Pemba: Migomo Imeanza Kushamiri CUF dhidi ya CCM

Pemba: Migomo Imeanza Kushamiri CUF dhidi ya CCM

View attachment 334432

#‎Pemba‬.
Wanachama wa CUF Wilaya ya, Majimbo yote matano (Wete, Kojani, Mgogoni, Mtambwe na Gando) leo wameafikiana ktk kikao chao kuendelea na mgomo rasmi juu ya CCM kwa mambo yote ya kijamii ikiwemo Arusi,Misiba,Biashara, Ugonjwa na hata magari na meli na kuazimana vitu/vfaa vya majumbani nk. (CUF kwa CUF na CCM kwa CCM tu mpaka kieleweke)
"Mikutano ya Matawi kwa sheiha zote za Wilaya ya Wete itafanyika kwa uhamasishaji zaidi, katika hatua hio bila kujali uzawa/udugu, din...i, kabila au tunapo toka.

Tumekubaliana kama aliefiliwa ni CUF mmoja au wawili au idadi yeyote basi kuungana nae ni kutokwenda kwenye msiba huo uliowakuta wana CCM waliomo ndani ya familia yake.
HAYO TUME KUBALIANA"
Alisema mmoja wa wafuasi hao wa CUF.

Nadhani nitakaposema kuwa hii hoja sio kweli mtanikubali, hili jengo lipo Wete Pemba, kwenye hayo maduka moja wapo Ni duka la rafiki yangu jina lake la Utani Anaitwa key, upande wa Pili kuna Makao makuu ya Cuf kwa Pemba Ndio kubwa.

Pemba Na Wapemba wameshajifunza siasa Na sasa wanaielewa sio tena wale wa miaka ya 90, tusitegemee kusikia tukio lolote tena kutoka Pemba litalofanywa na wananchi.

Kama una Swali lolote niulize kuhusu Pemba yote nitakuambia.
 
Wajinga hao. Wapemba wa Ilala Buguruni nendeni huko mkaungane na wasuria wa Pemba mpembuke vizuri

Wapemba wa Ilala nao wakienda huko wewe si utakufa njaa na kuzidi kuiangamiza serikali ya Mh. magufuli!!!??? Maana wao ndio moja wapo wa kundi linaloingizia mapato serikali ya Muungano.
 
Kuna vitu vingine wala co vya kucheka lakini iLife jambo linachekesha na linatia hasira sana.siasa siasa siasa
 
CCM mmelitibua na kulikoroga kweli kweli msimu simu huu- watu wanasusa bidhaa za Tanganyika na kununua mbadala. Ya wapi hiyo Kenya au Tanganyika? Amazing!
 
Kwani CCM walitarajia nini? Haya mambo yalikuwepo na ndio yalipelekea kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Kwa hiyo wasishangae yanapotokea haya kwa sababu wao (CCM) ndio wameikataa SUK kwa kusigina demokrasia huko visiwani.
 
View attachment 334432

#‎Pemba‬.
Wanachama wa CUF Wilaya ya, Majimbo yote matano (Wete, Kojani, Mgogoni, Mtambwe na Gando) leo wameafikiana ktk kikao chao kuendelea na mgomo rasmi juu ya CCM kwa mambo yote ya kijamii ikiwemo Arusi,Misiba,Biashara, Ugonjwa na hata magari na meli na kuazimana vitu/vfaa vya majumbani nk. (CUF kwa CUF na CCM kwa CCM tu mpaka kieleweke)
"Mikutano ya Matawi kwa sheiha zote za Wilaya ya Wete itafanyika kwa uhamasishaji zaidi, katika hatua hio bila kujali uzawa/udugu, din...i, kabila au tunapo toka.

Tumekubaliana kama aliefiliwa ni CUF mmoja au wawili au idadi yeyote basi kuungana nae ni kutokwenda kwenye msiba huo uliowakuta wana CCM waliomo ndani ya familia yake.
HAYO TUME KUBALIANA"
Alisema mmoja wa wafuasi hao wa CUF.
JECHA, SHEIN NA MAGUFURI hili lao wameyataka wenyewe
 
Sasa nyie wananchi wa Pemba mkifanyiana hivi mnamkomesha nani?

Wanasiasa wanaendelea na maisha yao Maalim akiumwa Shein anamjulia hali wewe babu yako akifariki auendi kumzika kisa ni mwana ccm.
Hawakomoi viongozi wanakomoa wanachama wa CCM
 
Unajua nilikua napata tabu sana kujua hasa chanzo cha ndugu kutengena kama ilivyo kwa Wakorea kaskazini na kusini ama ilivyokua kwa Ujerumani Magharibi na Mashariki ,ila sasa naanza kupata mwanga kidogo wa ndugu wa damu kutengana
 
Umenena ukweli mkuu. Politicians wakitanzania wengi wao ni wanafiki sana. Hata wabunge wakiwa bungeni na hasa wakiwa live mapovu huwatoka lakini ukiwakuta usiku wanakula kuku choma mitaa ya DOM wakifurahia na dada Poa.mambo ya kijamii yasiharibiwe na uamuzi wa wachache ambao family zao zimehamishiwa ughaibuni. Wapemba wawe na subira usuluhishi wa sintofahamu hii utapatikana soon.


Hebu acha kujibu kiwepes kwenye mambo mazito
 
Sishangai mana wana hicho kisiwa wengi wapo nyuma kielimu...sio ya dini wala sekula ndio mana hukaa na kutoa maamuz mabovu ya karne ya 6.Mana sijui watamkomoa nani since wote ni wa hapo hapo kisiwani.Stupidity
 
Hawa jamaa wakisema wana maanisha ila Ni hatua moja baya Sana kwa nchi maskini Kama Tanzania. Na uroho wa madaraka utafikisha nchi pabaya.
 
Hawa jamaa wakisema wana maanisha hila Ni hatua moja baya Sana kwa nchi maskini Kama Tanzania.
Tatizo sio wapemba wala cuf au ccm tatizo ni viongozi wetu kupora haki ya wanyonge na hayo ni mambo ya kawaida kwa Pemba na unguja tutaona mengi zaidi ya hayo watafute muafaka hili maisha yarudi kama zamani
 
Nimeamini pamoja ushindi "kishindo" Rais Shein atatawala kila kitu Unguja na Pemba lakini siyo myoyo ya Wanzazibari. Haki!
 
Mtahangaika saana kujadili hili hapo ni HUTU vs TUSI wanajuana
 
Nisijuliane hali na ndugu zangu kisa tofauti za kisiasa? wanasiasa wao wanasalimiana, wakiugua wanatembeleana, matibabu yao india, ulaya ama amerika, haya mwenzangu na mie ntafanyaje? sijazaliwa na siasa mie. Wazanzibar malizeni tofauti zenu za kisiasa kwa kumkomoa (kama kweli mnataka kumkomoa) Dr. shein ama mwl. Seif binafsi sio muanze kukomoana nyinyi kwa nyinyi tumieni akili na Mungu mumuombe awape subira na moyo wa kupendana.
 
ndugu wamoja hawa siasa mbovu zinawatenganisha ni kama ukanda wa gaza sasa..shein sura yake inaonesha hataki kabisa hana jinsi na yanayotokea ila jecha anaonesha kabisa anataka iwe ivyo...
 
Ulitaka wafanyeje ili ujue hawapendi kinachofanyika?
huo ni ujinga na upumbavu mkubwa, nimediriki kutumia lugha hii, kwani haipendezi kwa hao ndugu, hili ni tatizo la watawaliwa kutokujua majukumu yao, kwani wao wameacha majukumu yao ss wanaingilia majukumu ya watawala, wanakomoana wao wenyewe kwa ujinga wao, lakini watawala wanakula happy kwa sababu wamewajaza ujinga, Maalim na Shen watakaa pamoja watakunywa gahawa pomoja na kuzungumza, ila nyie wajinga mnajitenga kwa upumbavu wenu.
 
Back
Top Bottom