Paul Makonda Ameingia Mitini, hatahudhuria Power breakfast ya Clouds FM

Haya mambo ni magumu! Sidhani kama amesingiziwa. Haya yalikuwa yanafanyika sana tena sana. Makonda kijana wa juzi taarifa zake zipo NECTA, it is easy to trace!
Kwani NECTA hakuna watu wakuleta uthibitisho wa division zero ya Makonda? Mbona za mke wa Magufuli walileta.
 
Labda kaenda TBC...

Naona hii Clouds hivi sasa ndio Radio ya Taifa.

Inaelekea JPM anaisikiliza sana clouds ndo maana vijana wake wanapigana vikumbo kuitumia ili bwana mkubwa ausikie utendaji kazi wao uliotukuka wa kutumbua na kuumbua na kutishia...
anajitisha mwenyewe.. kwani njia ya muongo fupi.. na barabara ndefu haikosi kona
 
Imetangazwa hivi sasa kwamba RC wa Dar hatakuwepo leo asubuhi Clouds FM kama ilivyokuwa Imetangazwa jana.
Amepata majukumu ya kitaifa.

My Take:
Ukweli utajulikana tu kama yeye ni Daudi Albert Bashite au Paul Christian Makonda.
Waandishi wa Habari za kiuchunguzi fanyieni kazi hili suala liishe.
Mi nadhani amezingatia ushauri alopewa humu jana
 
Anakesi mahakamani, kwa hiyo hutakiwi mambo ya mahakama kuongelea kwenye vyombo vya habali, ameufyata, chezea Mbowe.
 
Kumkamata Makonda kama kafoji au hajafoji vyeti ni rahisi sana,Watafutwe watu waliosoma Pamba Miaka hiyo na Nyanza watoe ushuhuda wao,lakini pia,Daud Bashite anayesemekana alimuuzia Makonda vyeti atafutwe pia,Wazazi wa Makonda wafuatiliwe (Hapa Investigative Journalism lazima ihusike)ili kupata uhakika,je baba mzazi wa Makonda anaitwa nani?
 
Kumkamata Makonda kama kafoji au hajafoji vyeti ni rahisi sana,Watafutwe watu waliosoma Pamba Miaka hiyo na Nyanza watoe ushuhuda wao,lakini pia,Daud Bashite anayesemekana alimuuzia Makonda vyeti atafutwe pia,Wazazi wa Makonda wafuatiliwe (Hapa Investigative Journalism lazima ihusike)ili kupata uhakika,je baba mzazi wa Makonda anaitwa nani?


Ndio hapo hata Majirani wa hao Wazazi wanajulikana kwa jina gani ? mbona ni rahisi tu mhhh nashangaa inakuwa ishu ndeeefu
 
Duuuh lakini angeitwa kutoa list mpya ya wauza sembe angefika mapema hahaaa
Na angeitwa kumbembeleza scorpion angefika fastaaaa na selfie akapiga na insta akapost jaman mtoto Daud now kijasho kinamtoka hahaaa
 
Ofisi za Shigongo ziko upande wa pili wa barabara na zilipo ofisi za Necta, kwa nini wasiende kufuatilia??
 
Anataka akatengeneze kwanza vyeti ili avitumie kama uthibitisho.

Kila kitu kinawezekana chini ya ccm.hata marehemu anapiga kura
 
Double satandard,kumbuka wengine waliachishwa kazi kwa ajili ya vyeti feki
Hili jambo linalo zungumzwa yapata wiki nzima sasa si jambo dogo kabisa, inabidi lifikie tamati yake,na ili lifikie tamati yake mimi namshauri RC makonda (kwa ujasiri alioonyesha kwenye uongozi wake tangu akiwa kada UVCCM,DC,RC) atoke hadharani aitishe press conference pale ofcn kwake ili kukata mzizi wa fitina. Kama RC aliweza kusimamia issue ya scorpion na akaita press conference pale ofcn wake, hebu abebe ujasiri wa kumaliza hili jambo. Hakika anamweka Mh.Raisi katika wakati mgumu machoni pa Watanzania,kwamba amesimamia zoezi la watumishi hewa na wale wasio na sifa za vyeti kwenye ajira walizo kuwa nazo. Wote walishugulikiwa kufuatana na sheria za nchi. Sasa kijana wangu RC Makonda Kata mzizi huu wa hizi hadithi kwa kuwa mwenye ukweli ni wewe
 
Siyo amtengue. Aliyemteua angeagiza mamlaka husika (wizara ya elimu) ihakiki na impe taarifa! Akikaa kimya inatoa nafasi ya kila MTU kuja na tafsiri yake kuhusu ukimya huu!!! Double standards ni sumu katika jamii! Hatuhitaji amtengue bila kuhakiki, tuhuma zihakikiwe kama si za kweli asafishwe! Kama ni za kweli afanyiwe kama wanavyofanyiwa wengine wa jinsi hiyo! Wengine hufanyiwa hivyo hadharani!

Absolutely Chief.
 
Hivi wafanyakazi walio chini yake wanamuonaje kwa sasa.Boss aliyeghushi cheti cha Form fouur? au yeye anawatazamaje usoni anapowapa maagizo, hivi ana amani kweli?
 
Katibu MKUU necta asipofanyia kazi tuhuma hizi anajinyima uhalali wa kufanyia kazi tuhuma zozote nyingine kuhusu vyeti! Mbona rahisi tu! Ni kufuatilia vyeti vya hawa watu wawili wanaotuhumiwa kupeana vyeti kuanzia SHULE ya msingi hadi vyuoni. Ikibainika ni kweli nitasikitika sana maana wengi tunamheshimu kama Shujaa wa Taifa kuhusiana na vita dhidi ya madawa ya kulevya!
"Msema kweli ni mpenzi wa mungu"
Hili neno siku hizi naona kama limefutika kwa yule mtu
 
Back
Top Bottom