Pendekezo: Unaibu Katibu Mkuu CHADEMA apewe Ben Saanane!

Pendekezo: Unaibu Katibu Mkuu CHADEMA apewe Ben Saanane!

Kwaninavyo wafahamu wachagga lazima iwe hivyo,pia wananafasi MDEE,MNYIKA KWAVILE NI WAPARE wa kanda yao,sisi mikoa ya kusini (Minne) hatujapewa viti maalum(Ubunge) kuleta sura yakitaifa,tisa kumi alipofariki REGINA MTEMA wa(MORO)nafasi yake ikachukuliwa na Diwani wa KARATU,eti ndio wanataka nchi hii!!!
hili la kusini una maanisha nini mkuu, sijakuelewa!
 
Ni kibaraka cha Babu na ni mfitini sana, ni mtu hatari sana. Aheri ya shetani kuliko huyo. Alimfitini sana Zitto lakini hamuwezi hata kidogo na ameshindwa kabisa kumuangamiza Zitto na jitihada zake zote hizo sifuri
duh, kama siasa ndo hivo sijui kama tutafika...
 
Kweli chadema is dying, kama mhuni yule anafikiriwa nafasi kubwa kama ile ina mana ndio cream ya chama. Jitu linalisha watu sumu, siasa za matusi mitandaoni nk ndio mbora wenu? Ovyoooooo
mkuu hakuna ambaye hana makosa...je unaweza nitajia cream ya wanaccm?
 
Wewe!akamalize wenzake na sumu?!naona huitakii chadema mema wewe!


kitu cha maudhi hapa JF , ni kuna wale ambao wanona wanalazimika kuandika lolote kila siku ilimradi waonekane wanachangia. Na nia yao ni kuwaharibia majina wenzao, unaposema kuwa Ben ni muuaji, kwanza kamuua nani na unaushahidi gani kuwa ana tabia hiyo wacheni unafiki usio na msingi.

A person is innocent until proven guilty. Although i believe Ben still needs to be cross posted within the various entities of the party to garner more experience on the party leadership and steering, he should never rush, he is a very young Man will accomplish a lot with time and hard work.
 
Pia awe na simile maana naskia wadada hawakatizi mbele yake kwa mujibu wa Eddah Kishimba na Marafiki zake waliosoma nae.

Historia inaonyesha watu smart kiboko yao ni papuchi.Hata Clinton pamoja na kuwa smart alinusurika kuharibu taswira yake aliyoijenga kwa miaka 7 kisa ufuska wake na Monica Lewinsky.
Ushauri wa bure kwake aache tabia ya kujiamini kupita kiasi na Misimamo yake binafsi anapokua kwenye taasisi.
naajua CDM kikiwa na wanasiasa vichwa na ccm tukiwa na vichwa kama akina January Makamba,Paul Makonda,Sixtus Mapunda,Hussein Bashe,Anthony Mavunde na Mwanasheria wa Chama tutafanya siasa za nchi hii zibadilike.Kusema Kweli Ben ana uwezo mkubwa sana ila CDM kimjenge zaidi na kwa kuwa ana mvuto kwa vijana ingefaa akaongoza baraza la vijana ili iwe Sadifa Vs Ben Saanane vs Deo Kisandu wa NCCR Vs Katani wa CUF
Kisandu ameshinda tayari au wewe ndio kampeni meneja wake??
 
Mbona mna uchungu sana na yeye kuchukua mabinti?Ukienda FB na Twitter akina Edda Kishimba wapo kutwa nzima kumsema jamaa kuwa ni kiwembe.Sijui aliwafanya nini hadi wanaumia kiasi hicho.
Hayo ya Sani Abacha ilikuaje mkuu coz ndo nasikia kutoka kwako?

Sani Abacha alikua Rais na dikteta hatari wa Nigeria.Alikua akipenda sana sketi na pamoja na utemi wake aligonga totoz akiwa ametumia viagra vikamrestisha in piece.Mapigo ya moyo yalisimama.

Nadhani suala la akina Eddah ni masuala yao ya mapenzi maana Ben ni shemeji yetu Huku UVCCM.Si hata wao na Mwigulu wanaitana shemeji humu tafuta comment zake wakijibizana na Mwigulu.Kwa kweli dogo anapenda sketi hakuna mfano
 
Ni kweli sana ni kiwembe kwa mabinti hivyo asipoangalia ataishia Kama San Abacha maana yeye alikuwa wembe akaishia pabaya.

Hivi hata familia yake hawezi ongoza anaweza kuongoza watu walau 10? Lakini pia aende shule maana bado kimatendo na kiakili hajakuwa. Has a long way to go!!!! Bado sana na la muhimu aende shule

Naogopa kuchangia zaidi ya hapa maana tindikali itaninyemelea.Sipo tayari kuharibiwa uso wangu maana kuna watu ukiwagusa tu maanake you should get prepared for the worst.I am not prepared aisee!
 
Yeyote atakayeomba nafasi hiyo atapewa kama kura zikitosha,,,chadema tuko imara,,matatizo yetu tumeyamaliza wasaliti wameshatimuliwa,,,
 
Kamanda nani kakundanganya kuwa uchaguzi unakaribia Chadema?

Uchaguzi bado sana kwa mujibu wa Dr.Slaa uchaguzi utafanyika mpaka chama kiwe imara.

hahaha kumbe akae bench saaaaaaana
 
Una ufahamu wowote ni kwa nini alivyokufa Salome Mbatia nafasi yake ilijazwa na mchungaji Lwakatare?

Au umeamuwa tu kuja kujambajamba hapa utuachie uvundo!

Sasa dada nijuze, nijuavyo CCM ukanda auna nafasi.uwezo unazingatiwa ukiona upendeleo ujue uchaga umeingia.
 
Last edited by a moderator:
Siri ya mauaji
Jumatano, Aprili 03, 2013 07:30 Na Charles Mullinda
Sura za Habari Hii
Siri ya mauaji
Madai ya Shonza
Mwampamba
Kauli ya Saanane
Vituko vya Dk. Slaa
Habari Yote
Kurasa 1 kati ya 5

*Shonza, Mwampamba wafichua yaliyofichika Chadema
*Saanane amshambulia Zitto, amwita kigeugeu asiyeaminika
*Dk. Slaa aporomosha matusi mazito, Mbowe, Zitto kimya

[Baadhi ya picha mbalimbali za matukio ya vurugu za kisiasa]

Baadhi ya picha mbalimbali za matukio ya vurugu za kisiasa
WANASIASA wawili vijana ambao wamekuwa katika vita ya maneno na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, kuhusu madai waliyoyatoa kuwa anawindwa kuuawa, mwishoni mwa wiki iliyopita, walijitokeza katika ofisi za Mtanzania Jumatano na kufunua siri na matukio ya utesaji raia na mauaji ya kinyama ambayo yamekuwa yakitokea kwa nyakati tofauti kwenye shughuli za kisiasa hapa nchini.

Wanasiasa hao, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba, ambao wamefanya mahojiano ya ana kwa ana na gazeti hili, walisema madai waliyoyatoa awali kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa, alitajwa na kada wa chama hicho, Ben Saanane, kuwa alimtuma amuwekee sumu Zitto kwa lengo la kumuua ni ya kweli kwa sababu walimkamata akiwa nayo na alikiri jambo hilo na kumuomba msamaha Zitto kwa kitendo hicho.

Walidai, mbali na tukio hilo ambalo baada ya kuliibua limegusa hisia za wengi na kuzua mijadala mikali, yapo matukio mengine ya mauaji na majaribio ya kuua, ambayo yamekuwa yakiratibiwa na Chadema kwa lengo la kuwagombanisha wananchi na Serikali.

Shonza na Mwampamba walisema kuwa wapo tayari kutoa ushuhuda wa matukio hayo mahali popote watakapohitajika na walipoulizwa ni kwa nini baada ya kubaini kuwepo kwa vitendo hivyo, hawakutoa taarifa kwa vyombo vya sheria au taasisi za ulinzi na usalama, walisema mlengwa mkuu katika matukio hayo ambayo yalikuwa yakisababisha madhara kwa watu wengine hakuwa tayari siri hiyo kuanikwa.
 
Madai ya Shonza


Akizungumza mbele ya jopo la waandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania Jumatano, Shonza alidai kuwa, yeye na baadhi ya vijana wenzake waliokuwa wakiunda kundi Patriotic Movement, walimnasa Saanane akiwa na sumu hiyo katika Hotel ya Lunch Time iliyoko Ubungo, Dar es Salaam, ambao awali alidai kuwa ni dawa ya Panya, lakini alipobanwa alieleza kuwa ilikuwa sumu ambayo hakuitaja jina na kwamba alipewa na Dk. Slaa ili amuwekee Zitto kwa sababu alikuwa akimsumbua sana.

Alisema, sumu ingewekwa kwenye kinywaji cha Zitto akiwa katika kikao hicho, lakini hatua yake ya kutohudhuria ndiyo iliyomuokoa.

Shonza alisema, baada ya Saanane kukiri kuwa alitumwa na Dk. Slaa kumuwekea Zitto sumu, walimtaarifu wakati akiwa Marekani na aliporudi alikutana na kuwataka jambo hilo wasilifikishe polisi kwa sababu lingekivuruga chama na kwamba kwa sababu alikwishawajua wabaya wake atajilinda.

Alimtuhumu Zitto kwa kuficha ukweli na kumwita kiongozi mwoga, huku akimuonya kuwa iwapo ataendelea na tabia ya kukanusha ukweli atamuumbua hadharani kwa sababu anamjua vizuri.

"Ameongea hayo kwa sababu ana tabia ya kushindwa kuthibitisha kuwa ana uwezo wa kujiongoza yeye mwenyewe pamoja na wengine. Mtu wa maslahi Zitto, anatafuta huruma ya Chadema baada ya kuona amepukutika kisiasa kutokana na kukosa msimamo kiuongozi na hawezi tena kutetea wanyonge, ni mtu mwoga.

Mnapokuwa kwenye mapambano yeye yuko tayari kurudi nyuma, lakini huruma hiyo asitegemee kuipata Chadema, labda akubali kushaurika na kubadilika kama kweli anataka kutetea maslahi ya wanyonge," alisema Shonza.

Aidha, Shonza alimshambulia pia Saanane kwa kudai anakataa ukweli anaojua, kwa sababu tukio la kukamatwa kwake akiwa na sumu lilitokea akiwa mbele ya zaidi ya mtu mmoja na kusisitiza kuwa kada huyo wa Chadema anatumika na viongozi wa juu wa chama hicho kuwashughulikia baadhi ya wanachama wasiotakiwa.

Katika hili, Shonza alidai zaidi kuwa Saanane ni mtu hatari kwa sababu ndiye aliyeanzisha kundi la PM7, ambalo lilikuwa na lengo la kumpindua Mbowe kutoka kwenye wadhfa wake wa uenyekiti, lakini baadaye aliwageuka wenzake na kusababisha kufukuzwa katika chama.

"Saanane alikuwa anatumika kutuingiza mkenge. Alianzisha kile alichokiita mapinduzi, Patriotic Movement (PM7), lengo lilikuwa Pindua Mbowe, sisi hatukujua.

Tulikuwa saba katika PM7, Saanane alifanikiwa kutuchezea akili na alikuja na 'nick names' (majina bandia) yake. Mimi akaniita Benanzir Bhuto, Mchange akaitwa Mdude, Mwampamba- Joseph Kony, Zitto- Dogo kama tulivyozoea kumuita na yeye mwenyewe akajiita Cobra, wapo na wengine sikumbuki vizuri majina yao hapa.

Sisi vijana wakati mwingine tunatumika vibaya, sisi hatukujua ana ajenda yake, tulivyoshtuka akatukana na ndiyo yakatokea hayo yaliyotokea," anazidi kueleza Shonza
 
Mwampamba
Kwa upande wake Mwampamba ambaye aliandamana na Shonza katika ofisi za Mtanzania Jumatano, alidai kushangazwa na hatua ya Zitto kukanusha kauli ya Shonza iliyokuwa ikieleza namna Saanane alivyokamatwa akiwa na sumu aliyokuwa ametumwa kumuwekea Zitto.

Alisisitiza kuwa, Zitto anajua mipango inayopangwa ndani ya Chadema kwa ajili ya kummaliza na alimtaka aache tabia ya kufunika kombe ili mwanaharamu apite, kwa sababu inaweza kuwa na athari mbaya kwake.

"Zitto anajua mpango mzima wa kutaka kumalizwa kwa sumu na Ben Saanane, baada ya kutumwa na Dk. Slaa kwa sababu tulimwambia na alithibitisha mwenyewe pale Saanane alipomuomba msamaha, sisi ndiyo tulimbana Saanane hadi akaeleza ukweli wa mipango yao ya mauaji.

"Leo namshangaa anavyojikomba eti haamini kuwa anaweza kuuawa na hao jamaa. Lakini kwa Ben Saanane, namtaka atambue kuwa Ludovick alipokamatwa alikanwa na Dk. Slaa wakati ndiye alikuwa kijana wake mpenzi, sasa na yeye ipo siku atakimbiwa.

"Zitto anatakiwa aache tabia ya kufunika funika mambo, ajue nimemwokoa sana katika mambo mengi, mfano mauaji ya Morogoro yaliyopangwa na Chadema yalimlenga Zitto, alikuwa atolewe kafara. Yule muuza magazeti aliyepigwa risasi Morogoro akafa, siku hiyo ilikuwa afe Zitto," alidai Mwampamba.

Alipoulizwa ni kwanini viongozi wa Chadema wanataka kumuua Zitto, alisema ni kwa sababu ya uhusiano mbaya baina yake na vigogo hao ambao chanzo chake ni hatua ya kutaka kugombea urais na kutomuunga mkono Dk. Slaa katika harakati zake za kuwania urais mwaka 2010.

"Zitto hana uhusiano mzuri na viongozi wa juu wa Chadema. Nia yake ya kutaka kugombea urais hawaipendi, inawaudhi sana na amekuwa akitofautiana nao kwa mambo mengi, anajua kuwa anawindwa ndiyo maana hata oparesheni za M4C hashiriki.

"Mimi nilikuwa Chadema na nilikuwa karibu sana na Zitto, najua nini kilikuwa kinaendelea juu yake na najua baadhi ya mambo ya Chadema. Ninaijua mipango ya mauaji ya Chadema. Zitto aliwahi kuwekewa sumu Bagamoyo wakati wabunge wa chama hicho walipokuwa kwenye mkutano wao huko.

"Alinusurika kufa. Alipona baada ya sumu hiyo kutolewa mwilini mwake. Waliiflashi." Alidai Mwampamba.

Alidai kuwa Zitto alipata kunusurika katika ajali ya gari wakati akitokea Bagamoyo kuelekea Iringa, baada ya gari alilokuwa akitumia kulegezwa nati zinazofunga tairi. Tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya Zitto na Mbowe kutupiana maneno makali kwenye mkutano
 
hili la kusini una maanisha nini mkuu, sijakuelewa!

KUSINI namaanisha MTWARA LINDI SONGEA NA NJOMBE,hatujapewa viti maalumu,HAI MBOE alipata kura 24000 tu kapewa viti 3,wamepeana kindugu,wabunge wao wa viti maalum wakikutana inakuwa kama kikao cha ndoa yan wanafamilia.
 
Naona Masalia wameingia kazini kumchafu Ben kwa nguvu zote na vijana wa Lumumba.Atawatoa roho mwaka huu.
 
Back
Top Bottom