Uchaguzi 2020 Pendekezo la Kauli-Mbiu ya Upinzani katika Uchaguzi Mkuu 2020

Sophist

Platinum Member
Mar 26, 2009
4,484
3,400
Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020, ninawashauri wapinzani kutumia Kauli-Mbiu moja hata kama kila chama kinashindana kivya-vyake. Ni kwa njia hii upinzania utaweza kuichinjia CCM baharini ki-mkakati.
Ninawashauri kuchagua Kauli-Mbiu inayoelekea kufanana na hii:

Ondoa Balaa [la udikiteita], [Ruhusu] Imarisha Demokrasia, [Ruhusu] Imarisha Maendeleo ya Watu [siyo vitu].....Chagua...[jina la mgombea Uraia/Ubunge/Udiwani].

AU

Ondoa Balaa [la udikiteita] Nchini/jimboni/kwenye kata...[Ruhusu] Imarisha Demokrasia Nchini/jimboni/kwenye kata.....[Ruhusu] Imarisha Maendeleo ya Watu [siyo vitu] nchini/jimboni/kwenye kata.... Chagua... [jina la mgombea Urais, Ubunge/Udiwani].

Jaribuni italipa
 
Kushabikia Upinzani huu wa kina Lisu na kina Mbowe na vijana wao ni aina ya ujinga mkubwa,maana wananchi tunaona serikali ya sasa inafanya nini..kuna nyakati nyingi sana waTanzania wanapoteza muda tu kuwasikiliza na kuwashabikia wasanii wa kisiasa.
 
Kushabikia upinzani huu wa kina Lisu na kina Mbowe na vijana wao ni aina ya ujinga mkubwa,maana wananchi tunaona serikali ya sasa inafanya nini..kuna nyakati nyingi sana waTanzania wanapoteza muda tu kuwasikiliza na kuwashabikia wasanii wa kisiasa
Na kutuaminisha kuwa hayo yaliyofanywa na serkali hii ni makubwa utazani nchi hii hakuna kilichokua kimefanywa awali huo nao ni ujinga tena wa kiwango cha YULE YESU WENU WA CHATO(BURIGI)
 
Siku mkijenga hoja ya "Maendeleo ya Watu" ni nini na "Maendeleo ya Vitu" ni nini nikaelewa, nitawafuata.
 
Kushabikia upinzani huu wa kina Lisu na kina Mbowe na vijana wao ni aina ya ujinga mkubwa,maana wananchi tunaona serikali ya sasa inafanya nini..kuna nyakati nyingi sana waTanzania wanapoteza muda tu kuwasikiliza na kuwashabikia wasanii wa kisiasa

Serikali ifanyacho sio hisani bali ni wajibu wa serikali yoyote, hata serikali ya wakoloni ilifanya miradi ya maendeleo, kwani ni wajibu wa mkusanya kodi. Kwani wakiingia madarakani wapinzani, watavunja hicho kinachofanywa na serikali ya sasa?
 
Siku mkijenga hoja ya "Maendeleo ya Watu" ni nini na "Maendeleo ya Vitu" ni nini nikaelewa, nitawafuata.

Hakuna anayehitaji ufuasi wako, baki huko huko uliko, ili uone kitu ambacho wakoloni walisema watanzania hawawezi kujitawala iwapo watapewa uhuru.
 
Serikali ifanyacho sio hisani bali ni wajibu wa serikali yoyote, hata serikali ya wakoloni ilifanya miradi ya maendeleo, kwani ni wajibu wa mkusanya kodi. Kwani wakiingia madarakani wapinzani, watavunja hicho kinachofanywa na serikali ya sasa?
Kwa maudhui kumbe tayali unatambua kua serikali inafanya,basi na unyamaze maana pia serikali hiyo hiyo haiwezi kufanya kulinga na kila tamanio la mtu mmoja mmoja kama afikiriavyo yeye.

MUNGU mwenyewe anajua kila kitu kuhusu sisi na anatulinda lakini utakuta wako wanaomlaumu na kutokukubali uwepo wake,leo serikali?
 
Kwa maudhui kumbe tayali unatambua kua serikali inafanya,basi na unyamaze maana pia serikali hiyo hiyo haiwezi kufanya kulinga na kila tamanio la mtu mmoja mmoja kama afikiriavyo yeye. MUNGU mwenyewe anajua kila kitu kuhusu sisi na anatulinda lakini utakuta wako wanaomlaumu na kutokukubali uwepo wake,leo serikali?

Hakuna serikali yoyote duniani hii ambayo haijawahi kufanya chochote maana inakusanya kodi. Tofauti ni kuwa inafanya nini, na matakwa ya wananchi ni nini. Hapo ndio box la kura huamua wananchi wanataka nini.
 
CCM wao hawahitaji maneno lukuki.
Wakisema
"KANYAGA TWENDE!" tu, inatosha.
 
Kushabikia upinzani huu wa kina Lisu na kina Mbowe na vijana wao ni aina ya ujinga mkubwa,maana wananchi tunaona serikali ya sasa inafanya nini..kuna nyakati nyingi sana waTanzania wanapoteza muda tu kuwasikiliza na kuwashabikia wasanii wa kisiasa

Wewe na genge lako siyo wananchi bali nyinyi ni MATAGA wasaka tonge.
 
...vilevile, wasanii wa kizazi kipya wanaounga mkono upinzania wapenyezewe ujumbe huo na kuutungia nyimbo za kampeni Kwa ajili ya kuongeza hamasa. CCM watalala kwa amani tu.
 
Back
Top Bottom