Nilitaka kuandika
makala ndefu lakini nimeona niende moja kwa moja na kusema
ombi/pendekezo langu kama litampendeza Rais Kikwete.
KWA KUWA, matokeo ya kidato cha nne ambayo yametoka hivi karibuni
yameonesha kufeli kwa kutisha kwa watoto wetu katika mtihani wao;
KWA KUWA, kufeli huko kuna matokeo ya moja kwa moja katika maisha ya
wanafunzi hawa, familia zao na kwa taifa kwa u jumla;
KWA KUWA, matokeo hayo ni hasara kubwa kwa wazazi waliowekeza kwa
miaka minne ya elimu ya watoto hawa na kwa taifa katika kuwekeza vifaa,
walimu na miundo mbalimbali;
KWA KUWA, kuacha kundi kubwa la watoto hawa kurudi katika maisha
ya uraiani kutaongeza jamii ya watu ambao hawana elimu ya kutosha na
wasioweza kuajiriwa hata katika mifumo isiyo rasmi (pamoja na kushindwa
kujiajiri wenyewe);
KWA KUWA, kufeli kwa watoto hawa ninaamini siyo kosa lao peke yao
bali pia ni kosa la utawala na uongozi wetu, wazazi na jamii kwa
ujumla;
NINAAMINI KUWA, kutokuchukua uamuzi wa makusudi na wa lazima
kuwasaidia watoto hawa kuwapa nafasi nyingine ni kuwahukumu katika
maisha duni na kuwanyima kimsingi nafasi ya kuinuka wakati tayari
wameshaanguka
NINAAMINI KUWA, matokeo haya ni dhambi na aibu ya taifa letu hasa
katika nchi ambayo inajivunia kuwa ina 'shule nyingi, vyuo vingi,
walimu wengi, na teknolojia ya kisasa katika elimu;
NINAAMINI KUWA, Ni jukumu la uongozi wa kisiasa wa taifa kuchukua
hatua za haraka na za lazima kuwapa nafasi nyingine watoto hawa kuweza
kutengeneza waliposhindwa.
NINAAMINI KUWA, Taifa lina deni kwa watoto hawa, lina deni kwa
historia, lina deni kwa familia zao na kwa hakika kabisa lina deni kwa
maisha ya watoto hawa. Deni hili tusiliache likue lije kushindwa
kulipika. Naamini tunaweza kulilipa kabla halijaanza kuwa na riba
isiyokamatika!
Kutokana na mambo yote hayo juu na mengine ambayo nimeyaadhania,
ninaamini Utawala wa Rais Kikwete unaitwa na historia, unadaiwa na haki,
na unalazimishwa na wajibu kuwapa watoto hawa nafasi nyingine ya
kurudia mitihani ya kidato cha nne ili kuweza kuinua alama zao za
kufaulu, kusahihisha makosa yao na kuwapa nafasi ya kuweza kuendelea na
elimu ya kidato cha tano na cha sita. Kutokana na hili:
HIVYO BASI, Baraza la Mawaziri lifanye kikao cha dharura
kuhusiana na matokeo haya ya mitihani ambapo uamuzi wa kutengua matokeo
yote ya mtihani uchukuliwe na kuyafuta kabisa matokeo hayo;
NA HIVYO BASI, Baada ya kufuta matokeo hayo serikali iamue kuwa
watoto wote waliofanya mtihani huu uliopita watarudia mitihani yote ya
kidato cha nne ndani ya mwaka mmoja pamoja na watoto watakaokaa katika
mtihani wa mwaka huu au katika mtihani mwingine tofauti
NA HIVYO BASI, Watoto wote ambao katika mtihani huu wamepata daraja
la I na II watakuwa na uhuru wa ama kurudia mtihani wao ili kuthibitisha
kufaulu kwao au kuendelea na matokeo waliyonayo. Wakiamua kurudia basi
kama watafaulu alama za juu zaidi ya sasa watashika alama hizo kama
watapata alama za chini watashika alama zao za sasa;
NA HIVYO BASI, Wanafunzi waliopata daraja III na 0 nao itakuwa hivyo
hivyo, watapewa nafasi moja ya kurudia mitihani yote kuiinua viwango
vyao na wale watakaopata viwango vya juu kuliko vya sasa basi watasika
viwango hivyo na wale ambao watapata viwango vya chini kuliko sasa
watashika viwango vya sasa.
NA HIVYO BASI, Wanafunzi ambao sasa wamepata daraja la III na 0
endapo watarudia mitihani ijayo na wakainua viwango vyao na kuwa kati ya
daraja la I na II basi SERIKALI itawapa nafasi ya kusoma bore kidato
cha tano na cha sita katika shule za Sekondari za Serikali. Hii iwe
'AHADI YA TAIFA' (National Promise)
NA HIVYO BASI, ili kutoa motisha kwa shule na walimu ambao
wanawafundisha wanafunzi hawa na wengine basi serikali ianze kutoa
motisha kwa shule zote (zenye watahiniwa wengi) ambazo zitafaulisha
watoto wengi kwenye madaraja ya I na II. Motisha huu utakuwa kwa shule
na kwa jopo la walimu wa kidato cha nne.
- Shule ambayo haitatoa daraja 0 kuanzia sasa itapata zawadi ya shilingi
milioni 50 kwa matumizi ya sule
- Shule ambayo haitatoa daraja IV kuanzia sasa itapata zawadi ya silingi
milioni 75 kwa matumizi yake
- Walimu wanaofundisha shule hizo zikiwa na matokeo hayo watagawana
zawadi ya nusu ya tuzo hizo (Milioni 25 kama hakuna 0, milioni 37.5 kama
hakuna daraja la IV)
Tuzo hizo zinaweza kurudiwa kila mwaka endapo viwango hivyo vitaendelea.
NA HIVYO BASI, Mwalimu Mkuu wa shule ambazo zinafanya vibaya
zaidi watafukuzwa kazi, Afisa Elimu wa Wilaya yenye shule nyingi
zilizofanya vibaya nao watafukuzwa kazi.
NA HIVYO BASI, kuanzia sasa wanafunzi wote wanaopata daraja la IV
na 0 watakuwa wanapata automatic resit ya mtihani katika mwaka
unaofuatia. Na katika hili napendekeza wanafunzi wote waliopata madaraja
hayo katika miaka
big up sana mkubwa!