Pendekezo kwa Rais Kikwete kuhusu wanafunzi waliofeli...

Pendekezo kwa Rais Kikwete kuhusu wanafunzi waliofeli...

My point is that we should not let a generation of uneducated and miseducated bunch flood our streets. We have to correct the nation's mistake and I believe what we call education is a fundamental mistake by all of us.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
MMM ubarikiwe.

Ila naomba kuboresha au kutofautiana kidogo ktk approach, (emphasize on order):-

1) a) Waziri wa Elimu na wateuliwa wenzake wote Wizarani wajiuzulu.
b) Waziri wa TAMISEMI na wateuliwa wenzake wote Wizarani wajiuzulu2
c) NECTA waoneshe uwajibikaji. Pia DEDs na Maofisa Elimu mikoa na wilaya.

2) Matokeo haya yawe suspended (temporarily or else)

3) Tume huru iundwe kuchunguza matatizo tuliyonayo ktk mfumo na sera yetu ya Elimu. Ikiwezekana ndani ya siku 90 waje na majibu.

4) Maoni uliyotoa yaingie kama mojawapo ya mapendekezo ya muda mfupi na wa kati kwa msiba tuliopata.
(Ombi: Lakini lazima pawe na kipindi cha kuwafunza hawa watoto kabla ya kuwapa mtihani mwingine. Nadhani sote tunajua uchache/uduni wa elimu na mafunzo waliyopata ktk miaka yao minne)
 
Ninaelewa sympathy ya Mwanakijiji. Lakini kama mtoto kweli alipata sufuri ni pale mtoto hakufundishwa au hakujifunza au wasahihishaji wamesahihisha isivyo. Kama ni wasahihishaji wainue marks zao lakini kama ni vinginevyo kwamba walipata sufuri ya kweli hata ukiongeza marks bado ni sufuri, yaani chuo kikuu au kozi stahili ya ex-form IV hafundishiki, mwisho wa kozi ni sufuri kuongeza tatizo katika shughuli za maendeleo yetu. Ninachoshauri angalau ni kurudia form IV kwa gharama ya serikali kwa ajili ya kupewa cheti cha Division IV mwisho wa mwaka isipokuwa kwa wale watakaorudia kufanya mtihani watapewa stahili yao.
 
ndugu umeandika mengi mazuri lkn kumbuika kuna shule ambazo hazina waalimu wa masomo fulani na zingine hazina hata maabara. hata iweje wanafunzi wakarudia mitihani yao watafeli tu! we fikiria mwanafunzi kashindwa hata kupata dv 4 kwa miaka 4 sijui kama mwanafunzi huyohuyo ataweza kufaulu ndani ya mwaka mmoja. labda itokee wakamua kutunga mtihani au warudishe mtihani wa darasa la saba waliofanya kipindi cha nyuma wakati wanatafuta nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza.
 
Unapoteza nguvu yako kwimbimbai huyu mtu wimbo ambao hawezi kuuelewa. JK bwana, ni janga la Tanzania
 
Nimepata maswali mengi juu ya suluhisho lako nayo ni;

  1. 1.Hivi ni lazima katika kila mitihani kwa mwanafunzi kufaulu?
  2. Hivi kuna ulazima wowote kwa wanafunzi hawa kurudia mitihani yao eti kwa sababu wamefeli mitihani kwa vigezo vya mazingira yao,vipato vya wazazi/walezi wao?
  3. Hivi elimu ni cheti au maharifa? Kwa maana ya kuwa si kweli kwamba wale wote waliofeli mitihani yao eti wamefeli katika maisha yao,vipi wale wote walioipata elimu yao tena kwa kiwango kikubwa, je wana mchango gani hasa kwa wenzao ambao hawakuipata na wale ambao hawakuipata elimu wana hasara gani au faida gani kwa wale walioipata?
  4. Hivi ni haki kabisa kuifanya elimu kama sehemu ya majaribiox2 ya fikra za watu kuwatawala wenzao kifikra na kimkakati?
  5. Hivi elimu ni mojawapo ya masuala ya kifamilia au ni jukumu la serikali?
  6. Mwisho,Hivi takwimu zinasemaje kuhusu wale ambao walifeli mitihani yao na kuamua kurudia mitihani yao,je wali/wamefaulu kwa kiasi gani?.
Ni vema suala hili tukalichukulia kwa pande zote kwa kuwa ni suala mtambuka.
 
MMM ubarikiwe.

Ila naomba kuboresha au kutofautiana kidogo ktk approach, (emphasize on order):-

1) a) Waziri wa Elimu na wateuliwa wenzake wote Wizarani wajiuzulu.
b) Waziri wa TAMISEMI na wateuliwa wenzake wote Wizarani wajiuzulu2
c) NECTA waoneshe uwajibikaji. Pia DEDs na Maofisa Elimu mikoa na wilaya.

2) Matokeo haya yawe suspended (temporarily or else)

3) Tume huru iundwe kuchunguza matatizo tuliyonayo ktk mfumo na sera yetu ya Elimu. Ikiwezekana ndani ya siku 90 waje na majibu.

4) Maoni uliyotoa yaingie kama mojawapo ya mapendekezo ya muda mfupi na wa kati kwa msiba tuliopata.
(Ombi: Lakini lazima pawe na kipindi cha kuwafunza hawa watoto kabla ya kuwapa mtihani mwingine. Nadhani sote tunajua uchache/uduni wa elimu na mafunzo waliyopata ktk miaka yao minne)


Wakati mwingine suala la elimu liko kigenetiki na uchangiwa na mazingira na mfumo wa dunia,hawa unaowatuhumu hawakuwa kwenye vichwa vya watahiniwa.
 
Tuwapeleka JKT ambako watapatiwa msaada wa ukweli juu ya mustakabali wa maisha yao. huko watatusaidia kugundua vipaji vyao na kuwapatia maarifa ya fani mbalimbali za kazi
 
hii slogani ya kikwete ya tumethubutu, tumeweza, na tunasonga mbele kwa jinsi mambo yanavyokwenda na huu ukimya wake wa kutokuchukua hatua nafikiri huko kusonga mbele ni kuelekea kaburi
 
Swali: baraza la mitihani ndilo linatunga mitaalaya kufundishia?
Mzee Mwanakijiji
Ni wazi kuna kujichanganya kwa hali juu kati ya Wizara na baraza; ni hivi mitaala ya kufundishia ya wizara ni UKOCHA wa SOKA na mitaala ya kutungia mitihani ya baraza UKOCHA wa RIADHA hicho ndicho kinachofanyika; tatizo kubwa la kufeli lilianza miaka waliyobadili mfumo wa masomo; kwa maana hiyo watendaji wa hivyo vyombo viwili wote waondolewe; na itengenezwe tume ya wataalamu walioboboea kwenye masuala ya elimu; tume isiwajumuishe wanasiasa.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Chama, tatizo la watoto wetu kufeli siyo suala la Waislamu tu. Mwaka jana katika mjadala kama huu ambapo baadhi ya watu walionesha jinsi shule za Waislamu zilivyokuwa zimefeli mimi nilionesha jinsi ya shule zenye majina ya Kikristu nazo zilifelisha. Watu wengine wanapoona majina ya seminari za Kikatoli zinapofanya vizuri wanaweza kufikiria kuwa shule zote za Kikristu watoto wake wanafaulu kwa sababu ni za Kikristu na za Waislamu wanafeli kwa sababu watoto ni WAislamu. Matokeo ya mwaka huu kwa mfano shule ya TAQWA ya Mwanza ina watoto wamefanya vizuri kuliko shule nyingi za "St. Nanino".

Hata hivyo tukiangalia kwa kutazama 'dini' tunaweza tukakosa kabisa. Ni lazima tuangalie kuwa hawa watoto wa Kiislamu ni watoto wa Kitanzania. Kufeli kwao ni hasara kwa Taifa siyo kwa Uislamu! Wanapofeli watoto wa Kikristu Muislamu hapaswi kufurahia (kwamba we are even) bali kusikitika pia kwa sababu wanaofeli ni watoto wa Kitanzania. Hatuwezi kulitatua tatizo la elimu while holding parochial sentiments...

Ni tatizo letu, na linatuhusu sote equally.
Mzee Mwanakijiji
Wakati nilipogusia kuhusu malalamiko ya waislamu kuhusu baraza; sikulenga kwenye udini; lengo lilikuwa ni kugusia matatizo yaliyokuwepo ambayo ndiyo yalikuwa kiini cha malalamiko yale; laiti kama wadau wengi wangekaa chini na kuondoa hisia za kidini na kuangalia undani wa tatizo lenyewe nina uhakika leo tungekuwa tumefanikiwa kuondoa baadhi ya matatizo yanayoikabili sekta ya elimu; katika moja ya malalamiko yao ilikuwa utoaji wa matokeo kitu ambacho baraza walikiri sasa je tutajuaje kama hilo tatizo limeondoka au bado ni jinamizi linawaumiza watoto wetu?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Mapimbi wapo CCM na upimbi ni sifa moja kuu ya kuwa MwanaCCM halafu ndio unakuwa mfu.

Mbona Chadema wapo wengi tu na mmoja ndiye ninayejibishana naye!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
. Mtindo wa sasa wa makampuni makubwa kutoa madawati, mabati halafu wanakimbia haujasaidia kuinua elimu; makampuni yahamasishwe (ikiwemo motisha wa aina fulani katika kodi -tax incentive) kulea shule za sekondari. Tax breaks makampuni yatapata endapo shule wanazozilea hazitakuwa na madaraja ya IV na 0



Kwa kuwepo zawadi kwa kufanya vizuri / kutokuwepo kufanya vibaya kutapelekea kuchakachua.., hivi unadhani ni kwanini kuna watoto wameshinda Darasa la Sababu na hawajui hata kuandika.. ?

Yes you guessed it, kuchakachua ili shule zionekane wanafunzi wake wengi wanafaulu mitihani
 
Binafsi Hiyo taarifa ya raisi imekuwa suprise kwangu najaribu kuvuta picha nashindwa kuifananisha Na endapo angekuwa active kufunguka katika maswala yote yanayotokea nchini hasa yanayoanzia bungeni basi ningempa Credit Angalau Kama mmemuelewa vizuri kwa majibu aliyotoa hapo juu kumbe kilichotufikisha hapa ni uzembe wa serikali ndio maana katika majibu anaetakiwa kutekeleza ni serikali yenyewe
sasa kasahau jambo moja tena sio kuwa kasahau ila kajisahaulisha kama kawaida yake sisi ambao kodi zetu ndio zitatumika kuchapisha mitihani ya marudio tunataka awajibishwe mtu aliyefanya uzembe wa kutufikisha hapa kwasababu 2015 Mbali

AHSANTE
 
nilitaka kuandika makala ndefu lakini nimeona niende moja kwa moja na kusema ombi/pendekezo langu kama litampendeza rais kikwete.

kwa kuwa, matokeo ya kidato cha nne ambayo yametoka hivi karibuni yameonesha kufeli kwa kutisha kwa watoto wetu katika mtihani wao;

kwa kuwa
, kufeli huko kuna matokeo ya moja kwa moja katika maisha ya wanafunzi hawa, familia zao na kwa taifa kwa u jumla;

kwa kuwa
, matokeo hayo ni hasara kubwa kwa wazazi waliowekeza kwa miaka minne ya elimu ya watoto hawa na kwa taifa katika kuwekeza vifaa, walimu na miundo mbalimbali;

kwa kuwa, kuacha kundi kubwa la watoto hawa kurudi katika maisha ya uraiani kutaongeza jamii ya watu ambao hawana elimu ya kutosha na wasioweza kuajiriwa hata katika mifumo isiyo rasmi (pamoja na kushindwa kujiajiri wenyewe);

kwa kuwa, kufeli kwa watoto hawa ninaamini siyo kosa lao peke yao bali pia ni kosa la utawala na uongozi wetu, wazazi na jamii kwa ujumla;

ninaamini kuwa, kutokuchukua uamuzi wa makusudi na wa lazima kuwasaidia watoto hawa kuwapa nafasi nyingine ni kuwahukumu katika maisha duni na kuwanyima kimsingi nafasi ya kuinuka wakati tayari wameshaanguka

ninaamini kuwa, matokeo haya ni dhambi na aibu ya taifa letu hasa katika nchi ambayo inajivunia kuwa ina 'shule nyingi, vyuo vingi, walimu wengi, na teknolojia ya kisasa katika elimu;

ninaamini kuwa, ni jukumu la uongozi wa kisiasa wa taifa kuchukua hatua za haraka na za lazima kuwapa nafasi nyingine watoto hawa kuweza kutengeneza waliposhindwa.

ninaamini kuwa, taifa lina deni kwa watoto hawa, lina deni kwa historia, lina deni kwa familia zao na kwa hakika kabisa lina deni kwa maisha ya watoto hawa. Deni hili tusiliache likue lije kushindwa kulipika. Naamini tunaweza kulilipa kabla halijaanza kuwa na riba isiyokamatika!

Kutokana na mambo yote hayo juu na mengine ambayo nimeyaadhania, ninaamini utawala wa rais kikwete unaitwa na historia, unadaiwa na haki, na unalazimishwa na wajibu kuwapa watoto hawa nafasi nyingine ya kurudia mitihani ya kidato cha nne ili kuweza kuinua alama zao za kufaulu, kusahihisha makosa yao na kuwapa nafasi ya kuweza kuendelea na elimu ya kidato cha tano na cha sita. Kutokana na hili:

hivyo basi, baraza la mawaziri lifanye kikao cha dharura kuhusiana na matokeo haya ya mitihani ambapo uamuzi wa kutengua matokeo yote ya mtihani uchukuliwe na kuyafuta kabisa matokeo hayo;

na hivyo basi
, baada ya kufuta matokeo hayo serikali iamue kuwa watoto wote waliofanya mtihani huu uliopita watarudia mitihani yote ya kidato cha nne ndani ya mwaka mmoja pamoja na watoto watakaokaa katika mtihani wa mwaka huu au katika mtihani mwingine tofauti

na hivyo basi
, watoto wote ambao katika mtihani huu wamepata daraja la i na ii watakuwa na uhuru wa ama kurudia mtihani wao ili kuthibitisha kufaulu kwao au kuendelea na matokeo waliyonayo. Wakiamua kurudia basi kama watafaulu alama za juu zaidi ya sasa watashika alama hizo kama watapata alama za chini watashika alama zao za sasa;

na hivyo basi
, wanafunzi waliopata daraja iii na 0 nao itakuwa hivyo hivyo, watapewa nafasi moja ya kurudia mitihani yote kuiinua viwango vyao na wale watakaopata viwango vya juu kuliko vya sasa basi watasika viwango hivyo na wale ambao watapata viwango vya chini kuliko sasa watashika viwango vya sasa.

na hivyo basi, wanafunzi ambao sasa wamepata daraja la iii na 0 endapo watarudia mitihani ijayo na wakainua viwango vyao na kuwa kati ya daraja la i na ii basi serikali itawapa nafasi ya kusoma bore kidato cha tano na cha sita katika shule za sekondari za serikali. Hii iwe 'ahadi ya taifa' (national promise)

na hivyo basi, ili kutoa motisha kwa shule na walimu ambao wanawafundisha wanafunzi hawa na wengine basi serikali ianze kutoa motisha kwa shule zote (zenye watahiniwa wengi) ambazo zitafaulisha watoto wengi kwenye madaraja ya i na ii. Motisha huu utakuwa kwa shule na kwa jopo la walimu wa kidato cha nne.

- shule ambayo haitatoa daraja 0 kuanzia sasa itapata zawadi ya shilingi milioni 50 kwa matumizi ya sule
- shule ambayo haitatoa daraja iv kuanzia sasa itapata zawadi ya silingi milioni 75 kwa matumizi yake
- walimu wanaofundisha shule hizo zikiwa na matokeo hayo watagawana zawadi ya nusu ya tuzo hizo (milioni 25 kama hakuna 0, milioni 37.5 kama hakuna daraja la iv)

tuzo hizo zinaweza kurudiwa kila mwaka endapo viwango hivyo vitaendelea.

na hivyo basi, mwalimu mkuu wa shule ambazo zinafanya vibaya zaidi watafukuzwa kazi, afisa elimu wa wilaya yenye shule nyingi zilizofanya vibaya nao watafukuzwa kazi.

na hivyo basi, kuanzia sasa wanafunzi wote wanaopata daraja la iv na 0 watakuwa wanapata automatic resit ya mtihani katika mwaka unaofuatia. Na katika hili napendekeza wanafunzi wote waliopata madaraja hayo katika miaka mitano iliyopita na ambao wangependa kurudia mitihani wapewe nafasi hiyo na wao wakifaulu kama hapo juu serikali iwagharimie kidato cha tano na cha sita.

pamoja na hayo, baraza la mawaziri liangalie kwa kina haja ya kuufumua mfumo wetu wa elimu kukidhi changamoto ambazo tumeziona sasa. Baadhi ya mabadiliko hayo:

- kuondoa elimu kutoka kuwa suala la mfumo wa kitaifa (decentralization of the education system)
- kuweka miaka mitatu ya kwanza ya elimu kuwa ni ya lazima katika 3r (hisabati, kuandika, na kusoma)
- kuweka mwaka wa kwanza kwenye o'level kuwa wa kiingereza na hisabati na lugha (pre-secondary) - miaka mitatu ya mwiso kufanya elimu ya o'level
- serikali ikutanishe wadau wa elimu kutoka shule zinazofanya vizuri zaidi kushirikisha mawazo yao na wadau wa shule nyingine (kongamano la kitaifa kuhusu elimu - national education reform conference)
- makampuni na taasisi binafsi na za umma zitakiwe kuadopt shule za msingi na za sekondari na yashiriki katika uendeshaji na uboreshaji wake. Mtindo wa sasa wa makampuni makubwa kutoa madawati, mabati halafu wanakimbia haujasaidia kuinua elimu; makampuni yahamasishwe (ikiwemo motisha wa aina fulani katika kodi -tax incentive) kulea shule za sekondari. Tax breaks makampuni yatapata endapo shule wanazozilea hazitakuwa na madaraja ya iv na 0


mmm - bgm

* kwa kweli nimeandika kwa haraka bila kufikiria mengi zaidi na implication yake na hivyo ni mchango wangu kidogo tu wa mawazo ya nini tufanye sasa hivi na baadaye. Nina uhakika watu wengine wana mawazo bora zaidi. Jambo moja ambalo hatupaswi kukubali na kuliachilia ni matokeo haya kusimama. Ni lazima yatenguliwe kama tunaamini katika utu, usawa na haki kwa watoto wetu.
inaonekana unajua kilichowafeli na kwanini warudie hawa tu. Division zero hazijaanza hata enzi za mwalimu zilikuwepo. Tusonge mebele lakini serkali na kauli za kikwete kuwa kura za watumishi na hasa za waalimu hazimnyimi usingizi leo anaziona waziwazi. Kama anaakili inabidi awaangukie la sivyo hali ya mwakani hakuna cha div i wala ii ni iii kwenda chini
 
TV na simu -- umeme kwani upo nchi nzima? vijijini ambako nyingi ya shule zilizofanya vibaya zinapatikana umeme ni anasa.

Mwanakijiji, asante kwa kutoa mwongozo nini kifanyike kwa kipindi kifupi.
 
Naogopa kusema utakimbilia kuniban kwenye thread yako ila akili za kibinadamu kidogo zimeanza kurudi; najua huu ni msiba wa wengi mtakuja na kila aina ya suluhisho; kama unakumbuka mwaka jana waislamu walilamika sana kuhusu Wizara ya elimu na Baraza la mitihani; kama wengi wenu humu JF mngeelewa kilichokuwa kinalalamikiwa labda matokeo ya leo div 0 zingekuwa 1000 tu; ila nashukuru Mungu ukweli umeanza kujionesha.

Chama
Gongo la mboto DSM

Mimi nadhani tatizo ni kubwa kuliko linavofikiriwa. Kwa kiasi kikubwa(mawazo yangu) mmomonyoko wa maadili katika jamii una mchango mkubwa sana katika hili, wanaofeli sio sekondari tu bali hatu vyuoni na huko kuna baraza la mitihani?

Kuna mchangiaji mmoja ameshauri wazazi wawajibike kuwaondelea starehe watoto wao ikiwemo pamoja na maTV simu watoto wanalala usiku mwingi si kwa ajili ya kusoma bali kufanya mambo ya hovyo hovyo,hata mwanasiasa mmoja karibuni aliyekuwa anamtukana mwanasiasa mwingine ambaye aweza kuwa mzazi wake ni zao la mmomonyoko wa maadili, turudishe maadili hili la kufaulu litawezekana.

Haki Elimu nao watusaidie katika hili walikuja wakapiga kelele walimu wanawatenda wanafunzi sasa imefika hatua walimu hawana mamlaka juu ya wanafunzi tena hivi karibuni huko Pwani walimu wa kike walikimbia shule baada ya kutishiwa kubakwa na wanafunzi wao sasa hapo unategemea kuna kufundishana kweli? au kutakuwa na mwalimu mwenye nia ya dhati ya kumsaidia mwanafunzi ambaye tayari anajiona ni mkubwa mwenzie?
 
Back
Top Bottom