Pendekezo: SLAA amrithi SUMARI Arumeru!

Wanachama wenzangu wa chadema,kwa wakati huu tulionao tunalihitaji kwa hali na mali jimbo la arumeru hasa baada ya kulikosa jimbo la igunga jambo ambalo lilikifedhehesha sana chama.Kwanini nasema ilikua fedheha kwetu kushindwa igunga? Tatizo halikua kushindwa mana mnaposhindana ni lazima mmoja ashind,bali ilikua fedheha kwetu kama chama kikuu cha upinzani kushindwa na ccm dhaifi,ccm goi goi, ccm yenye minyukano ya kisiasa isiyokwisha n.k

Sasa ili kurejesha hadhi ya chama chetu ARUMERU ni lazima tushinde,hivyo ni muhimu kumsimamisha mgombea mwenye muscles za kutosha wa kitaifa itakua ni bora zaidi kwani kwa uzoefu wangu kama nilivyosema mahali fulani wa kufanya kazi makao makuu ya ccm kwa miaka mingi ccm pale itashusha timu nzima,kuanzia pinda, Salim, Mangula (hatari sana huyu) mpaka migiro na Lowassa pia.

Hivyo tujipange, mimi pia naunga mkono kama upo uwezekekano kijana mnayemtaja taja hapa bwana nasari samahani kama nimekosea jina lake asubiri kidogo panapo uchaguzi mkuu basi atagombea na kwa utendaji wa dr slaa kwa kipindi cha miaka miwili pale jimbono basi atamuandalia mazingira yenye uhakika kabisa kijana aweze kushinda mwaka 2015!

Slaa kama atasimama pale uwezekano wa kushinda ni mkubwa kama tutampa na sisi support ya kuongezea!ccm sio wagumu hivyo mimi nawafahamu ila tu tujipange vizuri.
 
Kwa mtindo huu wa Chadema.

Mimi naona wangemchagua kuwakilisha chama chake katika kugombea kiti cha UZINI zanzibar?
 
Wanachama wenzangu wa chadema,kwa wakati huu tulionao tunalihitaji kwa hali na mali jimbo la arumeru hasa baada ya kulikosa jimbo la igunga jambo ambalo lilikifedhehesha sana chama.

Kwanini nasema ilikua fedheha kwetu kushindwa igunga?Tatizo halikua kushindwa mana mnaposhindana ni lazima mmoja ashind,bali ilikua fedheha kwetu kama chama kikuu cha upinzani kushindwa na ccm dhaifi,ccm goi goi,ccm yenye minyukano ya kisiasa isiyokwisha n.k

Sasa ili kurejesha hadhi ya chama chetu ARUMERU ni lazima tushinde,hivyo ni muhimu kumsimamisha mgombea mwenye muscles za kutosha wa kitaifa itakua ni bora zaidi kwani kwa uzoefu wangu kama nilivyosema mahali fulani wa kufanya kazi makao makuu ya ccm kwa miaka mingi ccm pale itashusha timu nzima, kuanzia pinda, salim,mangula (hatari sana huyu) mpaka migiro na lowassa pia, hivyo tujipange, mimi pia naunga mkono kama upo uwezekekano kijana mnayemtaja taja hapa bwana nasari samahani kama nimekosea jina lake asubiri kidogo panapo uchaguzi mkuu basi atagombea na kwa utendaji wa dr slaa kwa kipindi cha miaka miwili pale jimbono basi atamuandalia mazingira yenye uhakika kabisa kijana aweze kushinda mwaka 2015!

Slaa kama atasimama pale uwezekano wa kushinda ni mkubwa kama tutampa na sisi support ya kuongezea!ccm sio wagumu hivyo mimi nawafahamu ila tu tujipange vizuri.

Dr Slaa ni Presidential material Kamwe hatagombea ubunge,hata kama chama chake hakitampendekeza tena basi sisi wananchi tutampendekeza, Mwache ajenge chama naasimamie swala la katiba
 
pELEKA JUKWAA LA JOKES MKUU;MAANA HAIINGII AKILINI KUMTAKA RAISI WETU KUGOMBEA UBUNGE!
Wewe huoni mchango wake sasa akiwa nje ya bunge kuwa ni mkubwa mno???
 
Siungi mkono hoja kutokana na fact walizotoa wajumbe mbalimbali hapo juu, inaonekana huyo dogo Joshua anaweza akashinda, kwahiyo basi kinachotakiwa ni kumpa support ya nguvu huyo dogo.
 
pELEKA JUKWAA LA JOKES MKUU;MAANA HAIINGII AKILINI KUMTAKA RAISI WETU KUGOMBEA UBUNGE!
Wewe huoni mchango wake sasa akiwa nje ya bunge kuwa ni mkubwa mno???

mh.slaa alikua na mchango mkubwa zaidi kwa kuimarisha chama akiwa bungeni kuliko sasa,huo ndio ukweli,akirudi kule hata hayo mambo ya posho za wabunge wanazokimbilia hawa wabunge wa sasa kasoro zitto zitakuwa hatarini,ndio mana wengi mnaopinga ama ni wabunge au mnanufaika kwa njia moja ama nyingine na ufisadi unaoendelea bungeni ambao zitto ameukata kata kata lakini wabunge wote wa chadema akiwemo kiongozi wa upinzani bungeni analamba,slaa ndio chaguo sahihi la mrithi wa kiti cha sumari arumeru,kama chadema inataka kukichukua iko kiti lakini,otherwise msimamisheni yeyote,mi nashauri tu
 
Jimbo la Arumeru hata asiposimama Dr. Slaa CDM itashinda.
Kueneza Chama Countrywide ni faida zaidi kuliko kunga'ang'ania eneo ambalo tunaweza kushinda.
Njoo tukaze buti
 
kwanini chadema wanaikataa idea hii,mbona iko poa tu,lengo ni kuongeza viti bungeni wadau ili upinzani uwe na meno zaidi kule,msipoteze nafasi hii kwa kuweka watu rahisi rahisi..
 
Hiyo level alikwisha ivuka, yeye ni mgombea Urais, na hata hakipokonywa basi atabaki kuwa hazina ya Chadema kwa kutoa ushauri na kujenga chama!
 
Keshachoka kisiasa huyu..
Kwa sasa tunahitaji dam mpya za zenye nguvu bungeni na kwenye ulingo wa siasa!
 
Dr. Slaa majukumu aliyonayo kwa sasa ni zaidi ya kuwa mbunge, kasi ya uwajibikaji na umahiri wa wabunge wa chadema unayoiona ni kutokana na kazi nzuri ya kuwapika wabunge hao inayofanywa na Katibu Mkuu wa chama Dr. Slaa, kuna kazi kubwa zaidi ya hiyo?

Wapendwa wa Chadema,
Mimi naomba Dr Slaa awanie ubunge Arumeru kusudi arudi Bungeni kuweka nguvu mpya

kweli hata mimi nina wazo hilo ila je sheria inamruhusu??maana aligombea urais huyu
 
Keshachoka kisiasa huyu..
Kwa sasa tunahitaji dam mpya za zenye nguvu bungeni na kwenye ulingo wa siasa!

Mnahitaji nyie akina nani? wavua gamba bila shaka mmechoka na ndio maana hapa tunazungumzia mambo ya chadema lakini vidudu watu hamchoki kujiingiza kwenye mambo yasiyowahusu.
 
kweli hata mimi nina wazo hilo ila je sheria inamruhusu??maana aligombea urais huyu

sheria kama haijabadilika, inamruhusu. Umesahau ya Mrema 1995? Aliwania urais, akapigwa chini akaibukia DSM. Lakini mimi sipendi agombee, awaachie vijana, awape mafunzo wawe tishioa kama yeye
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom