Patrick Assenga arejea CHADEMA akitokea CHAUMMA

Aliyekuwa Kada wa CHAUMMA, Patrick Assenga ametangaza kukihama chama hicho na kurejea Chama CHADEMA ambacho kimsingi ni chama alichokitumikia kwa miaka mingi kabla ya kuhama hapo

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Jumanne Mei 26.2026, Assenga amesema maamuzi ya kurejea CHADEMA yamekuja baada ya tafakuri ya kina ambayo ameifanya na kujiridhisha pasipo na shaka kwamba CHAUMMA haina mwelekeo na dhamira ya kweli ya kuiondoa CCM madarakani, badala yake amebaini kuwa CHADEMA ndio chama pekee cha siasa chenye dhamira ya kweli kwa Watanzania na kinachoweza kuiondoa CCM madarakani na kushika Dola

Kupitia mkutano huo na Wanahabari, Assenga amewaomba radhi viongozi wa ngazi mbalimbali wa CHADEMA, wanachama na Watanzania kwa ujumla wake kwa maamuzi aliyokuwa ameyachukua hapo awali ya kukihama chama hicho, akiamini kwamba maamuzi hayo aliyafanya bila kutafakari kwa kina.

Pia soma
Patrick Assenga avuliwa Uanachama CHADEMA
- Patrick Assenga ajutia kuondoka CHADEMA, amlaumu Boniface Jacob kwa kutokusema ukweli mapema. Amuomba Mungu ampe ujasiri

Welcome sir
 
Sasa tunasubiri kumpokea mw.kiti wa alipo kuwa pamoja na mw.kiti bosi wao kwani naye anaelekea kutambua haki ni msingi wa amani
 
Kwa hali ya sasa na kwa namna ya Wasaliti wanavyopiga Magoti kwa CHADEMA kuna haja ya kuanzisha kitengo maalum cha dharula cha usaili wa Wasaliti

Ningeomba pia niwe miongoni mwa Wajumbe wa Kamati hiyo
Ijapokuwa ng'ombe wengi waliopotea watarudi zizini, lakini wanaporudi watakatwa mikia ikiwa ni alama muhimu ya kuwatambua.
 
nani mwenye ubavu wa kumkataa pale chadema kwa mfano kamanda?

na kulivyo na ombwe la uongozi na ukosefu wa agenda,
kuna mtu anaweza kukataliwa kujiunga chadema kweli?

ikitokea,
basi itakua ni unafiki wa kiwango cha juu mno. :pulpTRAVOLTA:
Gentleman tuliza mihemko🐒
 
Ok, sasa nini kilimkengeua! Msiwaweke kwenye vyeo, wawe wanachama kama mimi!
Chadema wanashindwa nini kusajili wanachama wapya kwenye mikutano yao inayojaza wafuasi wengi,

Hili wimbi la kurudi kwa wasaliti wengi Lina agenda mbaya nyuma yake,
Mtu kama Selasini aliefanya mapinduzi Nccr leo unampokea aje kufanulya nini?

Kwa upuuzi huu utasikia hata Yeriko amerudi pamoja na matusi yote anayotukana,
Vyama vya upinzani viko vingi, wangeenda hata TLP,
 
Kwa hali ya sasa na kwa namna ya Wasaliti wanavyopiga Magoti kwa CHADEMA kuna haja ya kuanzisha kitengo maalum cha dharula cha usaili wa Wasaliti

Ningeomba pia niwe miongoni mwa Wajumbe wa Kamati hiyo
Kwa sifa zipi ulizonazo,unadhani unafaa kuwa ni miongoni mwa wasaili watu wanaorejea chadema?
 
Aliyekuwa Kada wa CHAUMMA, Patrick Assenga ametangaza kukihama chama hicho na kurejea Chama CHADEMA ambacho kimsingi ni chama alichokitumikia kwa miaka mingi kabla ya kuhama hapo

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Jumanne Mei 26.2026, Assenga amesema maamuzi ya kurejea CHADEMA yamekuja baada ya tafakuri ya kina ambayo ameifanya na kujiridhisha pasipo na shaka kwamba CHAUMMA haina mwelekeo na dhamira ya kweli ya kuiondoa CCM madarakani, badala yake amebaini kuwa CHADEMA ndio chama pekee cha siasa chenye dhamira ya kweli kwa Watanzania na kinachoweza kuiondoa CCM madarakani na kushika Dola

Kupitia mkutano huo na Wanahabari, Assenga amewaomba radhi viongozi wa ngazi mbalimbali wa CHADEMA, wanachama na Watanzania kwa ujumla wake kwa maamuzi aliyokuwa ameyachukua hapo awali ya kukihama chama hicho, akiamini kwamba maamuzi hayo aliyafanya bila kutafakari kwa kina.

Pia soma
Patrick Assenga avuliwa Uanachama CHADEMA
- Patrick Assenga ajutia kuondoka CHADEMA, amlaumu Boniface Jacob kwa kutokusema ukweli mapema. Amuomba Mungu ampe ujasiri

Mission imefeli so ni kuangalia namna ya kurud CDM, hawa kuku wawe wanachama wa kawaida tu
 
Back
Top Bottom