Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda ndiye ataongoza msafara wa Tanzania katika Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Morocco kuanzia Desemba 21, mwaka huu hadi Januari 18, mwakani.
Hilo limethibitishwa leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Palamagamba Kabudi wakati alipotembelea kambi ya Taifa Stars nchini Misri.
βTuna manaibu waziri wawili. Kuna mmoja ambaye mmeshamzoea, Mwinjuma (Hamisi) lakini pia sasa tuna Naibu Waziri wa pili, Paul Christian Makonda na katika mechi hizi za AFCON Morocco tutakuwa na Paul Christian Makonda,β amesema Kabudi.
Kabudi amesema kwamba Makonda ataungana na Taifa Stars kati ya Desemba 20 au 21 nchini Morocco.
Waziri Kabudi pia amewafikishia salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, wachezaji, maofisa wa benchi la ufundi la Taifa Stars na viongozi wa soka walioambatana na timu hiyo Misri.
View attachment 3517117