kwa taarifa yako kilichotokea Zanzibar ni zaidi ya siasaYaani kachomoka mzazi wako huendi kisa siasa?waliangalie jambo hili kwa mtizamo mwingine.
Wa Ccm,thats all....YOTE HAYA KISA UROHO TU WA MADARAKA.
Poleni sana kama siasa ndio inakufanya mtu muhasimiane na familia yako. Kitu kinacho nishangaza mnajiita waislam sasa hiyo dini yenu inasemaje kuhusu ndugu, jirani na hivyo mnavyotaka kuishi. Sasa huyo mzazi au kaka,au,mjomba wako akiwa ccm na Yuko Huko pemba je Ulimuangalia ukaona maisha yake bora kukushinda wewe au nyote mko sawa? Msifate mkumbo hao mnaowafata maisha yao manono. Walipo sema wazee damu nzito kuliko maji inamaana yake.
Huko Mungu yuko chini siasa iko juu, eti nimtelekeze mzazi wangu mtoto wangu ama Dada yangu kisa siasa, hiyo siasa nilizaliwa nayo ama nimeikuta tu. Kilichofanywa na CCM huko Zanzibar ikishurikiana na tume ya uchaguzi si cha kuungwa mkono, ila hunigombanishi na ndugu zangu sababu tu mapenzi yao kisiasa ni tofauti na mimi. Alafu pembeni nadai haki nada Demokrasia nini sasa maana ya haki nini maana Demokrasia, eti alafu uneanda msikitini mara tano, huku kifua kimejaa chuki, wanaojifanya wanaijua dini ndiyo watenda dhambi wakubwa.
Poleni sana kama siasa ndio inakufanya mtu muhasimiane na familia yako. Kitu kinacho nishangaza mnajiita waislam sasa hiyo dini yenu inasemaje kuhusu ndugu, jirani na hivyo mnavyotaka kuishi. Sasa huyo mzazi au kaka,au,mjomba wako akiwa ccm na Yuko Huko pemba je Ulimuangalia ukaona maisha yake bora kukushinda wewe au nyote mko sawa? Msifate mkumbo hao mnaowafata maisha yao manono. Walipo sema wazee damu nzito kuliko maji inamaana yake.
Najua ila yote kwa yote nipo tayari hata kutoa uhai wangu kwa ajili ya watu wangu wa karibu, na sio nipotayari kuwapoteza kwa sababu ya siasa. Ni kweli maneno ya siasa ni kila kitu, ila usisahau maneno ya haya pia ni kisiasa. Ni nani alalae kula kwa raha pale anapopata habari, mwanae/ mzazi wake anaumwa.Siasa ni kila kitu kama ulikuwa ujui. Bila Siasa hakuna nchi
View attachment 334432
#Pemba.
Wanachama wa CUF Wilaya ya, Majimbo yote matano (Wete, Kojani, Mgogoni, Mtambwe na Gando) leo wameafikiana ktk kikao chao kuendelea na mgomo rasmi juu ya CCM kwa mambo yote ya kijamii ikiwemo Arusi,Misiba,Biashara, Ugonjwa na hata magari na meli na kuazimana vitu/vfaa vya majumbani nk. (CUF kwa CUF na CCM kwa CCM tu mpaka kieleweke)
"Mikutano ya Matawi kwa sheiha zote za Wilaya ya Wete itafanyika kwa uhamasishaji zaidi, katika hatua hio bila kujali uzawa/udugu, din...i, kabila au tunapo toka.
Tumekubaliana kama aliefiliwa ni CUF mmoja au wawili au idadi yeyote basi kuungana nae ni kutokwenda kwenye msiba huo uliowakuta wana CCM waliomo ndani ya familia yake.
HAYO TUME KUBALIANA"
Alisema mmoja wa wafuasi hao wa CUF.
Kwa mujibu wa uislam ikiwa wote ndugu tena katika dini hamsemezani mkifa wote motoni, sasa hao cuf kwa kuwa wao ndio wanaoanzisha chuki hizo na kusababisha waislam kutosemezana na kusaidia wajiandae kwenye motoni, wanatoka katika uislam, katika hiloi sharifu hamadi moto wa jehanam unamsubiri kwa uroho wake unawasababishia waislam wachukiane na anabariki hizo chuki hana tofauti na kafiri,
SolutionUmesema kweli kabisa: Ila tunaomba fatwa ya watu walioandaliwa na ccm wanaovaa masoksi usoni kushambulia watu kwa silaha za moto, mapanga na visu kuwahujumu watu kisa tu ni wanacuf, lakini pia watu kubambikiziwa kesi na kulazwa ndani siku kadhaa na mateso mbali mbali, waislamu wanaofanywa matendo haya wanatakiwa kufanya nini?
Watu walitumia muda mwingi baada ya maumivu makali kufuta na kusahau yaliyopita halafu watu wachache kwa ulafi wa madaraka wanaturudisha tulipotoka!na walaaniwe!Kwani CCM walitarajia nini? Haya mambo yalikuwepo na ndio yalipelekea kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Kwa hiyo wasishangae yanapotokea haya kwa sababu wao (CCM) ndio wameikataa SUK kwa kusigina demokrasia huko visiwani.