Pengine serikali ya CCM imechanganyikiwa

Hii inaitwa political surprising, wakati mikataba ya bandari inasainiwa wakati ilileta mkwaruro wa kutojulikana ukomo wake, tayari ukomo umewekwa. Ili kuchanganya watu wagawanyike kuchambua mambo, uteuzi wa makonda aliyezua gumzo awamu ile ukachomekewa paaaa kimkakati. Haya wale dp waende kule na wa makonda waje huku, that is devide and rule. Jambo moja hufunika jingine muda upite maisha yaendelee
 
Mkuu alihitajika mtu kama Makonda kufufua chama maana Chama kililoose popularity na wanachama walipungua kwa 30%
So lazma warudishe watu kama makonda kwenye system
Magufuli alipoingia tuliambiwa kabla yake watu walikuwa wanaogopa kuvaa nguo za CCM ila ameifufua. Haya na sasa tunaambiwa tena Makonda ndiyo anakuja kuifufua. Hizi ni dalili za kuwa CCM iko kwenye siku zake za mwisho. Najua kwa ufinyu wa akili zako unaweza usione hili lakini muda utaamua.
 
Ila yupo vizuri katika amsha amsha kupitia hilo domo lake.

Daudi yupo vizuri ktk kutumia 🔫 tu na polccm guard, mambo ya amsha amsha kwa domo lake hawezi, hivyo uenezi hawezi domo zege huyo.
Anaamsha amsha wajinga wajinga ambao wako wengi sana kwenye mitaa ya Tanzania. Ule ujinga wa kufanya mambo bila kutumia akili huyu ni bingwa. Leo atashika suala la wajane, kesho atashika suala la vibaka, keshokutwa atashika suala la tezi dume... yaani ujinga ambao hauna matokeo yoyote bali unazidisha tatizo na kutumia muda na fedha bila matokeo. Bahati mbaya ni kuwa huwezi kuwadanganya watu muda wote.. kuna siku itafika...
 
Ilo najua mkuu na ndo maana makonda kawekwa ili kurudisha kidgo heshima..watu wamerudisha sana kadi...Zaidi ya kadi 20k zimerudishwa...
 
Hayo ndiyo malengo ya CCM, ila wananchi wajinga wanazidi kupungua so ipo siku watakosa wa kumdanganya.
 
MENEMENE TEKERI NA PERESI.
 
Watajua hawajui

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili sula la bandari mimi naona madhara yatasambaa na kusababisha mambo mengine mabaya zaidi. 1. Bandari itakuwa uchochoro wa kupitisha raslimali zetu kwa wingi sana 2. Waarabu hawatataka kabisa rais yoyote aongozi Tanzania bali watahakikisha rais fisadi wanayemtaka wao ataingia, hivyo watahakikishia suala la katiba linafanyika kulingana na matakwa yao.
 
Ilo najua mkuu na ndo maana makonda kawekwa ili kurudisha kidgo heshima..watu wamerudisha sana kadi...Zaidi ya kadi 20k zimerudishwa...
Sasa wewe kweli unaona Makonda ndiye kiongozi wa kurudisha heshima? Makonda anakwenda kuiporomosha zaidi. BTW kadi za vyama hazina uhusiano wowote na kuridhika kwa wananchi. Hata uwape kadi wananchi wote wa Tanzania bila kuboresha maisha ni bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…