Pemba: Migomo Imeanza Kushamiri CUF dhidi ya CCM

5523

JF-Expert Member
Nov 13, 2014
2,260
2,383
12920361_851464351666429_6862052667170825609_n.jpg

#‎Pemba‬.
Wanachama wa CUF Wilaya ya, Majimbo yote matano (Wete, Kojani, Mgogoni, Mtambwe na Gando) leo wameafikiana ktk kikao chao kuendelea na mgomo rasmi juu ya CCM kwa mambo yote ya kijamii ikiwemo Arusi,Misiba,Biashara, Ugonjwa na hata magari na meli na kuazimana vitu/vfaa vya majumbani nk. (CUF kwa CUF na CCM kwa CCM tu mpaka kieleweke)
"Mikutano ya Matawi kwa sheiha zote za Wilaya ya Wete itafanyika kwa uhamasishaji zaidi, katika hatua hio bila kujali uzawa/udugu, din...i, kabila au tunapo toka.

Tumekubaliana kama aliefiliwa ni CUF mmoja au wawili au idadi yeyote basi kuungana nae ni kutokwenda kwenye msiba huo uliowakuta wana CCM waliomo ndani ya familia yake.
HAYO TUME KUBALIANA"
Alisema mmoja wa wafuasi hao wa CUF.
 
Siasa za chuki zimerudi tena kama awali hii miaka 10 ilopita ndivyo waliviyokuwa wakiishi, imam akiwa CCM , wa C.U.F. haingii kuswali, Sijajua hawa watu wanamuabudu mungu yupi kwakweli alieagiza kuwatendea majirani mambo hayo, naomba hizi habari zisiwe za kweli.
 
Akili nyingine tope kweli, mnaacha kusaidiana kwa sababu ya wanasiasa!!
Mnadhani wanawajali kiasi hicho.
Ndugu, yajalini maisha yenu na jamii zenu.... wanasiasa watawagombanisha na mwisho wa siku hamtawaona.
 
Poleni sana kama siasa ndio inakufanya mtu muhasimiane na familia yako. Kitu kinacho nishangaza mnajiita waislam sasa hiyo dini yenu inasemaje kuhusu ndugu, jirani na hivyo mnavyotaka kuishi. Sasa huyo mzazi au kaka,au,mjomba wako akiwa ccm na Yuko Huko pemba je Ulimuangalia ukaona maisha yake bora kukushinda wewe au nyote mko sawa? Msifate mkumbo hao mnaowafata maisha yao manono. Walipo sema wazee damu nzito kuliko maji inamaana yake.
 
View attachment 334432

#‎Pemba‬.
Wanachama wa CUF Wilaya ya, Majimbo yote matano (Wete, Kojani, Mgogoni, Mtambwe na Gando) leo wameafikiana ktk kikao chao kuendelea na mgomo rasmi juu ya CCM kwa mambo yote ya kijamii ikiwemo Arusi,Misiba,Biashara, Ugonjwa na hata magari na meli na kuazimana vitu/vfaa vya majumbani nk. (CUF kwa CUF na CCM kwa CCM tu mpaka kieleweke)
"Mikutano ya Matawi kwa sheiha zote za Wilaya ya Wete itafanyika kwa uhamasishaji zaidi, katika hatua hio bila kujali uzawa/udugu, din...i, kabila au tunapo toka.

Tumekubaliana kama aliefiliwa ni CUF mmoja au wawili au idadi yeyote basi kuungana nae ni kutokwenda kwenye msiba huo uliowakuta wana CCM waliomo ndani ya familia yake.
HAYO TUME KUBALIANA"
Alisema mmoja wa wafuasi hao wa CUF.

Wajinga hao. Wapemba wa Ilala Buguruni nendeni huko mkaungane na wasuria wa Pemba mpembuke vizuri
 
Sasa nyie wananchi wa Pemba mkifanyiana hivi mnamkomesha nani?

Wanasiasa wanaendelea na maisha yao Maalim akiumwa Shein anamjulia hali wewe babu yako akifariki auendi kumzika kisa ni mwana ccm.
Umenena ukweli mkuu. Politicians wakitanzania wengi wao ni wanafiki sana. Hata wabunge wakiwa bungeni na hasa wakiwa live mapovu huwatoka lakini ukiwakuta usiku wanakula kuku choma mitaa ya DOM wakifurahia na dada Poa.mambo ya kijamii yasiharibiwe na uamuzi wa wachache ambao family zao zimehamishiwa ughaibuni. Wapemba wawe na subira usuluhishi wa sintofahamu hii utapatikana soon.
 
Siasa za chuki zimerudi tena kama awali hii miaka 10 ilopita ndivyo waliviyokuwa wakiishi, imam akiwa CCM , wa C.U.F. haingii kuswali, Sijajua hawa watu wanamuabudu mungu yupi kwakweli alieagiza kuwatendea majirani mambo hayo, naomba hizi habari zisiwe za kweli.
Huko Mungu yuko chini siasa iko juu, eti nimtelekeze mzazi wangu mtoto wangu ama Dada yangu kisa siasa, hiyo siasa nilizaliwa nayo ama nimeikuta tu. Kilichofanywa na CCM huko Zanzibar ikishurikiana na tume ya uchaguzi si cha kuungwa mkono, ila hunigombanishi na ndugu zangu sababu tu mapenzi yao kisiasa ni tofauti na mimi. Alafu pembeni nadai haki nada Demokrasia nini sasa maana ya haki nini maana Demokrasia, eti alafu uneanda msikitini mara tano, huku kifua kimejaa chuki, wanaojifanya wanaijua dini ndiyo watenda dhambi wakubwa.
 
View attachment 334432

#‎Pemba‬.
Wanachama wa CUF Wilaya ya, Majimbo yote matano (Wete, Kojani, Mgogoni, Mtambwe na Gando) leo wameafikiana ktk kikao chao kuendelea na mgomo rasmi juu ya CCM kwa mambo yote ya kijamii ikiwemo Arusi,Misiba,Biashara, Ugonjwa na hata magari na meli na kuazimana vitu/vfaa vya majumbani nk. (CUF kwa CUF na CCM kwa CCM tu mpaka kieleweke)
"Mikutano ya Matawi kwa sheiha zote za Wilaya ya Wete itafanyika kwa uhamasishaji zaidi, katika hatua hio bila kujali uzawa/udugu, din...i, kabila au tunapo toka.

Tumekubaliana kama aliefiliwa ni CUF mmoja au wawili au idadi yeyote basi kuungana nae ni kutokwenda kwenye msiba huo uliowakuta wana CCM waliomo ndani ya familia yake.
HAYO TUME KUBALIANA"
Alisema mmoja wa wafuasi hao wa CUF.

Hii siyo mara ya kwanza ilishatokea siku za nyuma kote Pemba na Zanzibar. Ni akili finyu tu inayowasumbua na Mtume wao ni mmoja tu akishasema yeye basi wote wanafuata bila ya kutafakali!!!
 
Back
Top Bottom