Pendekezo kwa Rais Kikwete kuhusu wanafunzi waliofeli...

Pendekezo kwa Rais Kikwete kuhusu wanafunzi waliofeli...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,240
Reaction score
44,485
Nilitaka kuandika makala ndefu lakini nimeona niende moja kwa moja na kusema ombi/pendekezo langu kama litampendeza Rais Kikwete.

KWA KUWA, matokeo ya kidato cha nne ambayo yametoka hivi karibuni yameonesha kufeli kwa kutisha kwa watoto wetu katika mtihani wao;

KWA KUWA
, kufeli huko kuna matokeo ya moja kwa moja katika maisha ya wanafunzi hawa, familia zao na kwa taifa kwa u jumla;

KWA KUWA
, matokeo hayo ni hasara kubwa kwa wazazi waliowekeza kwa miaka minne ya elimu ya watoto hawa na kwa taifa katika kuwekeza vifaa, walimu na miundo mbalimbali;

KWA KUWA, kuacha kundi kubwa la watoto hawa kurudi katika maisha ya uraiani kutaongeza jamii ya watu ambao hawana elimu ya kutosha na wasioweza kuajiriwa hata katika mifumo isiyo rasmi (pamoja na kushindwa kujiajiri wenyewe);

KWA KUWA, kufeli kwa watoto hawa ninaamini siyo kosa lao peke yao bali pia ni kosa la utawala na uongozi wetu, wazazi na jamii kwa ujumla;

NINAAMINI KUWA, kutokuchukua uamuzi wa makusudi na wa lazima kuwasaidia watoto hawa kuwapa nafasi nyingine ni kuwahukumu katika maisha duni na kuwanyima kimsingi nafasi ya kuinuka wakati tayari wameshaanguka

NINAAMINI KUWA, matokeo haya ni dhambi na aibu ya taifa letu hasa katika nchi ambayo inajivunia kuwa ina 'shule nyingi, vyuo vingi, walimu wengi, na teknolojia ya kisasa katika elimu;

NINAAMINI KUWA, Ni jukumu la uongozi wa kisiasa wa taifa kuchukua hatua za haraka na za lazima kuwapa nafasi nyingine watoto hawa kuweza kutengeneza waliposhindwa.

NINAAMINI KUWA, Taifa lina deni kwa watoto hawa, lina deni kwa historia, lina deni kwa familia zao na kwa hakika kabisa lina deni kwa maisha ya watoto hawa. Deni hili tusiliache likue lije kushindwa kulipika. Naamini tunaweza kulilipa kabla halijaanza kuwa na riba isiyokamatika!

Kutokana na mambo yote hayo juu na mengine ambayo nimeyaadhania, ninaamini Utawala wa Rais Kikwete unaitwa na historia, unadaiwa na haki, na unalazimishwa na wajibu kuwapa watoto hawa nafasi nyingine ya kurudia mitihani ya kidato cha nne ili kuweza kuinua alama zao za kufaulu, kusahihisha makosa yao na kuwapa nafasi ya kuweza kuendelea na elimu ya kidato cha tano na cha sita. Kutokana na hili:

HIVYO BASI, Baraza la Mawaziri lifanye kikao cha dharura kuhusiana na matokeo haya ya mitihani ambapo uamuzi wa kutengua matokeo yote ya mtihani uchukuliwe na kuyafuta kabisa matokeo hayo;

NA HIVYO BASI
, Baada ya kufuta matokeo hayo serikali iamue kuwa watoto wote waliofanya mtihani huu uliopita watarudia mitihani yote ya kidato cha nne ndani ya mwaka mmoja pamoja na watoto watakaokaa katika mtihani wa mwaka huu au katika mtihani mwingine tofauti

NA HIVYO BASI
, Watoto wote ambao katika mtihani huu wamepata daraja la I na II watakuwa na uhuru wa ama kurudia mtihani wao ili kuthibitisha kufaulu kwao au kuendelea na matokeo waliyonayo. Wakiamua kurudia basi kama watafaulu alama za juu zaidi ya sasa watashika alama hizo kama watapata alama za chini watashika alama zao za sasa;

NA HIVYO BASI
, Wanafunzi waliopata daraja III na 0 nao itakuwa hivyo hivyo, watapewa nafasi moja ya kurudia mitihani yote kuiinua viwango vyao na wale watakaopata viwango vya juu kuliko vya sasa basi watasika viwango hivyo na wale ambao watapata viwango vya chini kuliko sasa watashika viwango vya sasa.

NA HIVYO BASI, Wanafunzi ambao sasa wamepata daraja la III na 0 endapo watarudia mitihani ijayo na wakainua viwango vyao na kuwa kati ya daraja la I na II basi SERIKALI itawapa nafasi ya kusoma bore kidato cha tano na cha sita katika shule za Sekondari za Serikali. Hii iwe 'AHADI YA TAIFA' (National Promise)

NA HIVYO BASI, ili kutoa motisha kwa shule na walimu ambao wanawafundisha wanafunzi hawa na wengine basi serikali ianze kutoa motisha kwa shule zote (zenye watahiniwa wengi) ambazo zitafaulisha watoto wengi kwenye madaraja ya I na II. Motisha huu utakuwa kwa shule na kwa jopo la walimu wa kidato cha nne.

- Shule ambayo haitatoa daraja 0 kuanzia sasa itapata zawadi ya shilingi milioni 50 kwa matumizi ya sule
- Shule ambayo haitatoa daraja IV kuanzia sasa itapata zawadi ya silingi milioni 75 kwa matumizi yake
- Walimu wanaofundisha shule hizo zikiwa na matokeo hayo watagawana zawadi ya nusu ya tuzo hizo (Milioni 25 kama hakuna 0, milioni 37.5 kama hakuna daraja la IV)

Tuzo hizo zinaweza kurudiwa kila mwaka endapo viwango hivyo vitaendelea.

NA HIVYO BASI, Mwalimu Mkuu wa shule ambazo zinafanya vibaya zaidi watafukuzwa kazi, Afisa Elimu wa Wilaya yenye shule nyingi zilizofanya vibaya nao watafukuzwa kazi.

NA HIVYO BASI, kuanzia sasa wanafunzi wote wanaopata daraja la IV na 0 watakuwa wanapata automatic resit ya mtihani katika mwaka unaofuatia. Na katika hili napendekeza wanafunzi wote waliopata madaraja hayo katika miaka mitano iliyopita na ambao wangependa kurudia mitihani wapewe nafasi hiyo na wao wakifaulu kama hapo juu serikali iwagharimie kidato cha TANO na cha SITA.

PAMOJA NA HAYO, Baraza la Mawaziri liangalie kwa kina haja ya kuufumua mfumo wetu wa elimu kukidhi changamoto ambazo tumeziona sasa. Baadhi ya mabadiliko hayo:

- Kuondoa Elimu kutoka kuwa suala la mfumo wa kitaifa (decentralization of the education system)
- Kuweka miaka mitatu ya kwanza ya elimu kuwa ni ya lazima katika 3R (Hisabati, Kuandika, na Kusoma)
- Kuweka mwaka wa kwanza kwenye O'Level kuwa Wa Kiingereza na Hisabati na Lugha (Pre-Secondary) - miaka mitatu ya mwiso kufanya elimu ya O'level
- Serikali ikutanishe wadau wa elimu kutoka Shule zinazofanya vizuri zaidi kushirikisha mawazo yao na wadau wa shule nyingine (KONGAMANO LA KITAIFA KUHUSU ELIMU - NATIONAL EDUCATION REFORM CONFERENCE)
- Makampuni na taasisi binafsi na za umma zitakiwe kuadopt shule za msingi na za sekondari na yashiriki katika uendeshaji na uboreshaji wake. Mtindo wa sasa wa makampuni makubwa kutoa madawati, mabati halafu wanakimbia haujasaidia kuinua elimu; makampuni yahamasishwe (ikiwemo motisha wa aina fulani katika kodi -tax incentive) kulea shule za sekondari. Tax breaks makampuni yatapata endapo shule wanazozilea hazitakuwa na madaraja ya IV na 0


MMM - BGM

* Kwa kweli nimeandika kwa haraka bila kufikiria mengi zaidi na implication yake na hivyo ni mchango wangu kidogo tu wa mawazo ya nini tufanye sasa hivi na baadaye. NIna uhakika watu wengine wana mawazo bora zaidi. Jambo moja ambalo hatupaswi kukubali na kuliachilia ni matokeo haya kusimama. Ni LAZIMA yatenguliwe kama tunaamini katika utu, usawa na haki kwa watoto wetu.
 
this is a Qualification Test (QT) to the president
 
Naogopa kusema utakimbilia kuniban kwenye thread yako ila akili za kibinadamu kidogo zimeanza kurudi; najua huu ni msiba wa wengi mtakuja na kila aina ya suluhisho; kama unakumbuka mwaka jana waislamu walilamika sana kuhusu Wizara ya elimu na Baraza la mitihani; kama wengi wenu humu JF mngeelewa kilichokuwa kinalalamikiwa labda matokeo ya leo div 0 zingekuwa 1000 tu; ila nashukuru Mungu ukweli umeanza kujionesha.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Hapa kwanza ni kutafuta mzizi wa tatizo,

Hata wakirudia mara 70 kama walimu hawatimiziwi madai yao, ni kazi bure!
Kama wazazi hawataamua kunusuru watoto wao kwa kuwaondolea ma TV masebuleni na kuwanyang`anya simu za kuchart usiku kucha KWENYE FB NA TIGO ZA 250 hata serikali itowe nini ni bure!

Serikali pia kweli inatakiwa kubadili mfumo wake wa elimu na kuahakikisha unaendana na maisha ya sasa na pia kuweka kipaumbele juu ya elimu na kuwa serious kwa kuwapa motisha walimu ili waweze kuwafundisha watoto kwa bidii.
Walimu walipwe vizuri!
 
Nakubaliana na wewe kuhusu Decetralization ya organ ya elimu.

Napendekeza kuwe na mfumo wa assasments test kwa kila mwanafunzi na kila marks atakazo carry ndizo ziamaue kwenda kiadoto kinachofuata au la naulemwaka wa kidato cha nne iwe hivyo hivyo kama anatakiwa kufanya final exams au la.
 
Hivi na huyu naye mdini eti!?
Hivi ni kwa nini msianzishe mitaala yenu ya kiislamu? hii si ni elimu ya makafir kutoka magharibi? nadhani madrasat inatosha uislamu umekamilika hauitaji elimu ya kutoka kwa makafir.

Unajuwa maana ya Boko Haram?
 
Mzee Mwanakijiji,kwa mwanafunzi aliye pata daraja 0 au 1V,kutegemea kuna miujiza itatokea afaulu baada ya kurudia mitihani ni kujidanganya bure!
Kama mwanafunzi amesoma miaka minne halafu akapata 0,ina maana huyu hajaelewa CHOCHOTE katika aliyo fundishwa!
Suluhu yake si kurudia mtihani,labda aanze upya na kufundishwa form 1 hadi 1V kwa ule utaratibu wa miaka 2 ndipo afanye mtihani.
Hayo mengine,tupo pamoja.
 
Last edited by a moderator:
What if mwakani mambo yakawa hivi hivi? kwa watoto wakishaona kuna second chance....ndo watafanya vibaya zaidi...kwa matarajio kuwa wanayo nafasi nyingine...al in al ni mchango mzuri.
 
tatizo haliko baraza la mitihani bali liko kwa serikali yenyewe. baraza la mitihani likianza kuingiliwa na watu tutaunda taifa mbumbumbu kwani watakuwa wakichakachua matokeo ili wanafunzi waonekane wamefulu ili kulinda cheo. matokeo ya darasa la saba mwaka huu wameongeza alama ili watoto wapatikane wa kwenda sekondari za kata. je hili ni tatizo la baraza la mitihani? matokeo yake tutegemee zero nying miaka ijayo. naunga mkono wizara ya elimu isihusike na elimu ya sekondari na msingi wapewe TAMISEMI wenye shule na nyenzo. mulugo anashinda kuiga kelele tu badala ya kubadili mfumo wa elimu. mkimtoa ndalichako munaua elimu kwani atakaye kuja atafanya mambo kwa kuogopa watawala badala ya welede wa kazi
 
Naogopa kusema utakimbilia kuniban kwenye thread yako ila akili za kibinadamu kidogo zimeanza kurudi; najua huu ni msiba wa wengi mtakuja na kila aina ya suluhisho; kama unakumbuka mwaka jana waislamu walilamika sana kuhusu Wizara ya elimu na Baraza la mitihani; kama wengi wenu humu JF mngeelewa kilichokuwa kinalalamikiwa labda matokeo ya leo div 0 zingekuwa 1000 tu; ila nashukuru Mungu ukweli umeanza kujionesha.

Chama
Gongo la mboto DSM

Nina uhakika unawazungumzia wengine halinihusu mimi. Suala la kufeli au matatizo ya elimu hayawaathiri Waislamu tu. Wanaofeli ni watoto wa Kitanzania, Waislamu, Wakristu na Wenye imani za jadi... na hata wasioamini.
 
What if mwakani mambo yakawa hivi hivi? kwa watoto wakishaona kuna second chance....ndo watafanya vibaya zaidi...kwa matarajio kuwa wanayo nafasi nyingine...al in al ni mchango mzuri.

kwamba watakuwepo watoto wanafeli hilo siyo jambo geni; la maana ni kupunguza nafasi hizo. Na siyo tu kuwapa nafasi ya kurudia lakini ni kuutengeneza mfumo. Kama mashine inakoboa vibaya haijalishi nafaka unazoweka ni za shamba gani... na hautengenezi kwa kubadili nafaka... fix the machine...
 
Mzee Mwanakijiji,kwa mwanafunzi aliye pata daraja 0 au 1V,kutegemea kuna miujiza itatokea afaulu baada ya kurudia mitihani ni kujidanganya bure!
Kama mwanafunzi amesoma miaka minne halafu akapata 0,ina maana huyu hajaelewa CHOCHOTE katika aliyo fundishwa!
Suluhu yake si kurudia mtihani,labda aanze upya na kufundishwa form 1 hadi 1V kwa ule utaratibu wa miaka 2 ndipo afanye mtihani.
Hayo mengine,tupo pamoja.

Unaweza kuwa sahihi lakini mimi siamini kuwa watoto hawa hawana akili ya kufundishika. KUna tatizo kubwa sana ambalo ni lazima tulishughulikie... labda hata kuangalia mitihani. Fikiria tunasema hakuna "mitaala"; Baraza la Mitihani linatunga mitihani kwa kuangalia mitaala yake; halijali wanafunzi wamejifunza nini au hata kama wamejifunza wanachotakiwa kujifunza. Sasa unamtahini vipi mtoto kwa kitu ambacho hakufundishwa?
 
Watajiaandaa kwa mda gani Kama kwa miaka minne wamepata sifuri?Nadhani mapendekezo yako yawe kwa miaka ijayo!Kuhusu tatizo la baraza kama anavyosema CHAMA binafsi sioni mashiko, tusilaumu bure tatizo ni mfumo wa elimu kazi ya baraza si upendeleo tembelea tovuti yao.Elimu ina mapungufu mengi kuanzia aina ya walimu,incetives, vitendea kazi hadi malezi ya wanafunzi.Kukosewa kwa marks za sisi tuliobahatika kuwa waislam mara moja haiwezi kuwa sababu yakujerneralize takwimu hata wanafunzi wanapoharibu wenyewe.
 
Naoogopa kucomment maana nitaambiwa kuwa nina chonga kwa kuwa yeye ni muislamu: lakini walimu wakigoma serikali iko palepale kuzuia mgomo mahakamani.
 
Nina uhakika unawazungumzia wengine halinihusu mimi. Suala la kufeli au matatizo ya elimu hayawaathiri Waislamu tu. Wanaofeli ni watoto wa Kitanzania, Waislamu, Wakristu na Wenye imani za jadi... na hata wasioamini.

Ni kweli inawezekana hukuchangia ila uliwasoma wachangiaji wengi walivyokuja na majibu ya kashfa; kisa nini Waislamu walilalamika dhidi ya utendaji wa Wizara na Baraza; suala kubwa lilikuwa ni hili la kufeli wangi walichukulia kama dhihaka; kuna watu nawasubiri nisikia majibu yao ila nina uhakika wanakumbuka walichosema hawatatia mguu humu!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Back
Top Bottom