PreGE2025 Patrick Assenga avuliwa Uanachama CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Timu Lissu inafanya udiktekta. Mtu kupinga mtazamo wa chama haimaanishi afukuzwe uanachama.
 
Wewe shida yako nini?
 
Chama kinachopigania uhuru wa kutoa maoni chafanya udikteta kwa kufukuza wanachama wanaotoa maoni mbadala.
 
Misingi ya demokrasia kuifuata yote ni kazi ngumu mno.maana demokrasia inataka hata wachache,wenye mawazo tofauti na ya wengi,nao waheshimiwe!
inatakiwa mawazo yao wachache wasikilizwe, ila nao wasilazimishe mawazo yao kufuatwa
wakitoa mawazo yao na yakakataliwa wawe wapole
 
Fukuzeni mamluki wote hadi wabakie wanachama na viongozi waaminifu wa Cdm.

Mkicheka na nyani mtaambulia mabua.
 
Chama kinachopigania uhuru wa kutoa maoni chafanya udikteta kwa kufukuza wanachama wanaotoa maoni mbadala.
Maoni mbadala nje ya kikao ni usaliti, bahati nzuri kanuni hiyo viongozi hao wanaijua ni wimbo wao wa kila siku wa kimaadili.

Tena kati kati ya mkwamo unaopitia Cdm, huko ni kuonesha nia ya wazi ya kugawana fito.

Wacha wapumzishwe tu, maana hakuna namna.
 
Hakuna democracy chadema kwasasa, kinachoendelea ni udikteta, Nina imani mishale aliyopigwa Mbowe akipigwa Lissu na Heche watafukuza kilamtu 🤣
Wa Kishumundu wewe bila shaka. Mbowe ameondoka kiroho safi yale yalikuwa mambo ya kampeni mbona na Lissu naye alitukanwa saba. Shida mliokuwa mnabunya ruzuku pale HQ ndiyo mnaendelea kubweka na wewe kama siyo John Mrema bahati. Kubalini matokeo.
 
mbona kama unafoka sasa
 
Kama nje ni madikteta hivi kwenye hicho kikao ndo angepewa uhuru wa kutoa maoni?
 
Barua makini iliyoandikwa kitaalamu (professionalized letter) tena toka kwa kiongozi wa ngazi ya chini ya tawi tu...

Lakini barua za kina afande kamanda Jumanne Muliro (RPC - kanda maalumu DSM), ni hovyo, unprofessional utadhani viongozi hawa wenye dhamana kubwa kuongoza taasisi nyeti na muhimu, polisi kama hakwenda shule kabisa...

Kamanda mzima anaaindika "Father Charles Kitima alikuwa akipata kinywaji...🤔🤔🤔🤔"
 
Misingi ya demokrasia kuifuata yote ni kazi ngumu mno.maana demokrasia inataka hata wachache,wenye mawazo tofauti na ya wengi,nao waheshimiwe!
Mawazo tofauti yanaheshimiwa kwenye vikao halali lakini kupinga maamuzi halali ya vikao ni uhaini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…