Pendekezo kwa Rais Kikwete kuhusu wanafunzi waliofeli...

Pendekezo kwa Rais Kikwete kuhusu wanafunzi waliofeli...

kwa kiasi fulani namuunga mkono mkj, amini msiamini kuna watoto wamefeli lakini sio wajinga, tena wanasonononeka sana sasa, na hawajui wafanyeje, maana hawakutegemea majibu ya namna hiyo, hao wakipewa second chance wanaweza wakatoka, kama tu ni makosa ya kawaida yalifanyika, au bahati mbaya walipanic.
 
Yote ni kufunga mlango wakati zizi liko tupu; mifugo iliishaibiwa zamani na kwato hazionekani walikopita!
 
NECTA wametoa mfano wa shule ambako wote hawakujibu maswali ya Biology kwani hawajawahi kuwa na mwalimu wa hilo somo. Sasa wakirudia bila kupata kwanza mwalimu wa Biology si watashindwa tena kujibu tu?

Deal with the causes of the problem and not only the consequences.
 
Nilitaka kuandika makala ndefu lakini nimeona niende moja kwa moja na kusema ombi/pendekezo langu kama litampendeza Rais Kikwete.

KWA KUWA, matokeo ya kidato cha nne ambayo yametoka hivi karibuni yameonesha kufeli kwa kutisha kwa watoto wetu katika mtihani wao;

KWA KUWA
, kufeli huko kuna matokeo ya moja kwa moja katika maisha ya wanafunzi hawa, familia zao na kwa taifa kwa u jumla;

KWA KUWA
, matokeo hayo ni hasara kubwa kwa wazazi waliowekeza kwa miaka minne ya elimu ya watoto hawa na kwa taifa katika kuwekeza vifaa, walimu na miundo mbalimbali;

KWA KUWA, kuacha kundi kubwa la watoto hawa kurudi katika maisha ya uraiani kutaongeza jamii ya watu ambao hawana elimu ya kutosha na wasioweza kuajiriwa hata katika mifumo isiyo rasmi (pamoja na kushindwa kujiajiri wenyewe);

KWA KUWA, kufeli kwa watoto hawa ninaamini siyo kosa lao peke yao bali pia ni kosa la utawala na uongozi wetu, wazazi na jamii kwa ujumla;

NINAAMINI KUWA, kutokuchukua uamuzi wa makusudi na wa lazima kuwasaidia watoto hawa kuwapa nafasi nyingine ni kuwahukumu katika maisha duni na kuwanyima kimsingi nafasi ya kuinuka wakati tayari wameshaanguka

NINAAMINI KUWA, matokeo haya ni dhambi na aibu ya taifa letu hasa katika nchi ambayo inajivunia kuwa ina 'shule nyingi, vyuo vingi, walimu wengi, na teknolojia ya kisasa katika elimu;

NINAAMINI KUWA, Ni jukumu la uongozi wa kisiasa wa taifa kuchukua hatua za haraka na za lazima kuwapa nafasi nyingine watoto hawa kuweza kutengeneza waliposhindwa.

NINAAMINI KUWA, Taifa lina deni kwa watoto hawa, lina deni kwa historia, lina deni kwa familia zao na kwa hakika kabisa lina deni kwa maisha ya watoto hawa. Deni hili tusiliache likue lije kushindwa kulipika. Naamini tunaweza kulilipa kabla halijaanza kuwa na riba isiyokamatika!

Kutokana na mambo yote hayo juu na mengine ambayo nimeyaadhania, ninaamini Utawala wa Rais Kikwete unaitwa na historia, unadaiwa na haki, na unalazimishwa na wajibu kuwapa watoto hawa nafasi nyingine ya kurudia mitihani ya kidato cha nne ili kuweza kuinua alama zao za kufaulu, kusahihisha makosa yao na kuwapa nafasi ya kuweza kuendelea na elimu ya kidato cha tano na cha sita. Kutokana na hili:

HIVYO BASI, Baraza la Mawaziri lifanye kikao cha dharura kuhusiana na matokeo haya ya mitihani ambapo uamuzi wa kutengua matokeo yote ya mtihani uchukuliwe na kuyafuta kabisa matokeo hayo;

NA HIVYO BASI
, Baada ya kufuta matokeo hayo serikali iamue kuwa watoto wote waliofanya mtihani huu uliopita watarudia mitihani yote ya kidato cha nne ndani ya mwaka mmoja pamoja na watoto watakaokaa katika mtihani wa mwaka huu au katika mtihani mwingine tofauti

NA HIVYO BASI
, Watoto wote ambao katika mtihani huu wamepata daraja la I na II watakuwa na uhuru wa ama kurudia mtihani wao ili kuthibitisha kufaulu kwao au kuendelea na matokeo waliyonayo. Wakiamua kurudia basi kama watafaulu alama za juu zaidi ya sasa watashika alama hizo kama watapata alama za chini watashika alama zao za sasa;

NA HIVYO BASI
, Wanafunzi waliopata daraja III na 0 nao itakuwa hivyo hivyo, watapewa nafasi moja ya kurudia mitihani yote kuiinua viwango vyao na wale watakaopata viwango vya juu kuliko vya sasa basi watasika viwango hivyo na wale ambao watapata viwango vya chini kuliko sasa watashika viwango vya sasa.

NA HIVYO BASI, Wanafunzi ambao sasa wamepata daraja la III na 0 endapo watarudia mitihani ijayo na wakainua viwango vyao na kuwa kati ya daraja la I na II basi SERIKALI itawapa nafasi ya kusoma bore kidato cha tano na cha sita katika shule za Sekondari za Serikali. Hii iwe 'AHADI YA TAIFA' (National Promise)

NA HIVYO BASI, ili kutoa motisha kwa shule na walimu ambao wanawafundisha wanafunzi hawa na wengine basi serikali ianze kutoa motisha kwa shule zote (zenye watahiniwa wengi) ambazo zitafaulisha watoto wengi kwenye madaraja ya I na II. Motisha huu utakuwa kwa shule na kwa jopo la walimu wa kidato cha nne.

- Shule ambayo haitatoa daraja 0 kuanzia sasa itapata zawadi ya shilingi milioni 50 kwa matumizi ya sule
- Shule ambayo haitatoa daraja IV kuanzia sasa itapata zawadi ya silingi milioni 75 kwa matumizi yake
- Walimu wanaofundisha shule hizo zikiwa na matokeo hayo watagawana zawadi ya nusu ya tuzo hizo (Milioni 25 kama hakuna 0, milioni 37.5 kama hakuna daraja la IV)

Tuzo hizo zinaweza kurudiwa kila mwaka endapo viwango hivyo vitaendelea.

NA HIVYO BASI, Mwalimu Mkuu wa shule ambazo zinafanya vibaya zaidi watafukuzwa kazi, Afisa Elimu wa Wilaya yenye shule nyingi zilizofanya vibaya nao watafukuzwa kazi.

NA HIVYO BASI, kuanzia sasa wanafunzi wote wanaopata daraja la IV na 0 watakuwa wanapata automatic resit ya mtihani katika mwaka unaofuatia. Na katika hili napendekeza wanafunzi wote waliopata madaraja hayo katika miaka mitano iliyopita na ambao wangependa kurudia mitihani wapewe nafasi hiyo na wao wakifaulu kama hapo juu serikali iwagharimie kidato cha TANO na cha SITA.

PAMOJA NA HAYO, Baraza la Mawaziri liangalie kwa kina haja ya kuufumua mfumo wetu wa elimu kukidhi changamoto ambazo tumeziona sasa. Baadhi ya mabadiliko hayo:

- Kuondoa Elimu kutoka kuwa suala la mfumo wa kitaifa (decentralization of the education system)
- Kuweka miaka mitatu ya kwanza ya elimu kuwa ni ya lazima katika 3R (Hisabati, Kuandika, na Kusoma)
- Kuweka mwaka wa kwanza kwenye O'Level kuwa Wa Kiingereza na Hisabati na Lugha (Pre-Secondary) - miaka mitatu ya mwiso kufanya elimu ya O'level
- Serikali ikutanishe wadau wa elimu kutoka Shule zinazofanya vizuri zaidi kushirikisha mawazo yao na wadau wa shule nyingine (KONGAMANO LA KITAIFA KUHUSU ELIMU - NATIONAL EDUCATION REFORM CONFERENCE)
- Makampuni na taasisi binafsi na za umma zitakiwe kuadopt shule za msingi na za sekondari na yashiriki katika uendeshaji na uboreshaji wake. Mtindo wa sasa wa makampuni makubwa kutoa madawati, mabati halafu wanakimbia haujasaidia kuinua elimu; makampuni yahamasishwe (ikiwemo motisha wa aina fulani katika kodi -tax incentive) kulea shule za sekondari. Tax breaks makampuni yatapata endapo shule wanazozilea hazitakuwa na madaraja ya IV na 0


MMM - BGM

* Kwa kweli nimeandika kwa haraka bila kufikiria mengi zaidi na implication yake na hivyo ni mchango wangu kidogo tu wa mawazo ya nini tufanye sasa hivi na baadaye. NIna uhakika watu wengine wana mawazo bora zaidi. Jambo moja ambalo hatupaswi kukubali na kuliachilia ni matokeo haya kusimama. Ni LAZIMA yatenguliwe kama tunaamini katika utu, usawa na haki kwa watoto wetu.
Mzee Mwanakijiji mapendekezo mazuri sana ila hapo kwenye tuzo; serikali itaogopa maana tuzo zitaishia kule kwa shule za kanisa. Hata hivyo pamoja na uzuri wa mapendekezo; andiko hili kama lilivyo ungemgaia Mh.Kigwangala au Lusinde serikali ya CCM ingeweza kulifanyia kazi
 
Last edited by a moderator:
Mkuu. MMJ,

asante kwa ushauri wako mzuri.

Eneo la kutoa motisha kwa shule zilizofanya vizuri liliwahi kujaribiwa kilichotokea ni kuongezeka kwa udangavyifu na wizi wa mitihani ambapo waalimu walianza kuwasaidia wanafunzi wao majibu ilishule ifanye vizuri na shule zingine zilianza kufungua mtihani na kutoa maswali mapema kwa wanafunzi.

Waliofaulu naona waendelee tu lakini waliofeli ndio tutafute ufumbuzi wake.mapendekezo yako mengine yawemo katika kutafuta jibu sahihi.
 
Chama, tatizo la watoto wetu kufeli siyo suala la Waislamu tu. Mwaka jana katika mjadala kama huu ambapo baadhi ya watu walionesha jinsi shule za Waislamu zilivyokuwa zimefeli mimi nilionesha jinsi ya shule zenye majina ya Kikristu nazo zilifelisha. Watu wengine wanapoona majina ya seminari za Kikatoli zinapofanya vizuri wanaweza kufikiria kuwa shule zote za Kikristu watoto wake wanafaulu kwa sababu ni za Kikristu na za Waislamu wanafeli kwa sababu watoto ni WAislamu. Matokeo ya mwaka huu kwa mfano shule ya TAQWA ya Mwanza ina watoto wamefanya vizuri kuliko shule nyingi za "St. Nanino".

Hata hivyo tukiangalia kwa kutazama 'dini' tunaweza tukakosa kabisa. Ni lazima tuangalie kuwa hawa watoto wa Kiislamu ni watoto wa Kitanzania. Kufeli kwao ni hasara kwa Taifa siyo kwa Uislamu! Wanapofeli watoto wa Kikristu Muislamu hapaswi kufurahia (kwamba we are even) bali kusikitika pia kwa sababu wanaofeli ni watoto wa Kitanzania. Hatuwezi kulitatua tatizo la elimu while holding parochial sentiments...

Ni tatizo letu, na linatuhusu sote equally.


Mwanakijiji. Bravo for your input and thought catching thread. Ni kweli kabisa swala la kushindwa tusiliangalie kwa jicho la dini hata kidogo. Waislamu walilalalmikia takwimu zilizokuwa zimekosewa which is human error lakini yawezekana kuna wahanga wa human errors wengine sana na labda hawapati access ya kuweza ku-capture hizo errors na hivyo kiushia kukosa haki yao. Lakini hili la mwaka huu ni zaidi ya human errors bali ni janga la kitaifa ambalo linahitaji mjadala wa kitaifa ili lisijirudie. Si swala la shule za kiislamu au Kikristu. Lakini Watanzania tujifunze kuwa tunafatilia mambo, matukio na tafiti zinazofanywa.

Mwaka 2010 Watafiti wanaoitwa UWEZO walitoa matokeo ya tafiti yao moja kuhusu elimu ya shule msingi kwa nchi za A.Mashariki-Kenya, Uganda na Tanzania kwa vipimo vya hesabu (numeracy), Kiingereza na Kiswahili. Kenya ilionekana kufanya vizuri sana katka masomo yote hata iliposhindanishwa na Tanzania kwa Kiswahili bado Kenya iliizidi Tanzania. Labda kama sikufatilia lakini matokeo haya hayakuzusha mjadala mpana kati ya wasomi wetu .Nilitegemea matokeo haya yangejadiliwa na tukajiuliza kwanini hata Kiswahili -lugha ya taifa na kufundishia at Primary Level bado tulifanya vibaya. Sasa matokeo yake tumeyapata.

Na labda niendelee kuwaambia watu ambao wanafikiri swala la kufail ni la kidini au kikabila au kikanda wanajidangaya. Mkoa wa KAGERA hasa wilaya za Bukoba mjini na vijijini, Karagwe, Buleba na sasa kuna wilaya ya Misenyi iliyomegwa kutka mjini na vijijini zili[iga hatua kubwa kielimu kufatana na mfumo wa kikoloni wa Favouritism na hali hiyo iliendelea mpaka miaka ya mwanzo ya tisini. Sasa hivi ni kati mkoa unaofanya vibaya kielimu. Matokeo ya utafiti wa uwezo yanataja wilaya zilizokuwa za mwisho kwa hiyo assessment Bukoba vijijini iliyokuwemo. Sasa kama wilaya, mikoa na maeneo kama haya nao wanatakiwa wajiulize ni kwanini kama eneo na taifa kwa ujumla.

Leo nimemsikia Waziri kivuli wa elimu -Lymo kupitia CDM. Kati ya mambo aliyochangia moja ni kuzifanya shule hizi za kata kuwa na mchepuo wa ufundi kwa maana si wote wanaweza kwenda A-Level bali wachache na wengine wanaweza kujiajiri maana watakuwa na skills. Na Mwalimu MKOBA ameongezea kuwa wote wanaweza kwenda elimu ya juu. Sasa hawa tuanawaweka wapi. Ufundi ndio suluhu. Serikali ifate ushauri huu hata kama umetoka kwa wapinzani. Tuachane na majigambo ya kuwa tuna vyuo vikuu vingi lakini vyenye wahitimu wasiokuwa na tija maana wana poor background na ili wafaulru wanatumia mbinu za ajabu. Huu ni ukweli mchungu tuna wasomi wa vyeti wengi kuliko skills and knowledge
 
Wachangiaji wengi wametoa maoni mazuri (ukiacha wale wachache ambao wanaeleweka kwa kutoa pumba). Iko haja ya kutafuta jopo litakalochambua maoni haya na serikali iyafanyie kazi. Kwa kweli hali ni mbaya na hili ni janga ambalo linatakiwa kutolewa maamuzi magumu maka moja...
 
Walimu wastaafu wanambinu nzuri za ufundishaji kuliko hawa walimu wetu wa tiGO Faster

Na wewe utukome, we si umefundishwa na waalimu hawa hawa? Nani kakudanganya kuwa hatuna mbinu za kufundisha? Tena ushindwe, Tatizo la msingi hapa mnaliacha na kukimbilia kwenye matokeo ya tatizo. Tukigoma kudai maslahi yetu nyie mnakuwa wakwanza kutulaumu na kutuona kama wahaini. Sasa tufanye nini? Kazi ni moja tu, na bado!!!! Mwakani kutakuwa na kilio na kusaga meno. Tunajua kweli, hawa watoto hawatendewi haki, lakini tufanye nini? Tukiandamana tunapigwa virungu na vitisho vingi.
Sasa tunataka wananchi wenye watoto wao waliofeli waishinikize serikali walioiweka madarakani kuboresha mazingira ya kufundishia, Kuongeza vifaa vya kufundishia na kujifunzia, kuboresha mazingira ya mwalimu, (Nyumba za walimu na mahitaji ya muhimu kama umeme na maji viwepo), serikali iboreshe maslahi ya mwalimu ikiwa ni pamoja na mishahara, posho, na malipo ya ziada kwa waalimu wanaofundisha masomo ya sayansi, kwani tunateseka sana ikifika kipindi cha mitihani. Vinginevyo, wembe ni ule ule, unaacha notes watoto wanakopi unarudi staff kuandaa lesson plan, scheme of work na log book. Hizo ndizo kazi ambazo zinaendana na mishahara tunayolipwa.
 
Naogopa kusema utakimbilia kuniban kwenye thread yako ila akili za kibinadamu kidogo zimeanza kurudi; najua huu ni msiba wa wengi mtakuja na kila aina ya suluhisho; kama unakumbuka mwaka jana waislamu walilamika sana kuhusu Wizara ya elimu na Baraza la mitihani; kama wengi wenu humu JF mngeelewa kilichokuwa kinalalamikiwa labda matokeo ya leo div 0 zingekuwa 1000 tu; ila nashukuru Mungu ukweli umeanza kujionesha.

Chama
Gongo la mboto DSM

Waislam last year walilalamikia baraza la mitihani na Joyce Ndalichako na ni kwa mtihani wa dini yao,
lakini hii unaweza kuconclude kuwa sababu za kufeli wanafunzi ni baraza lamtihani?
 
Na wewe utukome, we si umefundishwa na waalimu hawa hawa? Nani kakudanganya kuwa hatuna mbinu za kufundisha? Tena ushindwe, Tatizo la msingi hapa mnaliacha na kukimbilia kwenye matokeo ya tatizo. Tukigoma kudai maslahi yetu nyie mnakuwa wakwanza kutulaumu na kutuona kama wahaini. Sasa tufanye nini? Kazi ni moja tu, na bado!!!! Mwakani kutakuwa na kilio na kusaga meno. Tunajua kweli, hawa watoto hawatendewi haki, lakini tufanye nini? Tukiandamana tunapigwa virungu na vitisho vingi.
Sasa tunataka wananchi wenye watoto wao waliofeli waishinikize serikali walioiweka madarakani kuboresha mazingira ya kufundishia, Kuongeza vifaa vya kufundishia na kujifunzia, kuboresha mazingira ya mwalimu, (Nyumba za walimu na mahitaji ya muhimu kama umeme na maji viwepo), serikali iboreshe maslahi ya mwalimu ikiwa ni pamoja na mishahara, posho, na malipo ya ziada kwa waalimu wanaofundisha masomo ya sayansi, kwani tunateseka sana ikifika kipindi cha mitihani. Vinginevyo, wembe ni ule ule, unaacha notes watoto wanakopi unarudi staff kuandaa lesson plan, scheme of work na log book. Hizo ndizo kazi ambazo zinaendana na mishahara tunayolipwa.

Hili nalo neno"
 
Wakuu haya mambo mazuri kuhusu elimu yetu hata siku moja hayatakuja kimiujiza. We need to invest heavily in education. Kuanzia kwenye utayarishaji wa walimu, ujenzi wa shule zenyewe, vitendea kazi, vitabu, teknohama etc. Same way kama wabunge na maofisa wa serikali wanavyokurupukia kila mshangingi mapya yakiingia, tufanye hivyo hivyo na kwenye elimu basi.

Tatizo serikali ya CCM inaona elimu ni kama mzigo na betcha kama kungekuwa na uwezekano wa kuongoza serikali bila kushghulika na masuala ya elimu nadhani serikali ya CCM ingeikimbilia upesi sana hiyo alternative. Mipango yote ya elimu Tanzania ni kutegemea misaada. Kwa nini tusiweke uzalendo mbele na kusema well, this is something we can do it on our own. Tukaahirisha mambo yote tukakomaa na elimu. Just imagine tukasema kuanzia leo katika kila tozo la VAT 2.5% iende kwenye elimu. Tukaweka siku ya elimu ya Taifa na siku hiyo ni kumobilize kila mwananchi kuchangia chochote alichonacho kuchangia matatizo ya kielimu in a short term, iwe ni fedha, ujuzi wa ufundi, nguvu kazi u name it. La msingi na ambalo limeahirishwa kwa muda mrefu ni kuongeza viwango na kuwa consistent juu ya nini maana ya shule.
 
Pendekezo lako ni zuri kwa asilimia kubwa ila bado halijaangalia kiini cha tatizo na linakimbilia kulekule kwenye kutafuta suluhu ya haraka ambayo bado haitatufaa kwa kujenga taifa la wasomi imara.

Haiingii akilini kuona hakuna mtoto mwenye akili wa kupata Div I ya point 7 au 8 kufikia mwanafunzi bora kuanza na point 9. Kwanza hapa napata shaka na aina ya mtihani waliofanya. Haiwezekani kama mtaala ni uleule uliotumika miaka 2 iliyopita huwezi kuniambia hawa wa mwaka huu ni vilaza kiasi hiki. Shule ni mazingira bora ya kusomea na ubora wa walimu shule ambazo zimekuwa vinara ktk matokea hasa za private zinajitahidi sana kuboresha mazingira lazima kuna shida ya mtihani wa mwaka huu.

Pili hizi shule zetu nyingine hata kama leo hii tukisema watoto wetu warudie masomo katika mwaka huu kama amekaa darasani kwa miaka 4 bila ya kuona mwalimu wa masomo kama hisabati, biology, chemistry na physics itakuwa ngumu kwake leo kuota na kwenda kufaulu katika mwaka wake mmoja. Hii ni moja ya sababu iliyotolewa na Mtendaji mkuu wa Necta ambayo kwangu inamashiko makubwa sana kwa mustakabali wa elimu. Watoto watafaulu vipi kama hawajawahi kufundishwa somo hili hivyo walichofanya ni kuingia na kuandika namba za mitihani kisha kutoka na kuondoka zao hapa nani wa kulaumiwa kama sio wizara ya elimu na serikali kwa ujumla wake?

Yapo mengi ambayo tunatakiwa kuyatanabaisha likiwemo pia tatizo la wanafunzi kutopenda kujifunza wao wenyewe hawasomi na wanafikiri shule ni lelemama unakwenda tu kisha muda ukifika utaondoka umefaulu bila kuweka jitihada. watoto hawa jitihada kubwa kwao ni kwenye muziki wa kizazi kipya na mitandao ya kijamii kama facebook. Tunahitaji kongamano la kitaifa kujadili namna bora ya kuweka mazingira ya kuinua kiwango chetu cha elimu na kujenga taifa la wasomi wenye maarifa ya kutosha kwa sasa tunajenga taifa la kijinga. Tunazidi kutizama katika wingi wa wanafunzi wanaomaliza kama mafanikio na kusahau wamemaliza kwa ufaulu upi.
Mr Professional uliyosema ni kweli, mtoto suruhisho sio kurudia mtiani pekee ila walimu wapewe motisha kama walivyo omba!! Serikali inyenyekee iwaombe walimu msamaha kwa kuwanyanyasa waboreshewe maslahi, walipwe madeni yao!! Serikali isifanye kiburi kuuwa watoto wa watu itafute budget sijui wapi ili iboreshe swala la elimu kama inavyo fanyaga wakati wa majanga na hili ni janga la kitaifa!!! Baraza la mawaziri, bunge letu tukufu na Raisi wa nchi wasifanye mzaha hili ni janga litafutiwe ufumbuzi wa haraka period!!!!

 
Mapendekezo yako ni mazuri ajabu, bahati mbaya umeyatoa kwa nchi isiyosikia. Ngoja nikukumbushe kitu kimoja Mwanakijiji, Nchi ikishauriwa na mtu ambaye hayuko kwenye system yao tena wa karibu kabisa na utawala, hawawezi kuufanyia kazi ushauri huo kwani wanafikiri wataaibika, watapuuza na kutoa visababu vya ajabu. Mapendekezo yako mengi uliyoandika hata sisi wadau wa elimu siku moja tulikaa na tukafikiri mambo hayo ndo serikali iyafanye baada ya matokeo kuwa mabaya, lakini hata hivyo naamini Serikali itakuja na tamko la ajabu au hata wanaweza kunyamaza kimya!! Ungekuwa nchi za wenzetu naamini wangekuchukuwa wewe na Mbatia na ingeundwa kamati maalum ili muweze kuangalia elimu yetu kwa undani kwa kutoa mapendekezo ya nini kifanyike
 
Napendekeza pia vile Vyuo vya Ualimu ambavyo vilikuwa vinafundisha masomo maalumu kama Hisabati na Sayansi virudishwe ( kwani vilikuwepo na Mungai akavifuta kwasababu anazozifahamu yeye. Nahisi siyo m-TZ).
 
Mr Professional uliyosema ni kweli, mtoto suruhisho sio kurudia mtiani pekee ila walimu wapewe motisha kama walivyo omba!! Serikali inyenyekee iwaombe walimu msamaha kwa kuwanyanyasa waboreshewe maslahi, walipwe madeni yao!! Serikali isifanye kiburi kuuwa watoto wa watu itafute budget sijui wapi ili iboreshe swala la elimu kama inavyo fanyaga wakati wa majanga na hili ni janga la kitaifa!!! Baraza la mawaziri, bunge letu tukufu na Raisi wa nchi wasifanye mzaha hili ni janga litafutiwe ufumbuzi wa haraka period!!!!


Asante sana mkuu Mtumishi Wetu kwangu mie bado hata kama mishahala ya walimu leo ikifikia mara 2 au 3 ya wanachookiomba nadhani inachangia kwa kiasi kisichozidi 10% ya tatizo zima. Tatizo ni kubwa kuliko tunavyolifikilia kila mmoja wetu kwa haraka haraka. kuna walimu ambao watoto wao wamepata 0 je nao waliwawekea watoto wao migomo hadi majumbani mwao. kwa nini asimfundishe mwanaye nyumbani walau apate A au B moja ambayo ingemwokoa na zero au ingepunguza Div IV nyingi hasa zilizo karibu na zero? ubongo wangu huu mdogo unanituma kuamini ya kuwa wapo walimu ambao wanakilio kikubwa kutokana na matokeo haya kutobangua we ulimalizia shule ipi yaani shule zote matokeo ni ya ovyo ovyo ovyo.

Hebu tuliangalie tatizo kimfumo zaidi, usimamizi wa mfumo mzima, mazingira elimu hii itolewapo, na vitendea kazi kwa ajiri ya kupata elimu bora.

Hebu tufumbue jicho la tatu kwa kuangalia wingi na utitiri wa shule hizi ambazo tuliwaambia watawala wetu mapema wakati wanatulazimisha kujenga kuwa ubora wa elimu haupimwi kwa wingi wa shule hizi bali utapimwa kwa namna watakavyoweza kuzihudumia na kutoa matunda bora wao wakaweka pamba masikioni na kutupuuza. Haiingii akilini kuwa na Shule 5000 usizoweza kuzihudumia kwa nini usizipunguze na kubakia na shule 2000 unazoweza kuzihudumia kikamilifu na watu tukaona matunda yake. Tuanze na kufunga shule zote zisizo na walimu au zenye walimu wachache na hakuna uwezekano wa kuzipatia waalimu kwa sasa kutokana na matatizo ya kibajeti zote hizi tuzifunge. Tujaze vitabu vya kiada na ziada mashuleni kote. Tuweke maabara na vifaa vyake mashuleni pia tupeleke waalimu wenye utaalamu kwa ajili ya maabara hizo. Lakini pia tunaweza kusimamisha mitihani hii kwa shule zote tunazoona zipo hoi mahututi walau kwa miaka miwili huku tukiwa tumewapelekea walimu wazuri na vifaa vyote vinilivyotaja hapo juu tutakuwa tumesaidia bila ya kusahau kufumua mitaala yote ya elimu pamoja na watendaji wake hasa wizara ya elimu kwa kushindwa kusimamia elimu ya nchi hii.

Baraza la mitihani limeonekana halina huruma wala chembechembe yake katika kuboresha elimu yetu naomba sana tuliache jinsi lilivyo maana shule sio sehemu ya kufaulu kwa kuonewa huruma au kwa kuibiwa mitihani ndo ufaulu. Baraza liboreshwe utendaji wake ila mama Ndalichako abakizwe na kuendelea kuwa mtendaji mkuu wa baraza hili.

Lakini pia tuangalie mfumo wetu wa udahili wa waalimu wetu kuanzia ngazi ya elimu ya msingi mpaka vyuoni kama kweli unamaslahi na tija kwa taifa kama hauna nao ufumuliwe waalimu wanatakiwa kuwa the best and not the rest kama ilivyo sasa. Wenye Div IV kwenye matokeo haya na III za mwishoni ndo watachukuliwa kwenda kuandaliwa kuwa walimu wa elimu ya msingi hapa tunakuwa hatujengi ila tumefunika uchafu chini ya kapeti siku ukivunda na kutoa harufu mbaya utatuumbua
 
Last edited by a moderator:
Naogopa kusema utakimbilia kuniban kwenye thread yako ila akili za kibinadamu kidogo zimeanza kurudi; najua huu ni msiba wa wengi mtakuja na kila aina ya suluhisho; kama unakumbuka mwaka jana waislamu walilamika sana kuhusu Wizara ya elimu na Baraza la mitihani; kama wengi wenu humu JF mngeelewa kilichokuwa kinalalamikiwa labda matokeo ya leo div 0 zingekuwa 1000 tu; ila nashukuru Mungu ukweli umeanza kujionesha.

Chama
Gongo la mboto DSM

unamaana pia tulaumu bunge kwa kutompa fursa DOGO JANJA kujadili hoja yake ya baraza la mitihani?
 
Naogopa kusema utakimbilia kuniban kwenye thread yako ila akili za kibinadamu kidogo zimeanza kurudi; najua huu ni msiba wa wengi mtakuja na kila aina ya suluhisho; kama unakumbuka mwaka jana waislamu walilamika sana kuhusu Wizara ya elimu na Baraza la mitihani; kama wengi wenu humu JF mngeelewa kilichokuwa kinalalamikiwa labda matokeo ya leo div 0 zingekuwa 1000 tu; ila nashukuru Mungu ukweli umeanza kujionesha.

Chama
Gongo la mboto DSM

:rockon:Wanajulikana waliokaa kidinidini tu wewe ndie unajua malalamikoya waislamu walikuwa wanataka nini,ulivyo na akili za kidini
 
naona ukiondoa hizo motisha za zawadi, .ni suala lingine muhimu kuangalia ufahamu wa mitaala kwa walimu wenyewe...
 
Back
Top Bottom