chikutentema
JF-Expert Member
- Dec 10, 2012
- 7,730
- 5,013
CDM hatupeani vyeo kama Maccm mlivyo
Sawa mkuu.Nitakuwa makini.
Teh teh teh teh! When fools argue, joining in may be foolish too.
kweli awe Mosha au mboya
genius Brain,
Kwanini unapenda kuzusha kitu ambacho unajua ni cha uongo?Mods wakithibitisha hiyo ID ni yangu basi wanipige Ban.
-Kwenye mada:Asanteni
Hujui chochote wewe kauzu.Sasa na wewe umeandika nini tena? Yale yale ya Matola!
"When fools argue, joining in may foolish you too". Nadhani umeelewa sasa.
CC: Boko haramu, THE BIG SHOW, nk
Hujui chochote wewe kauzu.
Kamanda nani kakundanganya kuwa uchaguzi unakaribia Chadema?
Uchaguzi bado sana kwa mujibu wa Dr.Slaa uchaguzi utafanyika mpaka chama kiwe imara.
Kamanda, unanishambulia mimi bure haya maneno ya kuwa Chadema hawawezi kufanya uchaguzi saizi mpaka chama kiwe imara yamesemwa na Dr. Slaa.Ritz,nilijua una akiri nzr kumbe kilaza kama nape,kwani katiba ya cdm inasema utafanyika uchaguzi baada ya miaka mingapi? kama hujui ni miaka mitano na hawa 2liwachagua mwaka 2009,ambapo miaka 5 ni mwakani,ko wamevunja katiba ipi? au wivu wa kike kwa ben sa8? haumuwezi hata kdg.
Teh teh teh teh! When fools argue, joining in may be foolish too.
Mkuu Ritz
Hao wanaosubiri uchaguzi Chadema wanajisumbua; babu na kundi lake wanajua wazi kuna mpasuko mkubwa ndani ya chama chao kwa sababu ya ukanda na ukabila; wanachojaribu kufanya ni kuonyesha eti ndani ya Chadema hali ni shwari inakuwaje katibu anaoposafiri majukumu haachiwi naibu katibu? Leo nimejifunza kumbe Mnyika ni wa kulekule? Mkuu naona Ben Saanane ameanza kujitungia thread nilitegema aseme atagombea kumbe anataka apewe hizi taratibu za kupeana kwa ukanda zimeota mizizi ndani ya Chadema; inabidi tuanze kuwapa somo la demokrasia
Hujue wewe unakipenda sana kiingereza bahati mbaya kabisa kiingereza akikupendi umeandika nini sana mimi binafsi sijakuelewa ngoja niwaulize hawa raia kama wamekuelewa.
Cc; chama, kahtaan, THE BIG SHOW, CHAMVIGA, Boko haram,
Ben Saanane, ni ukweli ulio wazi kwamba we ni kijana mwenye upeo mkubwa sana! If I were to decide ungekuwa ni moja ya viongozi wa juu CHADEMA! Jifunze kuvamia jukwaa kaka, hapo bado
Nyakageni na WanaJF,
Asante....
1: Uchaguzi ndani ya Chama bado na katiba ya chama ya mwaka 2006 ndiyo itakayotoa muongozo
2:Viongozi waliopo wanaendelea kufanya kazi na tunawasaidia katika ujenzi wa chama
3:Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu inahitaji uzoefu zaidi nje ya vigezo vya taaluma.Ni nafasi inayoshikiliwa na mtu ninayemheshimu kama kiongozi aliyechaguliwa kidemokrasia na ibara inayosimamia uchaguzi wa Naibu Katibu Mkuu ndiyo inayosimamia uchaguzi wa Katibu Mkuu baada ya Mapendekezo.
Ndani ya Chama wapo Kaka na Dada zangu walionizidi umri na uzoefu.Hizi ni tunu ninazozienzi katika utendaji wangu ndani na nje ya taasisi za kisiasa.Uzoefu wao ni wa muhimu zaidi katika kipindi hiki chenye changamoto
4:Nimetoa mchango wangu katika harakati za chama kabla sijawa kiongozi na au mtendaji wa chama makao makuu,siku zote ninaweka mbele maslahi ya chama kwa kushirikiana na wanachama na viongozi bila kujali vyeo
5:Mleta mada Makauri Jr Asante kwa kuwa na imani nami na wote walioonyesha imani yao kwangu kwa sababu walizo nazo.Mmenitia nguvu zaidi,sitaisaliti imani yenu kwangu kwa kubweteka bali njia pekee ya kuienzi imani hii ni kuebdelea kukitumikia chama na taifa letu kwa bidii kupitia nafasi niliyonayo.Nimeipitia thread hii kwa kina usiku huu
Kuna walionishauri kama wanachama,watanzania wasiokua na vyama au wenye vyama lakini vyama kinzani,kuna walioshauri kama Kaka na Dada zangu walionizidi umri na uzoefu (bila kujali umri).Mungu awabariki
Pia waliotoa mawazo hasi bila kujali itikadi zetu hata kama ni wa upande ule mwingine(CCM),nimewasikia na hii ndiyo demokrasia.Mmenisaidia kujijenga na kuinarisha ngozi yangu izidi kuwa ngumu
Wale waliotunga stori za uongo kwa nia ya kunichafua,wametekeleza wajibu wao waliotumwa/waliojituma.Sina tatizo kwani Ukiwa Mwanasiasa na ukasifiwa na watu hasa wapinzani wako kila siku basi ni bora uache siasa.Waliotunga stori za uongo na matusi,Hakika nao wameingia katika historia nyeusi katika kukuza demokrasia ya vyama vingi
Naomba niseme wazi,tunajiandaa na uchaguzi ndani ya chama.Muda ukifika kwa rehema zake Mwenyezi Mungu nitachukua hatua za kidemokrasia kwa nafasi ambayo nitaona ninaimudu kulingana na mahitaji ya muda na baada ya kutathmini mchango na matokeo ya mimi kuwa katika nafasi hiyo katika kukivusha chama katika kipindi hiki cha ukombozi wa pili endapo wanachama watanipa ridhaa kwa mujibu wa katiba ya chama chetu.
Nitatangaza nia yangu hadharani kama nilivyofanya tarehe 28/04/2011 nilipotangaza Rasmi mbele ya waandishi wa Habari pale Travertine Hotel nilipotangaza nia yangu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Vijana Taifa.Sina woga,napenda uwazi.
JF kama Mwalimu wangu,mlezi na rafiki katika safari yangu katika jangwa atakua wa kwanza kujua hatua nitakayopiga
Asanteni sana kwa kura ya imani (Hasi na Chanya),tuendelee kujenga chama chetu na tumuombe Mungu atutangulie mbele ya safari yetu.Jambo la Muhimu tuweke matumaini mbele juu ya mustakabali wa chama chetu kupitia mamlaka ya kikatiba,ili kiu na ndoto ya kuona Tanzania yenye Neema na ya kujivunia inafikiwa siku za usoni.Mbarikiwe!!!