Pendekezo: Kuanzishwe Kodi mpya ya Kusanyiko la watu

Pendekezo: Kuanzishwe Kodi mpya ya Kusanyiko la watu

Ungeandika tu kwa kifupi "SERIKALI IPIGE MARUFUKU MIKUTANI YA CHADEMA". kila mtu angekuelewa
Pole sana kwa kupata mawazo ya namna hiyo. Lengo hapa ni kuweka ubunifu hasa kwenye kuongeza pato kwa taifa.
 
Tanganyika ilitafuta uhuru wa nini toka kwa mkoloni mweupe kama mkoloni mweusi anawaza kumnyonya na kumkandamiza ndugu yake zaidi?🦍🦍
Unahisi walitafuta uhuru wa kukufanya wewe leo uishi bure?
 
Tumepata uhuru mwaka 1961 hata mtoa mada baba yake hajazaliwa.Enzi ya mkoloni ilikuwa hairuhusiwi kutembea zaidi ya watu watano au kukusanyika zaidi ya watu watano.
Leo anatokea mtu anataka hii sheria irudiwe.
Ukisema hivyo watu wa kwanza kuivunja ni CCM maana hawatafanya vikao
Nchi namba ya watu inazidi kuongezeka kila leo. Huo mwaka ulioutaja huenda hata mahitaji yake huwezi fananisha na leo.
Kwanini hutaki kuifanyia kitu Tanzania; unalalama nini Tanzania ikufanyie?
Pole kwa uchungu. Haya ni mawazo yasikupe uchungu mbaya.
 
Kwamba tukikusanyika kupiga kura tulipe kodi kwanza?
Rejea somo tajwa hapo juu. Hii iwe mahususi kwa wale wote wenye nia ya kujinufaisha na Umma. Mbona watu wa Mabango wanalipa kwanini wasiwe watu wanaokusanya watu huku wakinufaika rafiki.
 
Yaani Dhahabu, Almasi, Tanzanite na Gesi zinatupwa Ulaya na China kwa bei ya madafu halafu sisi tukamuliwe kodi ya kukusayika?.. Upo sawa ndugu?
Maendeleo ni hatua. Hakuna dhahabu au almasi wala Tanzanite ya kuokota. Uwekezaji hasa wa mitambo ya kisasa ya uchimbaji, uchenjuaji na utakatishaji mzuri. Unahisi mitambo itapatikana vipi ili hizo madini zisitupwe huko kwenye nchi ulizozitaja?
 
Habari Tanzania !.

Naomba kupendekeza wazo la kodi hasa toka chanzo kipya " KUSANYIKO LA WATU".

Pawepo na utaratibu wa kutoza Kodi sehemu ambapo mtu au watu au taasisi wanaotaka kunufaika na Umma kwa namna yoyote ile walipe Kodi ya kusanyiko ili liwe chachu kwa taifa letu. Kukusanya watu sehemu fulani kuna leta changamoto za Uharibifu wa miundombinu, kuzizorotesha huduma za jamii sehemu tukio linakofanyika nk. Tulijenge Taifa letu kwa pamoja.

Sasa naomba tujiwekeee utaratibu wa hii Kodi mpya ya Kusanyiko la watu/ Umma kwa mtu au watu, kikundi au taasisi walipie kwa mwaka.

NB

Taasisi za kidini pekee wasiguswe na hii huduma ya kodi.

Ahsante.
Mkipata msiba mpigwe kodi. Mkutano wa ujenzi wa shule msingi, kusaidia kwenye ajari, wizi, ujambazi, harusi unataka watu walipe kodi.
 
Mkipata msiba mpigwe kodi. Mkutano wa ujenzi wa shule msingi, kusaidia kwenye ajari, wizi, ujambazi, harusi unataka watu walipe kodi.
Mbona Maiti inatozwa tozo. Wewe unaishi dunia ipi hiyo ya ubwela?
 
Maendeleo ni hatua. Hakuna dhahabu au almasi wala Tanzanite ya kuokota. Uwekezaji hasa wa mitambo ya kisasa ya uchimbaji, uchenjuaji na utakatishaji mzuri. Unahisi mitambo itapatikana vipi ili hizo madini zisitupwe huko kwenye nchi ulizozitaja?
Ukishaachiwa mashimo ndo utatafuta maendeleo?
Kwani hayo madini hayawezi kudhamini huo uwekezaji mpaka upokee 15% kwenye uhai wote wa uchimbaji?
 
Habari Tanzania !.

Naomba kupendekeza wazo la kodi hasa toka chanzo kipya " KUSANYIKO LA WATU".

Pawepo na utaratibu wa kutoza Kodi sehemu ambapo mtu au watu au taasisi wanaotaka kunufaika na Umma kwa namna yoyote ile walipe Kodi ya kusanyiko ili liwe chachu kwa taifa letu. Kukusanya watu sehemu fulani kuna leta changamoto za Uharibifu wa miundombinu, kuzizorotesha huduma za jamii sehemu tukio linakofanyika nk. Tulijenge Taifa letu kwa pamoja.

Sasa naomba tujiwekeee utaratibu wa hii Kodi mpya ya Kusanyiko la watu/ Umma kwa mtu au watu, kikundi au taasisi walipie kwa mwaka.

NB

Taasisi za kidini pekee wasiguswe na hii huduma ya kodi.

Ahsante.
Bora ianzishwe kodi ya kutoa kodi, yaani kila senti unayolipa kama kodi nayo itozwe kodi kudhibiti upotevu wa mapato.
 
Back
Top Bottom