kufaidisha chama?

Hoja ya Umamluki wa Zitto nayo inaweza kupata maelezo: kwamba taaluma ya upelelezi tangu mwanzo wa historia ya binadamu imehusu neno moja tu katika lugha ya Kiingereza--neo EMBED.

Ku-embed ni kupandikiza mtu miongoni mwa jamii inayopelelezwa kwa namna ya kumwezesha kuonekana ni mmoja wao. Mpelelezi anayefaulu katika kazi yake ni yule anayemudu ku-embed mwenyewe, au kwa kuwezeshwa. Kwa maana hiyo, mpelelezi mzuri atazungumza lugha ya wenyeji, atavaa mavazi ya wenyeji, atakula chakula cha wenyeji, atafanya biashara kama wenyeji, hata atazaa na wenyeji, atakuwa mmoja wao, ataishi kama wao. Kumtambua mpelelezi aliye-embed vizuri ni ngumu sana. Unaweza usijue milele yote. Kwa wale waliosoma Biblia mifano ni mingi mule, mzuri kuliko yote ukiwa mfano wa Mpelelezi Delila, ambaye alitumia mbinu inayoitwa “honey trap” kumpeleleza Samsoni kwa niaba ya Wafilisti.

Waliobobea katika taalum ya upelelezi watasema njia pekee ya kumtambua mpelelezi miongoni mwenu ni kusoma “associations zake” nje yenu. Associations za nje ni mahusiano yake na watu waliopo nje ya kundi lenu. Kwa hiyo mtatizama mahusiano yake na watu kitaaluma, kidini, kimapenzi, kibiashara, kimichezo kwa namna iwayo yote itayoweza kutoa picha ya associations za suspect.

Mkipata undani wa hizo associations zake sasa mtasikiliza huwa anasema nini anapokutana na hao watu katika associations zake kwa siri. Mtamsikiliza kwa kutumia njia halali au njia haramu; au vyote kwa pamoja ikibidi. Kujua sana ilani za chama, na katiba zake, na sera zake, na historia yake, SI sababu tosha kumtoa mtu kwenye list ya mapandikizi. Pandikizi anatakiwa kuvijua vyote katika chama anachokipeleleza, sawasawa kabisa na shetani anavyojua vifungu katika Biblia.

Ili kujua kama Zitto ni Jasusi wa CCM, labda sasa CHADEMA watuambie waliupata wapi huu waraka unaoitwa mpango wa hujuma. Je waliupata kwenye Kambi ya CCM? Je waliupata kwenye associations zake nje ya chama?

Mwisho napenda kuwasihi WANACHADEMA kukubali kwamba pengine Zitto hana makosa. Na kama huu ndo ukweli, basi naomba Mbowe na Dk. Slaa watoe majibu ya haraka kuhusu kila alicholalamikia Zitto.

Achana na upuuzi wako.
Chadema sio Mbowe wala Slaa au Zitto. Vikao vya chama vikifanya maamuzi yawe ya makosa au sio makosa inabidi yaheshimiwe. Kamati kuu sio Mbowe na Slaa , kuna watu wengi wenye akili timamu.
Sisi tusiokuwa mashabiki wa watu tunaona hizi hatua zilizochukuliwa zitatia watu adabu wanajiona wako juu ya chama.
Msifanye tafukuri za kijinga hapa. Chadema sio kilabu ya pombe ya kila mnywwaji anabwatuka kivyake.
Chama makini usimamia maamuzi yake hata kama yana kosa
 
mh! OK. point noted...
 
kwanini unadownplay madhara ya sifa..na kuruhusu uncertainity kwa kiasi hichi.Haupo hata sure kw akile unachoandika.

HIvi unajua sifa hupersonalize national issues,hata maisha ya watu wengine..?
 
Bwana Highlander,pamoja na mawazo yako mazuri ya kuelimisha,naomba nikuulize swali moja:
Wakati Zitto anaenda kujibu tuhuma pale Serena hotel;ukumbi ule ambao angeutumia Zitto kujibu mapigo,uliandaliwa na kupambwa na Stellah Mwampamba na baadhi ya vijana wa ccm;---- uhusiano gani hapo?
Zito anaonekana kuchanganyikiwa ndio maana nafanya very silly decisions kama ya kuwa-flanked by defiant group of masalia type. Mentors wake wamshauri to remain dumb until his defense is delivered. When the decision is made he will have comfortable space to hit what he purports to be an unguided missile. (sic) Otherwise he is strategically committing political suicide.
 
[h=1]Mwanangu anatumiwa – Mama Zitto[/h]
maalum.jpg

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 18 November 2009

163

Features

salum_1.jpg

SHIDA Salum, mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA), Zitto Kabwe, ameibuka na kusema mwanaye anatumiwa kukivuruga chama chake.
Akizungumzia taarifa zinazoandikwa na baadhi ya magazeti kuhusu kinachoitwa mgogoro wa uongozi katika CHADEMA, kati ya Zitto na viongozi wenzake, Shida alisema, “hakuna mgogoro pale, kuna kikundi cha watu wanaotaka kumtumia mwanangu kufanikisha mambo yao.”
Akizungumza na gazeti hili juzi jijini Dar es Salaam, alidai kuna watu walio nje ya CHADEMA wanakula njama za kumgombanisha mwanawe na viongozi wenzake.
Alisisitiza, “kuna baadhi ya wanasiasa ndani ya CHADEMA wanaotumiwa na walio nje kugombanisha viongozi.”
Akaongeza, “Mambo ya uchaguzi yalikwisha kitambo na Zitto kwa moyo mmoja alikubali kumaliza tofauti zake na Mbowe (Freeman Mbowe) ndiyo maana akamuacha Mbowe kuwa mgombee pekee wa uenyekiti.”
Shida aliwatuhumu watu walio nje ya CHADEMA akisema ndio wanaopandikiza mbegu za chuki kwa lengo la kuwavuruga. Hata hivyo, hakuwataja.
Alisema kila mwenye akili timamu anajua kinachotafutwa, na nani mkweli na yupi anasingiziwa.
“Angalia wanaoandika haya. Kweli Zitto anaweza kutetewa na magazeti ya Habari Corporation yanayomilikiwa na Rostam Aziz halafu ukaamini kile kinachoandikwa?” alihoji.
Aliongeza, “Rostam yupi? Ni huyu tunayemjua au mwingine? Kwa wema upi alionao kwa chama chetu.”
Wiki iliyopita magazeti ya Rai na Mtanzania yalinukuu taarifa zikidai kuwa zimetolewa na Shida, kwamba anataka mwanawe aondoke kwenye chama hicho kwa kile ilichoeleza kuwa “kumwepuesha na yaliyomkuta Chacha Wangwe.”
Katika kujibu hilo, Shida anasema, “Mimi na Zitto tunajua katiba ya chama chetu. Tunafahamu taratibu za kuendesha chama. Yeye ni naibu katibu mkuu, mimi ni mjumbe wa Kamati Kuu. Tunajua nini maana ya uongozi, hivyo hatuwezi kukurupuka barabarani.
“Kwamba kama kuna malalamiko au tuhuma mathalani juu ya uteuzi wa wabunge wa viti maalum, basi sote ni sehemu ya hicho kinacholalamikiwa. Kutokana na hali hiyo, hatuwezi kujifanya hatuhusiki na tukatuhumu kupitia vyombo vya habari, tena magazeti yanayomilikiwa na mwanachama wa CCM.”
Shida alisema anajua kwa mapana chanzo cha yote yanayoandikwa na jitihada za kutaka kumgombanisha Zitto na viongozi wenzake, hasa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.
“Yote haya tunafahamu chazo chake. Si uchaguzi wa ndani ya chama. Uchaguzi ulishakwisha na Zitto kwa moyo mmoja alikubali kumuachia Mbowe uenyekiti ili kulinda maslahi ya chama,” alisema.
Alisema kuwa yeye kama mlezi, hawezi kuruhusu hali hiyo, hivyo atatumia nafasi yake ya mjumbe wa CC kuhakikisha kwamba tabia hiyo ya kugombanisha viongozi inakoma.
“Nikiwa mzazi, mlezi na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, siwezi kuruhusu Zitto kutumika kuingiza chama katika mgogoro. Nitasimama imara kuhakikisha kwamba CHADEMA inakuwa salama,” alisema.
Wiki iliyopita, Dk. Slaa aliwaondoa katika nafasi za utendaji David Kafulila aliyekuwa Afisa Habari na Danda Juju aliyekuwa Afisa anayeshughulika na Halmashauri na Bunge kwa kile kinachoelezwa kuwa utovu wa nidhamu kwa chama na viongozi wake.
Kafulila alinukuliwa na baadhi ya magazeti kuwa alibeza kikao cha viongozi wa juu wa chama hicho kilichofanyika Dodoma ambapo Mbowe na Dk. Slaa walikutana katika kikao cha kawaida na wabunge wa chama hicho na baadhi ya wakurugenzi.
Kafulila alisema mkutano huo wa viongozi haukuwa na maana; na alifika mbali zaidi kwa kuufananisha na vikao vya geto. Ni matamshi hayo na mengine yaliyomfanya Dk. Slaa kutumia mamlaka yake ya kikatiba kumuondoa Kafulila katika wadhifa huo.
Taarifa zinasema hoja ya kumuondoa Kafulila katika kikao ilitolewa na Msafiri Mtemelwa, mmoja wa viongozi wake na ambaye alikuwa meneja wa kampeni za Zitto wakati wa kuwania uenyekiti wa CHADEMA.
 
Zito anaonekana kuchanganyikiwa ndio maana nafanya very silly decisions kama ya kuwa-flanked by defiant group of masalia type. Mentors wake wamshauri to remain dumb until his defense is delivered. When the decision is made he will have comfortable space to hit what he purports to be an unguided missile. (sic) Otherwise he is strategically committing political suicide.
You are quite right brother Kapongoliso.Let him learn from your point.
 
Nimewiwa kumtetea Zitto Kabwe na Freeman Mbowe na Dk. Wilbrod Slaa. Nina mashaka sana hakuna mwenye makosa, na kwamba tunachokiona kama machafuko katika CHADEMA katika hizi siku mbili tatu unaweza uwe ni mgongano tu wa taaluma mbili ndani ya Chama.

Kama Zitto Kabwe alipata Elimu ya Political Economy pale Chuo Kikuu Mlimani au kwingineko, yeye ni Mwanasiasa wa Kusomea. Sifa za Wanasiasa duniani zinajulikana. Ni watu wa kutafuta sifa, kujikweza na kutaka dunia nzima isikie na kujua kwa uhakika ni kipi hasa walichofanya.

Kwa hiyo Siwezi kushangaa kama nitasikia Zitto Kabwe akijisifia kupandisha bendera ya CHADEMA akiwa na umri wa miaka 16. Huyu ni mwanasiasa wa kusomea, na hapo atakuwa anafanya siasa kadri ya mafunzo yake.

Nasita kumzungumzia sana Dk. Kitila Mkumbo kwa kuwa hakuna ninachokijua zaidi ya kwamba ni Mwalimu wa Chuo Kikuu. Lakini wote tunajua huwezi kumtenga sana mwalimu na siasa kwa kuwa hii ni taaluma inayohusu kujieleza, na mwanasiasa sharti ajue kujieleza. Kwa hiyo naomba nimwite Dk, Kitila Mkumbo kuwa na yeye ni mwanasiasa wa kusomea.

Nitamjadili zaidi Zitto Kabwe hapa kwa sababu mzozo unaoonekana kuwapo katika CHADEMA leo unaonekana kuwahusu zaidi watu wawili hata kama wengine wameingizwa humo: huu mgogoro unamhusu Zitto Kabwe na Freeman Mbowe.

Freeman Mbowe ni Mfanyabiashara kama mimi, japokuwa tunapishana viwango kwa mbali kama ardhi na nyota. Lakini ndege ni ndege tu—awe analala katika banda au kwenye mti; watakuwa na mambo yanafanana.

Sisi wafanyabiashara huwa tahupendi urasimu. We are doers. Kikao cha familia kikishakubaliana kuwa tunataka duka lijengwe hivi mahali, lipakwe rangi hii, tuweke nondo kwenye madirisha. Kitu cha muhimu ambacho huwa kinabakia hapo huwa ni results! Siyo Nani katoa hela, zilitoka saa ngapi, mkono gani ulizishika wakati zinatoka na upuuzi mwingine wa kuchelewesha results.

Nimeamka mapema sana leo kuandika mawazo haya kwa sababu sitaki kuona ugomvi katika CHAMA tegemeo la wananchi baada ya “CHAMA kaka” kuharibiwa. Pengine ni kweli Mbowe kafanya unilateral decisions katika mambo yanahusu fedha. Naamini hilo litakuwa lilifanywa kuharakisha results. Urasimu una desturi ya kuchelewesha sana results. Nionavyo mimi Chama kimefanya mambo mengi sana mazuri na kuna mafanikio makubwa yamefikiwa na yanaonekana hadi hapa tulipo chini ya uongozi wa Mbowe.

Tatizo ni kwamba mambo yanayofanywa na fedha za chama hayajapeleka sifa kwa kila mwanasiasa ambaye angependa fedha za CHAMA zitumike kumpa sifa na yeye pia. Hapa kuna tatizo la sifa!

Naamini Mbowe hajaiba fedha CHADEMA kama kambi ya Zitto inavyotuhumu. Naamini kinachoelezwa kuwa udikteta wa Freeman Mbowe katika CHADEMA ni mgongano wa mitizamo ya utendaji unaojitokeza kutokana na taaluma mbili kugongana. Zitto Kabwe angependa kila kinachotendeka kilete sifa kwake pia. KInachotendeka pale katika chama kinaleta sifa kwa mtu mmoja tu anayeamua kipi kifanyike.

Inawezekana kabisa ni kweli Mbowe anafanya maamuzi ya kiimla. Wafanyabiashara wengi wapo hivyo mara nyingi kwa sababu ya kuwahi kukamilisha lengo. Tupo Goal Oriented. Na ni rahisi sana kuwakwaza watu katika mazingira hayo kutokana na sifa za manunuzi say ya pikipiki zinunuliwe wapi kutokumpatia sifa na Zitto Kabwe. Maswali ambayo napenda kusikia wanaCHADEMA wakiuliza ni haya: Mbowe kaiba Sh. Ngapi? La pili likiwa hili: kwamba ni kitu gani katika manunuzi ya CHAMA kilipangwa kufanywa ili kufaidisha chama hakijafanywa na kufaidisha chama?

Hoja ya Umamluki wa Zitto nayo inaweza kupata maelezo: kwamba taaluma ya upelelezi tangu mwanzo wa historia ya binadamu imehusu neno moja tu katika lugha ya Kiingereza--neo EMBED.

Ku-embed ni kupandikiza mtu miongoni mwa jamii inayopelelezwa kwa namna ya kumwezesha kuonekana ni mmoja wao. Mpelelezi anayefaulu katika kazi yake ni yule anayemudu ku-embed mwenyewe, au kwa kuwezeshwa. Kwa maana hiyo, mpelelezi mzuri atazungumza lugha ya wenyeji, atavaa mavazi ya wenyeji, atakula chakula cha wenyeji, atafanya biashara kama wenyeji, hata atazaa na wenyeji, atakuwa mmoja wao, ataishi kama wao. Kumtambua mpelelezi aliye-embed vizuri ni ngumu sana. Unaweza usijue milele yote. Kwa wale waliosoma Biblia mifano ni mingi mule, mzuri kuliko yote ukiwa mfano wa Mpelelezi Delila, ambaye alitumia mbinu inayoitwa “honey trap” kumpeleleza Samsoni kwa niaba ya Wafilisti.

Waliobobea katika taalum ya upelelezi watasema njia pekee ya kumtambua mpelelezi miongoni mwenu ni kusoma “associations zake” nje yenu. Associations za nje ni mahusiano yake na watu waliopo nje ya kundi lenu. Kwa hiyo mtatizama mahusiano yake na watu kitaaluma, kidini, kimapenzi, kibiashara, kimichezo kwa namna iwayo yote itayoweza kutoa picha ya associations za suspect.

Mkipata undani wa hizo associations zake sasa mtasikiliza huwa anasema nini anapokutana na hao watu katika associations zake kwa siri. Mtamsikiliza kwa kutumia njia halali au njia haramu; au vyote kwa pamoja ikibidi. Kujua sana ilani za chama, na katiba zake, na sera zake, na historia yake, SI sababu tosha kumtoa mtu kwenye list ya mapandikizi. Pandikizi anatakiwa kuvijua vyote katika chama anachokipeleleza, sawasawa kabisa na shetani anavyojua vifungu katika Biblia.

Ili kujua kama Zitto ni Jasusi wa CCM, labda sasa CHADEMA watuambie waliupata wapi huu waraka unaoitwa mpango wa hujuma. Je waliupata kwenye Kambi ya CCM? Je waliupata kwenye associations zake nje ya chama?

Mwisho napenda kuwasihi WANACHADEMA kukubali kwamba pengine Zitto hana makosa. Na kama huu ndo ukweli, basi naomba Mbowe na Dk. Slaa watoe majibu ya haraka kuhusu kila alicholalamikia Zitto.

Mkuu umeanza uchambuzi wako vizuri na hata ukaonekana kufanikiwa kujenga hoja na kuoneka kuwa balanced lakini mwisho conclusion yako kama vile imekuumbua, imeweka wazi hoja yako kuwa yale mengine yote ilikuwa tu kuipaka qunini sukari. your conclusion does not logically follow from your analysis unless you ommitted something ..
 
WANANCHII wote waliokuwa wanafatitilia kipindi ndani ya startv na kupiga simu wameonyesha mashaka makubwa juu ya maamuzi ya kamati kuu kwamba yalipaswa vilevile yatumie busara na hekima.

MH ZITTO ni jembe hivyo inapaswa wawe makini na decision yoyote wanayoiendea. Wananchi wote waliopiga simu wanampa sapoti kubwa Mh. Zitto
 
Slaa katoa amri swala hili lisijadiliwe, lakini Godbless Lema na viongozi wengine wamepuuzia amri hiyo ya Slaa...
 
Habari wakuu,

Ingawa mimi si mwandishi wa habari na wala sifahama mambo mengi kuhusu taaluma hiyo lakini ninaamini katibu mkuu wa jukwaa la wahariri ndugu Neviel Meena amepotoaka ama kwa bahati mbaya au hata kwa makusudi.Kwa wasiofahamu Meena ndio mhariri wa gazeti la Mwananchi.

Kwa kifupi,leo katika kipindi cha Jicho letu ndani ya habari kinachorushwa na Star tv,Meena alikuwa ni mmoja wa wahariri walioalikwa sambamba na mhariri wa gazeti la Tanzania Daima,ndugu Anserbet Ngurumo.Katika majadilioni liliibuka swala la mh.Zitto kutokuhudhuria kikao ambacho kilimvua madaraka ambapo wahariri hao wote wawili walieleza kuwa Zitto hakuwepo kwenye kikao hicho tangu siku ya kwanza bali walieleza kuwa alifika siku ya pili saa mbili usiku wakati kikao kinaendelea.Meena alisema magazeti yaliandika kuwa mh.Zitto alifika saa 2:26 usiku na kuendelea na kikao mpaka usiku kabisa.

Baada ya maelezo hayo na mengine,muendesha kipindi kutoka Star tv ndugu Dotto aliruhusu simu kutoka kwa watazamaji na ndipo mwananchi mmoja akahoji inakuwaje wahariri hao wanasema Zitto hakuwepo bila kutoa sababu ya Zitto kutokuhudhuria.Ikumbukwe kuwa Zitto alikuwa nje kikazi kama mwenyekiti wa PAC na wahariri hao wanafahamu hilo.

Cha kushangaza jibu alilotoa Meena ni kuwa ilikuwa sio muhimu kwa wao kusema kuwa Zitto alikuwa wapi(kwa maneno mengine,haikuwa muhimu kwake
kuujulisha umma sababu ya Zitto kutokuwepo wakati kikao kinaanza)!

Hivi kweli hii kauli ni sahihi?

Kumbukeni hapa hoja kubwa ilikuwa ni Zitto kutoshiriki katika vikao mbalimbali vya chama na hata kwenye mikutano ya chama chake.

Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Simtetei Zitto lakini kwa kauli hii Meena amepotoka tena sio kidogo.
 
Back
Top Bottom